Mahakama yazuia ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 kuguswa kuanzia leo Juni 27, 2022

Mahakama yazuia ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 kuguswa kuanzia leo Juni 27, 2022

Maridhiano makubwa yameshafanyika, chadema hawataki vile viti na hata kama wakitolewa still hawatapeleka watu wengine

Ni kama swala la ruzuku Tu mpaka Leo hawataki Kwa sababu zao binafsi

Viongozi wakuu wamefaidika na maridhiano ya kwao Kwa manufaa yao

Lisu kalipwa pesa zake mbowe nae biashara zake zimefunguliwa vizuri
Mkuu, kidogo ninakubaliana nawe, lakini kikubwa sikubaliani kabisa na dhana yako.

Viongozi wa CHADEMA, kupewa HAKI zao, kama huko ndiko unakokuita "kufaidika binafsi", basi unakosea. Huko si kufaidika kwa fadhira, bali ni kupata HAKI walizokuwa wameporwa. Lissu kapata HAKI zake, hana sababu za kushukuru sana kupita kiasi.

Mbowe kapata HAKI zake, za kutoonewa kwa kesi isiyokuwa na mbele wala nyuma

Kupata HAKI kwa hawa viongozi ni faida kwa CHADEMA, kwa sababu sasa viongozi wao watashughulikia maswala ya chama chao bila ya kupotezewa muda.

Unaposema "swala la ruzuku hawataki kwa sababu zao", hapa pia inaonyesha huna uelewa au unajifanya tu hujui mambo yallivyo. Ya nini wachukue ruzuku wakati hawatambui matokeo ya uchaguzi uliofanyika? Hivi unaelewa ruzuku inatolewa kwa misingi gani? Unadhani hiyo ni hongo kwa vyama ili vikubali inayoyataka CCM?

Kupeleka watu wengine kuchukua nafasi ya Halima Mwenye Mbwa ni kuhalalisha haramu. Kama huelewi jielimishe.
 
27 .06.2022
MAHAKAMA KUU
KANDA YA DAR ES SALAAM

MISC. CASE 27 / 2022 HIGH COURT OF TANZANIA

CHADEMA YAIBUKA NA PINGAMIZI DHIDI YA MAOMBI MAPYA YA HALIMA MDEE & 18 WENGINE. PINGAMIZI LA CHADEMA KUSIKILIZWA TAREHE 29 JUNE 2022

Kweli cdm wajitenge na hayo mazungumzo waendelee kimpango wao. Wanapoteza Muda tu.
Kitu ambacho cdm hawajui Ni kuwa wamefika hapo kwa uwezo wa Mungu tu...hawakustahili kuwa hapo. Wakitaka kusubiri fadhila za CCM wakamuacha Mungu wao aliowapigiania kipindi chote Cha shida wamekwisha! Warudi njia walikuwepo ndo Ina Mungu wao.
 
Hahaha..... tatizo siyo Chadema bwashee

Hizi kumbukumbu zitabaki milele lakini Chadema inaweza Kufa

Mkuuu kumbu kumbu tulizonazo kichwani ni kuondokewa na Baba Wa taifa JKN na Mzee wa kazi chuma Ya Chato JPM,hayo mengine kayawekeni kwenye kumbu kumbu zenu.
Chama badala ya kutumia Pesa kujenga Ofisi pale Ufipa wanakalia kuonea wivu Wanawake Covid 19,Na kuendesha makesi yasiyo na Tija kwa chama chao.
 
..Nadhani uendawazimu.

..Kama kina Halima wangejitetea kule kwenye baraza kuu lakini wakafukuzwa halafu wakaenda mahakamani then kungekuwa na sababu ya kujibu hoja zao.

..Ndio maana nasema Cdm wasiende mahakamani.

Wewe ndo unasema wasiende ila Wao wataenda mana wanataka akina mdee wafukuzwe ili weweke mademu zao,na hilo Bunge la MAHAWALA hatulitaki kabsaa,bora wabaki hawa tu.
 
