Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri - 2, Septemba 2026

Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri - 2, Septemba 2026

Tunakupenda wewe tuu uanzishe uzi au la kila mtu aanzishe wake na mods msiunganishe...
Yani inaboaga mtu anajua uzi ni wa ku update kila dkk halafu anaweka title na maneno machache anasepa....🫤🫤
Manyanza ametusaidia, kabla ya hapa tulikuwa tunazama X kwa Hilda, sasa Manyanza yupo haraka zaidi ya Hilda ndio maana tumezama humu. Ukilinganisha unaona tofauti ndogo sana jambo ambalo ni kawaida katika uandishi.
 
Payge JamiiForums Maxence Melo
celix
Reviser
Wand
Boqin
Payge
Zenora


HABARI WAKUU NA VIONGOZI WA JAMII FORUMS.

Naomba kuwasilisha ombi langu kwa heshima, lakini pia kwa msisitizo wa kutaka usawa na haki katika matumizi ya jukwaa hili.

Kuna jambo ambalo naomba viongozi wa JamiiForums mlitafakari kwa kina. Mtu ambaye hayupo eneo la tukio, wala hayupo mahakamani, anawezaje kupewa nafasi ya kuanzisha uzi wa “LIVE” na kuendelea kuutangaza, wakati mwingine ambaye yupo moja kwa moja eneo la tukio anazuiwa kufanya LIVE?
Kwa mfano, mtu akiwa Mbeya au sehemu nyingine, anaweza kuanzisha uzi unaosema “Mahakama Kuu Dar es Salaam LIVE” na kuendelea kutoa taarifa kupitia uzi huo, hata kama yeye mwenyewe hayupo mahakamani na hana uwezo wa kuthibitisha kinachoendelea kwa wakati huo. Wakati huo huo, mtu ambaye yupo ndani au karibu na eneo la tukio, anayeshuhudia kinachoendelea moja kwa moja, ananyimwa fursa ya kurusha taarifa LIVE.
Hapa ndipo tunapojiuliza: Je, kigezo cha kuruhusu LIVE ni nini?
Kama hoja ni kuhakikisha taarifa zinazotolewa ni sahihi, basi kimantiki mtu aliye eneo la tukio ana nafasi kubwa zaidi ya kutoa taarifa sahihi na za wakati huo kuliko mtu aliye mbali na eneo hilo.

Kama kuna kanuni au sababu za kiusalama, kisheria au za kiutendaji zinazozuia mtu aliyepo mahakamani kufanya LIVE, basi tunaomba kanuni hizo ziwekwe wazi na zitumike kwa usawa kwa kila mtu. Tusije tukawa na mazingira ambayo mtu mmoja anaruhusiwa kufanya jambo fulani kwa sababu hayupo eneo la tukio, lakini mwingine anayefanya jambo hilo akiwa eneo la tukio anazuiwa.
JamiiForums ni jukwaa kubwa la mijadala na taarifa. Kwa hiyo, tunatarajia misingi ya haki, uwazi, usawa na kanuni zinazofanana itumike kwa wanachama wote bila upendeleo.

Suala hapa si kumzuia mtu mwingine kutoa taarifa. Hoja yangu ni kwa nini anayetoa taarifa akiwa mbali na tukio apewe uhuru zaidi kuliko yule aliyepo kwenye tukio lenyewe?
Naomba viongozi wa JamiiForums mlitazame jambo hili kwa jicho la usawa na mlitafakari upya, kwa sababu kama lengo ni kupata taarifa za haraka na sahihi kutoka eneo la tukio, basi anayekuwa eneo hilo anapaswa angalau kuwa na nafasi sawa ya kutoa taarifa kama wengine.

Tunaomba usawa wa kanuni, uwazi wa vigezo na haki sawa kwa wanachama wote.
Asanteni.
Kuna watu waaanzisha threads ili kuvuruga utoaji wa taarifa kwa wengine mfano ni ndugu "mawele" katika kuripoti mwenendo wa kesi ya MK
Soyo vahati mbaya bali ni makusudi ni vyema JF ikaaangalia hambo hili
 
S
Mahakamani leo tena kesi inaendelea kwa Upande wa Mawakili wa Serikali kumuuliza Mswali ya Dodoso Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika


Pia soma: Kesi ya Uhaini: John Mnyika Kuendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri kuendelea leo 1, Septemba 2026

Leo September 2, 2026 Last time tuliishia sehemu 327 so leo tunaendelea na


Sehemu ya 328

Mahakama imeanza. Majaji wameingia.

Mh. Tundu Lissu ameingia na kupokolewa na Makofi mengi ya wahudhuriaji wa hapa Mahakamani.

Shahidi (DW 2) wa utetezi nae alifika mapema sana saa mbili kamili asubuhi.

