TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 7.
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka, kuna lolote hapo?
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, hili jibu ni tofauti na la kwanza. Hapakuwa na haja ya ufafanuzi.
Jaji Ndunguru: Ndiyo maana nasema tujikite kwenye yale yaliyozungumzwa tu, na tukifanya hivyo hakuna matatizo.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, nitashangaa Wakili wa Serikali kaka ataniunga mkono kwa lolote. Huyu anataka ninyongwe, hawezi kunitakia jema.
Lissu: Shahidi, uliulizwa kama kutishia vyombo vya dola ni kumtishia Rais au walinzi wa amani.
Mnyika: Ili tishio limlenge Rais au mlinzi wa amani, lazima limlenge Rais au mlinzi wa amani. Matishio mengine ya uhalifu hayamlengi Rais wala mlinzi wa amani.
Lissu: Asante.
Uliulizwa kama unajua kesi inaamriwa kwa ushahidi. Ukasema kesi zote zilifutwa kwa sababu ni za uongo na kubambikiza. Hebu fafanua jibu lako.
Mnyika: Kesi zilifutwa kwa sababu hazikuwa na ushahidi wa maana, kwa hiyo zilikuwa za uongo.
Lissu: Ukaulizwa kama umesikia hotuba ya Jaji Chande, ukasema umemsikia.
Ukaulizwa kama umesikia Jaji Chande kwamba baadhi ya matukio yaliratibiwa na wanasiasa.
Ukaulizwa kama inahusiana na hotuba yangu ya tarehe 03 Aprili 2025. Hebu fafanua.
Mnyika: Hakuna uhusiano wowote na hotuba ya Jaji Chande. Wewe ulitoa hotuba tarehe 03 Aprili 2025...
Nassoro Katuga: Hapakuwa na swali la namna hiyo. Lengo la swali halikuwa linahusu hotuba nzima; ni kipande cha maneno kuhusu hotuba ya Mwenyekiti kuzuia uchaguzi na hotuba ya Jaji Chande vinafanana au havifanani.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, mimi natumia notisi zilizoandikwa mwenyewe. Naomba nisomewe na Mahakama hayo maswali yanayohusiana na Jaji Chande.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI