Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri - 2, Septemba 2026

Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri - 2, Septemba 2026

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Mahakamani leo tena kesi inaendelea kwa Upande wa Mawakili wa Serikali kumuuliza Mswali ya Dodoso Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika

1788327206595.png

Pia soma: Kesi ya Uhaini: John Mnyika Kuendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri kuendelea leo 1, Septemba 2026

Leo September 2, 2026 Last time tuliishia sehemu 327 so leo tunaendelea na


Sehemu ya 328

Mahakama imeanza. Majaji wameingia.

Mh. Tundu Lissu ameingia na kupokolewa na Makofi mengi ya wahudhuriaji wa hapa Mahakamani.

Shahidi (DW 2) wa utetezi nae alifika mapema sana saa mbili kamili asubuhi.

Mh. John Mnyika. Mheshimiwa Tundu Lissu ameingia akiwa amepiga Kombati safi kabisa ya Kaki na vibe lake liko juu sana. Nywele zake naona zinaendelea kuwa ndefu siku hadi siku.

Karani anasoma namba ya kesi akiwa amekaa upande wa kulia kidogo na kushoto kwa majaji kwa mbele.

Anasimama Ajuaye anatambulisha Kikundi Cha Serikali cha siku zote. Anasema wako tayari kuendelea na Cross Examination.

Anasimama Job Mrema kwenda kuendelea na Maswali ya Dodoso.

Job Mrema: Anakumbushwa alipoishiwa. Anaendelea sasa. Utakubaliana na mimi kama inavyosomeka kwenye hati ya mashitaka kuhusu msimamo unaashiria uasi. Sasa matukio yaliyotokea Tar. 29/10/2025

Mnyika: Hayana uhusiano kabisa na Mshitakiwa yeye alikamatwa Tarehe 09/04 na mambo ya Uchaguzi yalitokea mshitakiwa akiwa jela siku nyingi. Uhusiano unatoka wapi?

Job Mrema: Chadema inaamini katika Demokrasia?

Mnyika: Sahihi.

Job Mrema: Inawezekana Mwenyekiti akatoa hotuba bila kukuhusisha wewe?

Mnyika: Hakuna yakunishirikisha mimi kwasababu No reforms, No Election ilishaamuliwa na vikao na wote tulikuwa tunajua nini maana ya No Reforms, No Election.

Jobe Mrema: Wewe Mnyika umewahi kufungua shauri la Kikatiba?

Mnyika: Sijawahi

Job Mrema: Je Mwenyekiti nae aliwahi kufungua kesi hiyo?

Mnyika: Hajawahi

Job Mrema: Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaweka misingi ya kisheria?

Mnyika: Ni sahihi pamoja na Mikataba ya Kimataifa.

Job Mrema: Unaamini mhimili wa Mahakama katika utoaji wa Haki?

Mnyika: Mhimili nauamini lakini nina shida na Majaji wanaotoa haki baadhi yao hawaaminiki kabisa.

Job Mrema: Kutokana na ushahidi wako kuhusiana na sheria kandamizi sasa ili sheria iweze kusemwa kuwa ni kandamizi ni lazima sheria hiyo isemwe na Mahakama?

Mnyika: Sio sahihi hata Mahakama imesema katika Kesi Na. 28/2018 ya Said Kubenea ilisema kuhusu masuala ya kisiasa yanapaswa kutatuliwa kisiasa sio lazima Mahakama iseme kuhusu jambo hilo.

Jaji Ndunguru: Hivi uliyeuliza swali maana yake ni nini? Unamaanisha nini?

Job Mrema: Nimemuuliza umewahi kufungua shauri la Kikatiba?

Mnyika: Sijawahi

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba kwa mujibu wa Sheria. Mahakama imetoa sheria ya kusikiliza mashauri ya Kikatiba?

Mnyika: Sahihi

Job Mrema: Namna pekee ambayo mtu ni mstaarabu na anajielewa asiporidhishwa njia bora ni kuiwasilisha jambo hilo Mahakamani?

Mnyika: Sikubaliani na wewe.

Job Mrema: Wakati Mshitakiwa anakuandaa alikwambia mambo gani?

Mnyika: Aliniambia kuhusu taratibu za Mahakama na kusikiliza maelekezo ya Majaji.

Job Mrema: UnamjuaIshengoma Mutembei Barongo ambae ni Katibu wa Chadema Mikocheni?

Mnyika: Simjui.

Job Mrema: Unajua kama Katibu Mkuu kuwa Ishengoma ni Katibu wa CHADEMA Mikocheni?

Mnyika: Hayo ni maoni yako mimi sifahamu? Na hii inafurahisha mawakili wa serikali ni watambuzi wa wanachama wa CHADEMA kuliko Katibu Mkuu wa Chadema.

Job Mrema: Makatibu wa Kata utaratibu wao wa kazi ni upi?

Mnyika: Ni wenyeviti wa Sekretarieti kwenye ngazi ya Kata na wanaripoti majukumu yao kwa viongozi wa Jimbo. Sio Mkoa wala Kanda.

Job Mrema: Ikitokea kuna ushahidi ukitolewa huoni kama kiti chako kitakuwa kwenye mashaka? Kwamba hata wanachama wako huujui.

Mnyika: Hilo sio miongoni mwa jambo linaloweza kukitia kwenye mashaka kiti cha Katibu Mkuu wa Chama. Chadema ina Makatibu wa Kata zaidi ya 1000.


Sehemu ya 329

Job Mrema: Ni sahihi ubaguzi ni kinyume na Katiba yetu ya Tanzania?

Mnyika: Ni sahihi.

Job Mrema: Yale makusanyo ya Tonetone kuna uamuzi ulifanyika kuwa kuna wachache wanufaike na wachache wasinufaike angali wengine wapo?

