binti kiziwi
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 16,966
- 47,296
Asante.Ingekuwa sio sahihi wasingemwacha siku zote hizo
Yah najua ni sahihi naulizia ni kawaida? au ni strange/rare.
Asante.Ingekuwa sio sahihi wasingemwacha siku zote hizo
Kwa kipi?Timu Lisu mtapona kweli naona Mnyika anapelekwa mputamaseko
Naona Serikali inapigwa knockout hapaTUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 7.
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka, kuna lolote hapo?
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, hili jibu ni tofauti na la kwanza. Hapakuwa na haja ya ufafanuzi.
Jaji Ndunguru: Ndiyo maana nasema tujikite kwenye yale yaliyozungumzwa tu, na tukifanya hivyo hakuna matatizo.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, nitashangaa Wakili wa Serikali kaka ataniunga mkono kwa lolote. Huyu anataka ninyongwe, hawezi kunitakia jema.
Lissu: Shahidi, uliulizwa kama kutishia vyombo vya dola ni kumtishia Rais au walinzi wa amani.
Mnyika: Ili tishio limlenge Rais au mlinzi wa amani, lazima limlenge Rais au mlinzi wa amani. Matishio mengine ya uhalifu hayamlengi Rais wala mlinzi wa amani.
Lissu: Asante.
Uliulizwa kama unajua kesi inaamriwa kwa ushahidi. Ukasema kesi zote zilifutwa kwa sababu ni za uongo na kubambikiza. Hebu fafanua jibu lako.
Mnyika: Kesi zilifutwa kwa sababu hazikuwa na ushahidi wa maana, kwa hiyo zilikuwa za uongo.
Lissu: Ukaulizwa kama umesikia hotuba ya Jaji Chande, ukasema umemsikia.
Ukaulizwa kama umesikia Jaji Chande kwamba baadhi ya matukio yaliratibiwa na wanasiasa.
Ukaulizwa kama inahusiana na hotuba yangu ya tarehe 03 Aprili 2025. Hebu fafanua.
Mnyika: Hakuna uhusiano wowote na hotuba ya Jaji Chande. Wewe ulitoa hotuba tarehe 03 Aprili 2025...
Nassoro Katuga: Hapakuwa na swali la namna hiyo. Lengo la swali halikuwa linahusu hotuba nzima; ni kipande cha maneno kuhusu hotuba ya Mwenyekiti kuzuia uchaguzi na hotuba ya Jaji Chande vinafanana au havifanani.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, mimi natumia notisi zilizoandikwa mwenyewe. Naomba nisomewe na Mahakama hayo maswali yanayohusiana na Jaji Chande.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Mkuu kiufupi tu kesi ya uhaini kwa TAL hapa haipo!! Hapa mawakili wa serikali wanatafuta mlango mwingine wa kutokea ili waingize kesi nyingine mpya ionekane CDM ni tatizo ndo zile kesi unaachiliwa huru alafu unafika getini unaambiwa una kesi nyingine ya kujibuNatamani kufahamu uhusiano uliopo kati ya malipo ya posho ya tone tone kwa baadhi ya viongozi wa Chadema kutokana na hali ngumu ya kiuchumi wanayopitia, na uhaini wa Lissu!!! Kwangu mimi naona hakuna uhausiano wowote ule.
sasa hyu mrema anatafu nini maswali haya? kuwa Mnyika haminiki? anataka ku achieve/establish nini? takatakaMahakamani leo tena kesi inaendelea kwa Upande wa Mawakili wa Serikali kumuuliza Mswali ya Dodoso Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika
Pia soma: Kesi ya Uhaini: John Mnyika Kuendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri kuendelea leo 1, Septemba 2026
Leo September 2, 2026 Last time tuliishia sehemu 327 so leo tunaendelea na
Sehemu ya 328
Mahakama imeanza. Majaji wameingia.
Mh. Tundu Lissu ameingia na kupokolewa na Makofi mengi ya wahudhuriaji wa hapa Mahakamani.
Shahidi (DW 2) wa utetezi nae alifika mapema sana saa mbili kamili asubuhi.
Mh. John Mnyika. Mheshimiwa Tundu Lissu ameingia akiwa amepiga Kombati safi kabisa ya Kaki na vibe lake liko juu sana. Nywele zake naona zinaendelea kuwa ndefu siku hadi siku.
