TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 6.
MAENDELEO YA KESI – 02/09/2026
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, haya matatizo uliyoeleza yamekuwa yakiwakabili wagombea wa vyama vyote au wagombea fulani fulani tu?
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, matatizo haya yamekuwa yakiwakabili CHADEMA na vyama kadhaa vya upinzani.
Lissu: Ukisema vyama kadhaa, maana yake nini?
Amani Sam Golugwa: Kadhia hii imekuwa ikiwapata vyama vingine vya upinzani kama ACT na CUF. Kadhia hii haijawahi kukipata Chama cha Mapinduzi.
Lissu: Shahidi, kwa kuwa umekitaja Chama cha Mapinduzi, naomba uwaeleze Waheshimiwa Majaji kama umewahi kusikia mgombea yeyote wa CCM, awe wa kitongoji, kijiji, mtaa, udiwani, ubunge au urais, tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, kama amewahi kuondolewa katika uchaguzi.
Anasimama Job Mrema.
Job Mrema: Waheshimiwa Majaji, mshtakiwa Tundu Antipas Lissu haruhusiwi kumpeleka shahidi katika maswali ambayo yanampeleka katika majibu. Naomba hilo swali lisiingie.
Jaji Ndunguru: Haturekodi maswali, na halikuwa hajajibu.
Lissu: Naomba kurudia swali.
Lissu: Shahidi, tueleze kwa ufahamu wako kama unamfahamu mgombea yeyote wa CCM ambaye amewahi kuenguliwa, iwe katika kitongoji, kijiji, udiwani, ubunge au urais, tangu mwaka 1995 tulipoanza mfumo wa vyama vingi.
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wangu, sijawahi kusikia mgombea wa Chama cha Mapinduzi wa nafasi zote hizo kuenguliwa.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji ufahamu wako wa taarifa rasmi za chaguzi kuanzia mwaka 1995 mpaka 2020, kama umesoma hizo taarifa za Tume.
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wangu sijawahi kusoma kwenye tovuti ya Tume au hard copy kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji ufahamu wako kuhusu Tume ya Uchaguzi na hizi chaguzi za vyama vingi kuanzia mwaka 1995 hadi 2020.
Amani Sam Golugwa: Sijawahi kusoma kwenye tovuti ya Tume.
Jaji Ndunguru: Hatujakuelewa.
Lissu: Narudia swali. Jibu tena kwa makini.
Amani Sam Golugwa: Nazifahamu.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama hizo taarifa zimethibitisha kuhusu kuenguliwa kwa hao wagombea.
Amani Sam Golugwa: Nimekuwa nikisoma taarifa za Tume zikionyesha kwamba kuna tatizo la wagombea kuenguliwa.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, kuhusu taarifa za waangalizi wa ndani TEMCO.
Anasimama Job Mrema.
Job Mrema: Waheshimiwa Majaji, ukiangalia swali analoulizwa shahidi, inaonekana shahidi anapewa kwanza taarifa, halafu yeye ndiye anazielezea. Kwa kifupi, huyu shahidi hana content. Tuone, Waheshimiwa Majaji, Mahakama hii kwamba hii siyo sawa.
Lissu: Ni objection au ni leading question? Nitarudia, sitochoka kurudia.
Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji kama umesoma taarifa za uchaguzi za waangalizi wa ndani TEMCO.
Amani Sam Golugwa: Sijawahi kusoma ripoti ya TEMCO, ila nimewahi kumsikia Mwenyekiti Lissu akifafanua mada kuhusu TEMCO kama waangalizi wa ndani.
Lissu: Wewe hujawahi kusoma?
Amani Sam Golugwa: Sijawahi kusoma.
Lissu: Umewahi kusoma taarifa za watazamaji wa nje wa uchaguzi?
Amani Sam Golugwa: Nimesoma taarifa za watazamaji wa nje wa uchaguzi.
Lissu: Waeleze hizo ulizosoma.
Amani Sam Golugwa: Nimewahi kusoma taarifa ya waangalizi kutoka Afrika iliyoongozwa na Rais mstaafu wa Botswana, Masisi.
Nimesoma taarifa ya SADC ambayo iliongozwa na Spika mstaafu wa Malawi.
Nimesoma taarifa ya Jumuiya ya Ulaya ambayo iliongozwa na Mbunge kutoka Ulaya.
Nimesoma taarifa ya taasisi ya Thabo Mbeki.
Lissu: Hizo ulizosoma zilikuwa za uchaguzi gani?
Amani Sam Golugwa: Hizo nilizosoma ni za uchaguzi wa 2025.
Lissu: Hizo ulizosoma zinasemaje kuhusu mfumo wa uchaguzi wa Tanzania?
Tuanze na ripoti ya Umoja wa Afrika iliyoongozwa na Masisi.
Maana tukisema za Ulaya wataanza kusema, “Oooh, Wazungu hivi...”
Amani Sam Golugwa: Ilisema uchaguzi wa Tanzania hauna viwango na haujakidhi matakwa na miongozo ya kidemokrasia.
Pili, waangalizi walishuhudia vituoni wapiga kura wakipewa kura nyingi na wasimamizi wakiingiza kura kwenye masanduku ya kura nyingi.
Na hivyo kusema uchaguzi huo hauna uadilifu na haufai kuitwa uchaguzi.
Lissu: Asante.
Anasimama Wakili wa Serikali Ajuaye Zegeli.
Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu, tunaona muda umeisha. Kwa ridhaa yenu, tunaomba tuhairishe shauri mpaka kesho asubuhi ili tuweze kuendelea na kesi.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa?
Lissu: Niko sawa, Waheshimiwa Majaji, kuhairisha mpaka kesho.
Jaji Ndunguru: Basi, kwa maslahi ya muda, shauri linaahirishwa hadi kesho saa 3:00 asubuhi. Shahidi, utaendelea kuwa chini ya kiapo.
Amani Sam Golugwa: Asante.
MAJAJI WANATOKA.
Lissu: Kawambieni hao wanaochukua hela Lumumba, wanaosema kwamba nitakaa sana gerezani, waambieni nipo tayari kukaa hata miaka 10.
Hakuna kutembelewa gerezani usiku.
Kwanza, sijawahi kuwaona hata hapa Mahakamani.
Kama mtu ananipenda, aje Mahakamani hapa au afanye kazi ya chama.
WAACHE UJINGA.
Watu ukumbini wanampigia makofi Mwenyekiti Lissu kwa maneno hayo.
Asanteni kwa leo.
TUKUTANE KESHO ASUBUHI.