Mie Kuna mshenzi alinikausha sauti kabisa, kesi ya kufukuzwa kazi, ninawakilisha shirika, jamaa aliyefukuzwa akaniomba tuonane mie nilipofika jioni maana kesi ilikuwa Tanga nikaona huyu mtu anataka kunicompromise uonekane nilikuwa nae hotel.
Nikahama hotel nikahamia Nyumbani Hotel jamaa akanisaka sikuonana nae maana alitaka anipe hela na niliona kesi yake ipo straight Hana haki na procedure zilifuatwa sikuwa na namna ya kumsaidia .
Ile naingia mahakamani akaanza kunilaumu nikamwambia mie sio Wakili wake na asinipigie tena sababu Sina mpango wa kumsaidia kesi yake ni nyoofu ajiandae kusepa kwanza hakuwa na hela ya maana mteja wangu amenilipa vizuri sana na malazi na safari ananilipa hela nzuri sana .
Jamaa akasema tutaona mie mtoto wa kidigo mie nikamshangaa tu, nikamwambia ukiniroga mie utakuwa unapoteza muda maana Sina ugomvi nawe, kazi umeharibu mwenyewe, aliyekufukuza kazi ni HR na umeshindwa kumroga HR uniroge mie .
Babu Ile naingia kwa Jaji marehemu Lugaziya J sauti ikakata, nikaahirisha kutafuta dawa pharmacy, nikakimbia Bombo hospital pale nnje Kuna pharmacy nikapiga dawa naona naongea fresh kabisa.
Basi nikarudi nikamwambia Karani nipo tayari akitoka kusikiliza anipangie tuingie, Ile nimeingia tena sauti ikakata tena.
This time Jaji nae akaogopa anaongea mambo mengi kwa yule mshtakiwa akamwambia yeye amekaa mahakamani zaidi ya miaka 30 anaijua vizuri akasema aache uhuni wake.
Kesi iliahirishwa but ananiambia Kama unasafiri usiondoke leo 😃 nami nikaona heri nifuate maneno ya wazee.nikaondoka kesho yake. Jamaa siku kesi inaitwa tena anashangaa nipo akajisemea confession aliweka kitu barabarani nisingepona nikamwambia kesi hii nachoweza kukusaidia ni ulipwe kidogo sitabishia 😃😃😃😃 Ila hakurudi kazink.
Uchawi upo. Siku nyingine nitawasimulia yaliyonikuta Mahakama Kuu Tabora Kuna wachawi kule dah