Karani anasoma namba ya kesi akiwa amekaa upande wa kulia kidogo na kushoto kwa majaji kwa mbele.
Anasimama Ajuaye anatambulisha Kikundi Cha Serikali cha siku zote. Anasema wako tayari kuendelea na Cross Examination.
Anasimama Job Mrema kwenda kuendelea na Maswali ya Dodoso.
Job Mrema: Anakumbushwa alipoishiwa. Anaendelea sasa. Utakubaliana na mimi kama inavyosomeka kwenye hati ya mashitaka kuhusu msimamo unaashiria uasi. Sasa matukio yaliyotokea Tar. 29/10/2025
Mnyika: Hayana uhusiano kabisa na Mshitakiwa yeye alikamatwa Tarehe 09/04 na mambo ya Uchaguzi yalitokea mshitakiwa akiwa jela siku nyingi. Uhusiano unatoka wapi?
Job Mrema: Chadema inaamini katika Demokrasia?
Mnyika: Sahihi.
Job Mrema: Inawezekana Mwenyekiti akatoa hotuba bila kukuhusisha wewe?
Mnyika: Hakuna yakunishirikisha mimi kwasababu No reforms, No Election ilishaamuliwa na vikao na wote tulikuwa tunajua nini maana ya No Reforms, No Election.
Jobe Mrema: Wewe Mnyika umewahi kufungua shauri la Kikatiba?
Mnyika: Sijawahi
Job Mrema: Je Mwenyekiti nae aliwahi kufungua kesi hiyo?
Mnyika: Hajawahi
Job Mrema: Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaweka misingi ya kisheria?
Mnyika: Ni sahihi pamoja na Mikataba ya Kimataifa.
Job Mrema: Unaamini mhimili wa Mahakama katika utoaji wa Haki?
Mnyika: Mhimili nauamini lakini nina shida na Majaji wanaotoa haki baadhi yao hawaaminiki kabisa.
Job Mrema: Kutokana na ushahidi wako kuhusiana na sheria kandamizi sasa ili sheria iweze kusemwa kuwa ni kandamizi ni lazima sheria hiyo isemwe na Mahakama?
Mnyika: Sio sahihi hata Mahakama imesema katika Kesi Na. 28/2018 ya Said Kubenea ilisema kuhusu masuala ya kisiasa yanapaswa kutatuliwa kisiasa sio lazima Mahakama iseme kuhusu jambo hilo.
Jaji Ndunguru: Hivi uliyeuliza swali maana yake ni nini? Unamaanisha nini?
Job Mrema: Nimemuuliza umewahi kufungua shauri la Kikatiba?
Mnyika: Sijawahi
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba kwa mujibu wa Sheria. Mahakama imetoa sheria ya kusikiliza mashauri ya Kikatiba?
Mnyika: Sahihi
Job Mrema: Namna pekee ambayo mtu ni mstaarabu na anajielewa asiporidhishwa njia bora ni kuiwasilisha jambo hilo Mahakamani?
Mnyika: Sikubaliani na wewe.
Job Mrema: Wakati Mshitakiwa anakuandaa alikwambia mambo gani?
Mnyika: Aliniambia kuhusu taratibu za Mahakama na kusikiliza maelekezo ya Majaji.
Job Mrema: UnamjuaIshengoma Mutembei Barongo ambae ni Katibu wa Chadema Mikocheni?
Mnyika: Simjui.
Job Mrema: Unajua kama Katibu Mkuu kuwa Ishengoma ni Katibu wa CHADEMA Mikocheni?
Mnyika: Hayo ni maoni yako mimi sifahamu? Na hii inafurahisha mawakili wa serikali ni watambuzi wa wanachama wa CHADEMA kuliko Katibu Mkuu wa Chadema.
Job Mrema: Makatibu wa Kata utaratibu wao wa kazi ni upi?
Mnyika: Ni wenyeviti wa Sekretarieti kwenye ngazi ya Kata na wanaripoti majukumu yao kwa viongozi wa Jimbo. Sio Mkoa wala Kanda.
Job Mrema: Ikitokea kuna ushahidi ukitolewa huoni kama kiti chako kitakuwa kwenye mashaka? Kwamba hata wanachama wako huujui.
