Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri - 2, Septemba 2026

Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri - 2, Septemba 2026

Jana nilisema huyo Ishengoma aliyejitokeza juzi kwenye vyombo vya habari akikiri kutumiwa na cdm kufanya Vurugu siku ya uchaguzi, ni mpango maalum unaopangwa n jamuhuri kuchomeka ushahidi wake kwenye hii kesi. Jamuhuri ilimtoa hadharani kimkakati ili anachosema kitumike kuhadaa umma na iwiane na hukumu ambayo mahakama imepewa iiandike.

Ni vyema mashahadi wa cdm wakaambiwa kuhusu hii mbinu na kuiweka wazi mapema huko mahakamani.
Manyanza
Kwenye dunia ya sasa hili kueleweka kwa umma bila kuwa na shaka nalo ni ngumu sana
 
Payge JamiiForums Maxence Melo
celix
Reviser
Wand
Boqin
Payge
Zenora

HABARI WAKUU NA VIONGOZI WA JAMII FORUMS.

Naomba kuwasilisha ombi langu kwa heshima, lakini pia kwa msisitizo wa kutaka usawa na haki katika matumizi ya jukwaa hili.

Kuna jambo ambalo naomba viongozi wa JamiiForums mlitafakari kwa kina. Mtu ambaye hayupo eneo la tukio, wala hayupo mahakamani, anawezaje kupewa nafasi ya kuanzisha uzi wa “LIVE” na kuendelea kuutangaza, wakati mwingine ambaye yupo moja kwa moja eneo la tukio anazuiwa kufanya LIVE?
Kwa mfano, mtu akiwa Mbeya au sehemu nyingine, anaweza kuanzisha uzi unaosema “Mahakama Kuu Dar es Salaam LIVE” na kuendelea kutoa taarifa kupitia uzi huo, hata kama yeye mwenyewe hayupo mahakamani na hana uwezo wa kuthibitisha kinachoendelea kwa wakati huo. Wakati huo huo, mtu ambaye yupo ndani au karibu na eneo la tukio, anayeshuhudia kinachoendelea moja kwa moja, ananyimwa fursa ya kurusha taarifa LIVE.
Hapa ndipo tunapojiuliza: Je, kigezo cha kuruhusu LIVE ni nini?
Kama hoja ni kuhakikisha taarifa zinazotolewa ni sahihi, basi kimantiki mtu aliye eneo la tukio ana nafasi kubwa zaidi ya kutoa taarifa sahihi na za wakati huo kuliko mtu aliye mbali na eneo hilo.

Kama kuna kanuni au sababu za kiusalama, kisheria au za kiutendaji zinazozuia mtu aliyepo mahakamani kufanya LIVE, basi tunaomba kanuni hizo ziwekwe wazi na zitumike kwa usawa kwa kila mtu. Tusije tukawa na mazingira ambayo mtu mmoja anaruhusiwa kufanya jambo fulani kwa sababu hayupo eneo la tukio, lakini mwingine anayefanya jambo hilo akiwa eneo la tukio anazuiwa.
JamiiForums ni jukwaa kubwa la mijadala na taarifa. Kwa hiyo, tunatarajia misingi ya haki, uwazi, usawa na kanuni zinazofanana itumike kwa wanachama wote bila upendeleo.

Suala hapa si kumzuia mtu mwingine kutoa taarifa. Hoja yangu ni kwa nini anayetoa taarifa akiwa mbali na tukio apewe uhuru zaidi kuliko yule aliyepo kwenye tukio lenyewe?
Naomba viongozi wa JamiiForums mlitazame jambo hili kwa jicho la usawa na mlitafakari upya, kwa sababu kama lengo ni kupata taarifa za haraka na sahihi kutoka eneo la tukio, basi anayekuwa eneo hilo anapaswa angalau kuwa na nafasi sawa ya kutoa taarifa kama wengine.

Tunaomba usawa wa kanuni, uwazi wa vigezo na haki sawa kwa wanachama wote.
Asanteni.
Kumbe unakuwaga na akili hivi, nashangaa unavyonipingaga bila hoja nzito.
 
Gereji yako iko wapi?

Sasa umeongea, shauri hili tunalifunga, kwa heshima na taadhima naomba unipigie jioni.
Objection
Garage ipo huku.

894777.jpg

Aaah, sidanganyiki, hakuna kuongea hadi kesi iishe.

Heche asituangushe kwenye ushahidi, hakawii kushikwa hasira akaharibu interview
 
Jana nilisema huyo Ishengoma aliyejitokeza juzi kwenye vyombo vya habari akikiri kutumiwa na cdm kufanya Vurugu siku ya uchaguzi, ni mpango maalum unaopangwa n jamuhuri kuchomeka ushahidi wake kwenye hii kesi. Jamuhuri ilimtoa hadharani kimkakati ili anachosema kitumike kuhadaa umma na iwiane na hukumu ambayo mahakama imepewa iiandike.