Mh. John Mnyika. Mheshimiwa Tundu Lissu ameingia akiwa amepiga Kombati safi kabisa ya Kaki na vibe lake liko juu sana. Nywele zake naona zinaendelea kuwa ndefu siku hadi siku.

Karani anasoma namba ya kesi akiwa amekaa upande wa kulia kidogo na kushoto kwa majaji kwa mbele.

Anasimama Ajuaye anatambulisha Kikundi Cha Serikali cha siku zote. Anasema wako tayari kuendelea na Cross Examination.

Anasimama Job Mrema kwenda kuendelea na Maswali ya Dodoso.

Job Mrema: Anakumbushwa alipoishiwa. Anaendelea sasa. Utakubaliana na mimi kama inavyosomeka kwenye hati ya mashitaka kuhusu msimamo unaashiria uasi. Sasa matukio yaliyotokea Tar. 29/10/2025

Mnyika: Hayana uhusiano kabisa na Mshitakiwa yeye alikamatwa Tarehe 09/04 na mambo ya Uchaguzi yalitokea mshitakiwa akiwa jela siku nyingi. Uhusiano unatoka wapi?

Job Mrema: Chadema inaamini katika Demokrasia?

Mnyika: Sahihi.

Job Mrema: Inawezekana Mwenyekiti akatoa hotuba bila kukuhusisha wewe?

Mnyika: Hakuna yakunishirikisha mimi kwasababu No reforms, No Election ilishaamuliwa na vikao na wote tulikuwa tunajua nini maana ya No Reforms, No Election.

Jobe Mrema: Wewe Mnyika umewahi kufungua shauri la Kikatiba?

Mnyika: Sijawahi

Job Mrema: Je Mwenyekiti nae aliwahi kufungua kesi hiyo?

Mnyika: Hajawahi

Job Mrema: Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaweka misingi ya kisheria?

Mnyika: Ni sahihi pamoja na Mikataba ya Kimataifa.

Job Mrema: Unaamini mhimili wa Mahakama katika utoaji wa Haki?

Mnyika: Mhimili nauamini lakini nina shida na Majaji wanaotoa haki baadhi yao hawaaminiki kabisa.

Job Mrema: Kutokana na ushahidi wako kuhusiana na sheria kandamizi sasa ili sheria iweze kusemwa kuwa ni kandamizi ni lazima sheria hiyo isemwe na Mahakama?

Mnyika: Sio sahihi hata Mahakama imesema katika Kesi Na. 28/2018 ya Said Kubenea ilisema kuhusu masuala ya kisiasa yanapaswa kutatuliwa kisiasa sio lazima Mahakama iseme kuhusu jambo hilo.

Jaji Ndunguru: Hivi uliyeuliza swali maana yake ni nini? Unamaanisha nini?

Job Mrema: Nimemuuliza umewahi kufungua shauri la Kikatiba?

Mnyika: Sijawahi

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba kwa mujibu wa Sheria. Mahakama imetoa sheria ya kusikiliza mashauri ya Kikatiba?

Mnyika: Sahihi

Job Mrema: Namna pekee ambayo mtu ni mstaarabu na anajielewa asiporidhishwa njia bora ni kuiwasilisha jambo hilo Mahakamani?

Mnyika: Sikubaliani na wewe.

Job Mrema: Wakati Mshitakiwa anakuandaa alikwambia mambo gani?

Mnyika: Aliniambia kuhusu taratibu za Mahakama na kusikiliza maelekezo ya Majaji.

Job Mrema: UnamjuaIshengoma Mutembei Barongo ambae ni Katibu wa Chadema Mikocheni?

Mnyika: Simjui.

Job Mrema: Unajua kama Katibu Mkuu kuwa Ishengoma ni Katibu wa CHADEMA Mikocheni?

Mnyika: Hayo ni maoni yako mimi sifahamu? Na hii inafurahisha mawakili wa serikali ni watambuzi wa wanachama wa CHADEMA kuliko Katibu Mkuu wa Chadema.

Job Mrema: Makatibu wa Kata utaratibu wao wa kazi ni upi?

Mnyika: Ni wenyeviti wa Sekretarieti kwenye ngazi ya Kata na wanaripoti majukumu yao kwa viongozi wa Jimbo. Sio Mkoa wala Kanda.

Job Mrema: Ikitokea kuna ushahidi ukitolewa huoni kama kiti chako kitakuwa kwenye mashaka? Kwamba hata wanachama wako huujui.

Mnyika: Hilo sio miongoni mwa jambo linaloweza kukitia kwenye mashaka kiti cha Katibu Mkuu wa Chama. Chadema ina Makatibu wa Kata zaidi ya 1000.


Sehemu ya 329

Job Mrema: Ni sahihi ubaguzi ni kinyume na Katiba yetu ya Tanzania?

Mnyika: Ni sahihi.