Mnyika: Hilo sio miongoni mwa jambo linaloweza kukitia kwenye mashaka kiti cha Katibu Mkuu wa Chama. Chadema ina Makatibu wa Kata zaidi ya 1000.
Sehemu ya 329
Job Mrema: Ni sahihi ubaguzi ni kinyume na Katiba yetu ya Tanzania?
Mnyika: Ni sahihi.
Job Mrema: Yale makusanyo ya Tonetone kuna uamuzi ulifanyika kuwa kuna wachache wanufaike na wachache wasinufaike angali wengine wapo?
Mnyika: Sio Ubaguzi. Na ungetaka walipwe wote ukirudi ofisini mshauri Boss wako mwanasheria Mkuu wa Serikali alipe pesa zetu zaidi ya Milioni 400 ili tuwalipe wafanyakazi wetu wote. Hizo posho ni ndogo tu. Job
Mrema: Zaidi ya milioni 39 za Tonetone zimetolewa kati ya Tarehe 18 na 19 August 2026?
Mnyika: Hizo Habari nazisikia kutoka kwako.
Job Mrema: Ikitokea wanachama wa Chadema wamepata ushahidi wakasema kuna pesa zimetoka huoni kiti chako kitakuwa rehani?
Mnyika: Tutasubiri kuona kama kuna aliyeidhinisha pesa kutoka ni nani na kwa sababu gani?
Job Mrema: Kutoa pesa za Tonetone kwa mujibu wa ibara ya 4.1.2 ni kuwaonea?
Mnyika: Anaisoma hiyo ibara. Inasema kukandamiza watu kwa rangi, dini
Job Mrema: Ndio maana wengine hamkuwalipa?
Mnyika: Mimi Katibu Mkuu ndio ninayejua kwamba kwa hali tuliyonayo. Alipwe Mlinzi pekee. Kwasababu yeye yuko ofisini kila siku na sio mfanyakazi mwingine. Wewe unajua nini kuhusu haya mambo kuliko mimi?
Job Mrema: Ibara ya 3.2.4 inasema kama inavyosema hapo?
Mnyika: anaisoma na kusema inasema hivyo. Job Mrema: Sasa kama hizo fedha chache zimelipwa kwa ubaguzi unasemaje kuhusu hilo?
Mnyika: Sisi hatuna Ubaguzi wenye ubaguzi ni nyie Serikali ambao mmezuia fedha za Chadema. Ndio maana Chadema tunapambana fedha za umma zibaki salama.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kuwa ukiaminika kwa dogo utaaminika kwa kubwa?
Mnyika: Chadema inaaminika kwa dogo na kwa kubwa pia. Ndio maana watanzania wameendelea kuiunga mkono.
Sehemu ya 330
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu
John Mnyika.
Job Mrema: Huoni kwamba kwa uzoefu wa miaka 10 ya Kutunga Sheria huoni haujakitendea Haki Chadema kwa kutokishauri Chama cha Chadema kutumia Mahakama?
Mnyika: Nimekishauri vizuri kabisa chama. Tumekaa kwenye Maridhiano, tumeenda Bunge kupeleka maoni yetu kuhusu mabadiliko ya sheria hakuna lililofanyika. Mahakama kwenye kesi ya kubenea ilisema masuala ya kisiasa yatatuliwe kisiasa ndio maana tukaja na No Reforms: No Election.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kuwa Ishengoma ni Katibu wa Chadema?
Mnyika: Nitakubalianaje na jambo gani sasa ambalo silijui???
Job Mrema: Ni sahihi kuwa kwenye hiyo clip ya Bwana Mutembei alisema vurugu za Oktoba 29 zilipangwa na Chadema?
Mnyika: Nilikwambia hiyo Clip siijui, simjui Mutembei na hata hayo unayosema sio sahihi na sikubaliani na wewe kwa chochote kuhusu hilo.
Job Mrema: Mimi nimemaliza
Mheshimiwa Jaji. Anasimama
Ajuaye: Tumemaliza Jamhuri wote.
Jaji Ndunguru: Haya Utetezi vipi nafikiri re examination itakuwa fupi sana?
Tundu Lissu: Siwezi kuahidi kabisa ila nitasema yale ya muhimu tu ndio nitamuuliza.
Naomba nianze sasa.
