Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri - 2, Septemba 2026

Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri - 2, Septemba 2026

Payge JamiiForums Maxence Melo
celix
Reviser
Wand
Boqin
Payge
Zenora


HABARI WAKUU NA VIONGOZI WA JAMII FORUMS.

Naomba kuwasilisha ombi langu kwa heshima, lakini pia kwa msisitizo wa kutaka usawa na haki katika matumizi ya jukwaa hili.

Kuna jambo ambalo naomba viongozi wa JamiiForums mlitafakari kwa kina. Mtu ambaye hayupo eneo la tukio, wala hayupo mahakamani, anawezaje kupewa nafasi ya kuanzisha uzi wa “LIVE” na kuendelea kuutangaza, wakati mwingine ambaye yupo moja kwa moja eneo la tukio anazuiwa kufanya LIVE?
Kwa mfano, mtu akiwa Mbeya au sehemu nyingine, anaweza kuanzisha uzi unaosema “Mahakama Kuu Dar es Salaam LIVE” na kuendelea kutoa taarifa kupitia uzi huo, hata kama yeye mwenyewe hayupo mahakamani na hana uwezo wa kuthibitisha kinachoendelea kwa wakati huo. Wakati huo huo, mtu ambaye yupo ndani au karibu na eneo la tukio, anayeshuhudia kinachoendelea moja kwa moja, ananyimwa fursa ya kurusha taarifa LIVE.
Hapa ndipo tunapojiuliza: Je, kigezo cha kuruhusu LIVE ni nini?
Kama hoja ni kuhakikisha taarifa zinazotolewa ni sahihi, basi kimantiki mtu aliye eneo la tukio ana nafasi kubwa zaidi ya kutoa taarifa sahihi na za wakati huo kuliko mtu aliye mbali na eneo hilo.

Kama kuna kanuni au sababu za kiusalama, kisheria au za kiutendaji zinazozuia mtu aliyepo mahakamani kufanya LIVE, basi tunaomba kanuni hizo ziwekwe wazi na zitumike kwa usawa kwa kila mtu. Tusije tukawa na mazingira ambayo mtu mmoja anaruhusiwa kufanya jambo fulani kwa sababu hayupo eneo la tukio, lakini mwingine anayefanya jambo hilo akiwa eneo la tukio anazuiwa.
JamiiForums ni jukwaa kubwa la mijadala na taarifa. Kwa hiyo, tunatarajia misingi ya haki, uwazi, usawa na kanuni zinazofanana itumike kwa wanachama wote bila upendeleo.

Suala hapa si kumzuia mtu mwingine kutoa taarifa. Hoja yangu ni kwa nini anayetoa taarifa akiwa mbali na tukio apewe uhuru zaidi kuliko yule aliyepo kwenye tukio lenyewe?
Naomba viongozi wa JamiiForums mlitazame jambo hili kwa jicho la usawa na mlitafakari upya, kwa sababu kama lengo ni kupata taarifa za haraka na sahihi kutoka eneo la tukio, basi anayekuwa eneo hilo anapaswa angalau kuwa na nafasi sawa ya kutoa taarifa kama wengine.

Tunaomba usawa wa kanuni, uwazi wa vigezo na haki sawa kwa wanachama wote.
Asanteni.
Sawa kabisa mwisho wa siku wana merge alafu wanatuchanganyia Habari zazieleweki unaenda mbele unakuta unarudishwa tena nyuma kusoma vitu ambavyo ushasoma.
 
Katuga mbona anapata muhaho sana? Maswali ya dodoso walifanya wao, afu sahivi yakiwa yanatolewa ufafanuzi kwenye Re Adam's wanapinga na kukakataa? Sasa shida nini? Wanakataa vitu walivyoleta wao wenyewe, hii ni maajabu. Khaaah
 
Yani Hawa mawakili wa serikali ni rahisi sana kuwajua hatua wanayotaka kuipiga Yani Kuna muda nilikuwa namuona Mnyika anatumia akili kubwa sana kupangua maswali ya mitego kumbe tatizo ni la mawakili hawatumii akili hata kidogo na Mnyika ndiyo anatumia huo ujinga wao Kila wanachotaka kukifanya anakuwa kawazidi hatua moja mbele Yani anawajibu maswali kama yupo akilini mwao😀😀wanajionyesha waziwazi kabisa wanachotaka kukitengeneza
Sio kana kwamba hawajui wanachofanya walishapanga, sasa wamekutana na upande wa mshtakiwa wamejipanga mara mbili yake.
 
Mimi ningekua katuga ninge ieleza mahakama

Kesi ifungwe maana nakula posho za Bure pia ni kujifedhehesha na kuharibu jina la ukoo na heshima ya taaluma ya uwakili
Shida ni hadidu rejea.

Subiria ile tume iliyoundwa kuhusu 29 October uone mambo itakayoleta. Vitu wakakavyokutana navyo kwa ground na watakachoandika na kukabidhi tofauti.
 
Lissu: Sawa.

Sasa, Shahidi, ukaulizwa kwamba kama ni kweli au si kweli chama chako kilipata fursa ya kutoa maoni mbele ya Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge.

Majibu yako yakawa ulizuiliwa: “Sikutoa maoni yote ya mabadiliko ya Kikatiba kwa sababu yalikataliwa.”

Nataka ufafanuzi hapo kwa maoni yako kuzuiwa.

Mnyika: Maoni yote ambayo tulitaka kuwasilisha kuwezesha kupata mabadiliko ya Kikatiba, mathalani matokeo ya Rais kupingwa Mahakamani na maamuzi ya Tume kupitiwa na Mahakama.

Kipaza sauti kilikuwa kinazimwa na unaambiwa maoni hayo hayapokelewi.

Ukweli ni kwamba CCM haiwezi kuwa na mapenzi na hii nchi
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 11.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nina swali moja la mwisho. Mawili ya mwisho.

Enhee, Katibu Mkuu, unakumbuka uliulizwa maswali juu ya uteuzi wako wewe? Nani aliyekuteua?

Majibu yako yakawa umeteuliwa na Mwenyekiti na kuthibitishwa na Baraza Kuu. Ulikuwa na maana gani?

Mnyika: Nilikuwa na maana kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA anapeleka mapendekezo kwa Baraza Kuu, na Baraza Kuu ndilo linalothibitisha na kumteua Katibu Mkuu.

Kwa hiyo, pendekezo la Mwenyekiti linaweza kukataliwa na Baraza Kuu.

Na Katibu Mkuu anawajibika kwa Baraza Kuu, siyo kwa Mwenyekiti.

Ila atafanya kazi kwa kushauriana na kushirikiana na Mwenyekiti.

Lissu: Katibu Mkuu, ulisomewa Katiba ya CHADEMA, Ibara ya 4.1.1, ukaulizwa kama lengo la CHADEMA ni kushika madaraka ya dola.

Ukasema ndiyo, ila siyo lengo muhimu zaidi. Ulikuwa na maana gani?

Mnyika: Nilikuwa na maana kwamba kushika dola siyo an end, bali the means.

Katika hiyo hiyo Ibara ya 4 kuna malengo mengine ya muhimu zaidi, ikiwemo kutetea mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Ikiwemo kuhamasisha mabadiliko ya kimfumo na ya kisheria.

Kilele kikiwa kuleta demokrasia, uhuru na maendeleo ya watu.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, sina maswali zaidi ya re-examination.

Jaji Ndunguru: Shahidi, umeshamaliza kutoa ushahidi wako. Nakuruhusu tuweze kuendelea na mashahidi wengine.

Mnyika: Nashukuru, Waheshimiwa Majaji. Mungu awabariki.

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka?

Ajuaye: Waheshimiwa Majaji, imebakia dakika 10 kwenda mapumziko. Naomba tuhairishe shauri kwa saa 1 na dakika 10, ikiwapendeza.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, naomba iwe saa 8:30, kama ambavyo tumekuwa tunafanya, ili nikae na shahidi wangu.

Nahitaji kukaa naye ili nimuandae.

Jaji Ndunguru: Shauri linahairishwa hadi saa 8:30, ambapo tutaendelea na upande wa utetezi.

MAJAJI WANATOKA.

TUKUTANE SAA 8:30 MCHANA.
 
Mh! Ngoja kwanza, nisije nikawa nakupa wadhifa wa juu sana...ukiwa Ajuaye, mie ntakua nani? Zingatia elimu ya juu kabisa nnayomiliki ni form sita.
Hivi unakumbuka mara ya kwanza kuniambia kuhusu form 6 tulibishana 😂😂 Tulibishana kama Katuga na JJ jana.

Mimi (katuga) Nilikuwa nakubishia wewe Mnyika mwenye ukweli wote (Afisa masuhuri)

😂💔
 
Hivi unakumbuka mara ya kwanza kuniambia kuhusu form 6 tulibishana 😂😂 Tulibishana kama Katuga na JJ jana.

Mimi (katuga) Nilikuwa nakubishia wewe Mnyika mwenye ukweli wote (Afisa masuhuri)

😂💔

Hebu waambie majaji kwanini unaniwekea ka alama ka moyo uliovunjika kwenye majibu yako kila unaponinukuu?