Mnyika: Sio Ubaguzi. Na ungetaka walipwe wote ukirudi ofisini mshauri Boss wako mwanasheria Mkuu wa Serikali alipe pesa zetu zaidi ya Milioni 400 ili tuwalipe wafanyakazi wetu wote. Hizo posho ni ndogo tu. Job

Mrema: Zaidi ya milioni 39 za Tonetone zimetolewa kati ya Tarehe 18 na 19 August 2026?

Mnyika: Hizo Habari nazisikia kutoka kwako.

Job Mrema: Ikitokea wanachama wa Chadema wamepata ushahidi wakasema kuna pesa zimetoka huoni kiti chako kitakuwa rehani?

Mnyika: Tutasubiri kuona kama kuna aliyeidhinisha pesa kutoka ni nani na kwa sababu gani?

Job Mrema: Kutoa pesa za Tonetone kwa mujibu wa ibara ya 4.1.2 ni kuwaonea?

Mnyika: Anaisoma hiyo ibara. Inasema kukandamiza watu kwa rangi, dini

Job Mrema: Ndio maana wengine hamkuwalipa?

Mnyika: Mimi Katibu Mkuu ndio ninayejua kwamba kwa hali tuliyonayo. Alipwe Mlinzi pekee. Kwasababu yeye yuko ofisini kila siku na sio mfanyakazi mwingine. Wewe unajua nini kuhusu haya mambo kuliko mimi?

Job Mrema: Ibara ya 3.2.4 inasema kama inavyosema hapo?

Mnyika: anaisoma na kusema inasema hivyo. Job Mrema: Sasa kama hizo fedha chache zimelipwa kwa ubaguzi unasemaje kuhusu hilo?

Mnyika: Sisi hatuna Ubaguzi wenye ubaguzi ni nyie Serikali ambao mmezuia fedha za Chadema. Ndio maana Chadema tunapambana fedha za umma zibaki salama.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kuwa ukiaminika kwa dogo utaaminika kwa kubwa?

Mnyika: Chadema inaaminika kwa dogo na kwa kubwa pia. Ndio maana watanzania wameendelea kuiunga mkono.


Sehemu ya 330

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu

John Mnyika.

Job Mrema: Huoni kwamba kwa uzoefu wa miaka 10 ya Kutunga Sheria huoni haujakitendea Haki Chadema kwa kutokishauri Chama cha Chadema kutumia Mahakama?

Mnyika: Nimekishauri vizuri kabisa chama. Tumekaa kwenye Maridhiano, tumeenda Bunge kupeleka maoni yetu kuhusu mabadiliko ya sheria hakuna lililofanyika. Mahakama kwenye kesi ya kubenea ilisema masuala ya kisiasa yatatuliwe kisiasa ndio maana tukaja na No Reforms: No Election.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kuwa Ishengoma ni Katibu wa Chadema?

Mnyika: Nitakubalianaje na jambo gani sasa ambalo silijui???

Job Mrema: Ni sahihi kuwa kwenye hiyo clip ya Bwana Mutembei alisema vurugu za Oktoba 29 zilipangwa na Chadema?

Mnyika: Nilikwambia hiyo Clip siijui, simjui Mutembei na hata hayo unayosema sio sahihi na sikubaliani na wewe kwa chochote kuhusu hilo.

Job Mrema: Mimi nimemaliza

Mheshimiwa Jaji. Anasimama

Ajuaye: Tumemaliza Jamhuri wote.

Jaji Ndunguru: Haya Utetezi vipi nafikiri re examination itakuwa fupi sana?

Tundu Lissu: Siwezi kuahidi kabisa ila nitasema yale ya muhimu tu ndio nitamuuliza.

Naomba nianze sasa.

Mhe. Lissu: Sasa umeulizwa sana kuhusu kifungu cha 7 kuhusu Sheria ya habari kisome na ujibu ulimaanisha nini?

Mnyika: Anakisoma na kusema hiyo sheria inawapa uhuru na haki ya kutafuta habari na baadae kuwa huru kuisambaza au kutoisambaza na kifungu hiki kinawafanya wanahabari kuwa wamiliki wa habari husika na sio mtu mwingine.

Mhe. Lissu: Umeulizwa kuhusu maneno yangu na uhusiano wa matukio ya October?

Mnyika: Maneno yalitolewa Tarehe 03/04 na mshitakiwa akakamatwa Tarehe 09/04 na matukio ya Oktoba yakaja kutokea Mshitakiwa akiwa yuko Mahabusu.

Anasimama Katuga: Mheshimiwa asiende mbali huko.

Jaji: Anayosema shahidi tulishayaandika kwahiyo hakuna shida.
Tundu Lissu: Uliulizwa kuhusu maana ya Uasi, sasa nakupa Kamusi ile ile usome.

Mnyika: Uasi ni kupinga mambo ndani ya taasisi au sheria kandamizi hiyo ndio maana ya kwanza.

Mhe. Lissu: Kwahiyo umeelewaje hapo?

Mnyika: Uasi sio tu kupinga serikali bali hata kwenye taasisi kupinga mifumo mibovu nao pia ni uasi.

Mhe. Lissu: Wamesema kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba haukuwa huru na haki?

Mnyika: Kuna ripoti mbalimbali zimesema ikiwemo Common wealth Anasimama

Katuga: Hizo ripoti naziogopa asiende huko hakuzitaja kabisa

Mhe. Lissu: Sasa ripoti zinawapa presha usiende huko.

Katuga: Sio Presha tu zinanipa hadi Kisukari.

Mnyika: Basi uchaguzi wa Oktoba haukuwa huru na haki na haukuwezesha watu kushiriki kwa uhuru na haki.

Mhe. Lissu: Kesi ya Mbowe ulisema ya uongo fafanua sasa licha ya kwamba alikutwa na kesi ya kujibu?

