Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 42,525
- 74,605
Mtu wenu huyu
😂😂Katuga sasa anasubmit nini mbona kama anajiongelesha mwenyewe
😂😂Katuga sasa anasubmit nini mbona kama anajiongelesha mwenyewe
Ndiyo mie ni layman, surprise gani? Km alipigwa risasi kwenye eneo muhimu na lenye ulinzi maalumu, itakua hii case uchwara? Kila mtu anajua hukumu yake nini. Nitolee ashuo zako hapa.Huijui Sheria Wewe, wait for a big suprise
Haswaa.Kaishiwa,mwenzao kawafunika
Anataka pia kupendekeza vijiadhabu vidogo vidogo ili tu kumuondolea TAL credibility kwenye kugombea madaraka ya umma. Yeye alishasema hakuna hiyo! Ni ama umnyonge au umuachie huru. Katuga asilete Ukatuga (Ukilaza) wake kuturubuni hapa.Katuga umesema utaenda kwenye kesi moja kwa moja ila naona unazunguka mbuyu
Hakuna submission yapo ni maneno tuSEHEMU YA 3.
Nassoro Katuga anaendelea:
Lakini pili, kuna ku-manifest by overt act.
Lakini tatu, kuna ku-manifest by deed.
Kwa kuwa maneno yaliyotumika ni “or”, tukachukua manifestation by deed.
Nia yake kwa kitendo cha deed — maneno.
Waheshimiwa Majaji, kwenye manifestation by overt act na deed yanaonyesha kuwa yapo similar.
Neno “deed”, kwa maana ya Black’s Law Dictionary, Third Edition, limetafsiriwa kuwa “Deed is something that is done.”
Lakini the same dictionary ime-define “overt act” kuwa “an outward, physical manifestation.”
Inaendelea mbele kusema “an overt act can constitute evidence of participation in conspiracy even though the act itself is not...”
Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, mtaona wazi haya maneno “overt act” na “deed” — they are not similar.
Ndiyo maana, Waheshimiwa Majaji, kuonyesha utofauti kwenye kesi ya Hatibu Ghandi and Others vs Jamhuri, TLR 196, Na. 12, katika ukurasa wa 67.
Walisema maneno ya individual hayatengenezi uhaini.
Ndiyo wanachojadili, Waheshimiwa — overt act.
Kwa hiyo, kwenye kesi hii, ili overt act iwe proved, lazima aonekane amefanya nini.
Kwenye hii kesi hakukuwa na hii manifestation by deed.
Lakini, Waheshimiwa Majaji, tunaona pia ni busara niwaalike kwenye tafsiri ya manifestation katika Oxford Dictionary, Edition ya Nane.
Ime-define “manifest” as “to show something clearly, an attitude or quality” — ndiyo maana yake.
Waheshimiwa Majaji, tumeiambia Mahakama hii Tukufu, manifestation iliyofanyika hapa ni manifestation by deed.
Deed ya nini? Kitendo chake cha kutoa na kusambaza maneno.
Waheshimiwa Majaji, hata neno “utter” limekuwa defined katika kifungu cha 5:
“Includes or dealing with or an attempt to use or deal with...”
As I said before, “utter” ni kitendo; lazima kiambatane na kitu gani mbele.
Wee ndio zaidi hujui kabisa.Kaa kimya hujui kitu
Tunamsoma hata kwa lugha ya kisheria, japo ni layman ila hakuna kitu.Wakati kesi inaanza mliponda hivi hivi mwisho wa siku mwamba akakutwa na kesi ya kujibu ....ukimsoma Katuga kiufipa kweli utasema anapuyanga lakini ukimsoma kisheria anatumia vifungu kumjibu Lisu kuhusu hati ya mashitaka
Jamani sasa mbona hakuna updates? Au CCM wameweka mpira kwapani?Leo ni siku ambayo kesi ya Lissu inaendelea mahakamani. Tunaomba Manyanza utuletee hiyo Update.
MAHAKAMA IMEANZA MAWAKILI WA SERIKALI WANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO.
SEHEMU YA 1.
Jumanne, Septemba 29, 2026
Lissu ameingia kwa kushangiliwa sana.
Majaji nao wameingia.
Mawakili wa Serikali wawili leo siwaoni. Hayupo Ajuaye Zegeli na Job Mrema.