Mhe. Lissu: Sasa umeulizwa sana kuhusu kifungu cha 7 kuhusu Sheria ya habari kisome na ujibu ulimaanisha nini?
Mnyika: Anakisoma na kusema hiyo sheria inawapa uhuru na haki ya kutafuta habari na baadae kuwa huru kuisambaza au kutoisambaza na kifungu hiki kinawafanya wanahabari kuwa wamiliki wa habari husika na sio mtu mwingine.
Mhe. Lissu: Umeulizwa kuhusu maneno yangu na uhusiano wa matukio ya October?
Mnyika: Maneno yalitolewa Tarehe 03/04 na mshitakiwa akakamatwa Tarehe 09/04 na matukio ya Oktoba yakaja kutokea Mshitakiwa akiwa yuko Mahabusu.
Anasimama Katuga: Mheshimiwa asiende mbali huko.
Jaji: Anayosema shahidi tulishayaandika kwahiyo hakuna shida.
Tundu Lissu: Uliulizwa kuhusu maana ya Uasi, sasa nakupa Kamusi ile ile usome.
Mnyika: Uasi ni kupinga mambo ndani ya taasisi au sheria kandamizi hiyo ndio maana ya kwanza.
Mhe. Lissu: Kwahiyo umeelewaje hapo?
Mnyika: Uasi sio tu kupinga serikali bali hata kwenye taasisi kupinga mifumo mibovu nao pia ni uasi.
Mhe. Lissu: Wamesema kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba haukuwa huru na haki?
Mnyika: Kuna ripoti mbalimbali zimesema ikiwemo Common wealth Anasimama
Katuga: Hizo ripoti naziogopa asiende huko hakuzitaja kabisa
Mhe. Lissu: Sasa ripoti zinawapa presha usiende huko.
Katuga: Sio Presha tu zinanipa hadi Kisukari.
Mnyika: Basi uchaguzi wa Oktoba haukuwa huru na haki na haukuwezesha watu kushiriki kwa uhuru na haki.
Mhe. Lissu: Kesi ya Mbowe ulisema ya uongo fafanua sasa licha ya kwamba alikutwa na kesi ya kujibu?
Mnyika: Hakukutwa na hatia ya ugaidi na kumekuwa na tabia ya kubambikwa kesi na kwa Mwenyekiti Mbowe kama Mtendaji mkuu wa Chama , najua hakuwahi kupanga Ugaidi na Chama hakijawahi kuwa na Mipango hiyo.
Mhe. Lissu: Pia uliulizwa kama ni kweli alishitakiwa na watu wengine walikuwa ni Makomandoo wa Jeshi na ukasema walikuwa ni walinzi wake na wanaharakati pia.
Mnyika: Waliwahi kutumikia jeshi na kuondoka Jeshini na wakajiunga na harakati na Mwenyekiti akawapanga kuwa walinzi wake.
Katuga: Anasimama hili la kwamba walikuwa makomandoo wasiliseme kabisa.
Mhe. Lissu: Nawish nisiseme kuwa hii ni non sense, sitasema hivyo lakini sioni umaana wa hili swali. Lazima ufafanuzi ufanyike na huwezi kumtisha mtu kuwa utafanya cross sasa cross gani utafanya hapa?
Katuga: this court is not your mother
Mhe. Lissu: It is not your mother either. Wewe nani kakudanganya hii Mahakama ni Mama ako?
Jaji Ndunguru. Sasa Shahidi aulizwe swali tumuache ajibu.
Part 231 itaendelea kwenye post inayofuata,
Kwangu mimi hili ni igizo tu maana sioni concrete evidence yoyote ya maana, haya maigizo ya dodoso yaishe tu haraka.
The real show itaanza Lissu akirudi uraiani rasmi.
Wanatafuta kichaka kingine cha kukimbilia hawa bila shaka. Ni rahisi sana kuwatabiri.Tena ni upuuzi kabisa, wamehama kwenye case ya msingi, wamehamia kwenye fedha za chama na tone tone.
Hii sio kwa bahati mbaya, baada ya uhaini kuonekana hauna mashiko, kesi nyingine inatengenezwa kianaTena ni upuuzi kabisa, wamehama kwenye case ya msingi, wamehamia kwenye fedha za chama na tone tone.