Mnyika: Hakukutwa na hatia ya ugaidi na kumekuwa na tabia ya kubambikwa kesi na kwa Mwenyekiti Mbowe kama Mtendaji mkuu wa Chama , najua hakuwahi kupanga Ugaidi na Chama hakijawahi kuwa na Mipango hiyo.

Mhe. Lissu: Pia uliulizwa kama ni kweli alishitakiwa na watu wengine walikuwa ni Makomandoo wa Jeshi na ukasema walikuwa ni walinzi wake na wanaharakati pia.

Mnyika: Waliwahi kutumikia jeshi na kuondoka Jeshini na wakajiunga na harakati na Mwenyekiti akawapanga kuwa walinzi wake.

Katuga: Anasimama hili la kwamba walikuwa makomandoo wasiliseme kabisa.

Mhe. Lissu: Nawish nisiseme kuwa hii ni non sense, sitasema hivyo lakini sioni umaana wa hili swali. Lazima ufafanuzi ufanyike na huwezi kumtisha mtu kuwa utafanya cross sasa cross gani utafanya hapa?

Katuga: this court is not your mother

Mhe. Lissu: It is not your mother either. Wewe nani kakudanganya hii Mahakama ni Mama ako?

Jaji Ndunguru. Sasa Shahidi aulizwe swali tumuache ajibu.


Sehemu ya 331

Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Re-Examination Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika

Mhe. Lissu: Mwenyekiti Mbowe alishitakiwa na watu wengine na ukasema walikuwa ni walinzi wake na wanaharakati? Fafanua.

Mnyika: Walikuwa Makomando zamani, wakawa walinzi wa Mbowe na kwa kuwa mlinzi wa Mwenyekiti walikuwa wanafanya kazi ya harakati na wakawa wanaharakati.

Katuga anachekacheka.

Jaji anamuuliza vipi?

Katuga: Majibu yalikuwa sahihi kabisa ya awali.

Mhe. Lissu: Mheshimiwa mimi siwezi kuwachukulia poa vichekocheko vya watu walionishitaki kwa Uhaini.

Jaji: Tuendelee

Mhe. Lissu: Kuvitishia vyombo vya ulinzi na Rais ukasema Mshitakiwa hakufanya hivyo fafanua?

Mnyika: Hakuna mahali kokote mshitakiwa alimtishia Rais wala Serikali hakuna alipotaja watu hao na vyombo hivyo.

Mhe, Lissu: Ulitaja kesi nyingi na kusema kesi zote zilikuwa za uongo?

Mnyika: zilifutwa kwasababu hakuna ushahidi uliowasilishwa Mahakamani na zilifutwa kwasababu za uongo na hakuna aliyekutwa na hatia.

Mhe. Lissu: Umeulizwa Maswali kuhusu Hotuba ya Jaji Chande kuhusiana na matukio ya Oktoba na Siku zilizofuata. Ulisema inatofautiana na Hotuba yangu?

Mnyika: Hotuba yako ilikuwa inahusu msimamo wa No Reforms: No Election na Chande alikuwa anazungumzia mambo tofauti kabisa.

Mh. Lissu anaendelea na Maswali Msawazo, Maswali Fukia Mashimo, Maswali Sawazisha. A.K.A Rejoinder kwa kitaalamu.

Mhe. Lissu: Shahidi uliulizwa kuhusiana na Hotuba Yangu na ueleze kama ulisema ni sahihi au sio sahihi kama lengo la Hotuba yangu lilikuwa ni kuishinikiza Serikali? Ukasema Hapana.

Mnyika: Lengo lilikuwa ni kuwaunganisha watanzania na wadau mpaka serikali ikubali kuwezesha uchaguzi huru na haki na wasipokubali msimamo wa No Reforms: No Election.

Mhe. Lissu: Ulisema mliendelea na harakati hadi Tarehe 09/06 ulimaanisha nini?

Mnyika: Tarehe 10/06 Mahakama ilitoa zuio la kufanya shughuli za kisiasa na kuzuia matumizi ya mali za Chama. Hadi Tar. 15/04/2026. Ambapo ni baada ya Uchaguzi kabisa. Ni siku 309 tulizuiwa kutumia chochote kile.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuwa uasi ni njia ya Kidemokrasia naomba fafanua maana yake?

Mnyika: Uasi ni kupinga au kukataa kwa nguvu kubwa na hizo njia za kidemokrasia kwa kutumia kufanya mikutano, kufanya vikao hizo zote ni haki za kisiasa. Haiwezi kuwa ni kosa zilizopo kwenyw sheria ya vyama vya siasa na Katiba ya nchi na mikataba ya kimataifa imeridhia.

Mhe. Lissu: Umemaliza kuelezea hapo?

Mnyika: Hapo tayari. Tuendeleee sasa.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuwa Chama chako kilikuwa kilishajiandaa kushiriki uchaguzi wa mwaka jana?

Mnyika: Katika Mkutano wa Tarehe 21/01 uliopitisha No Reforms No Election .......

Mhe. Lissu: Angalia usifike mbali watasimama hao.

Mnyika: Tulijiandaa kuruhusu watia kuelezea nia zao na pia kungomesha Chama.

Mhe.Lissu: Katuga alikwambia kuhamasisha uasi ni kosa? Ukamjibu kuwa Mwalimu Nyerere alisema tunahitaji vijana waasi wa mifumo kandamizi.

Mnyika: Maneno ya uasi yana tafsiri ya ziada ambayo ilitumika na mwalimu nyerere na halikuwa kosa la uhaini wala kosa lolote. Hakuwahi kushitakiwa hadi leo. Haliwezi kuwa neno sahihi kutumika na Nyerere halafu likawa baya kutumika na Tundu Lissu.

Mhe. Lissu: Uliulizwa pia kwamba huo Mkutano ulikuwa na Mwenyekiti au vipi? Fafanua.