Ni vyema mashahadi wa cdm wakaambiwa kuhusu hii mbinu na kuiweka wazi mapema huko mahakamani.
Manyanza
Exactly, Maoni yenye kufaa na yanayopaswa kipewa sikio sikivu
 
😂😂😂😂 Utatekwa muone! Tena wapo karibu hapo tu 😅

😭

Hivi Tata Heche mbona huwa ana utulivu mkubwa sana? Au mnahofia kisa kanda maalumu.
Mie sina makuu, naweza kwenda mwenyewe wanaponihitaji. Wote tutakufa, kila mmoja wetu, hata hao wanaomzungusha TAL kwa kesi wanayojua kabisa ni suala la uhai na kifo, watakufa.

Lakini wajiulize, utanyamazisha wangapi? Kikubwa ni kujitathmini waone kipi kinasababisha watu wapaze sauti na kuwachoka, wafanye mabadiliko.

Hata usilie, huko nnakotarajia kwenda, wewe tayari ulishaenda kitambo.

Heche yuko vizuri sana, tatizo ni akina Ajuaye na Katuga, wanaweza kukutia ndimu ikarusha ngumi au ukajaa jazba, ukaanza kujibu kwa hasira bila utulivu, hiyo ndio hofu yangu.
 
🤔🤐🤐🤐 let's 👀
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 11.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nina swali moja la mwisho. Mawili ya mwisho.

Enhee, Katibu Mkuu, unakumbuka uliulizwa maswali juu ya uteuzi wako wewe? Nani aliyekuteua?

Majibu yako yakawa umeteuliwa na Mwenyekiti na kuthibitishwa na Baraza Kuu. Ulikuwa na maana gani?

Mnyika: Nilikuwa na maana kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA anapeleka mapendekezo kwa Baraza Kuu, na Baraza Kuu ndilo linalothibitisha na kumteua Katibu Mkuu.

Kwa hiyo, pendekezo la Mwenyekiti linaweza kukataliwa na Baraza Kuu.

Na Katibu Mkuu anawajibika kwa Baraza Kuu, siyo kwa Mwenyekiti.

Ila atafanya kazi kwa kushauriana na kushirikiana na Mwenyekiti.

Lissu: Katibu Mkuu, ulisomewa Katiba ya CHADEMA, Ibara ya 4.1.1, ukaulizwa kama lengo la CHADEMA ni kushika madaraka ya dola.

Ukasema ndiyo, ila siyo lengo muhimu zaidi. Ulikuwa na maana gani?

Mnyika: Nilikuwa na maana kwamba kushika dola siyo an end, bali the means.

Katika hiyo hiyo Ibara ya 4 kuna malengo mengine ya muhimu zaidi, ikiwemo kutetea mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Ikiwemo kuhamasisha mabadiliko ya kimfumo na ya kisheria.

Kilele kikiwa kuleta demokrasia, uhuru na maendeleo ya watu.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, sina maswali zaidi ya re-examination.

Jaji Ndunguru: Shahidi, umeshamaliza kutoa ushahidi wako. Nakuruhusu tuweze kuendelea na mashahidi wengine.

Mnyika: Nashukuru, Waheshimiwa Majaji. Mungu awabariki.

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka?

Ajuaye: Waheshimiwa Majaji, imebakia dakika 10 kwenda mapumziko. Naomba tuhairishe shauri kwa saa 1 na dakika 10, ikiwapendeza.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, naomba iwe saa 8:30, kama ambavyo tumekuwa tunafanya, ili nikae na shahidi wangu.

Nahitaji kukaa naye ili nimuandae.

Jaji Ndunguru: Shauri linahairishwa hadi saa 8:30, ambapo tutaendelea na upande wa utetezi.

MAJAJI WANATOKA.

TUKUTANE SAA 8:30 MCHANA.
Kazi yako imetukuka 👏👏👏
 
Hofu yangu kubwa ipo kwa heche, naogopa sana kama hatashikwa na jazba akatoka kwenye mstari, hawa jamaa wanajua kukera, usipokua makini, unaweza kuingia kwenye mfumo wao wakakupiga wanavyotaka wenyewe KO.

Sina hakika kwa Heche, japo ni mtulivu ila anaweza kutoka nje ya mstari, na naona huyu ndiye target yao kuu.
Muhimu Heche Atulie na asiwe na papara.
 
Namimi nipo kama ni Heche ndani ya kizimba🦘

Kama niyeye Heche
Basi Watanzania tupo tayali kupumbazwa nayeye leo❗️

tuache kuwaza mambo ya msingi ili
kushuhudia Cinema yake
Ya kutupumbaza na kupumbazika

HECHE OYEEEE
SHEMEJI JUUUU juu zaidi🤠
 
Payge JamiiForums Maxence Melo
celix
Reviser
Wand
Boqin
Payge
Zenora

HABARI WAKUU NA VIONGOZI WA JAMII FORUMS.

Naomba kuwasilisha ombi langu kwa heshima, lakini pia kwa msisitizo wa kutaka usawa na haki katika matumizi ya jukwaa hili.