Mkuu hii tabia inakera sana na hapo mtu unaweza ukaonekana una IDs mbili tofauti. Nimeshatoa msimamo kama hii tabia ya kuunganisha nyuzi itaendelea na kesho sitoposti tena updatesHii updates ipo chini ya mawele au manyanza? Mbona mods mnatuvuruga maana mwingine yupo mbele mwingine nyuma mala stori inarudiwa na wote wawili kaa
Mawakili wa serikali wahuni wanakula posho za serikali na bado wanataka tone tone .Natamani kufahamu uhusiano uliopo kati ya malipo ya posho ya tone tone kwa baadhi ya viongozi wa Chadema kutokana na hali ngumu ya kiuchumi wanayopitia, na uhaini wa Lissu!!! Kwangu mimi naona hakuna uhausiano wowote ule.
Sa hizi watu wameanza kuflow na propaganda za mitandaoni, eti story za Ishengoma ndio zinatumika kama sehemu ya dodoso😁😁😁🙌🏽🙌🏽, sema anayewaagiza Hawa jamaa, sijui tu.....
Ni kama pumzi imewakata hivi, majaji nao kimyaaa
Usiache mkuu, dawa ya hili ni kuwaambia waache hii tabia ... Ikishindikana ndio uchukue uamuzi mwingineMkuu hii tabia inakera sana na hapo mtu unaweza ukaonekana una IDs mbili tofauti. Nimeshatoa msimamo kama hii tabia ya kuunganisha nyuzi itaendelea na kesho sitoposti tena updates
Umeona eeh! Hapo ndipo tunapojua they are desperate. Kesi imewashinda, sasa hivi wanahangaika kutafuta namna ya kuipaka matope CHADEMA ionekane haifuati taratibu zake za ndani ili tu wawafurahishe waliowatuma.Tena ni upuuzi kabisa, wamehama kwenye case ya msingi, wamehamia kwenye fedha za chama na tone tone.
Watatengeneza kesi gani sasa hawa wafa maji! Ya ugaidi au uhujumu uchumi na kuendesha genge la uhalifu? Kwa maana hizi ndizo kesi zao kuu za kuwanyamazisha wakosoaji wao.Hii sio kwa bahati mbaya, baada ya uhaini kuonekana hauna mashiko, kesi nyingine inatengenezwa kiana
Wakuu tuelewesheni ambao hatujawahi kuwa mahakamani wala kujua vingi kuhusu kesi, ni kawaida shahidi kufanyiwa cross examination siku 3? Asubuhi mpaka jioni?
Yani Hawa mawakili wa serikali ni rahisi sana kuwajua hatua wanayotaka kuipiga Yani Kuna muda nilikuwa namuona Mnyika anatumia akili kubwa sana kupangua maswali ya mitego kumbe tatizo ni la mawakili hawatumii akili hata kidogo na Mnyika ndiyo anatumia huo ujinga wao Kila wanachotaka kukifanya anakuwa kawazidi hatua moja mbele Yani anawajibu maswali kama yupo akilini mwao😀😀wanajionyesha waziwazi kabisa wanachotaka kukitengenezaHii sio kwa bahati mbaya, baada ya uhaini kuonekana hauna mashiko, kesi nyingine inatengenezwa kiana
hii haitoshi kumtia mtu hatiani. Je ukimuuliza kuwa nipe mipango yako uliyokuwa unapanga ya kufanya uhaini akasema nilipanga kwenda mahakamani kupinga uchaguzi, utamtia hatiani? Uhaini siyo kitu chepesi kama katuga et al wanavyokifikiria...wajinga!" mimi ni haini..."
Sasa hivi mawakili wetu wa serikali wamekata pumzi kabisa wamebaki kuingia Facebook kutafuta viclip vya kina ishengoma wavipachike kwenye ushahidi wao😀😀mara wanaingiza mambo ya tone tone mara sijui milioni ngapi zimepotea yan mpaka najiuliza wanamshtaki TAL au wanaishitaki CDM na ukiangalia ni chama kilikuwa kimefungiwa Hadi mama yetu kapata 98%
re examination ni ya moto haswaa. najifunza si vizuri kuleta maswali ya ukakasi au nje ya mashtaka ukijihisi utachimba jambo kumbe unajitengenezea mtihani mwingine mzito mbeleni ambao pakiitajika clarification inakupa tena mtihani/ulakini kwa ku prove wrong approaches zako.