Karani wa Mahakama anajiandaa kusoma kesi: Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya 2025, Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.
Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, anasimama.
Nassoro Katuga:
“Waheshimiwa Majaji wa Mahakama hii Tukufu, iw apendeze, naitwa Nassoro Katuga, nipo pamoja na:
1. Ignasi Mwinuka, Wakili wa Serikali Mkuu;
2. Tawabu Issa, Wakili Mwandamizi;
3. Cuthbert Mbilinyi, Wakili wa Serikali;
4. Winiwa Kasara, Wakili wa Serikali.
Sisi kwa pamoja tunaiwakilisha Jamhuri.
Mshtakiwa yupo mbele yenu.
Waheshimiwa Majaji, shauri leo limekuja kwa ajili ya kuleta mawasilisho, specific kwa upande wa Jamhuri kuleta mawasilisho.
Upande wa Jamhuri tupo tayari.”
Jaji Ndunguru:
“Mshtakiwa?”
Lissu:
“Waheshimiwa Majaji, nipo tayari.”
Jaji:
“Tuendelee upande wa Mashitaka.”
Nassoro Katuga:
“Naomba kutoa ahadi, Waheshimiwa Majaji, kwamba tutakuwa na mawasiliano ambayo si marefu.
Tuta-focus na shauri lililopo mbele yetu.
Waheshimiwa Majaji, nitaanza tu submission. Naitwa Nassoro Katuga.
Waheshimiwa Majaji, mshtakiwa ameshtakiwa kwa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Urekebu wa Mwaka 2022.
Ambapo, Waheshimiwa Majaji, kuhusiana na taarifa ya shitaka hili, inaelezwa kwamba tarehe 23 Aprili 2025, ndani ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitengeneza nia ya kuchochea umma kuweza kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa nia ya kuitisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (for the purpose of intimidating the Executive), kwa kudhihirisha nia hiyo kwa kutoa maneno yafuatayo:
‘Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, wanasema hivi: Msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli, ni kweli kwa sababu tutazuia uchaguzi, hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko. Kwa hiyo tunaenda kukinukisha, huu uchaguzi tutauvuruga, tutauvuruga kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana.’
Haya maneno ndiyo Jamhuri imeleta mbele yenu, mbele ya sheria kuyaangalia.
Kwamba maneno haya ndiyo, Waheshimiwa Majaji, tunatuhumu au kutafsiri in favour of the Republic.
Kwamba mshtakiwa alitoa maneno haya kwa nia ya kuitisha Serikali ili apate mabadiliko, ambayo aliyetafsiri ni ‘mabadiliko’.
Waheshimiwa Majaji, kifungu ambacho nimekirejea cha 39(2), upande wa Jamhuri tulikifanyia research kama Mahakama ilishawahi kuki-test.
Tafiti zilionyesha kwamba Mahakama zetu katika mashauri ya uhaini ni mashauri ambayo yalishitakiwa chini ya kifungu cha 39(a).
Waheshimiwa Majaji, samahani, kama itawapendeza, naomba nimuingize Job Mrema katika kolamu ya upande wa Jamhuri. Alikuwa amepata dharura, sasa amefika.
Waheshimiwa Majaji, kwa kuwa tumejiridhisha kwamba haijawahi kutumika katika Mahakama zetu, tuweze sasa kutafsiri hati ya mashitaka pamoja na kifungu kilichotumika cha 39.
Ili kuweza kuona ni vitu gani Mahakama yenu Tukufu ilianza kuangalia ushahidi, basi ni kitu gani upande wa Jamhuri ulipaswa kuthibitisha.
Naomba kwa kuanza kuwaalika katika kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.
Kifungu chenyewe kinasema:
‘Mtu yeyote ambaye yupo chini ya utii, awe Tanzania au nje ya Tanzania, atengeneze nia either kufanyika au kusababisha kufanyika au kutengeneza nia ya kuchochea.’
Kwa mujibu wa kifungu cha 135 cha CPA, Sura ya 20, Urekebu wa Mwaka 2023, kinaelezea kwamba mashitaka lazima yawe na maelezo ya kosa la shitaka husika pamoja na maelezo ya shitaka.
Ambayo sheria inasema hayo maelezo lazima yatie information ya jinsi shitaka lilivyofanyika.