Mnyika: Yes niliwaambia haukuwa na Mwenyekiti wa Mkutano na mikutano kama hiyo huwa haina minutes. Inakuwa na taarifa tu ya namna ulivyofanyika. Mimi ndio nilikuwa msimamizi mkuu wa huo mkutano.


Sehemu ya 332

Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Re-Examination Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu namna mtandao wa Jambo ulivyorushwa hayo matangazo na ukasema uamuzi wa kurusha Matangazo ulikuwa sio uamuzi wenu bali wa wale waandishi?

Katuga: Hatujaelewa swali?

Jaji Ndunguru: Hebu rudia aelewa swali.

Jaji Kareyamaha: Sisi tumeandika kuwa shahidi alisema suala la kuchapisha ni uamuzi wao wenyewe hakuna anayewalazimisha?

Mhe.,Lissu: Kumbe mnaandika vizuri kabisa proceedings. Basi hapo twende. Mimi nashitakiwa na uhaini sina haraka ya chochote.

Mhe. Lissu: Sasa uliulizwa kuhusu wakurugenzi kusimamia uchaguzi. Ukasema utaratibu umekuwa mbaya zaidi kwenye sheria mpya iliyowafanyia marekebisho. Hebu fafanua.

Katuga: Hilo hatukuuliza.

Mhe. Lissu: Tusomeee. Proceedings hapo Jaji. Zinasomwa na Lissu anasema sasa, ulisema hukutoa maoni yote ya mabadiliko ya Katiba kwenye ile kamati ya Katiba na Sheria. Hebu fafanua.

Mnyika: Maoni yote ya kutaka kurekebisha Katiba mathalani ya matokeo ya Urais kupingwa mahakamani, muundo wa tume huru yalikataliwa na mara zote kipaza sauti kilikuwa kinazimwa na hatukuruhusiwa kuyasema na walisema hayataingia kwenye rekodi.

Mhe. Lissu: Uliulizwa baada ya maoni yenu kukataliwa huko Bungeni ndio mkarudi kwenye mkakati wenu wa kuzuia Uchaguzi na ukasema hapana ulikuwa ni mkakati wa Chadema toka Tar. 03/12 fafanua.

Mnyika: Uamuzi wa No Reforns No Election ulifanyika toka mwezi december kwahiyo uhamasishaji wa wananchi dhdi ya uasi kwa mifumo kandamizi ulianza toka mwezi December, 2024. Haukutokana kabisa na maoni kukataliwa ulikuwa ni uamuzi endelevu hadi mabadiliko yatakapopatikana.

Mhe. Lissu: Ahsante. Ulisema hukupiga kura kwasababu hakukuwa na uchaguzi, ulikuwa na maana gani?

Mnyika: Hakukuwa na Uchaguzi huru, Haki na Halali. Chama kilifungiwa, hakikushiriki huo uchaguzi na mazingira hayakuwa ya haki. Sasa kuna uchaguzi gani hapo? Nisingeweza nikiwa kama Katibu Mkuu wa Chama kushiriki uchaguzi wa aina hiyo.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kama nina nina kinga yoyote ya kushitakiwa kama nikivunja sheria na ukasema sina hatia yoyote. Ulikuwa unaendelea hapo na ukaweka lakini sasa....

Katuga: Waheshimiwa hakukuwa na lakini aliishia hapo.

Mhe. Lissu: Sasa nisomewe record tafadhali. Mimi sijaja hapa kumsikiliza kila anachosema Wakili wa Serikali. Majaji wanatafuta. Wanasema hebu jibu Shahidi tuone.

Mnyika: Nilisema hana kinga kwasababu mara zote amekuwa akishitakiwa na hajawahi kukutwa na hatia yoyote.

Mhe. Lissu: Ulisema kuwa Katibu Mkuu ni mteuliwa wa Baraza Kuu la Chama na sio Mwenyekiti? Fafanua.

Mnyika: Ni sahihi Katibu Mkuu anapendekezwa na Mwenyekiti lakini anathibitishwa na Baraza Kuu. Hilo Baraza Kuu linaweza kumkataa au kumkubalia. Na utendaji wa Katibu Mkuu anawajibika kwa Kamati Kuu na Baraza Kuu na sio kwa Mwenyekiti. Mwenyekiti wanashauriana tu.

Mhe. Lissu: Ulisomewa Katiba ya Chadema ibara ya 4.1.1 na kuulizwa kuwa lengo la Chadema ni kushika Dola na ukasema ndio na sio lengo pekee na muhimu zaidi?

Mnyika: Nilikuwa na maana kuwa kushika dola sio lengo pekee. Yako malengo ya kijamii, kisiasa na yote hayo ni malengo ya Chadema ba huwezi kusema lengo fulani ni muhimu kuliko mengine. Ikiwemo kutetea mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeiridhia kilele kikiwa ni kuleta demokrasia, uhuru na maendeleo ya watu.

Mh. Lissu: Waheshimiwa Majaji sina maswali zaidi ya Re Examination.

Jaji Ndunguru: Sasa Shahidi tunakuruhusu ukaendleee na majukumu mengine.

Mnyika: Ahsanteni na Mungu awabariki sana. Tunaahirisha kwa muda wa lisaa na nusu.

Na upate muda wa kuandaaa mashahidi wako pia.

Tukutane saa nane nusu.



Hahidi wa tatu wa Lissu, Amani Golugwa anaanza kutoa Ushahidi wake baada ya John Mnyika kuhitimisha


Sehemu ya 333

Amani Golugwa anaanza


Mahakama imerejea mchana huu.

Na Ajuaye anasema wako tayari kumsikiliza Shahidi wa no. 3 wa Utetezi.

Anasimama Mhe. Lissu anasema na mimi niko tayari shahidi wangu anaitwa Amani Sam Golugwa.

Unaitwa Nani?