Job Mrema: Yale makusanyo ya Tonetone kuna uamuzi ulifanyika kuwa kuna wachache wanufaike na wachache wasinufaike angali wengine wapo?

Mnyika: Sio Ubaguzi. Na ungetaka walipwe wote ukirudi ofisini mshauri Boss wako mwanasheria Mkuu wa Serikali alipe pesa zetu zaidi ya Milioni 400 ili tuwalipe wafanyakazi wetu wote. Hizo posho ni ndogo tu. Job

Mrema: Zaidi ya milioni 39 za Tonetone zimetolewa kati ya Tarehe 18 na 19 August 2026?

Mnyika: Hizo Habari nazisikia kutoka kwako.

Job Mrema: Ikitokea wanachama wa Chadema wamepata ushahidi wakasema kuna pesa zimetoka huoni kiti chako kitakuwa rehani?

Mnyika: Tutasubiri kuona kama kuna aliyeidhinisha pesa kutoka ni nani na kwa sababu gani?

Job Mrema: Kutoa pesa za Tonetone kwa mujibu wa ibara ya 4.1.2 ni kuwaonea?

Mnyika: Anaisoma hiyo ibara. Inasema kukandamiza watu kwa rangi, dini

Job Mrema: Ndio maana wengine hamkuwalipa?

Mnyika: Mimi Katibu Mkuu ndio ninayejua kwamba kwa hali tuliyonayo. Alipwe Mlinzi pekee. Kwasababu yeye yuko ofisini kila siku na sio mfanyakazi mwingine. Wewe unajua nini kuhusu haya mambo kuliko mimi?

Job Mrema: Ibara ya 3.2.4 inasema kama inavyosema hapo?

Mnyika: anaisoma na kusema inasema hivyo. Job Mrema: Sasa kama hizo fedha chache zimelipwa kwa ubaguzi unasemaje kuhusu hilo?

Mnyika: Sisi hatuna Ubaguzi wenye ubaguzi ni nyie Serikali ambao mmezuia fedha za Chadema. Ndio maana Chadema tunapambana fedha za umma zibaki salama.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kuwa ukiaminika kwa dogo utaaminika kwa kubwa?

Mnyika: Chadema inaaminika kwa dogo na kwa kubwa pia. Ndio maana watanzania wameendelea kuiunga mkono.


Sehemu ya 330

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu

John Mnyika.

Job Mrema: Huoni kwamba kwa uzoefu wa miaka 10 ya Kutunga Sheria huoni haujakitendea Haki Chadema kwa kutokishauri Chama cha Chadema kutumia Mahakama?

Mnyika: Nimekishauri vizuri kabisa chama. Tumekaa kwenye Maridhiano, tumeenda Bunge kupeleka maoni yetu kuhusu mabadiliko ya sheria hakuna lililofanyika. Mahakama kwenye kesi ya kubenea ilisema masuala ya kisiasa yatatuliwe kisiasa ndio maana tukaja na No Reforms: No Election.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kuwa Ishengoma ni Katibu wa Chadema?

Mnyika: Nitakubalianaje na jambo gani sasa ambalo silijui???

Job Mrema: Ni sahihi kuwa kwenye hiyo clip ya Bwana Mutembei alisema vurugu za Oktoba 29 zilipangwa na Chadema?

Mnyika: Nilikwambia hiyo Clip siijui, simjui Mutembei na hata hayo unayosema sio sahihi na sikubaliani na wewe kwa chochote kuhusu hilo.

Job Mrema: Mimi nimemaliza

Mheshimiwa Jaji. Anasimama

Ajuaye: Tumemaliza Jamhuri wote.

Jaji Ndunguru: Haya Utetezi vipi nafikiri re examination itakuwa fupi sana?

Tundu Lissu: Siwezi kuahidi kabisa ila nitasema yale ya muhimu tu ndio nitamuuliza.

Naomba nianze sasa.

Mhe. Lissu: Sasa umeulizwa sana kuhusu kifungu cha 7 kuhusu Sheria ya habari kisome na ujibu ulimaanisha nini?

Mnyika: Anakisoma na kusema hiyo sheria inawapa uhuru na haki ya kutafuta habari na baadae kuwa huru kuisambaza au kutoisambaza na kifungu hiki kinawafanya wanahabari kuwa wamiliki wa habari husika na sio mtu mwingine.

Mhe. Lissu: Umeulizwa kuhusu maneno yangu na uhusiano wa matukio ya October?

Mnyika: Maneno yalitolewa Tarehe 03/04 na mshitakiwa akakamatwa Tarehe 09/04 na matukio ya Oktoba yakaja kutokea Mshitakiwa akiwa yuko Mahabusu.

Anasimama Katuga: Mheshimiwa asiende mbali huko.

Jaji: Anayosema shahidi tulishayaandika kwahiyo hakuna shida.
Tundu Lissu: Uliulizwa kuhusu maana ya Uasi, sasa nakupa Kamusi ile ile usome.

