Expensive life
JF-Expert Member
- May 2, 2020
- 4,095
- 13,016
Sema hii combination ya lissu na mnyika 🔥
Kumbe Ishengoma ni mchezo wa kubuni ili kutoa backup kwenye hii Kesi?😂Mahakamani leo tena kesi inaendelea kwa Upande wa Mawakili wa Serikali kumuuliza Mswali ya Dodoso Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika
Pia soma: Kesi ya Uhaini: John Mnyika Kuendelea kumtetea Tundu Lissu Mahakamani. Maswali ya Dodoso kutoka Jamhuri kuendelea leo 1, Septemba 2026
Leo September 2, 2026 Last time tuliishia sehemu 327 so leo tunaendelea na
Sehemu ya 328
Mahakama imeanza. Majaji wameingia.
Mh. Tundu Lissu ameingia na kupokolewa na Makofi mengi ya wahudhuriaji wa hapa Mahakamani.
Shahidi (DW 2) wa utetezi nae alifika mapema sana saa mbili kamili asubuhi.
Mh. John Mnyika. Mheshimiwa Tundu Lissu ameingia akiwa amepiga Kombati safi kabisa ya Kaki na vibe lake liko juu sana. Nywele zake naona zinaendelea kuwa ndefu siku hadi siku.
Karani anasoma namba ya kesi akiwa amekaa upande wa kulia kidogo na kushoto kwa majaji kwa mbele.
Anasimama Ajuaye anatambulisha Kikundi Cha Serikali cha siku zote. Anasema wako tayari kuendelea na Cross Examination.
Anasimama Job Mrema kwenda kuendelea na Maswali ya Dodoso.
Job Mrema: Anakumbushwa alipoishiwa. Anaendelea sasa. Utakubaliana na mimi kama inavyosomeka kwenye hati ya mashitaka kuhusu msimamo unaashiria uasi. Sasa matukio yaliyotokea Tar. 29/10/2025
Mnyika: Hayana uhusiano kabisa na Mshitakiwa yeye alikamatwa Tarehe 09/04 na mambo ya Uchaguzi yalitokea mshitakiwa akiwa jela siku nyingi. Uhusiano unatoka wapi?
Job Mrema: Chadema inaamini katika Demokrasia?
Mnyika: Sahihi.
Job Mrema: Inawezekana Mwenyekiti akatoa hotuba bila kukuhusisha wewe?
Mnyika: Hakuna yakunishirikisha mimi kwasababu No reforms, No Election ilishaamuliwa na vikao na wote tulikuwa tunajua nini maana ya No Reforms, No Election.
Jobe Mrema: Wewe Mnyika umewahi kufungua shauri la Kikatiba?
Mnyika: Sijawahi
Job Mrema: Je Mwenyekiti nae aliwahi kufungua kesi hiyo?
Mnyika: Hajawahi
Job Mrema: Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaweka misingi ya kisheria?
Mnyika: Ni sahihi pamoja na Mikataba ya Kimataifa.
Job Mrema: Unaamini mhimili wa Mahakama katika utoaji wa Haki?
Mnyika: Mhimili nauamini lakini nina shida na Majaji wanaotoa haki baadhi yao hawaaminiki kabisa.
Job Mrema: Kutokana na ushahidi wako kuhusiana na sheria kandamizi sasa ili sheria iweze kusemwa kuwa ni kandamizi ni lazima sheria hiyo isemwe na Mahakama?
Mnyika: Sio sahihi hata Mahakama imesema katika Kesi Na. 28/2018 ya Said Kubenea ilisema kuhusu masuala ya kisiasa yanapaswa kutatuliwa kisiasa sio lazima Mahakama iseme kuhusu jambo hilo.
Jaji Ndunguru: Hivi uliyeuliza swali maana yake ni nini? Unamaanisha nini?
Job Mrema: Nimemuuliza umewahi kufungua shauri la Kikatiba?
Mnyika: Sijawahi
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba kwa mujibu wa Sheria. Mahakama imetoa sheria ya kusikiliza mashauri ya Kikatiba?
Mnyika: Sahihi
Job Mrema: Namna pekee ambayo mtu ni mstaarabu na anajielewa asiporidhishwa njia bora ni kuiwasilisha jambo hilo Mahakamani?
Mnyika: Sikubaliani na wewe.
Job Mrema: Wakati Mshitakiwa anakuandaa alikwambia mambo gani?
Mnyika: Aliniambia kuhusu taratibu za Mahakama na kusikiliza maelekezo ya Majaji.
Job Mrema: UnamjuaIshengoma Mutembei Barongo ambae ni Katibu wa Chadema Mikocheni?
Mnyika: Simjui.
Job Mrema: Unajua kama Katibu Mkuu kuwa Ishengoma ni Katibu wa CHADEMA Mikocheni?