Hilo la kidato cha sita ni jambo mtambuka. Hakuna mtu hua analielewa.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 10.

Jaji Ndunguru: Moja ya mapendekezo ni kwamba Wakurugenzi na watumishi wa umma wasishiriki katika uchaguzi.

Akajibu: Ni kweli kwamba Wakurugenzi na watumishi wa umma wameondolewa katika uchaguzi.

Imeishia hapo.

Lissu: Sawa.

Sasa, Shahidi, ukaulizwa kwamba kama ni kweli au si kweli chama chako kilipata fursa ya kutoa maoni mbele ya Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge.

Majibu yako yakawa ulizuiliwa: “Sikutoa maoni yote ya mabadiliko ya Kikatiba kwa sababu yalikataliwa.”

Nataka ufafanuzi hapo kwa maoni yako kuzuiwa.

Mnyika: Maoni yote ambayo tulitaka kuwasilisha kuwezesha kupata mabadiliko ya Kikatiba, mathalani matokeo ya Rais kupingwa Mahakamani na maamuzi ya Tume kupitiwa na Mahakama.

Kipaza sauti kilikuwa kinazimwa na unaambiwa maoni hayo hayapokelewi.

Lissu: Sasa, Shahidi, baada ya kujibu hilo swali, ukaulizwa kwamba baada ya maoni yenu kukataliwa, ndiyo mkarudi kuweka mkakati wa kuzuia uchaguzi.

Ukajibu: Hapana. Mkakati wa kuzuia uchaguzi ulifanyika tarehe 03 Desemba 2024.

Fafanua hapo.

Mnyika: Kukataliwa kwa maoni kwenye Kamati haikuwa ndiyo mwanzo wa kupanga mkakati.

Mkakati wa kuhamasisha wananchi ili waasi dhidi ya mifumo kandamizi ulianza tangu Desemba 2024.

Lissu: Shahidi, uliulizwa kama ulipiga kura tarehe 29 Oktoba 2025. Ukasema hukupiga kura kwa sababu hapakuwa na uchaguzi.

Ulikuwa na maana gani?

Mnyika: Hapakuwa na uchaguzi kwa sababu hapakuwa na uchaguzi huru, wa haki na wa kisheria, wenye kuwezesha wengine kushiriki, na chama changu hakikuwa kimeshiriki uchaguzi.

Lissu: Shahidi, uliulizwa kama mimi nina kinga yoyote ya kutoshitakiwa nikivunja sheria.

Ukasema mimi sina kinga yoyote na sijavunja sheria.

Nassoro Katuga: (Anasimama.)

Jaji Ndunguru: Hebu rudia swali lako.

Ukiacha “hana kinga”, hapo kunahitaji ufafanuzi?

Nassoro Katuga: Nadhani ilikuwa wazi kama alivyoeleza, kama Mwenyekiti wa CHADEMA na kama mwendelezo wa Mwenyekiti kushitakiwa.

Hii lakini haitokani na swali la cross-examination. Naomba rekodi za Mahakama, Waheshimiwa.

Jaji Ndunguru: Hebu uliza swali.

Lissu: Ulikuwa na maana gani uliposema hana kinga anapovunja sheria, lakini hana kosa?

Mnyika: Amekuwa akishitakiwa kwa makosa mbalimbali, lakini katika hili hakuwa na sababu ya kushitakiwa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Kutoka kwenye maswahi haya Tathimini yangu inasema:
🔴 Conviction: 55%
🟢 Acquittal: 45%
kwa sababu admission ya Mnyika kwamba:
Mkakati wa kuzuia uchaguzi ulifanyika tarehe 03 Desemba 2024
 
Hivi Mnyika na Lissu wanakutana muda gani kutengeneza alignment ya maswali na majibu yao? Naona kama ni mtu mmoja anajiuliza na kujijibu, kumbe ni watu wawili

Hofu yangu kubwa ipo kwa heche, naogopa sana kama hatashikwa na jazba akatoka kwenye mstari, hawa jamaa wanajua kukera, usipokua makini, unaweza kuingia kwenye mfumo wao wakakupiga wanavyotaka wenyewe KO.
 
Hebu waambie majaji kwanini unaniwekea ka alama ka moyo uliovunjika kwenye majibu yako kila unaponinukuu?

Hilo la kidato cha sita ni jambo mtambuka. Hakuna mtu hua analielewa.
Waheshimiwa majaji huyu mtu ananivunja moyo mara kwa mara ndio maana natumia ka moyo kaliko vunjika kama msisitizo, imagine hapo ni form 6 liva tu na upo hapo!

Nje ya mahakama: Wewe na JJ ni dugu moya?
 
Back
Top Bottom