Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri - 2, Septemba 2026

Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri - 2, Septemba 2026

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 3.

Lissu: Ni ushenzi gani ulioona katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, ushenzi ni mwingi, ila ili nisipoteze muda niseme machache katika mchakato wa kiuchaguzi.

Kwenye uteuzi wa wagombea wa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani, kulikuwa na matatizo kuanzia kwenye kuchukua ile fomu ya Tume.

Watumishi wa Tume walikuwa wanawakwepa wagombea wetu.

Makusudi hawawapi fomu.

Makusudi wanaondoka ofisini.

Kwa makusudi wanakataa kupokea fomu.

Pindi tunarudisha fomu za wagombea wa CHADEMA, watumishi wa Tume walikuwa wanashirikiana na wagombea wa CCM.

Kama fomu umejaza 9, wanaandika 79.

Utawekewe pingamizi kwamba hujui kusoma na kuandika.

Utawekewa pingamizi la uraia.

Lissu: Vipi kampeni za uchaguzi huo?

Amani Sam Golugwa:

Kampeni zililenga kuwapendelea wagombea wa chama kimoja, CCM, katika kata na majimbo kupitia Kamati za Maadili.

Lissu: Unazungumzia uchaguzi wa vijiji na mitaa au uchaguzi Mkuu?

Lissu: Eleza, uchaguzi wa vijiji na mitaa unasimamiwa na nani?

Amani Sam Golugwa: Unasimamiwa na Watendaji wa Vijiji na Mitaa. (Samahani, nilijikuta nazungumzia hadi uchaguzi Mkuu.)

Wagombea wachache waliopenya, kampeni ziligubikwa na vurugu zilizonekana kupangwa, kulindwa na ratiba iliyotengenezwa kimkakati kuvionea vyama vya upinzani.

Mikutano ya vyama vingine, ikiwemo CHADEMA, ilivurugwa na watendaji.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, utaratibu wa mawakala wa wagombea au wa vyama ulikuwaje katika uchaguzi huo?

Amani Sam Golugwa: Utaratibu wa mawakala, ambao kimsingi wanamwakilisha mgombea, walitakiwa kwenda kuapishwa kwa msimamizi wa uchaguzi, Mtendaji wa Kijiji au Mtaa.

Msimamizi ndiye atakayenda na utambulisho katika kituo.

Halafu wakala anapoenda katika kituo cha kupigia kura, ndiyo atakuta utambulisho wake.

Mawakala wa CHADEMA walipoenda katika vituo, hawakukuta hivi viapo ambavyo ndiyo utambulisho wa wakala.

Msimamizi wa kituo alikuwa anawajibu kwamba waende kulalamika kwa Mtendaji wa Kijiji au Mtaa.

Wakati huo, utambulisho wa CCM upo na wakala yupo ndani.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Pamoja na yote lkn kwa hii Kesi na kwa hatua ya mh Lissu
kuwaingiza kama Mashahidi wake
Kimbembe kile kakutananacho John Mnyika na wengine watapita vilevile

Basi ile ela ya tone tone wanastahili kuitafuna
Ile kazi ngumu sio poa ‼️

tusione tu wanajibu!
nyomi wavaa Suti Macho yote kwako kodoo kukutazama
👀👀👀👀👀
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 4.

Mawakala wetu walizuiwa na kufukuzwa vituoni.

Wakati wakala wetu hakuwepo ndani, na muda huo ndiyo ushenzi ulifanyika.

Ipo katika public domain nilipogombana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari.

Jaji Ndunguru: Twende taratibu, na usisahau kwamba unaongozwa na mshtakiwa.

Lissu: Ukiwa muongeaji sana, meza kuu inakusubiri.

Nassoro Katuga anasimama: Waheshimiwa Majaji, tunaomba asimtishe shahidi.

MAHAKAMA KICHEKO.

Jaji Ndunguru: Hata akimtisha, si shahidi wake.

MAHAKAMA KICHEKO.

Lissu: Sasa shahidi, elezea nini kilitokea wakati wa matokeo, wakati kwa nchi nzima baada ya ushenzi wote huo.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa kumbukumbu zangu, CCM walishinda kwa 99.2% ya vijiji na mitaa.

CHADEMA waliambulia 0.9%, na kwa Kanda ya Kaskazini, ambapo ndiyo nilikuwa Katibu wa Kanda, CCM walishinda kwa 98.7% katika vijiji, vitongoji na mitaa ya Kanda ya Kaskazini.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ni nini utofauti wa uchaguzi huo wa 2024 na uchaguzi kama huo wa 2019 wakati wa John Pombe Magufuli?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa mambo mengi ya ovyo niliyoyaona katika mzunguko wote huo, hapakuwa na tofauti yoyote ya mambo yaliyotokea.