Mnyika: Hayo ni maoni yako mimi sifahamu? Na hii inafurahisha mawakili wa serikali ni watambuzi wa wanachama wa CHADEMA kuliko Katibu Mkuu wa Chadema.
Job Mrema: Makatibu wa Kata utaratibu wao wa kazi ni upi?
Mnyika: Ni wenyeviti wa Sekretarieti kwenye ngazi ya Kata na wanaripoti majukumu yao kwa viongozi wa Jimbo. Sio Mkoa wala Kanda.
Job Mrema: Ikitokea kuna ushahidi ukitolewa huoni kama kiti chako kitakuwa kwenye mashaka? Kwamba hata wanachama wako huujui.
Mnyika: Hilo sio miongoni mwa jambo linaloweza kukitia kwenye mashaka kiti cha Katibu Mkuu wa Chama. Chadema ina Makatibu wa Kata zaidi ya 1000.
Sehemu ya 329
Job Mrema: Ni sahihi ubaguzi ni kinyume na Katiba yetu ya Tanzania?
Mnyika: Ni sahihi.
Job Mrema: Yale makusanyo ya Tonetone kuna uamuzi ulifanyika kuwa kuna wachache wanufaike na wachache wasinufaike angali wengine wapo?
Mnyika: Sio Ubaguzi. Na ungetaka walipwe wote ukirudi ofisini mshauri Boss wako mwanasheria Mkuu wa Serikali alipe pesa zetu zaidi ya Milioni 400 ili tuwalipe wafanyakazi wetu wote. Hizo posho ni ndogo tu. Job
Mrema: Zaidi ya milioni 39 za Tonetone zimetolewa kati ya Tarehe 18 na 19 August 2026?
Mnyika: Hizo Habari nazisikia kutoka kwako.
Job Mrema: Ikitokea wanachama wa Chadema wamepata ushahidi wakasema kuna pesa zimetoka huoni kiti chako kitakuwa rehani?
Mnyika: Tutasubiri kuona kama kuna aliyeidhinisha pesa kutoka ni nani na kwa sababu gani?
Job Mrema: Kutoa pesa za Tonetone kwa mujibu wa ibara ya 4.1.2 ni kuwaonea?
Mnyika: Anaisoma hiyo ibara. Inasema kukandamiza watu kwa rangi, dini
Job Mrema: Ndio maana wengine hamkuwalipa?
Mnyika: Mimi Katibu Mkuu ndio ninayejua kwamba kwa hali tuliyonayo. Alipwe Mlinzi pekee. Kwasababu yeye yuko ofisini kila siku na sio mfanyakazi mwingine. Wewe unajua nini kuhusu haya mambo kuliko mimi?
Job Mrema: Ibara ya 3.2.4 inasema kama inavyosema hapo?
Mnyika: anaisoma na kusema inasema hivyo. Job Mrema: Sasa kama hizo fedha chache zimelipwa kwa ubaguzi unasemaje kuhusu hilo?
Mnyika: Sisi hatuna Ubaguzi wenye ubaguzi ni nyie Serikali ambao mmezuia fedha za Chadema. Ndio maana Chadema tunapambana fedha za umma zibaki salama.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kuwa ukiaminika kwa dogo utaaminika kwa kubwa?
Mnyika: Chadema inaaminika kwa dogo na kwa kubwa pia. Ndio maana watanzania wameendelea kuiunga mkono.
Sehemu ya 330
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu
John Mnyika.
Job Mrema: Huoni kwamba kwa uzoefu wa miaka 10 ya Kutunga Sheria huoni haujakitendea Haki Chadema kwa kutokishauri Chama cha Chadema kutumia Mahakama?
Mnyika: Nimekishauri vizuri kabisa chama. Tumekaa kwenye Maridhiano, tumeenda Bunge kupeleka maoni yetu kuhusu mabadiliko ya sheria hakuna lililofanyika. Mahakama kwenye kesi ya kubenea ilisema masuala ya kisiasa yatatuliwe kisiasa ndio maana tukaja na No Reforms: No Election.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kuwa Ishengoma ni Katibu wa Chadema?
Mnyika: Nitakubalianaje na jambo gani sasa ambalo silijui???
Job Mrema: Ni sahihi kuwa kwenye hiyo clip ya Bwana Mutembei alisema vurugu za Oktoba 29 zilipangwa na Chadema?
Mnyika: Nilikwambia hiyo Clip siijui, simjui Mutembei na hata hayo unayosema sio sahihi na sikubaliani na wewe kwa chochote kuhusu hilo.
Job Mrema: Mimi nimemaliza
Mheshimiwa Jaji. Anasimama
Ajuaye: Tumemaliza Jamhuri wote.
Jaji Ndunguru: Haya Utetezi vipi nafikiri re examination itakuwa fupi sana?