Mnyika: Uasi ni kupinga mambo ndani ya taasisi au sheria kandamizi hiyo ndio maana ya kwanza.

Mhe. Lissu: Kwahiyo umeelewaje hapo?

Mnyika: Uasi sio tu kupinga serikali bali hata kwenye taasisi kupinga mifumo mibovu nao pia ni uasi.

Mhe. Lissu: Wamesema kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba haukuwa huru na haki?

Mnyika: Kuna ripoti mbalimbali zimesema ikiwemo Common wealth Anasimama

Katuga: Hizo ripoti naziogopa asiende huko hakuzitaja kabisa

Mhe. Lissu: Sasa ripoti zinawapa presha usiende huko.

Katuga: Sio Presha tu zinanipa hadi Kisukari.

Mnyika: Basi uchaguzi wa Oktoba haukuwa huru na haki na haukuwezesha watu kushiriki kwa uhuru na haki.

Mhe. Lissu: Kesi ya Mbowe ulisema ya uongo fafanua sasa licha ya kwamba alikutwa na kesi ya kujibu?

Mnyika: Hakukutwa na hatia ya ugaidi na kumekuwa na tabia ya kubambikwa kesi na kwa Mwenyekiti Mbowe kama Mtendaji mkuu wa Chama , najua hakuwahi kupanga Ugaidi na Chama hakijawahi kuwa na Mipango hiyo.

Mhe. Lissu: Pia uliulizwa kama ni kweli alishitakiwa na watu wengine walikuwa ni Makomandoo wa Jeshi na ukasema walikuwa ni walinzi wake na wanaharakati pia.

Mnyika: Waliwahi kutumikia jeshi na kuondoka Jeshini na wakajiunga na harakati na Mwenyekiti akawapanga kuwa walinzi wake.

Katuga: Anasimama hili la kwamba walikuwa makomandoo wasiliseme kabisa.

Mhe. Lissu: Nawish nisiseme kuwa hii ni non sense, sitasema hivyo lakini sioni umaana wa hili swali. Lazima ufafanuzi ufanyike na huwezi kumtisha mtu kuwa utafanya cross sasa cross gani utafanya hapa?

Katuga: this court is not your mother

Mhe. Lissu: It is not your mother either. Wewe nani kakudanganya hii Mahakama ni Mama ako?

Jaji Ndunguru. Sasa Shahidi aulizwe swali tumuache ajibu.


Sehemu ya 331

Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Re-Examination Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika

Mhe. Lissu: Mwenyekiti Mbowe alishitakiwa na watu wengine na ukasema walikuwa ni walinzi wake na wanaharakati? Fafanua.

Mnyika: Walikuwa Makomando zamani, wakawa walinzi wa Mbowe na kwa kuwa mlinzi wa Mwenyekiti walikuwa wanafanya kazi ya harakati na wakawa wanaharakati.

Katuga anachekacheka.

Jaji anamuuliza vipi?

Katuga: Majibu yalikuwa sahihi kabisa ya awali.

Mhe. Lissu: Mheshimiwa mimi siwezi kuwachukulia poa vichekocheko vya watu walionishitaki kwa Uhaini.

Jaji: Tuendelee

Mhe. Lissu: Kuvitishia vyombo vya ulinzi na Rais ukasema Mshitakiwa hakufanya hivyo fafanua?

Mnyika: Hakuna mahali kokote mshitakiwa alimtishia Rais wala Serikali hakuna alipotaja watu hao na vyombo hivyo.

Mhe, Lissu: Ulitaja kesi nyingi na kusema kesi zote zilikuwa za uongo?

Mnyika: zilifutwa kwasababu hakuna ushahidi uliowasilishwa Mahakamani na zilifutwa kwasababu za uongo na hakuna aliyekutwa na hatia.

Mhe. Lissu: Umeulizwa Maswali kuhusu Hotuba ya Jaji Chande kuhusiana na matukio ya Oktoba na Siku zilizofuata. Ulisema inatofautiana na Hotuba yangu?

Mnyika: Hotuba yako ilikuwa inahusu msimamo wa No Reforms: No Election na Chande alikuwa anazungumzia mambo tofauti kabisa.

Mh. Lissu anaendelea na Maswali Msawazo, Maswali Fukia Mashimo, Maswali Sawazisha. A.K.A Rejoinder kwa kitaalamu.

Mhe. Lissu: Shahidi uliulizwa kuhusiana na Hotuba Yangu na ueleze kama ulisema ni sahihi au sio sahihi kama lengo la Hotuba yangu lilikuwa ni kuishinikiza Serikali? Ukasema Hapana.

Mnyika: Lengo lilikuwa ni kuwaunganisha watanzania na wadau mpaka serikali ikubali kuwezesha uchaguzi huru na haki na wasipokubali msimamo wa No Reforms: No Election.