Lakini kifungu cha 138(a)(iii) kinaelekeza kwamba technical terms hazitakiwi kutumika.
Inatakiwa itumike ordinary language, lugha ya kawaida.
Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, mtaona kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d), kinaelekeza kwamba ili mtu ashitakiwe kwa kosa la uhaini la aina hii:
Kwanza ni lazima awe mtu mwenye utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwetu ilichukua mshtakiwa ni mtu wa Jamhuri ya Tanzania akiwa Tanzania, tukaacha ‘elsewhere’.
Hati yetu ya mashitaka ikachukua ‘forms an intention to instigate’ — nia ya kuchochea.
Tukaachana na maneno ‘forms’ zingine za ‘intention to defect’.
Ikaachana na ‘intention to persuade’, ‘to counsel’, ‘to...’
‘Intention to instigate the public’ — umma kwa ujumla wake, nitaeleza hapa kwa nini.
Hati ya mashitaka ikaeleza watu wamechochewa kufanya nini.
Mshtakiwa akichochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 — General Election, Waheshimiwa.
Waheshimiwa Majaji, hati yetu ya mashitaka imeachana na neno ‘deed’, ikachukua neno ‘for the purpose of intimidating the Executive’.
Na hapa ikaachana na maneno ‘intimidating Legislature’ na ikachukua ‘intimidating the Executive’.
Ukiendelea na hati ya mashitaka, ile nia ya mshtakiwa kudhihirisha nia yake...
Hati ya mashitaka ikaachana na maneno ‘manifestation ya hiyo nia by publication by overt act’, ikaachwa.
Lakini ikachukuliwa ‘manifestation by his deed’ — alidhihirisha nia kwa kitendo chake.
Kitendo gani, Waheshimiwa?
Kutoa maneno ambayo nimeshayatoa, Waheshimiwa.
Waheshimiwa Majaji, sehemu zote ambazo nilikuwa naiambia Mahakama Tukufu kwamba hati ya mashitaka imeacha haya, imechukua haya.
Imeacha ‘manifestation by publication’, ikachukua ‘manifestation by deed’ kwa mujibu wa kifungu cha 39.
Neno lililotumika ni ‘or’.
Kwa tafsiri nyepesi, pale ambapo inatumika ‘or’, hayo maneno siyo similar.
Kwa maana nyingine, yanatumika disjunctively; huwezi kuyachukua yote kama kiroba ukapachika katika hati ya mashitaka.
Inamaanisha ulichukua yote hayo ukayaweka, hiyo act inakuwa defective.
Ili maneno haya kuwa sawa, kama kuna ‘or’, lazima kuna maneno yaongezwe kuyafanya yawe similar, mfano neno ‘similar’ lenyewe au maneno mengine yanayoonyesha similarity.
Unless ilitumika ‘or’, kuna sheria inatumika kutaka yaongezwe.
Ukiyaweka yote, hiyo hati ya mashitaka inakuwa defective.
Waheshimiwa Majaji, haya tunayozungumza siyo maneno yetu.
Pale ambapo ‘or’ inatumika, siyo maneno yetu bali maneno ya Bungeni na kutungwa sheria.
Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya Kwanza, na Urekebu wa 2023, kifungu cha 13.
Kwa ridhaa yenu, kifungu kinasomeka hivi...
Haya ndiyo maneno ambayo nimeyakopa katika submission.
Ndiyo maana hati yetu ya mashitaka iliruka baadhi ya maneno ili kufanya hati yetu isiwe defective na iwe yenye kueleweka.
Hati ya mashitaka ni nyaraka muhimu inayomfahamisha mshtakiwa mashitaka anayoshitakiwa nayo na kumweka sasa katika position ya kujitetea.”
SEHEMU YA 2
Nassoro Katuga anaendelea:
“Waheshimiwa Majaji, kifungu cha 39(2)(d) kimeanza kwa neno ‘any person who, being under...’
Waheshimiwa Majaji, hili neno ‘any person’ halijam-exclude mtu yeyote, unless ana immunity kisheria.
Mtu mwingine anaweza kusema yeye ana cheo fulani au ni kiongozi wa chama cha siasa.
Kifungu hicho hakijachagua huyo ‘any person’ anatokea wapi.
