mzalendo namba moja
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 807
- 1,634
Angalieni watu wako active, otherwise mnamnyonya damu huyu mwenye kutoa updates..Tayari taarifa hii ilikuwa imeshaanzishwa na membel
Angalieni watu wako active, otherwise mnamnyonya damu huyu mwenye kutoa updates..Tayari taarifa hii ilikuwa imeshaanzishwa na membel
Ndio ninalowaambia JamiiForums , mtu anaanzisha uzi wa updates saa 2 asubuhi wakati Mahakama inaanza saa 3 je ikighairi ? Mimi naanzisha uzi tayari Mahakama imeshaanza. PaygeJamaa mshamba sana.
Kakimbilia kwenda kuanzusha uzi hayupo mahakamani, wala hatoi updates za kinachoendelea mahakamani.
Huu ni upumbavu sana.
Jamii forum ni GT.
Usirudie huo upumbavu aisee.
Haya maswali mbona yapo kichadema zaidi badali ya case ya Lissu. Mambo ya ubaguzi wa malipo chadema na uhaini Kuna connection ganiWAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN MNYIKA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 4.
Job Mrema: Shahidi, kama nilikusikiliza vizuri, ulieleza Mahakama una miaka 10 ya uzoefu katika kutunga sheria.
Mnyika: Ndiyo, nina ufahamu kidogo. Nilikuwa Mbunge.
Job Mrema: Huoni kama hujaitendea haki CHADEMA kwa kutokishauri vizuri, kwa kutokutumia Mahakama katika kudai haki zenu?
Mnyika: Nimekishauri vizuri, kama Mahakama inavyosema kwamba siyo mashauri yote yanatatuliwa na Mahakama; mengine ni ya kisiasa.
Nimetumia njia zote za kushiriki na kutoa maoni, Kamati ya Maridhiano na Kamati ya Bunge. Hatukusikilizwa na tulitumia njia zote.
Job Mrema: Nimekuuliza njia za kisheria, siyo kisiasa.
Mnyika: Siasa na sheria huwezi kuzitenganisha kwa sababu ni mapacha.
Job Mrema: Kwa kumalizia, maswali machache. Kwa kuwa umeieleza Mahakama hii kwamba wewe binafsi kama Katibu Mkuu humfahamu Ishengoma Mtembei Balongo, sasa utakubaliana na mimi huyo Bwana Mtembei ni Katibu wa Kata ya Mikocheni?
Mnyika: Waheshimiwa Majaji, siwezi kukubaliana na mambo yanayosemwa na Wakili tu hapa Mahakamani. Kwa hiyo, sikubaliani naye.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwa mujibu wa video clip iliyosambaa katika mitandao ya kijamii, kwamba mipango ya vurugu na kuzuia uchaguzi imetokana na mipango ya ndani ya chama chenu?
Mnyika: Waheshimiwa Majaji, siwezi kukubaliana na Wakili. Nitashangaa kama unataka nukuu ya taasisi kwa jambo ambalo silijui la mtaani.
Job Mrema: Kwa mujibu wa hiyo clip, Bwana Mtembei anaeleza kuvuruga uchaguzi ilikuwa ni mipango ya muda mrefu ya chama chenu.
Mnyika: Hiyo clip unaijua wewe, mimi siijui.
Job Mrema: Waheshimiwa Majaji, nimemaliza maswali.
Jaji Ndunguru: Tuendelee.
Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, tumemaliza maswali ya dodoso kwa shahidi huyu.
Jaji Ndunguru: Re-examination...
Lissu: (Anasimama) Asante, Waheshimiwa Majaji.
Jaji Ndunguru: Naamini itakuwa fupi.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, siwezi kuahidi itakuwa fupi kutokana na urefu wa cross-examination. Ninachoweza kuahidi, nitauliza yale ya muhimu tu.
Lissu: Shahidi, nitakuuliza maswali ya ufafanuzi. Jibu kwa sauti na kwa ufasaha, usitoe hotuba.
Nianze na maswali ya leo ya Wakili Job Mrema.
Uliulizwa swali kuhusu Sheria ya Habari, kifungu cha 7(1), kama ni jukumu la vyombo vya habari kutafuta habari.
Hebu angalia tena. Baada ya kuulizwa ni haki ya vyombo vya habari, ukasema ni haki na uhuru. Naomba ufafanue hapo.
Mnyika: Naomba nisome nakala ya sheria.
Lissu: Hii hapa, kifungu cha 7(1), soma.
Mnyika: Waheshimiwa Majaji, 7(1): “Every media house and journalist shall enjoy the following rights:
(a) Freedom to collect
(b) To edit
(c) To publish or broadcast news.”
Lissu: Fafanua jibu lako sasa.
Mnyika: Kwamba vyombo vya habari vina uhuru wa kuchukua habari, kuchakata au kufanya vyovyote vile, na kuchapisha habari hiyo.
Na uhuru na haki hiyo inavifanya vyombo vya habari ndiyo wamiliki wa habari waliyoikusanya au kuichukua.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE
Jamaa anatafuta credit kwa wepesi sana au lugha nyepesi wananamsaidia kuoata credit kourahisi kwa kuwa na uzi uliosomwa na kufwatiliwa na wengi pasipo kutumia nguvu siyo sahihi hii.Ndio ninalowaambia JamiiForums , mtu anaanzisha uzi wa updates saa 2 asubuhi wakati Mahakama inaanza saa 3 je ikighairi ? Mimi naanzisha uzi tayari Mahakama imeshaanza. Payge
Amemnyima mwenzake nafasi, kazi yake ni kuwahi na kukaa kimya... Hili JamiiForums walione na kurekebisha, amemeza anayeleta updatesJamaa mshamba sana.