Isipokuwa kwa jambo moja tu, kwamba mwaka 2019 hata zoezi la kurudisha fomu lilikuwa ni vita, na kwa sehemu kubwa fomu za wagombea wa CHADEMA hazikupokelewa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Nassoro Katuga : Unajua Mahakama siyo Mama yako.

Lissu : its not your mother either

Jaji Ndunguru : Subirini kidogo.

MAHAKAMA INAKUWA KIMYA KIDOGO.

Jaji Ndunguru naomba uturejeshe katika hilo swali.

Duh! Kwa hiyo Katuga alijua Mahakama sio ya Mama yake Lissu ni ya Mama yake yeye?
nimeipenda hii🤣🤣
 
Naona hii kesi sio ya kuisha Leo Wala kesho!! Yani sasa hivi wanatumia maneno ya ishengoma kama ushahidi?? Kwa hiyo akitokea mwingine tena kesho watamtumia tena na huyo??? Kwa hiyo na CDM wakitumia kauli za yule mwanamke aliyesema akipewa uraisi hata dakika moja anawapoteza CDM itakuwa sahihi? Na vipi CDM wakitumia kauli ya CHALAMILA alivyosema Dereva atakayepinga atapotezwa na familia yake itamsahau?? Aiseeee mahakama za Tanzania ni za hovyo sana naomba tu wananchi tuendelee tukikamata mwizi tunachoma moto basi au kurogana ila habari za mahakama ni kupoteza muda tu
Kabisa
 
Hakuna ukomo wa muda katika cross-examination. Zipo kesi mawakili wanakuwa wengi na wote wanauliza maswali kwa kadiri wanavyoona inafaa. Ni uwanja wao, wanaisaidia mahakama kufikia uamuzi.

Kuhusu hii kesi: Mnyika ndie shahidi muhimu upande wa utetezi, na ushahidi wake ndio kesi yenyewe, hivyo usishangae kufanyiwa cross kwa muda mrefu. Mnyika ndie shahidi pekee ambae amebomoa ushahidi muhimu wa Uhaini ambao ni "njama, nia, kitendo, taasisi na matokeo". Utaona maswali mengi anaulizwa kuhusu maeneo hayo.

Amefanikiwa kuonyesha kwamba hakukua na njama yeyote, kaonueshq kwamba ajenda na "No reforms, no election" ni ya chama sio ya Mwenyekiti, Kaonyesha kwamba hakukua na maelekezo wala malipo kwa waandishi wa habari, akiwemo shahidi wa kuona wa Jambo TV, pia kaonyesha hakukuwa na ajenda ila mada, kadhalika kaonyesha Mkutano ule haukuandaliwa na Mwenyekiti (Mshitakiwa) ila ni Secretariat ambayo muandaaji ni yeye (Katibu Mkuu), Mwenyekiti alialikwa tuu kuchangia mada na alialikwa na Makamu Katibu Mkuu (Golugwa).

Kiujumla: Shahidi huyu amefanikiwa kuonyesha kwamba hakuna Uhaini wa mtu mmoja na kwamba Mwenyekiti alikuwa anatekeleza ajenda za chama na sio zake binafsi.
Fact
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 5.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kanuni za kuendesha huo uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji zilitungwa na nani?

Amani Sam Golugwa: Kanuni za kuendesha uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilitungwa na Waziri.

Lissu: Waziri gani?

Amani Sam Golugwa: Waziri wa TAMISEMI.

Lissu: Anaitwa nani?

Amani Sam Golugwa: Mchengerwa; mkwe wa Rais.

Lissu: Mohammed Mchengerwa.

Nassoro Katuga: Mheshimiwa Jaji, shahidi amesema Mohammed, kasema Mchengerwa.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, hilo siyo la kubishana kwa sababu mawaziri wanakuwa gazetted, siyo siri.

Jaji Ndunguru: Nafikiri shahidi ajielekeze katika kujibu swali analoulizwa.

Tukiandika “mkwe” ukaletewa Gazette la Serikali utuonyeshe Waziri anayeitwa Mkwe, utaonyesha?

Tujielekeze kujibu maswali.

Lissu: Asante. Haya, waeleze Waheshimiwa Majaji, wasimamizi wa huo uchaguzi katika mamlaka za Serikali kama majiji, manispaa, wilaya na miji walikuwa akina nani?

Amani Sam Golugwa: Walikuwa Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa, Wilaya na Miji.

Lissu: Wasimamizi wa uchaguzi katika ngazi za Mitaa na Vijiji walikuwa akina nani?

Amani Sam Golugwa: Wasimamizi katika hizo ngazi walikuwa ni Watendaji wa Mitaa na Vijiji.