Ndiyo maana kwanza tumeanza kuchambua.
Waheshimiwa Majaji, narudi kwenye kifungu cha 39(2)(d), kinasema mtu yeyote akichochea, lakini hati yetu imetumia neno ‘public’.
Kuna neno ‘any person’, lakini Jamhuri imetumia neno ‘public’.
Waheshimiwa Majaji, hati ya mashitaka kwa upande wa Jamhuri imetumia neno ‘public’ kuweka clarity, kufanya hati ya mashitaka ieleweke kuendana na ushahidi wa upande wa Jamhuri ulioutoa.
Hii inafanyika kuendana na kifungu cha 135 cha CPA.
Waheshimiwa Majaji, tumetumia neno ‘to instigate the public’ kuendana na kifungu cha 135, kufanya hati ya mashitaka kueleweka kuendana na ushahidi wa upande wa Jamhuri ulioutoa.
Waheshimiwa Majaji, kama tulivyoeleza awali, kifungu cha 135 kinataka maelezo ya kosa yaeleweke katika kiwango ambacho mshtakiwa aweze kujitetea na in conformity na ushahidi uliotolewa.
Waheshimiwa Majaji, neno ‘any person’ linafanana na neno ‘public’.
Waheshimiwa, ‘any person’ na ‘a group of people’ yamekuwa included kwenye ‘public’.
Yametafsiriwa katika kifungu cha 5 cha Kanuni ya Adhabu, Waheshimiwa.
Siyo tu akimaanisha watu wote wa Tanzania Bara, lakini hata yule mkazi au anayetumia eneo fulani na any number of those people.
Kwa hiyo, ‘public’ inazungumzia watu.
Na Waheshimiwa Majaji, katika kuandaa taarifa za mashitaka, kama ‘any person’ refers to a person, you have to mention.
Kama unataka ku-refer maneno yako yaende kwa ‘any person’, lazima utaje huyo person.
Na kama hati yako itarefer ‘group of people’, lazima utaje hilo group.
So, neno ambalo linajumuisha kama alikuwa amechochea mtu mmoja au kikundi fulani, neno sahihi kutumia ni ‘public’.
Na hii, Waheshimiwa Majaji, ni kwa mujibu wa kifungu cha 5.
Waheshimiwa Majaji, kwa ushahidi wa Jamhuri ulivyokuwa, Jamhuri inamtuhumu kuchochea umma.
Mshtakiwa wakati anachochea hakulenga kikundi fulani na hakumlenga mtu fulani ambaye sasa upande wa Jamhuri amtaje, na hakumlenga.
Ndiyo inakuja sasa tafsiri ambayo ni whether a person or a group of people.
Waheshimiwa Majaji, hakuna namba kamili inayoweza kutoa tafsiri ya ‘a group of people’.
Kwa hiyo, umma utakuwa ni ‘a group of people’.
Na hii sasa tunaipata kwenye tafsiri ya hilo neno lilivyotumika.
Waheshimiwa Majaji, tukirudi kwenye swala zima la kudhihirisha (manifestation) kwa mujibu wa kifungu cha 39:
Nia ya kutenda uhaini inadhihirishwa vipi?
Kwa mujibu wa kifungu hiki, manifestation inaweza kusababishwa kwa kusambaza maandishi au michoro.”
Kutamka ni kutenda kweli jamani? Hata kama hatujaenda shule, hapa Katuga katulisha matango pori😅🤣😂By his deed of uttering.
Big surprise gani wakati tunafahamu hukumu ilishaandaliwa kabla hata ya mtuhumiwa kukamatwa!Huijui Sheria Wewe, wait for a big suprise
Yaan hata sielewi, mara anasema akikutwa na hatia, mahakama Inaweza kutumia utashi wake kutoa hukumu. Anachanganya tu mambo hapa.Katuga umesema utaenda kwenye kesi moja kwa moja ila naona unazunguka mbuyu
Aibu tunaona sisi 😂😂😂Kutamka ni kutenda kweli jamani? Hata kama hatujaenda shule, hapa Katuga katulisha matango pori😅🤣😂
Hapa katuga analenga niniSEHEMU YA 5.
Nassoro Katuga anaendelea:
Kazi ya hati ya mashitaka ni kutoa reasonable information.
