Jaji Wewe Hii Bhaghoha Sana
MMashughuli Gete Gete
 
Tatizo wengi bado hamjui siasa za manipulation nchi za Africa, sasa muwe tayari kupokea hukumu ya rufaa ya serkali kwenye kesi hiyo hiyo,.......hapo serikali inatafuta official recognition ya mahakama zoezi liko pale pale.
 
Kwa mahakama za Tanzania kesi zote zinazoihusu serekali,serekali haijawahi kushindwa hata siku moja,hukumu ya kwanza inaweza ikashindwa,kwenye rufaa inashinda kwa kutumia wale majaji ambao kwenye uchaguzi utasikia wanagombea nafasi mbalimbali kupitia chama cha CCM.
 
26 September 2024 tunaona ujeuri wa Serikali kufika mahakamani kutetea tangazo lake haramu la tarehe 02 Agosti 2024 katika gazeti la serikali lililotolewa na waziri wa TAMISEMI kufukuza wakaazi wa Ngorongoro ingawa waziri hana mamlaka na siyo sahihi kutoa amri kuwahamisha


TOKA MAKTABA :

Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673​


AMRI YA MAREKEBISHO YA AMRI YA MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA KATIKA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA) YA MWAKA 2024

1. Amri hii itajulikana kama Amri ya Marekebisho ya Amri ya Mgawanyo wa Maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya Mwaka 2024 na itasomwa pamoja na Amri ya Mgawanyo wa Maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya Mwaka 2019 ambayo hapa imerejewa kama "Amri kuu".

2. Amri kuu inarekebishwa katika Jedwali kwa kufuta kata, vijiji na vitongoji katika Halmashauri za Wilaya ya Ngorongoro, Bahi, Chemba, Kasulu, Kakonko, Hai na Rombo kama ilivyoainishwa katika Jedwali.

Hili ni Tangazo la Serikali namba 673 la Agosti 2, 2024.

Kwa mujibu wa tangazo hili, vitongoji 96 na vijiji 25 vya Ngorongoro vimefutwa.
 
Samia akimuweka mkwewe tamisemi ili aweze kufanikisha malengo yake batili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…