Kuna jambo ambalo naomba viongozi wa JamiiForums mlitafakari kwa kina. Mtu ambaye hayupo eneo la tukio, wala hayupo mahakamani, anawezaje kupewa nafasi ya kuanzisha uzi wa “LIVE” na kuendelea kuutangaza, wakati mwingine ambaye yupo moja kwa moja eneo la tukio anazuiwa kufanya LIVE?
Kwa mfano, mtu akiwa Mbeya au sehemu nyingine, anaweza kuanzisha uzi unaosema “Mahakama Kuu Dar es Salaam LIVE” na kuendelea kutoa taarifa kupitia uzi huo, hata kama yeye mwenyewe hayupo mahakamani na hana uwezo wa kuthibitisha kinachoendelea kwa wakati huo. Wakati huo huo, mtu ambaye yupo ndani au karibu na eneo la tukio, anayeshuhudia kinachoendelea moja kwa moja, ananyimwa fursa ya kurusha taarifa LIVE.
Hapa ndipo tunapojiuliza: Je, kigezo cha kuruhusu LIVE ni nini?
Kama hoja ni kuhakikisha taarifa zinazotolewa ni sahihi, basi kimantiki mtu aliye eneo la tukio ana nafasi kubwa zaidi ya kutoa taarifa sahihi na za wakati huo kuliko mtu aliye mbali na eneo hilo.

Kama kuna kanuni au sababu za kiusalama, kisheria au za kiutendaji zinazozuia mtu aliyepo mahakamani kufanya LIVE, basi tunaomba kanuni hizo ziwekwe wazi na zitumike kwa usawa kwa kila mtu. Tusije tukawa na mazingira ambayo mtu mmoja anaruhusiwa kufanya jambo fulani kwa sababu hayupo eneo la tukio, lakini mwingine anayefanya jambo hilo akiwa eneo la tukio anazuiwa.
JamiiForums ni jukwaa kubwa la mijadala na taarifa. Kwa hiyo, tunatarajia misingi ya haki, uwazi, usawa na kanuni zinazofanana itumike kwa wanachama wote bila upendeleo.

Suala hapa si kumzuia mtu mwingine kutoa taarifa. Hoja yangu ni kwa nini anayetoa taarifa akiwa mbali na tukio apewe uhuru zaidi kuliko yule aliyepo kwenye tukio lenyewe?
Naomba viongozi wa JamiiForums mlitazame jambo hili kwa jicho la usawa na mlitafakari upya, kwa sababu kama lengo ni kupata taarifa za haraka na sahihi kutoka eneo la tukio, basi anayekuwa eneo hilo anapaswa angalau kuwa na nafasi sawa ya kutoa taarifa kama wengine.

Tunaomba usawa wa kanuni, uwazi wa vigezo na haki sawa kwa wanachama wote.
Asanteni.
Umeeleza vyema, naona wamesikiliza maoni yetu na kuyafanyia kazi, sasa uzi unasoma kwa usahihi.
 
Aiseeeee!

🤣🤣🤣🤣

Kuna kitu kimoja kuhusu matusi watu wengi huwa wana ki-overlook, ukimtukana mtu make sure hilo tusi halikuhusu, Kwahiyo katuga alikuwa anajua mahakama ni mama yake? Au hakutegemea kurudishiwa hiyo kejeli!

Lissu anakupokea kadri ya unavyokuja, katuga anapanick mapema, sijui kaahidiwa nini huyu wakili uchwara, Lol
 
Wanakera hawa Mods na sisi ndio tunaowafanya wakae ofisini, sasa kwanini wanakuwa wanafanya vitu vya hovyo?

Unaunganishaje uzi wa mtu ambaye hayupo live na yule anayeleta updates live ?

Wapigieni kelele waache hii tabia
Achana nao hao, we si unajua kuwa mods wote ni mbwaaaaa mixer kengee. Dawa yao hawa ni kuwapiga miti tu kama Dudubaya anavyosemaga
 
Ndio ninalowaambia JamiiForums , mtu anaanzisha uzi wa updates saa 2 asubuhi wakati Mahakama inaanza saa 3 je ikighairi ? Mimi naanzisha uzi tayari Mahakama imeshaanza. Payge
Tunakupenda wewe tuu uanzishe uzi au la kila mtu aanzishe wake na mods msiunganishe...
Yani inaboaga mtu anajua uzi ni wa ku update kila dkk halafu anaweka title na maneno machache anasepa....🫤🫤
 
Sina hakika kwa Heche, japo ni mtulivu ila anaweza kutoka nje ya mstari, na naona huyu ndiye target yao kuu.
Muhimu Heche Atulie na asiwe na papara.
Nilikuwa na shaka na Mnyika, ila ameenda vizuri, Heche yupo vizuri sana sema huwa hapendi upuuzi, na hapa lazima wamwingizie upuuzi ili ajae upepo... Tuamini atajengwa vizuri.
 
Back
Top Bottom