Mhe. Lissu: Ulisema mliendelea na harakati hadi Tarehe 09/06 ulimaanisha nini?

Mnyika: Tarehe 10/06 Mahakama ilitoa zuio la kufanya shughuli za kisiasa na kuzuia matumizi ya mali za Chama. Hadi Tar. 15/04/2026. Ambapo ni baada ya Uchaguzi kabisa. Ni siku 309 tulizuiwa kutumia chochote kile.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuwa uasi ni njia ya Kidemokrasia naomba fafanua maana yake?

Mnyika: Uasi ni kupinga au kukataa kwa nguvu kubwa na hizo njia za kidemokrasia kwa kutumia kufanya mikutano, kufanya vikao hizo zote ni haki za kisiasa. Haiwezi kuwa ni kosa zilizopo kwenyw sheria ya vyama vya siasa na Katiba ya nchi na mikataba ya kimataifa imeridhia.

Mhe. Lissu: Umemaliza kuelezea hapo?

Mnyika: Hapo tayari. Tuendeleee sasa.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuwa Chama chako kilikuwa kilishajiandaa kushiriki uchaguzi wa mwaka jana?

Mnyika: Katika Mkutano wa Tarehe 21/01 uliopitisha No Reforms No Election .......

Mhe. Lissu: Angalia usifike mbali watasimama hao.

Mnyika: Tulijiandaa kuruhusu watia kuelezea nia zao na pia kungomesha Chama.

Mhe.Lissu: Katuga alikwambia kuhamasisha uasi ni kosa? Ukamjibu kuwa Mwalimu Nyerere alisema tunahitaji vijana waasi wa mifumo kandamizi.

Mnyika: Maneno ya uasi yana tafsiri ya ziada ambayo ilitumika na mwalimu nyerere na halikuwa kosa la uhaini wala kosa lolote. Hakuwahi kushitakiwa hadi leo. Haliwezi kuwa neno sahihi kutumika na Nyerere halafu likawa baya kutumika na Tundu Lissu.

Mhe. Lissu: Uliulizwa pia kwamba huo Mkutano ulikuwa na Mwenyekiti au vipi? Fafanua.

Mnyika: Yes niliwaambia haukuwa na Mwenyekiti wa Mkutano na mikutano kama hiyo huwa haina minutes. Inakuwa na taarifa tu ya namna ulivyofanyika. Mimi ndio nilikuwa msimamizi mkuu wa huo mkutano.


Sehemu ya 332

Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Re-Examination Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu namna mtandao wa Jambo ulivyorushwa hayo matangazo na ukasema uamuzi wa kurusha Matangazo ulikuwa sio uamuzi wenu bali wa wale waandishi?

Katuga: Hatujaelewa swali?

Jaji Ndunguru: Hebu rudia aelewa swali.

Jaji Kareyamaha: Sisi tumeandika kuwa shahidi alisema suala la kuchapisha ni uamuzi wao wenyewe hakuna anayewalazimisha?

Mhe.,Lissu: Kumbe mnaandika vizuri kabisa proceedings. Basi hapo twende. Mimi nashitakiwa na uhaini sina haraka ya chochote.

Mhe. Lissu: Sasa uliulizwa kuhusu wakurugenzi kusimamia uchaguzi. Ukasema utaratibu umekuwa mbaya zaidi kwenye sheria mpya iliyowafanyia marekebisho. Hebu fafanua.

Katuga: Hilo hatukuuliza.

Mhe. Lissu: Tusomeee. Proceedings hapo Jaji. Zinasomwa na Lissu anasema sasa, ulisema hukutoa maoni yote ya mabadiliko ya Katiba kwenye ile kamati ya Katiba na Sheria. Hebu fafanua.

Mnyika: Maoni yote ya kutaka kurekebisha Katiba mathalani ya matokeo ya Urais kupingwa mahakamani, muundo wa tume huru yalikataliwa na mara zote kipaza sauti kilikuwa kinazimwa na hatukuruhusiwa kuyasema na walisema hayataingia kwenye rekodi.

Mhe. Lissu: Uliulizwa baada ya maoni yenu kukataliwa huko Bungeni ndio mkarudi kwenye mkakati wenu wa kuzuia Uchaguzi na ukasema hapana ulikuwa ni mkakati wa Chadema toka Tar. 03/12 fafanua.

Mnyika: Uamuzi wa No Reforns No Election ulifanyika toka mwezi december kwahiyo uhamasishaji wa wananchi dhdi ya uasi kwa mifumo kandamizi ulianza toka mwezi December, 2024. Haukutokana kabisa na maoni kukataliwa ulikuwa ni uamuzi endelevu hadi mabadiliko yatakapopatikana.