Mimi nimejikita zaidi demokrasia na utawala wa sheria.
Mdau uko kichama zaidi bila kujari wabunge haramu wanatumia kodi yako na yangu. Na ni ishara ya uovyo ngazi ya nchi.
CDM inaweza hata kufa lakin Taifa lipo tu. Onyesha bas unajari sheria, kanuni na taratibu bila kujari siasa za vyama. Usipende sana uovyo!
Hope una watoto. Unataka wawe na namna gani ya kufikiri na kutenda?
Kujari = kujali. Ukiona umeweza kuandika vizuri urudi tujadili haya mambo ya kitaifa.
 
Hahaha..... tatizo siyo Chadema bwashee

Hizi kumbukumbu zitabaki milele lakini Chadema inaweza Kufa
Hivi kwani kesi imesikilizwa?
Hao wameomba wasiguswe ubunge wao, ni haki yao lakini litakapokuja mahakamani ktk utetezi ndo hapo hao kina mdee wataangukia pua.
 
Tuliwaambia mkatutukana hafukuzwi mtu CHADEMA na hafukuziki ovyo!!!!
KUNA MAANA FULAN KUWA PALE BUNGENI NA MKUU WENU ANAJUA FIKA ….

Kama hajui wawafungulie kesi ya kufoji saini ya Mnyika!

Wajinga ndo waliwao , kaeni kushabikia msiyoyajua!!

Nasikia CHADEMA ngazi za chini wamemwangukia KINANA asaidie Bahati nzuri Memo nimeipata! Who is KINANA then ? You are jocking
Cc Evarist Chahali
Britanicca
Sasa jamani kwani kesi imeanza?
Tusubiri mabishano ya kisheria.
Hiyo ni court injuction tu ambayo hata kichaa anaweza weka zuio asiitwe kichaa na mahakama ikampa hyo haki ya kutoitwa kichaa hadi daktari athibitishe
 
CHAMA CHA MIHEMKO HICHO.
hawawezi kukuelewa.
Kama haukuwapeleka bungeni utawafukuza vipi ubunge?
Aliyewapeleka bungeni akawaapisha ndo anajua jinsi ya kuwafukuza ubunge
We kweli jinga, yaan mtu atumie vyeti vyoko kupata ajira halafu na wewe ukae tu usubiri mwajiri amfukuze.
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda la kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale itakaposikiliza maombi ya rufaa yao.

Chanzo: MwanaHalisi

===========

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda kuhusu kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale Mahakama hiyo itakaposikiliza maombi ya Rufaa yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya CHADEMA kupitia kwa mawakili wake akiwemo Peter Kibatala, kuwasilisha pingamizi la awali wakipinga maombi mapya ya akina Mdee dhidi yao ambapo wanaiomba mahakama hiyo iwape kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.

Mdee na wenzake wamefungua maombi Mahakama Kuu dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema (iliyosajiliwa) wakiomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

Sambamba na maombi hayo ya ridhaa namba 27 ya mwaka 2022, pia wamefungua maombi ya amri ya zuio dhidi ya NEC na Spika, kutochukua hatua dhidi ya uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama.

Maombi hayo yaliyopangwa kusikilizwa na Jaji Mustapha Ismail yametajwa leo Jumatatu Juni 27,2022, ndipo mawakili wa Chadema wakaibua pingamizi, dhidi ya maombi hayo ya zuio.

Niwaonavyo hawa makamanda bado ni loyal kwa CDM na wanaendelea kuwa na mapenzi na chama chao. Shida pekee iliyopo ni kwamba wana tofauti za kimtazamo na top brass ya CDM.