Amani Sam Golugwa.

Una mika mingapi: 49

Unaishi wapi: Goba

Kazi yako? Mimi ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara.

Dini yako?

Mkristo. Sasa fanya kuapa hapo.

Anaapa, Mimi Amani Golugwa naapa nitatoa ushahidi wa kweli na Mungu unisaidie.

Anashusha chini Biblia.

Mhe. Lissu: Sasa umesema wewe ni Naibu Bara umeishikilia toka lini?

Golugwa: Nimekuwa Naibu Katibu Mkuu toka January 22, 2025.

Mhe. Lissu: Kabla ya nafasi hiyo ulikuwa na nafasi gani kwenye Chama?

Golugwa: Nimekuwa Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini toka mwaka 2013 mwezi wa 02

Mhe. Lissu: Katibu wa Kanda ya Kaskazini una maana gani?

Golugwa: Namaanisha Mikoa minne. Tanga, Arusha, Kilimanjaro. Manyara. Na hiyo ndio Kanda ya Kaskazini.

Mhe. Lissu: Kabla ya hapo ulikuwa na nafasi gani?

Golugwa: Nimeshika nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha kutoka 2014 hadi 2019. Kutoka 2008 hadi 2014 nilikuwa Katibu wa Mkoa wa Chadema. Huko Arusha.

Mhe. Lissu: Kama kuna nafasi nyingine uliwahi kuishikilia nje ya hizo?

Golugwa: Mwaka 2020 niliteuliwa na Chama kuwa Kampeni Manager wa aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chadema

Mh. Tundu Lissu. Mhe. Lissu: Walikuwa wanakuita Mnikulu?

Golugwa: Sahihi.

Mhe. Lissu: Umeingia Chama hiki lini?

Golugwa: Toka 2007 hadi leo nimekuwa Mwanachama wa CHADEMA. Takribani miaka 19.

Mhe. Lissu: Mtu anapataje nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara?

Golugwa: Ili mtu awe Naibu Katibu Mkuu jina lake litapendekezwa na Mwenyekiti wa Chama kwa maana atatafuta mwanachama mwenye uwezo atapendekeza mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Chama na Katiba yetu imeelekeza atapeleka jina moja aliloliteua kwa wanachama wengi na wajumbe wa Baraza Kuu watafanya wajibu wa kuthibitisha kwa huyo aliyependekezwa.

Mhe. Lissu: Majukumu ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema ni 1. msaidizi wa Katibu Mkuu. Anamsaidia Katibu Mkuu.2. Mwandishi wa Kumbukumbu za Vikao vya Chama. 3. Amepewa nafasi kwamba ndie mkuu na msimamizi wa Itifaki katika vikao na mikutano ya Chama.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji wasifu wako wa kitaaluma?

Golugwa: Elimu ya Chuo nimesoma masuala ya Uhasibu. Nimesoma uhasibu chuo cha Uhasibu Arusha hadi ngazi ya stashada ya uzamili yaani Post Graduate Diploma in Accountancy.

Mhe. Lissu: Uzoefu wako katika eneo hilo la Uhasibu?

Golugwa: Nimefanya kazi ya Uhasibu nikianza ngazi ya Accounts Assistant na kufanya kazi ya Uhasibu hadi mwaka 2015. Toka mwaka 2001 kwenye maeneo tofauti tofauti.

Mhe. Lissu: Sasa tuzungumze hii kesi. Wanasema nilitoa maneno ya kuitishia serikali ya Jamhuri ya Muungano na kukinukisha? Golugwa: Huo Mkutano nina ufahamu.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji Mkutano uliandaliwa na nani na ulifanyikia wapi? Golugwa: Huu Mkutano uliandaliwa na Sekretarieti ya Chama baada ya Katibu Mkuu kuleta wazo kwenye sekretarieti kwamba watia nia ni wadau muhimu hivyo tuandae Mkutano wa kukutana na watia nini? Sekretarieti ilifanya maandalizi yote ya Mkutano. Mhe. Lissu: Sekretarieti ni akina nani?

Golugwa: Hii sekretarieti ninayozungumzia ni 1. Katibu Mkuu wa Chama, 2. Manaibu wawili wa Zanzibar na Bara,3. Makatibu wa Mabaraza ya Chama yaani Wanawake, Vijana na Wazeee. 4. Wakurugenzi wa Chama 5. Pamoja na Wataalamu wa Chama ambao wameteuliwa na Mwenyekiti kuwa Sekretarieti ya Chama.

Mhe. Lissu: Jumla ni watu wangapi?

Golugwa: Ni watu 14.

Mhe. Lissu: Sekretarieti ni Chombo cha aina gani kwa muundo wa Chadema?

Golugwa: Sekretarieti ya Chadema ndicho chombo cha kiutendaji kinachofanya kazi za kila siku za Chama kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama.

Sehemu ya 334

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Tanzania Bara Amani Golugwa.

Mhe. Lissu: Umesema watia nia hawa watia nia ni akina nani?

Golugwa: Hawa watia nia ni wanachama wa Chadema ambao aidha walipitishwa na kuwa wagombea kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 katika nafasi Udiwani, Ubunge na Urais na kwamba bado nia yao ya kutaka kugombea nafasi hizo bado walikuwa nayo. Na wengine ni wale ambao hawajawahi kupitishwa wala kugombea kwenye hizo nafasi nilizozitaja na hivyo mwaka 2025 walikuwa na nia wapate fursa waombe kwenye michakato ya ndani na wapitishwe kwenye nafasi hizo. Na hao ndio Watia nia.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji hao watia nia walitaka kugombea uchaguzi gani?

Golugwa: Ni Uchaguzi wa mwaka 2025.

Mhe. Lissu: Lengo la kuwaita hao watia nia lilikuwa ni lengo gani?