Mhe. Lissu: Ahsante. Ulisema hukupiga kura kwasababu hakukuwa na uchaguzi, ulikuwa na maana gani?

Mnyika: Hakukuwa na Uchaguzi huru, Haki na Halali. Chama kilifungiwa, hakikushiriki huo uchaguzi na mazingira hayakuwa ya haki. Sasa kuna uchaguzi gani hapo? Nisingeweza nikiwa kama Katibu Mkuu wa Chama kushiriki uchaguzi wa aina hiyo.

Mhe. Lissu: Uliulizwa kama nina nina kinga yoyote ya kushitakiwa kama nikivunja sheria na ukasema sina hatia yoyote. Ulikuwa unaendelea hapo na ukaweka lakini sasa....

Katuga: Waheshimiwa hakukuwa na lakini aliishia hapo.

Mhe. Lissu: Sasa nisomewe record tafadhali. Mimi sijaja hapa kumsikiliza kila anachosema Wakili wa Serikali. Majaji wanatafuta. Wanasema hebu jibu Shahidi tuone.

Mnyika: Nilisema hana kinga kwasababu mara zote amekuwa akishitakiwa na hajawahi kukutwa na hatia yoyote.

Mhe. Lissu: Ulisema kuwa Katibu Mkuu ni mteuliwa wa Baraza Kuu la Chama na sio Mwenyekiti? Fafanua.

Mnyika: Ni sahihi Katibu Mkuu anapendekezwa na Mwenyekiti lakini anathibitishwa na Baraza Kuu. Hilo Baraza Kuu linaweza kumkataa au kumkubalia. Na utendaji wa Katibu Mkuu anawajibika kwa Kamati Kuu na Baraza Kuu na sio kwa Mwenyekiti. Mwenyekiti wanashauriana tu.

Mhe. Lissu: Ulisomewa Katiba ya Chadema ibara ya 4.1.1 na kuulizwa kuwa lengo la Chadema ni kushika Dola na ukasema ndio na sio lengo pekee na muhimu zaidi?

Mnyika: Nilikuwa na maana kuwa kushika dola sio lengo pekee. Yako malengo ya kijamii, kisiasa na yote hayo ni malengo ya Chadema ba huwezi kusema lengo fulani ni muhimu kuliko mengine. Ikiwemo kutetea mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeiridhia kilele kikiwa ni kuleta demokrasia, uhuru na maendeleo ya watu.

Mh. Lissu: Waheshimiwa Majaji sina maswali zaidi ya Re Examination.

Jaji Ndunguru: Sasa Shahidi tunakuruhusu ukaendleee na majukumu mengine.

Mnyika: Ahsanteni na Mungu awabariki sana. Tunaahirisha kwa muda wa lisaa na nusu.

Na upate muda wa kuandaaa mashahidi wako pia.

Tukutane saa nane nusu.

Safi sana.Mungu ibariki CHADEMA na watu wake.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI.

KESI INAREJEA TENA

1. Majaji wanaingia pamoja na Lissu kwa wakati mmoja.

2. Mawakili wa Serikali nao wapo tayari.

3. Ukumbini ameingia Amani Sam Golugwa, amependeza katika uniform za kaki, na amekaa jirani na kizimba. Huenda akawa ndiye shahidi wa tatu wa upande wa utetezi.

4. Watu wamerejea mahakamani/ukumbini.

MAHAKAMA IPO KIMYA KWA MUDA

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu, kolamu ipo vilevile.

Shauri linakuja kuendelea kwa upande wa utetezi kujitetea, na upande wa mashitaka tupo tayari kuendelea.

Jaji Ndunguru: Upande wa mshtakiwa...?

Lissu: Waheshimiwa Majaji, na mimi nipo tayari kuendelea.

Naomba kuita shahidi wangu wa tatu, anaitwa Amani Sam Golugwa.

Amani Golugwa anasimama.

Jaji Ndunguru: Tutajie majina yako.

Amani Sam Golugwa: Amani Sam Golugwa.

Jaji Ndunguru: Umri wako?

Amani Sam Golugwa: Miaka 49.

Jaji Ndunguru: Unaishi wapi?

Amani Sam Golugwa: Naishi Goba.

Jaji Ndunguru: Shughuli yako?

Amani Sam Golugwa: Mimi ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara.

Jaji Ndunguru: Dini yako?

Amani Sam Golugwa: Mkristo.

Shahidi anaapa.

“Mimi, Amani Sam Golugwa, naapa mbele ya Mahakama hii tukufu ya kwamba ushahidi nitakaoutoa utakuwa wa kweli, ukweli mtupu; Mwenyezi Mungu nisaidie.”

Jaji Ndunguru: Utamuongoza au atajiongoza?

Lissu: Nitamuongoza, hawa waliobaki hawana mambo mengi sana.

Jaji Ndunguru: Lakini ni mengi.