Kutoa taarifa kosa gani limepatikana, kosa gani kalitenda.
Sentensi hizi zimekamilika; hazihitaji ku-clarify ili kuleta maana.
Waheshimiwa Majaji, kwa kuelekeza kwa kirefu sana kwa sababu ni shitaka kubwa, naomba niguse kidogo kwenye adhabu.
Waheshimiwa Majaji, kifungu hiki cha 39(2)(d) kinasema mshtakiwa akikutwa na hatia basi atakuwa “liable”.
Underline neno “shall be liable”, if not to bold.
Inamaanisha adhabu katika shitaka hili ni kuanzia sifuri (condition) up to death penalty.
Neno “shall be liable”, ambalo linaipa Mahakama hii discretion, siyo maneno yangu. Naomba niwape:
Bahati John vs Jamhuri, Criminal Appeal No. 114 ya mwaka 2019, TanzLII 2022, katika ukurasa wa sita.
Mahakama ya Rufaa ilirejea kesi ya Opoya vs Uganda (1967) 752, Court of Appeal for East Africa.
Ilisema kwamba “they are not mandatory but provide the sentence...”
Inamaanisha Mahakama, kwa utashi wake, inaweza ku-impose penalty.
Kwa maana nyingine ya kisheria, haipo under maximum.
Inaipa Mahakama yetu utashi wa hukumu in case kuna hatia.
Siyo tu kwenye hiyo case, bali kuna Sentence Guidelines za CJ za mwaka 2023.
Maneno yanamaanisha Mahakama kuwa na utashi.
Aya ya kwanza, aya ndogo ya 6(1).
Hii Guidelines imeelezea maneno gani yakitumika kwenye sheria, Mahakama inapewa discretion ya kutoa adhabu.
Na neno “liable” ni moja wapo ya maneno ambayo yanatoa discretion kwa Mahakama.
Naomba sasa twende kwenye hoja ya msingi — jukumu la Jamhuri ambalo tunaambiwa ni kuthibitisha.
Waheshimiwa Majaji, tupo aware kwamba jukumu hili kwa Jamhuri tumepewa katika kifungu cha 3(2) cha Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6, Urekebu wa 2023.
Kwa kuanza, Waheshimiwa Majaji, kwa tafsiri ya kifungu cha 39(2)(d) na kwa ushahidi uliotolewa,
it’s our submission kwamba jukumu la kuthibitisha kwa mujibu wa kifungu cha 3(2)(a) limetimilishwa.
Lakini pia, mbali na upande wa Jamhuri kuthibitisha, tunajua ni sheria kuzingatia ushahidi wa defence wakati wanaamua.
Waheshimiwa, mtaona upande wa utetezi hawajauteteresha hata kidogo, zaidi ya “sijui”, “sikumbuki” kuwa nyingi.
Waheshimiwa Majaji, kifungu ambacho tumekirejea cha 3(2)(a) kinataka kuthibitisha beyond reasonable doubt.
Waheshimiwa, ku-prove beyond reasonable doubt haimaanishi kuthibitisha pasipo kuacha kivuli.
Hiyo siyo tafsiri sahihi ya kifungu cha 3.
Nimeona hii kwenye hoja ya sifuri mpaka kunyonga aliyosema..Ila Lissu alikua mbele ya muda kusema hakuna nusu uhaini 😁.Anataka pia kupendekeza vijiadhabu vidogo vidogo ili tu kumuondolea TAL credibility kwenye kugombea madaraka ya umma. Yeye alishasema hakuna hiyo! Ni ama umnyonge au umuachie huru. Katuga asilete Ukatuga (Ukilaza) wake kuturubuni hapa.
chadema wanaleta utotomsisahau cattons of drinking water kwajili ya mtuhumiwa kizimbani plz 🐒
Na hapo bado yupo kwenye tafsiri ya hati ya mashtaka. Bado hajaingia kwenye ushahidi wa magari ya Heche aiambie mahakama idadi ya magari ya Heche ina uhusiano gani na uhaini wa Lissu. Leo maji atayaita mmma!😅🤣😂Katuga mbona anapuyanga sana? Yaan anarudia maneno hayo hayo submissions yote, au hakuna kingine? Maana naona anarudia kutamka maneno Yale Yale tu.
Khaaah.