Vikao vya maamuzi vya vyama yetu vya kisiasa huwa ni rubber stamp tu ya kurasimisha decisions za wenyeviti. Yeyote anayekosana na mwenyekiti huwa hasilimiki. Historia imesheheni mifano mingi ya hao wahanga. Sasa hivi Ayatollah Mbowe akiachia kiti, akakichukua mtu mwingine ambaye hana mtazamo tofauti na kina Mdee, utashangaa wajumbe wa CC na BK watakavyobadili gia angani. Wanaweza kutangaza msamaha usiokuwa na masharti yoyote kwa Mdee na wenzake.

Wenyeviti wa vyama vya siasa waache selfishness na kuweka maslahi ya vyama vyao mbele. Hulka zao za dictatorship hazina manufaa yoyote kwa vyama vyao.
 
Ww Una uchungu na Kodi yako Kwa watu 19 Tu? Mbona hulalamiki Kodi yako Kwa mambo mengine?

Wakina mdee wakitoka Kodi yako itakuwa itakuwa imejenga barabara ?
Mambo mengine kama yapi?? Taja ambako kodi inatumika hovyo.
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda la kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale itakaposikiliza maombi ya rufaa yao.

Chanzo: MwanaHalisi

===========

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda kuhusu kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale Mahakama hiyo itakaposikiliza maombi ya Rufaa yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya CHADEMA kupitia kwa mawakili wake akiwemo Peter Kibatala, kuwasilisha pingamizi la awali wakipinga maombi mapya ya akina Mdee dhidi yao ambapo wanaiomba mahakama hiyo iwape kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.

Mdee na wenzake wamefungua maombi Mahakama Kuu dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema (iliyosajiliwa) wakiomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

Sambamba na maombi hayo ya ridhaa namba 27 ya mwaka 2022, pia wamefungua maombi ya amri ya zuio dhidi ya NEC na Spika, kutochukua hatua dhidi ya uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama.

Maombi hayo yaliyopangwa kusikilizwa na Jaji Mustapha Ismail yametajwa leo Jumatatu Juni 27,2022, ndipo mawakili wa Chadema wakaibua pingamizi, dhidi ya maombi hayo ya zuio.
mmmh
 
Pole ya Nini? Wewe ndio nikupe pole kwa kudhani temporary injuction ndio hukumu. Mnasema ubunge usiguswe je uanachama?
Huna akili wewe! Uanachama ni pesa ule? Cha msingi kwao ni Ubunge tu. Kweli Halima na wenzake ni mpango wa Mungu
 
Ngoja Tusubilie maamuzi ya Jaji Mustapha Ismail Kambona Leo.Jaji Ismail ni mdg wao wa mwisho na Mzee Membe. Hapa hii kesi haita isha hadi uchaguzi ujao. Case have been taken by event [emoji3]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda la kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale itakaposikiliza maombi ya rufaa yao.

Chanzo: MwanaHalisi

===========

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda kuhusu kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale Mahakama hiyo itakaposikiliza maombi ya Rufaa yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya CHADEMA kupitia kwa mawakili wake akiwemo Peter Kibatala, kuwasilisha pingamizi la awali wakipinga maombi mapya ya akina Mdee dhidi yao ambapo wanaiomba mahakama hiyo iwape kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.

Mdee na wenzake wamefungua maombi Mahakama Kuu dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema (iliyosajiliwa) wakiomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

Sambamba na maombi hayo ya ridhaa namba 27 ya mwaka 2022, pia wamefungua maombi ya amri ya zuio dhidi ya NEC na Spika, kutochukua hatua dhidi ya uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama.

Maombi hayo yaliyopangwa kusikilizwa na Jaji Mustapha Ismail yametajwa leo Jumatatu Juni 27,2022, ndipo mawakili wa Chadema wakaibua pingamizi, dhidi ya maombi hayo ya zuio.

Halima Mdee yatakupata yaliyompata Kamanda Alfonce Mawazo.​

Punguzeni jazba wajuba, Halima na wenzake they are done ni suala la muda tu.

Wenyewe wanajua,

Spika anajua,

Ccm wanajua,

Na wa Tz wanajua pia.
 
Back
Top Bottom