Golugwa: Lengo ni kuwaeleza na kuwafafanulia juu ya msimamo wa Chama. Uliopitishwa na Mkutano Mkuu ule wa No Reforms: No Election na huo msimamo ukawa umefafanuliwa na Kamati Kuu ya Chama kwa kauzimiwa. Hilo ndio lilikuwa Lengo.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji unaposema No Reforms: No Election huu msimamo ulikuwa unahusu nini hasa?

Golugwa: Waheshimiwa Majaji msimamo huu kimsingi ulianza au ulizaliwa baada ya uchaguzi wa serikali za Mitaa wa mwaka 2024. Nikiwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini alituambia Makatibu wa Kanda tuandike Ripoti ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulivyofanyika na mimi kama mtendaji ambae nilikuwa sehemu ya Uchaguzi huo kwa kusimamia kanda ya kaskazini. Nilitoa ripoti yenye madudu mengi ya hovyo yaliyojitokeza. Na Katibu Mkuu alitutaka tuandike maoni yenu kuhusiana na nini Chama kifanye. Kuhusu hayo mambo ya hovyo tuliyoyaona kwenye uchaguzi.

Mimi kwenye ripoti niliandika: yalikuwa hivi. Kwa ushenzi huu niliouona Chama kisishiriki uchaguzi mwingine wowote bila kushinikiza mabadiliko kwenye mifumo ya Uchaguzi.

Jaji Ndunguru: Hebu rudia, Kwa USHENZI HUUU

Golugwa: Kwa Ushenzi huu Chama kisishiriki Uchaguzi mwingine wowote mpaka kushinikiza mabadiliko ya sheria za Uchaguzi na Makatibu wengine wa Kanda zingine kila mmoja kwa lugha yake wote tulitoa taarifa au ripoti zinazofanana. Na ndipo Kamati Kuu ikaketi Ikayachakata mapendekezo ya Makatibu wa Kanda na wajumbe wenyewe wa Kamati Kuu wakajadili na kutafakari kwa uhalisia wanaojua.

Basi kama sikosei Tar. 10/12/2024 Mwenyekiti wa Chama wa Kipindi hicho Mh. Freeman Mbowe akatoa tamko rasmi la Chama kuhusu msimamo ulioazimia kwamba hatutakuwa tayari kwenda kwenye Uchaguzi mwingine wowote bila mabadiliko ya Mifumo ya Uchaguzi. Halafu akasema kwa Kingereza NO REFORMS: NO ELECTION.

Mhe. Lissu: Anazunguka zunguka pale kizimbani anasikiliza nondo kutoka kwa Amani Golugwa. Kwa ushenzi niliouona. Hebu waeleze majaji ni Ushenzi gani uliouona?

Golugwa: Ushenzi ni mwingi sana. Kwenye uteuzi wagombea wa Chadema na vyama vingine vya upinzani kulikuwa na matatizo kuanzia kwenye kuchukua fomu ya tume. Watumishi wa Tume wanawakwepa wagombea wetu kwa makusudi hawawapi fomu, wanaondoka ofisini. Kwa makusudi walikuwa wanakataaa kuzipokea fomu.

Pindi tulipozirudisha fomu watumishi wa tume walikuwa wanashirikiana na wagombea wa ccm kutengeneza sababu kuengua wagombea wetu. Mfano umeandika 1971 wataongeza 9 utaambiwa umezaliwa 1979 uteunguliwa. Walikuwa wanaweka pingamizi la hujui kusoma na kuandika. Utaenguliwa. Utawekewa pingamizi na uraia utaenguliwa.


Sehemu ya 335

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Tanzania Bara Amani Golugwa

.Mhe. Lissu: Sasa eleza suala la kampeni za Uchaguzi huo zilikuwaje?

Golugwa: Kampeni za Uchaguzi huo zililenga kuegemea kukipendelea Chama kimoja. Chama cha Mapinduzi.

Mhe. Lissu: Uzungumzie matatizo ya wakati wa kampeni serikali za mitaa?

Golugwa: Kwa wagombea wachache waliopenya. Kampeni ziligubikwa na vurugu na ratiba kwa sehemu kubwa ilitengenezwa kimkakati kuvionea vyama vya upinzani. Na mara nyingi. Mikutano ya Chadema na vyama vingine vya upinzani iliionekana kufanyiwa hujuma kwa kupelekwa maeneo ya mbali na watu.

Mhe. Lissu: Utaratibu wa mawakala wa wagombea ulikuwaje?

Golugwa: Mawakala ambao wanamuwakilisha mgombea na Chama ulihitaji Wakala kwenda kuapishwa kwenye ofisi ya Kata akiwa na Barua ya Chama na baada ya uapisho ule utaratibu uliowekwa ni kwamba siku ya Uchaguzi msimamizi ndie atakaeenda na hati ya kiapo kwenye kituo cha kufanyia Uchaguzi kwahiyo Utambulisho Wakala utapelekwa kwenye kituo atakuta kiapo chake ambacho ndio utambulisho wake.

Mhe. Lissu: Na kilitokea nini?

Golugwa: Mawakala wa Chadema hawakukuta hivyo viapo ambavyo ndio Utambulisho wao. Kwahiyo msimamizi msaidizi kwenye kile kituo akawa watoa mawakala wetu hadi utambulisho wenu utakapopatikana na shughuli za Uchaguzi zilikuwa zikiendelea. Lakini watu wa CCM wao mawakala wake walikuwepo kila kituo na viapo vyao. Mawakala wetu wakazuiwa kuingia kwenye vituo vya kupiga kura wakawa nje. Nendeni mkafuatilie huko.

Huo muda ambapo mawakala wetu hawapo ndani ndio ushenzi wa kuingiza kura ukafanyika. Niligombana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha saa sita Mchana Mkurugenzi anasema kulikuwa na shida kidogo lakini tumeshasort mambo yote yako sawa.