Lissu: Unasema Wakurugenzi ndiyo walisimamia katika hizo ngazi za halmashauri na majiji. Waeleze Waheshimiwa Majaji, hao Wakurugenzi ni wateule wa nani?

Amani Sam Golugwa: Hao Wakurugenzi ni wateule wa Rais, kwa maana wanateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, huyo Waziri aliyetunga kanuni ni mteule wa nani?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, Waziri aliyetunga kanuni hizi ni mteule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, na hiyo Wizara ya TAMISEMI ipo chini ya nani?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, wajibu, hiyo Wizara ya TAMISEMI ipo chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lissu: Kwenye ushahidi wako ulisema ulipeleka taarifa ya huo uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Katibu Mkuu na Makatibu wengine 09 wa kanda tofauti, hata kama ujumbe kwa njia tofauti tofauti.

Waeleze Waheshimiwa Majaji, huo unaouita ushenzi ulioona katika Serikali za Mitaa, waeleze Waheshimiwa Majaji kama vilevile umekuwepo katika uchaguzi Mkuu kwa ufahamu wako.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, mambo ya ovyo niliyoyaona katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa niliyaona pia katika uchaguzi Mkuu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama uliona mambo hayo ya ovyo katika uchaguzi Mkuu mmoja au katika chaguzi Kuu zote.

Amani Sam Golugwa: Kwa kipindi ambacho nimekuwa kiongozi wa Chama, nimeyaona mambo hayo kwenye uchaguzi wa mwaka 2020, na niliyaona kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, na niliyaona, nikashangaa na nikastaajabu mpaka nikaogopa kwenye matukio ya 2025.

Lissu: Kwenye tatizo la kwanza la wagombea kunyimwa fomu au kushindwa kurudisha fomu kwenye uchaguzi Mkuu, elezea kama umeliona katika uchaguzi Mkuu.

Amani Sam Golugwa: Nimeliona na nimelishuhudia swala la kunyimwa fomu katika uchaguzi Mkuu.

Au wanafunga milango, wanaondoka, wanaiacha ofisi.

Hivyo nimeshuhudia katika uchaguzi Mkuu wagombea kunyimwa fomu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, juu ya kuwepo kwa tatizo la wagombea kurudisha fomu.

Amani Sam Golugwa: Nimeliona na kushuhudia tatizo la kurudisha fomu.

Wagombea wanashindwa kurudisha fomu.

Lissu: Wagombea gani?

Amani Sam Golugwa: Wagombea wa Udiwani, Ubunge na Urais.

Wahusika kufunga ofisi ili wasitoe fomu, au anakuwepo lakini anakataa kupokea fomu.

Mbaya zaidi...

Lissu: Wewe unaiona hiyo timu hapo? We jiongeze tu.

MAHAKAMA KICHEKO.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji juu ya kuwepo kwa tatizo la kuenguliwa baada ya wagombea kuwa wamerudisha fomu.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wangu lipo tatizo la wagombea wanapokuwa wamewasilisha fomu kuenguliwa kwa sababu zingine zisizo na maana, nje ya zile sifa mahususi zilizoainishwa katika kanuni na sheria ya uchaguzi.

Kazi yako ni njema mkuu Manyanza
 
Halafu JamiiForums msiwe mnaunganisha nyuzi mnachanganya watu, wekeni live huu uzi
Hebu kwanza. Mbona sielewi?

Kwani utaratibu upoje hapa.
Mara nyingi nimekuwa nikiona maandishi ya mkuu 'Mawele'; halafu na mengine ya wewe mkuu 'Manyanza'
Wote mnafanya kazi nzuri ya kutoa taarifa za huko mahakamani kwa sisi tulio nje ya mahakama.

Sasa ninajaanza kuona hapa ni kama kuna mashindano kati ya waleta taarifa hizi?

Sioni sababu ya kuwalaumu watu wa JF. Sijui kama wanaunganisha au vipi. La muhimu kwetu sote ni taarifa za mahakamani zifike huku nje.

Hakuna ushindani hapa. Wote mnafanya kazi nzuri ya kuchangia mapambano.
 
Ripoti inayotolewa na 'Mawele', ambayo imefikia 332' inatiririka vizuri kabisa, sasa sijui tatizo lipo wapi hapa!
Mkuu nashindwa kuelewa mpaka sasa kwamba hujaona tatizo,najua wewe ni mtu makini sana

Maana kama umefuatilia uzi mambo yamefanunuliwa vizur sana kwanini uzi usiunganishwe

Au nawe siku hizi umeanza kucomment kama wale wanaosema "Sijasoma lakini najua uzi utakuwa unasema hivi"

SITAKI KUAMINI JUU YA HILI
 
Back
Top Bottom