Mahakamani kuna siri gani? Niliwahi kwenda kwa Mganga wa Kienyeji ili Hakimu na mashahidi washindwe kuongea au kuzungumza Mahakamani

Mahakamani kuna siri gani? Niliwahi kwenda kwa Mganga wa Kienyeji ili Hakimu na mashahidi washindwe kuongea au kuzungumza Mahakamani

Wanabodi,

Nayaandika haya sio kwa kufurahisha bali ni mambo yaliyonikuta na sitaki kuyakumbuka kabisa lakini kwa yaliyomtokea shahidi namba 13 wa upande wa jamuhuri Kamanda Swilla kwa kuugua...
Aiseee....!
Huyo mganga anipe dawa ya kufungua lango kuu la benki na strong room!

Nikisema ........FUNGUKA!
NOTI zinatoka zenyewe, na kupiga saluti, na kuingia garini kwangu!
 
Wanabodi,

Nayaandika haya sio kwa kufurahisha bali ni mambo yaliyonikuta na sitaki kuyakumbuka kabisa lakini kwa yaliyomtokea shahidi namba 13 wa upande wa jamuhuri Kamanda Swilla kwa kuugua ghafla kizimbani na muda mwingi kuomba ruhusa kwenda...
mleta thread japokuwa kisa chako kime base kwa watuhumiwa tu wa kesi mahakamani lakini katika uhalisia mpaka watumishi wa mahakama wengi wako vizuri sababu usipofanya hivyo kuzimu dakika sifuri tu.

Ninavyovisa vingi sana vya kutisha but,kuhusu mahakama nnavyo kama vitatu.

Kuna mheshimiwa XXX
wa mahakama fulani ilikuwa jamaa fulani apigwe mvua ya miaka sababu ushahidi ote upo mezani ilikuwa ni kwenda kupigwa nyundo tu.

mheshimiwa week moja kabla ya kwenda kumaliza kesi akaenda kuweka mambo sawa mkoa fulani.

Akiwa anatoka yupo njiani anatoka mtuhumiwa nae akaingia ndani kabla ya kuongea mganga akamwambia huyo aliyetoka fanya kila njia urudi nae hapa,jamaa ndo kwenda na kurudi nae wanafika kumbe ote ndo wahusika,ikabidi wawekane tu chini kuyasolve

Siku 5 kabla ya kesi mzee magu anatangaza kuwa ote waliokamatwa na hela za ufisadi wazirudishe wataachiwa huru
 
Wanabodi,

Nayaandika haya sio kwa kufurahisha bali ni mambo yaliyonikuta na sitaki kuyakumbuka kabisa lakini kwa yaliyomtokea shahidi namba 13 wa upande wa jamuhuri Kamanda Swilla kwa kuugua ghafla kizimbani na muda mwingi kuomba ruhusa kwenda washroom au maliwato siyo mambo ya kucheka huwa yanatokea...
Mzee wa ulozi Mshana Jr unatafutwa huku utoe ushuhuda
 
Mkiona mtu kateuliwa kuwa jaji /hakimu basi mnasema kala shavu hivi najuwa wanayoyapitia.

Kuna dada mmoja alinisimulia mme wake alifungwa kwa kesi ya magendo na dawa za kulevya walimkamata navyò.kaswekwa ndani muda ukapita. Eti kuna mtu akamwambie aende kwa mganga wamtengeneze hakimu siku ya hukumu asikumbuke chochote.

Sasa huko alokwenda kwa mganga mambo walofanya naogopa hata kuandika hapo. Mimi siwezi fanya hicho kitu hata kama mme nampenda kiasi hicho bora nihonge pesa tu.

Alienda kwa mganga wakafanya waliyofanya siku ya hukumu dada huyo mahakamani anamiona mme wake , pale mahakamani kuna dawa nayo aliweka.

Eti wakati wa hukumu hakimu akasema " huyu nae bado huko hapa kesi yake haina mashiko na aondoke atakuwa anakuja kureport hapa kila siku😂😂😂 mwanaume akatoka na kesi ya madawa ikaishia hapo.

Ilikuwaje huyo dada akanisimulia? Siku moja akawa anamuongelea mme wake eti tangu waachane hajawahi fanikiwa eti au ni maneno alomwambia wakati wanaachana?

Huyo dada anasema baada ya mme wake kuachiwa, wakarudi nyumbani baada ya miezi 7 akamfumania na rafiki yake ndo chanzo cha kuachana.