Mhe. Lissu: Sasa sema matokeo ya huo Uchaguzi kwa kanda ya Kaskazini na Nchi nzima kama unajua. Baada ya Ushenzi wote huu?

Golugwa: Waheshimiwa Majaji kwa nchi nzima CCM walishinda kwa asilimia 99.2 ya Vijiji na Vitongoji na Mitaa yote nchi nzima. Chadema na vyama vya upinzani waliambulia asilimia 0.8 na kwa kanda ya kaskazini walishinda kwa asilimia 98.7.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji tofauti ya Uchaguzi huo na ule wa 2019 kati ya ule wa Magufuli?

Golugwa: Kwa mambo mengi ya hovyo niliyoyaona na yaliyotokea. Katika mzunguko mzima hapakuwa na tofauti yoyote ya mambo yaliyotokea. 2019 suala la kurudisha fomu lilikuwa ni vita.

Part 336 itaendelea kwenye post inayofuata,

PART 336: MHE. LISU AENDELEA KUMHOJI SHAHIDI WAKE KUHUSU UCHAGUZI​

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza shahidi wake, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Tanzania Bara, Amani Golugwa.

Mhe. Lissu: Kanuni za kuendesha huo uchaguzi zilitungwa na nani?

Golugwa: Kanuni za kuendesha huo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilitungwa na Waziri mwenye dhamana ya TAMISEMI.

Mhe. Lissu: Anaitwa nani?

Golugwa: Anaitwa Mchengerwa.

Mhe. Lissu: Mohamed si ndiyo?

Katuga: Hiyo Mohamed haikuwepo kabisa. Anaweka mshitakiwa.

Mhe. Lissu: Mawaziri huwa wanakuwa gazetted, hata sitaki tusumbuane. Na Mchengerwa ni mmoja tu. Kwa hiyo mtajua kipindi hicho walikuwa akina nani?

Golugwa: Anaitwa Mohamed Mchengerwa, Waheshimiwa Majaji.

Mhe. Lissu: Wasimamizi kwenye ngazi ya wilaya ni akina nani, na kule vijijini?

Golugwa: Walikuwa ni wakurugenzi kwa ngazi ya wilaya, na huko vijijini walikuwa ni watendaji wa serikali za mitaa.

Mhe. Lissu: Hawa wakurugenzi unaosema huwa ni wateule wa nani?

Golugwa: Wanateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Lissu: Na huyo Waziri aliyetunga kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa naye ni mteule wa nani?

Golugwa: Naye ni mteule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Lissu: Na Wizara ya TAMISEMI iko chini ya nani?

Golugwa: Iko chini ya Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Lissu: Ulipeleka taarifa kwa Katibu Mkuu, na makatibu wengine tisa walipeleka ripoti ya namna hiyo hiyo kwa ujumbe wa aina hiyo hiyo. Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, huo uzembe ulikuwepo na kwenye Uchaguzi Mkuu pia.

Golugwa: Mambo ya hovyo niliyoyaona kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mambo hayo hayo niliyaona kwenye Uchaguzi Mkuu.

Mhe. Lissu: Umeyaona kwenye uchaguzi mkuu mmoja au zote zilizopita?

Golugwa: Kwa kipindi ambacho nimekuwa kiongozi wa Chama, nimeyaona mambo hayo kwenye uchaguzi wa mwaka 2020, niliyaona mwaka 2015, na niliyaona mpaka nikaogopa, nikashangaa na kustaajabu kwenye matukio ya mwaka 2025 kwenye unaoitwa Uchaguzi.

Mhe. Lissu: Masuala ya fomu unayaonaje kwenye chaguzi nyingine?

Golugwa: Nimeona na kushuhudia katika Uchaguzi Mkuu watu wanakwenda kuchukua fomu, mhusika anakataa kutoa fomu au anafunga mlango, anaondoka na kuiacha ofisi. Nimeshuhudia wagombea kunyimwa fomu.

Mhe. Lissu: Uwepo wa tatizo la wagombea kurudisha fomu ukoje kwa wale waliopewa?

Golugwa: Nimeona na kushuhudia wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge wanafika kwenye ofisi, na unamuona kwa macho hivi anaondoka.

PART 337: GOLUGWA ATOA MAELEZO KUHUSU WAGOMBEA KUENGULIWA NA RIPOTI ZA KIMATAIFA​

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza shahidi wake, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Tanzania Bara, Amani Golugwa.

Mhe. Lissu: Umeshuhudia tatizo la wagombea kuenguliwa baada ya kurudisha fomu?

Golugwa: Nafahamu lipo tatizo la wagombea kuenguliwa.

Mhe. Lissu: Haya matatizo yamekuwa yakiwakabili wagombea wa vyama vyote au CHADEMA pekee?

Golugwa: Yamekuwa yakiwapata wagombea wa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani, isipokuwa CCM.

Mhe. Lissu: Je, umewahi kumuona mgombea wa CCM aliyeenguliwa?

Golugwa: Hawajawahi kabisa kuenguliwa.

Mhe. Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu ripoti za kimataifa ulizosoma.

Golugwa: Ripoti za SADC, Umoja wa Afrika, EU na Taasisi ya Thabo Mbeki. Hizi zote zilikuwa za mwaka 2025.

Mhe. Lissu: Anza na ripoti ya Umoja wa Afrika kwanza.

Mhe. Lissu amesema ripoti hiyo ilieleza kuwa Uchaguzi wa Tanzania haukuwa na viwango na haukukidhi matakwa na miongozo ya chaguzi za kidemokrasia duniani.

Aidha, amesema waangalizi walishuhudia wapiga kura wakipewa kura na wasimamizi wa uchaguzi na kuziingiza kwenye masanduku ya kura.