Tundu Lissu: Siwezi kuahidi kabisa ila nitasema yale ya muhimu tu ndio nitamuuliza.
Naomba nianze sasa.
Mhe. Lissu: Sasa umeulizwa sana kuhusu kifungu cha 7 kuhusu Sheria ya habari kisome na ujibu ulimaanisha nini?
Mnyika: Anakisoma na kusema hiyo sheria inawapa uhuru na haki ya kutafuta habari na baadae kuwa huru kuisambaza au kutoisambaza na kifungu hiki kinawafanya wanahabari kuwa wamiliki wa habari husika na sio mtu mwingine.
Mhe. Lissu: Umeulizwa kuhusu maneno yangu na uhusiano wa matukio ya October?
Mnyika: Maneno yalitolewa Tarehe 03/04 na mshitakiwa akakamatwa Tarehe 09/04 na matukio ya Oktoba yakaja kutokea Mshitakiwa akiwa yuko Mahabusu.
Anasimama Katuga: Mheshimiwa asiende mbali huko.
Jaji: Anayosema shahidi tulishayaandika kwahiyo hakuna shida.
Tundu Lissu: Uliulizwa kuhusu maana ya Uasi, sasa nakupa Kamusi ile ile usome.
Mnyika: Uasi ni kupinga mambo ndani ya taasisi au sheria kandamizi hiyo ndio maana ya kwanza.
Mhe. Lissu: Kwahiyo umeelewaje hapo?
Mnyika: Uasi sio tu kupinga serikali bali hata kwenye taasisi kupinga mifumo mibovu nao pia ni uasi.
Mhe. Lissu: Wamesema kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba haukuwa huru na haki?
Mnyika: Kuna ripoti mbalimbali zimesema ikiwemo Common wealth Anasimama
Katuga: Hizo ripoti naziogopa asiende huko hakuzitaja kabisa
Mhe. Lissu: Sasa ripoti zinawapa presha usiende huko.
Katuga: Sio Presha tu zinanipa hadi Kisukari.
Mnyika: Basi uchaguzi wa Oktoba haukuwa huru na haki na haukuwezesha watu kushiriki kwa uhuru na haki.
Mhe. Lissu: Kesi ya Mbowe ulisema ya uongo fafanua sasa licha ya kwamba alikutwa na kesi ya kujibu?
Mnyika: Hakukutwa na hatia ya ugaidi na kumekuwa na tabia ya kubambikwa kesi na kwa Mwenyekiti Mbowe kama Mtendaji mkuu wa Chama , najua hakuwahi kupanga Ugaidi na Chama hakijawahi kuwa na Mipango hiyo.
Mhe. Lissu: Pia uliulizwa kama ni kweli alishitakiwa na watu wengine walikuwa ni Makomandoo wa Jeshi na ukasema walikuwa ni walinzi wake na wanaharakati pia.
Mnyika: Waliwahi kutumikia jeshi na kuondoka Jeshini na wakajiunga na harakati na Mwenyekiti akawapanga kuwa walinzi wake.
Katuga: Anasimama hili la kwamba walikuwa makomandoo wasiliseme kabisa.
Mhe. Lissu: Nawish nisiseme kuwa hii ni non sense, sitasema hivyo lakini sioni umaana wa hili swali. Lazima ufafanuzi ufanyike na huwezi kumtisha mtu kuwa utafanya cross sasa cross gani utafanya hapa?
Katuga: this court is not your mother
Mhe. Lissu: It is not your mother either. Wewe nani kakudanganya hii Mahakama ni Mama ako?
Jaji Ndunguru. Sasa Shahidi aulizwe swali tumuache ajibu.
Sehemu ya 331
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Re-Examination Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika
Mhe. Lissu: Mwenyekiti Mbowe alishitakiwa na watu wengine na ukasema walikuwa ni walinzi wake na wanaharakati? Fafanua.
Mnyika: Walikuwa Makomando zamani, wakawa walinzi wa Mbowe na kwa kuwa mlinzi wa Mwenyekiti walikuwa wanafanya kazi ya harakati na wakawa wanaharakati.
Katuga anachekacheka.
Jaji anamuuliza vipi?
Katuga: Majibu yalikuwa sahihi kabisa ya awali.
Mhe. Lissu: Mheshimiwa mimi siwezi kuwachukulia poa vichekocheko vya watu walionishitaki kwa Uhaini.
Jaji: Tuendelee
Mhe. Lissu: Kuvitishia vyombo vya ulinzi na Rais ukasema Mshitakiwa hakufanya hivyo fafanua?
Mnyika: Hakuna mahali kokote mshitakiwa alimtishia Rais wala Serikali hakuna alipotaja watu hao na vyombo hivyo.
Mhe, Lissu: Ulitaja kesi nyingi na kusema kesi zote zilikuwa za uongo?