Sasa anasema wakati anaondoka na watoto wake alimwambi mmewe haya maneno, " wewe mwanaume kwa sababu yako nilienda kwa mganga nikafanya vitu ambavyo sikuwahi fanya ili utoke jela unawezaje kulala na rafiki yangu kitandani kwangu? Hutokaa ufanikiwe" akaondoka na watoto. Anasema mpaka leo mmewe hana hata mia.

Mimi kila siku nakuwa mahakamani nachekaga sana. Kwenye milango ya kuingia mahakamani wanasema ndo watuhumiwa/ ndugu za washitakiwa ndo wanawekaga madawa.hayo madawa yanawalenga mahakimu/ majaji wala sio sisi watu wa kawaida.uchawi upo.
 
Mie Kuna mshenzi alinikausha sauti kabisa, kesi ya kufukuzwa kazi, ninawakilisha shirika, jamaa aliyefukuzwa akaniomba tuonane mie nilipofika jioni maana kesi ilikuwa Tanga nikaona huyu mtu anataka kunicompromise uonekane nilikuwa nae hotel.

Nikahama hotel nikahamia Nyumbani Hotel jamaa akanisaka sikuonana nae maana alitaka anipe hela na niliona kesi yake ipo straight Hana haki na procedure zilifuatwa sikuwa na namna ya kumsaidia .

Ile naingia mahakamani akaanza kunilaumu nikamwambia mie sio Wakili wake na asinipigie tena sababu Sina mpango wa kumsaidia kesi yake ni nyoofu ajiandae kusepa kwanza hakuwa na hela ya maana mteja wangu amenilipa vizuri sana na malazi na safari ananilipa hela nzuri sana .

Jamaa akasema tutaona mie mtoto wa kidigo mie nikamshangaa tu, nikamwambia ukiniroga mie utakuwa unapoteza muda maana Sina ugomvi nawe, kazi umeharibu mwenyewe, aliyekufukuza kazi ni HR na umeshindwa kumroga HR uniroge mie .

Babu Ile naingia kwa Jaji marehemu Lugaziya J sauti ikakata, nikaahirisha kutafuta dawa pharmacy, nikakimbia Bombo hospital pale nnje Kuna pharmacy nikapiga dawa naona naongea fresh kabisa.

Basi nikarudi nikamwambia Karani nipo tayari akitoka kusikiliza anipangie tuingie, Ile nimeingia tena sauti ikakata tena.

This time Jaji nae akaogopa anaongea mambo mengi kwa yule mshtakiwa akamwambia yeye amekaa mahakamani zaidi ya miaka 30 anaijua vizuri akasema aache uhuni wake.

Kesi iliahirishwa but ananiambia Kama unasafiri usiondoke leo 😃 nami nikaona heri nifuate maneno ya wazee.nikaondoka kesho yake. Jamaa siku kesi inaitwa tena anashangaa nipo akajisemea confession aliweka kitu barabarani nisingepona nikamwambia kesi hii nachoweza kukusaidia ni ulipwe kidogo sitabishia 😃😃😃😃 Ila hakurudi kazink.

Uchawi upo. Siku nyingine nitawasimulia yaliyonikuta Mahakama Kuu Tabora Kuna wachawi kule dah
 
Usisahau mkuu pole Sana[emoji23][emoji23][emoji23], Kuna watu uchawi wanauskia tu afu wanabisha.
Mie Kuna mshenzi alinikausha sauti kabisa, kesi ya kufukuzwa kazi, ninawakilisha shirika, jamaa aliyefukuzwa akaniomba tuonane mie nilipofika jioni maana kesi ilikuwa Tanga nikaona huyu mtu anataka kunicompromise uonekane nilikuwa nae hotel...
 
Mie Kuna mshenzi alinikausha sauti kabisa, kesi ya kufukuzwa kazi, ninawakilisha shirika, jamaa aliyefukuzwa akaniomba tuonane mie nilipofika jioni maana kesi ilikuwa Tanga nikaona huyu mtu anataka kunicompromise uonekane nilikuwa nae hotel....
Mimi Kuna mkinga alinifunga tulipofika kwa hakimu nilijiskia Kama Kuna mbingu ananichukua Kila hakimu ananihuliza mi nakubali naona wazee na odience wanscheka kurudi mahabusu nawasalimulia wanasema pole Sana mungu saidia miezi minne nje ila waking no wachawi nyoko
 
Back
Top Bottom