Hata hivyo, wakati Mhe. Lissu akiendelea na maelezo hayo, Ajuaye alisimama na kusema muda umeisha, hivyo wataendelea na ushahidi huo kesho.

Jaji Ndunguru: Anaahirisha shauri hadi kesho saa tatu asubuhi.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1.

MAHAKAMA INAANZA HAPA

1. Lissu anaingia ukumbini, unasimama na kumpigia makofi.

2. Majaji nao wanaingia haraka, Lissu hapati muda wa kusalimiana na watu.

3. Shahidi (Mnyika) yupo Mahakamani tayari.

4. Mawakili wa Serikali wapo Mahakamani pia.

5. Mahudhurio siyo makubwa. Naambiwa huko nje foleni ni kubwa, magari hayatembei kabisa. Watu watafika kwa kuchelewa sana.

SAA 9:46 ASUBUHI

Karani wa Mahakama anajiandaa kusoma kesi Criminal Session, kesi namba 605 ya mwaka 2005.

Wakili wa Serikali Ajuaye Zegeli anawatambulisha mawakili wenzake.

“Iwapendendeze:

1. Nassoro Katuga, Wakili wa Serikali Mkuu.
2. Tawabu Issa, Wakili wa Serikali Mwandamizi.
3. Job Mrema, Wakili wa Serikali Mkuu.
4. Cuthbert Mbilinyi, Wakili wa Serikali.
5. Kasara, Wakili wa Serikali.

Wote tunawakilisha Jamhuri.”

Mshtakiwa Tundu Antipas Lissu yupo kizimbani.

Shauri linakuja kwa ajili ya utetezi. Tupo tayari kuendelea.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, upo tayari?

Lissu: Nipo tayari, Waheshimiwa Majaji.

Jaji Ndunguru: Shahidi.

Mnyika anapanda kizimbani.

Jaji Ndunguru: Shahidi, unakumbushwa kiapo chako.

Tuendelee.

Ajuaye: Anaendelea kumaliza wakili Job Mrema, ambaye alimalizia tulipoishia jana.

Job Mrema: Shahidi, habari za asubuhi?

Mnyika: Salama.

Job Mrema: Upo sawa?

Mnyika: Nipo sawa.

Job Mrema: Waheshimiwa Majaji, naomba niendelee kumuhoji shahidi. Ikiwapendeza, naomba nikumbushwe.

Jaji Ndunguru: Jaja, uliishia pale kwenye fujo, ukampa kamusi asome, na swali lilikuwa bado halijaulizwa.

Job Mrema: Shahidi, jana nilikupa kamusi usome maana ya neno “fujo”.

Mnyika: Sahihi, kwa mujibu wa kamusi ile.

Job Mrema: Swali langu ni kwamba utakubaliana na mimi kwamba...

Waheshimiwa Majaji, naomba nimsomee shtaka.

Utakubaliana na mimi?

“Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, msimamo huu unaashiria uasi. Ni kweli, ni kweli, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi.

Hivyo ndiyo tutapata mabadiliko; huu uchaguzi tutauvuruga kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana.”

Maneno haya yana maana kwamba matukio ya tarehe 29 Oktoba yalikuwa yana uhusiano na maneno haya.

Mnyika: Hayana uhusiano kabisa. Mtuhumiwa alizungumza tarehe 03 Aprili 2025.

Hayana uhusiano kabisa.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba demokrasia inatoa fursa ya kusikilizwa watu wachache?

Mnyika: Ni sahihi kwamba wengi wape, ila wachache wasikilizwe.

Job Mrema: Ni sahihi kwamba wewe ni Katibu wa Mwenyekiti ambaye ni mshtakiwa?

Mnyika: Siyo sahihi.

Job Mrema: Ni sahihi wewe ndiyo umemshauri Mwenyekiti awe anatoa hotuba zake bila kukuhusisha wewe?

Mnyika: Hapakuwa na haja ya kushauriana, jambo la maamuzi ya kikao ni utekelezaji tu.

Job Mrema: Ni sahihi kwamba kama unadai haki zako, siyo sawa kuathiri haki za watu wengine?

Job Mrema: Ni sahihi kwamba hukufungua shauri la kudai haki zako kikatiba kwa jina lako?

Mnyika: Ni sahihi kwamba sijawahi kufungua.

Job Mrema: Ni hivyo hivyo pia kwa Mwenyekiti wako, Tundu Antipas Lissu. Amewahi kufungua kesi ya kikatiba Mahakamani kwa mujibu wa taarifa zako na ufahamu wako?

Mnyika: Ni sahihi, hajawahi kwa sababu alikuwa gerezani.

Job Mrema: Ni sahihi kwamba nchi inaongozwa na Katiba?

Mnyika: Ni sahihi.

Job Mrema: Ni sahihi wewe kama Katibu unaamini na mihimili ya Mahakama?

Mnyika: Ni sahihi, pamoja kwamba sikubaliani na maamuzi ya baadhi ya majaji.

Job Mrema: Wewe jibu swali langu tu, mengine sijakuuliza.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba, kwa ushahidi wako hapa Mahakamani, uliposema kuhusu sheria kandamizi, ili sheria iwe kandamizi lazima Mahakama iseme sheria hiyo ni kandamizi?

Mnyika: Sikubaliani na wewe, kwa sababu kuna mashauri ya Mahakama yanasema kwamba baadhi ya sheria zishughulikiwe kisiasa, ikiwemo kesi ya Kubenea na kesi ya Mtikila.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba hujataja vifungu mahususi na sheria gani kandamizi unayotaja na kurejea?

Mnyika: Nikipewa muda wa kujikumbusha, naweza kukutajia kesi hizo kwa undani.

Job Mrema: Utajikumbusha ukirudi nyumbani kwako?

Mnyika: Nakumbuka kesi ya Kubenea hapa, kesi namba 28 ya 2024.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Back
Top Bottom