Lissu: Waambie Waheshimiwa Majaji umekuwa Naibu Katibu Mkuu tangu lini.

Amani Sam Golugwa: Tangu 22 Januari 2025.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kabla ya kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara ulikuwa na nafasi gani?

Amani Sam Golugwa: Nimekuwa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Februari 2013 mpaka nilipothibitishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.

Lissu: Unaposema Kanda ya Kaskazini unamaanisha nini?

Amani Sam Golugwa: Ninaposema Kanda ya Kaskazini namaanisha mikoa minne: Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Hiyo ndiyo inaunda Kanda ya Kaskazini kwa muundo wetu wa kichama.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kabla ya kuwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini ulikuwa na nafasi gani?

Amani Sam Golugwa: Nimeshika pia nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, kutoka 2014 mpaka 2019.

Waheshimiwa Majaji, kabla ya hapo, kutoka 2008 mpaka 2014, nilikuwa Katibu wa Mkoa wa Arusha wa CHADEMA.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kuna nafasi nyingine yoyote ya kichama ambayo umewahi kushikilia, kama umeitaja.

Amani Sam Golugwa: Mwaka 2020 niliteuliwa na Chama kuwa Meneja wa Kampeni wa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu.

Lissu: Nilikuwa nakuita Mnikulu.

Sasa tukimalizie hii sehemu ya chama. Waeleze Waheshimiwa Majaji, umekuwa ndani ya hiki chama kwa muda gani?

Amani Sam Golugwa: Nimeingia toka mwaka 2007 mpaka leo nimekuwa mwanachama wa chama hiki.

Lissu: Naomba uwaeleze Waheshimiwa Majaji, mtu anapataje nafasi ya Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara?

Amani Sam Golugwa: Ili mtu aweze kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara CHADEMA, mbali na uanachama wake unaoaminika, jina lake litapendekezwa na Mwenyekiti wa Chama.

Mwenyekiti atatafuta miongoni mwa wanachama mtu mwenye uwezo na atapendekeza mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Chama.

Mwenyekiti atapeleka jina moja alilolichagua miongoni mwa wengi.

Kisha wajumbe wa Baraza Kuu watafanya wajibu wao wa kuthibitisha hilo jina baada ya kusikia wasifu na uwezo wa huyo mwanachama aliyependekezwa.

Lissu: Sasa shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji majukumu ya Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, wajibu wa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA:

Kwanza ni msaidizi wa Katibu Mkuu (anamsaidia Katibu Mkuu).

Ndiyo mwandishi wa kumbukumbu za vikao vya chama.

Tatu, Naibu Katibu Mkuu amepewa wajibu katika Mwongozo wa Itifaki ya Chama kwamba ndiye Mkuu na Msimamizi wa Itifaki katika vikao na mikutano ya Chama.

Lissu: Tuache hayo ya wasifu kichama kidogo. Waeleze Waheshimiwa Majaji wasifu wako wa kitaaluma.

Wewe una taaluma gani?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, elimu yangu ya chuo nimesoma masuala ya uhasibu.

Lissu: Umesoma uhasibu chuo gani?

Amani Sam Golugwa: Nimesoma Chuo cha Uhasibu Arusha, Stashahada ya Udhamiri katika Uhasibu.

Lissu: Stashahada ya Udhamiri inaitwaje kwa Kiingereza?

Amani Sam Golugwa: Ni Post Graduate Diploma.

Lissu: Nasikia kuna makelele ya fedha katika chama. Nataka uwaeleze Majaji uzoefu wako wa masuala ya fedha.

Amani Sam Golugwa: Nimefanya kazi ya uhasibu toka mwaka 2001 mpaka 2015 kwenye maeneo tofauti tofauti.

Lissu: Shahidi, nataka sasa tuzungumze hii kesi ya uhaini inayonikabili na ambayo nimekuita uje utoe ushahidi wa utetezi.

Ninatuhumiwa kwamba kwenye mkutano uliofanyika 3 Aprili mwaka jana, nilitoa maneno yenye nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, na hayo maneno yanasema hivi:

“Wanasema kitu kimoja sahihi hapa; wanasema hivi, msimamo huu unaashiria uasi. Ni kweli, msimamo huu unaashiria uasi...

Huu uchaguzi tutausimamisha, tutausimamisha kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana.”

Waeleze Waheshimiwa Majaji kama huu mkutano unaufahamu.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, huo mkutano nina ufahamu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, huo mkutano uliandaliwa na nani na ulifanyikia wapi?

Amani Sam Golugwa: Huu mkutano uliandaliwa na Chama baada ya Katibu Mkuu kuleta wazo kwenye Sekretarieti kwamba watia nia ni wadau muhimu, hivyo tuandae mkutano kukutana nao.

Na Sekretarieti ikafanya maandalizi, na mkutano ukafanyika kwenye ukumbi wa makao makuu ya Chama, Mikocheni.

