Mahakamani 29 Septemba 2026: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

SEHEMU YA 5.

Nassoro Katuga anaendelea:

Kazi ya hati ya mashitaka ni kutoa reasonable information.

Kutoa taarifa kosa gani limepatikana, kosa gani kalitenda.

Sentensi hizi zimekamilika; hazihitaji ku-clarify ili kuleta maana.

Waheshimiwa Majaji, kwa kuelekeza kwa kirefu sana kwa sababu ni shitaka kubwa, naomba niguse kidogo kwenye adhabu.

Waheshimiwa Majaji, kifungu hiki cha 39(2)(d) kinasema mshtakiwa akikutwa na hatia basi atakuwa “liable”.

Underline neno “shall be liable”, if not to bold.

Inamaanisha adhabu katika shitaka hili ni kuanzia sifuri (condition) up to death penalty.

Neno “shall be liable”, ambalo linaipa Mahakama hii discretion, siyo maneno yangu. Naomba niwape:

Bahati John vs Jamhuri, Criminal Appeal No. 114 ya mwaka 2019, TanzLII 2022, katika ukurasa wa sita.

Mahakama ya Rufaa ilirejea kesi ya Opoya vs Uganda (1967) 752, Court of Appeal for East Africa.

Ilisema kwamba “they are not mandatory but provide the sentence...”

Inamaanisha Mahakama, kwa utashi wake, inaweza ku-impose penalty.

Kwa maana nyingine ya kisheria, haipo under maximum.

Inaipa Mahakama yetu utashi wa hukumu in case kuna hatia.

Siyo tu kwenye hiyo case, bali kuna Sentence Guidelines za CJ za mwaka 2023.

Maneno yanamaanisha Mahakama kuwa na utashi.

Aya ya kwanza, aya ndogo ya 6(1).

Hii Guidelines imeelezea maneno gani yakitumika kwenye sheria, Mahakama inapewa discretion ya kutoa adhabu.

Na neno “liable” ni moja wapo ya maneno ambayo yanatoa discretion kwa Mahakama.

Naomba sasa twende kwenye hoja ya msingi — jukumu la Jamhuri ambalo tunaambiwa ni kuthibitisha.

Waheshimiwa Majaji, tupo aware kwamba jukumu hili kwa Jamhuri tumepewa katika kifungu cha 3(2) cha Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6, Urekebu wa 2023.

Kwa kuanza, Waheshimiwa Majaji, kwa tafsiri ya kifungu cha 39(2)(d) na kwa ushahidi uliotolewa,

it’s our submission kwamba jukumu la kuthibitisha kwa mujibu wa kifungu cha 3(2)(a) limetimilishwa.

Lakini pia, mbali na upande wa Jamhuri kuthibitisha, tunajua ni sheria kuzingatia ushahidi wa defence wakati wanaamua.

Waheshimiwa, mtaona upande wa utetezi hawajauteteresha hata kidogo, zaidi ya “sijui”, “sikumbuki” kuwa nyingi.

Waheshimiwa Majaji, kifungu ambacho tumekirejea cha 3(2)(a) kinataka kuthibitisha beyond reasonable doubt.

Waheshimiwa, ku-prove beyond reasonable doubt haimaanishi kuthibitisha pasipo kuacha kivuli.

Hiyo siyo tafsiri sahihi ya kifungu cha 3.
 
Hakuna submission yapo ni maneno tu
Wenyewe wafanye wanachotaka lakn sio kwa hizi ngonjera aisee.
 
Jamani sasa mbona hakuna updates? Au CCM wameweka mpira kwapani?

Yaani ukimsikiliza Tundu Lissu akitema nondo halafu ukamsikiliza huyu wakili wa CCM, ndugu Katuga, unaona kabisa ni kama ardhi na mbingu.

Tundu Lissu kamwaga nondo hadi maCCM wanatafutana. Hivi "a group of people" au "any person" ni sawa na public kweli jamani? Hata kama mtu hukuenda shule ndio ukubali kudanganyika kiasi hiki?
 
Hapa katuga analenga nini

Mbona kama anamfanyia Lissu mitigating factor

Dizain fulan wanataka akutwe na hatia then adhabu asipewe ya kunyongwa apewe punishment nyingine
 
Anataka pia kupendekeza vijiadhabu vidogo vidogo ili tu kumuondolea TAL credibility kwenye kugombea madaraka ya umma. Yeye alishasema hakuna hiyo! Ni ama umnyonge au umuachie huru. Katuga asilete Ukatuga (Ukilaza) wake kuturubuni hapa.
Nimeona hii kwenye hoja ya sifuri mpaka kunyonga aliyosema..Ila Lissu alikua mbele ya muda kusema hakuna nusu uhaini 😁.
 
Katuga mbona anapuyanga sana? Yaan anarudia maneno hayo hayo submissions yote, au hakuna kingine? Maana naona anarudia kutamka maneno Yale Yale tu.
Khaaah.
Na hapo bado yupo kwenye tafsiri ya hati ya mashtaka. Bado hajaingia kwenye ushahidi wa magari ya Heche aiambie mahakama idadi ya magari ya Heche ina uhusiano gani na uhaini wa Lissu. Leo maji atayaita mmma!😅🤣😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…