Kakimbilia kwenda kuanzusha uzi hayupo mahakamani, wala hatoi updates za kinachoendelea mahakamani.
Huu ni upumbavu sana.
Jamii forum ni GT.
Usirudie huo upumbavu aisee.
Sasa mambo ya tonetone yanahusika vipi na kesi ya msingi hawa mawakili w serikali wanakula hela za bureWAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN MNYIKA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 3.
Job Mrema: Shahidi, nina swali moja hapa. Ni sahihi kuwa ubaguzi ni kinyume na Katiba yetu ya Tanzania? Inakataa ubaguzi.
Mnyika: Ni sahihi.
Job Mrema: Kama nilisikia vizuri katika ushahidi wako wa jana, katika yale makusanyo ya tonetone, wachache wanufaike na wachache wasipate. Huoni kwamba wachache kupewa michango ya tonetone na wengine kukosa ni ubaguzi huo?
Mnyika: Siyo ubaguzi. Ndiyo, fedha zilizopo haziruhusu kulipa wote. Ukitaka tulipe wote, mshauri Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipe fedha zetu mnazoshikilia, zaidi ya milioni 400, atulipe na wote watapata.
Job Mrema: Ni zaidi kwamba kati ya tarehe 18 na 19 Agosti kuna zaidi ya shilingi milioni 39 zilitolewa kwenye akaunti.
Mnyika: Sifahamu.
Job Mrema: Wewe kama Katibu Mkuu wa CHADEMA, ikitokea wanachama wa CHADEMA wakajitokeza kuonyesha hiyo milioni 39 ilitoka, huoni huo Ukatibu wako Mkuu utakuwa umeuweka rehani?
Mnyika: Mimi ndiyo ninayesaini fedha kutoka. Nasubiri mtu mwingine aje aseme zimetokaje.
Job Mrema: Kwa mujibu wa Ibara ya 4(1)(2) ya Katiba ya CHADEMA, huoni hiyo kulipa wachache tonetone ikakiuka ibara hii?
Mnyika: Naomba nisome. (Anasoma.) “Kukuza, kulinda na kutetea haki za binadamu katika ulimwengu...... kupinga ukandamizaji dhidi ya rangi, ukanda na jinsia.”
Kulipa watu wachache tonetone hakujakiuka ukandamizaji.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi, ni sahihi Ibara ya CHADEMA inasema haya: 3(2)(4), CHADEMA inaamini katika kusimamia rasilimali chache za nchi ili kuboresha?
Mnyika: (Anasoma.) Ni sahihi.
Job Mrema: Kama kwenu hakuko salama katika masuala ya fedha, zimelipwa kwa wachache, wewe kama Katibu Mkuu unapata wapi ujasiri wa kutetea hili la pato la Taifa?
Mnyika: Sisi hatuna ubaguzi, tumelipa kwa kile kilichopo.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi, ukishindwa kuaminika kwa dogo, huwezi kuaminika kwa makubwa?
Mnyika: Nakubaliana na wewe, lakini sisi tunaaminika kwa madogo na makubwa.
Job Mrema: Hayo mengine sijakuuliza.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Kigezo chao nani amewahi, hata kama hana kitu anafanyaJamaa anatafuta credit kwa wepesi sana au lugha nyepesi wananamsaidia kuoata credit kourahisi kwa kuwa na uzi uliosomwa na kufwatiliwa na wengi pasipo kutumia nguvu siyo sahihi hii.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. walipaswa kuzingatia swala muda na usahihi wa muda kudhibitidha kilicho live na kisicho live kulingana muda mana kutangulia siyo kufika.
Inategemea na mazingira uzi mtu anaanzisha saa 2 asubuhi, mimi nakuja kuanzisha saa 3 ambapo Mahakama imeanza nani ambaye yupo live ?Kigezo chao nani amewahi, hata kama hana kitu anafanya
Naona wameona kwenye kesi ya uhaini wamemkosa wanamtafuta kwenye ukakatatishaji wa helaSasa aya mambo ya tone tone na uhaini wa lissu vinausika vipi
Ni wazi ilitengenezwa ije itumike kwa matumizi hayaSa hizi watu wameanza kuflow na propaganda za mitandaoni, eti story za Ishengoma ndio zinatumika kama sehemu ya dodoso😁😁😁🙌🏽🙌🏽, sema anayewaagiza Hawa jamaa, sijui tu.....
Ni kama pumzi imewakata hivi, majaji nao kimyaaa
Utakuwa umetukatili manyanza,piga kazi!Inategemea na mazingira uzi mtu anaanzisha saa 2 asubuhi, mimi nakuja kuanzisha saa 3 ambapo Mahakama imeanza nani ambaye yupo live ?
JamiiForums hili liangalieni na kesho kama mtu anaanzisha uzi saa 2 wakati hata Mahakama haijaanza, na mimi nikaja kuanzisha saa 3 pale Mahakama itakapoonza. Sitoleta tena nyuzi za updates Mahakamani.
Endapo mtakuwa mnaunganisha nyuzi zangu za Mahakamani na mtu ambaye haposti updates.
Huu sio uzi wa Mpira hakuna ushabiki hapa watu wanapata darasa