Lissu: Hiyo Sekretarieti inaundwa na akina nani?

Amani Sam Golugwa: Hii Sekretarieti ninayoizungumzia ni:

Katibu Mkuu wa Chama.

Manaibu Katibu Wakuu wawili, kwa maana ya Bara na Zanzibar.

Makatibu wa Mabaraza ya Chama (Vijana, Wanawake na Wazee).

Wakurugenzi wa Kurugenzi za Chama (Directorates).

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, sijui nitaje Wakurugenzi wenyewe?

Lissu: Mimi ndiyo nakuuliza swali, usininyang’anye haki yangu. Taja wengine.

Amani Sam Golugwa: Na wataalamu wanaoteuliwa na Mwenyekiti.

Lissu: Jumla ni watu wangapi?

Amani Sam Golugwa: (Anahesabu.)

Kumi na nne.

Lissu: Kwa mujibu wa Muundo wa CHADEMA, Sekretarieti ni kitu gani?

Amani Sam Golugwa: Sekretarieti ndiyo chombo cha utendaji kinachofanya kazi za kila siku za Chama kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 2.

Lissu: Sasa unasema kwamba Katibu Mkuu alikuja na wazo la kwamba muandae mkutano wa wadau muhimu, watia nia.

Watia nia ni akina nani?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, watia nia ni wanachama wa CHADEMA ambao aidha walipitishwa na kuwa wagombea kwenye uchaguzi wa 2020 katika nafasi za udiwani, ubunge na urais, na kwamba bado nia yao ya kutaka kugombea nafasi hizo bado walikuwa nayo.

Na wengine katika kundi hilo la watia nia ni wale ambao hawajawahi kupitishwa wala kugombea nafasi hizo nilizotaja (fresh kabisa).

Na hivyo, 2025 walikuwa na nia na wao wagombee kupitia CHADEMA, waombe nafasi ndani ya Chama na wapitishwe kuwa wagombea wa ubunge, udiwani na urais.

Hao ndiyo watia nia.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji hao watia nia walikuwa na nia ya kugombea uchaguzi gani?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hawa watia nia walikuwa na nia ya kugombea katika uchaguzi wa 2025.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, lengo la kuwaita hao watia nia kuja katika mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025 lilikuwa ni lengo gani?

Amani Sam Golugwa: Lengo lilikuwa ni kuwaeleza na kuwafafanulia juu ya msimamo wa Chama uliopitishwa na Mkutano Mkuu, kwa maana ya wazo la “No Reform, No Election”, na msimamo huo ukawa umefafanuliwa na Kamati Kuu ya Chama kwa kuazimiwa.

Hilo ndiyo lilikuwa lengo la kuwaeleza na kuwafafanulia lengo na “No Reform, No Election.”

Lissu: Huu msimamo wa “No Reform, No Election” ulikuwa unahusu nini hasa? Naomba ufafanuzi.

Amani Sam Golugwa: Msimamo huu ulianza au ulizaliwa baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.

Nikiwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini, Katibu Mkuu alituambia makatibu wa kanda tuandike ripoti ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa jinsi ulivyofanyika.

Na mimi kama mtendaji ambaye nilikuwa sehemu ya uchaguzi huo, kwa kusimamia Kanda ya Kaskazini, nilitoa ripoti yenye kuonyesha madudu mengi ya ovyo yaliyojitokeza.

Na Katibu Mkuu alitutaka makatibu wa kanda tuandike maoni yetu kuhusiana na yaliyotokea ambayo tuliona ya ovyo yaliyojitokeza.

Mimi kwenye ripoti niliandika:

“Naomba Waheshimiwa Majaji niseme katika ripoti niliyomtumia Katibu Mkuu nilitumia maneno makali.

Niliandika hivi:

‘Kwa ushenzi huu nilioona, Chama kisishiriki uchaguzi mwingine wowote, uchaguzi mwingine wowote, bila kushinikiza mabadiliko ya kiuchaguzi.’”

Mimi na makatibu wenzangu, kila mmoja kwa lugha yake, tulitoa pendekezo linalofanana.

Nikachakata mapendekezo ya makatibu wa kanda, na wajumbe wenyewe wa Kamati Kuu wakajadili na kutafakari kwa jinsi wanavyojua.

Nasi tarehe 10 mwezi wa Desemba, Mwenyekiti wa Chama kipindi hicho, Mheshimiwa Freeman Mbowe, akatoa tamko rasmi la Chama.

Msimamo wa Kamati Kuu uliazimiwa kwamba hatutakuwa tayari kwenda kwenye uchaguzi mwingine wowote bila ya mabadiliko ya Kikatiba na kisheria.

Akasema kwa Kiingereza, “No Reform, No Election.”


WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Back
Top Bottom