Mnyika: zilifutwa kwasababu hakuna ushahidi uliowasilishwa Mahakamani na zilifutwa kwasababu za uongo na hakuna aliyekutwa na hatia.
Mhe. Lissu: Umeulizwa Maswali kuhusu Hotuba ya Jaji Chande kuhusiana na matukio ya Oktoba na Siku zilizofuata. Ulisema inatofautiana na Hotuba yangu?
Mnyika: Hotuba yako ilikuwa inahusu msimamo wa No Reforms: No Election na Chande alikuwa anazungumzia mambo tofauti kabisa.
Mh. Lissu anaendelea na Maswali Msawazo, Maswali Fukia Mashimo, Maswali Sawazisha. A.K.A Rejoinder kwa kitaalamu.
Mhe. Lissu: Shahidi uliulizwa kuhusiana na Hotuba Yangu na ueleze kama ulisema ni sahihi au sio sahihi kama lengo la Hotuba yangu lilikuwa ni kuishinikiza Serikali? Ukasema Hapana.
Mnyika: Lengo lilikuwa ni kuwaunganisha watanzania na wadau mpaka serikali ikubali kuwezesha uchaguzi huru na haki na wasipokubali msimamo wa No Reforms: No Election.
Mhe. Lissu: Ulisema mliendelea na harakati hadi Tarehe 09/06 ulimaanisha nini?
Mnyika: Tarehe 10/06 Mahakama ilitoa zuio la kufanya shughuli za kisiasa na kuzuia matumizi ya mali za Chama. Hadi Tar. 15/04/2026. Ambapo ni baada ya Uchaguzi kabisa. Ni siku 309 tulizuiwa kutumia chochote kile.
Mhe. Lissu: Uliulizwa kuwa uasi ni njia ya Kidemokrasia naomba fafanua maana yake?
Mnyika: Uasi ni kupinga au kukataa kwa nguvu kubwa na hizo njia za kidemokrasia kwa kutumia kufanya mikutano, kufanya vikao hizo zote ni haki za kisiasa. Haiwezi kuwa ni kosa zilizopo kwenyw sheria ya vyama vya siasa na Katiba ya nchi na mikataba ya kimataifa imeridhia.
Mhe. Lissu: Umemaliza kuelezea hapo?
Mnyika: Hapo tayari. Tuendeleee sasa.
Mhe. Lissu: Uliulizwa kuwa Chama chako kilikuwa kilishajiandaa kushiriki uchaguzi wa mwaka jana?
Mnyika: Katika Mkutano wa Tarehe 21/01 uliopitisha No Reforms No Election .......
Mhe. Lissu: Angalia usifike mbali watasimama hao.
Mnyika: Tulijiandaa kuruhusu watia kuelezea nia zao na pia kungomesha Chama.
Mhe.Lissu: Katuga alikwambia kuhamasisha uasi ni kosa? Ukamjibu kuwa Mwalimu Nyerere alisema tunahitaji vijana waasi wa mifumo kandamizi.
Mnyika: Maneno ya uasi yana tafsiri ya ziada ambayo ilitumika na mwalimu nyerere na halikuwa kosa la uhaini wala kosa lolote. Hakuwahi kushitakiwa hadi leo. Haliwezi kuwa neno sahihi kutumika na Nyerere halafu likawa baya kutumika na Tundu Lissu.
Mhe. Lissu: Uliulizwa pia kwamba huo Mkutano ulikuwa na Mwenyekiti au vipi? Fafanua.
Mnyika: Yes niliwaambia haukuwa na Mwenyekiti wa Mkutano na mikutano kama hiyo huwa haina minutes. Inakuwa na taarifa tu ya namna ulivyofanyika. Mimi ndio nilikuwa msimamizi mkuu wa huo mkutano.
Part 332 inaendelea kwenye post inayofuata,
Mnyika: Nimekishauri vizuri kabisa chama. Tumekaa kwenye Maridhiano, tumeenda Bunge kupeleka maoni yetu kuhusu mabadiliko ya sheria hakuna lililofanyika. Mahakama kwenye kesi ya kubenea ilisema masuala ya kisiasa yatatuliwe kisiasa ndio maana tukaja na No Reforms: No Election.
Twende break kwanza tutarudi baada ya lisaa limoja.Waheshimiwa majaji huyu mtu ananivunja moyo mara kwa mara ndio maana natumia ka moyo kaliko vunjika kama msisitizo, imagine hapo no form 6 liva tu na upo hapo!
Nje ya mahakama: Wewe na JJ ni dugu moya?
🔥 🔥 🔥Sema hii combination ya lissu na mnyika 🔥
Endapo.... endapo....Endapo atakutwa na hatia adhabu yake ni " kunyongwa hadi kufa"
aise.
Mimi ndiye shahidi waniamini niko chini ya kiapo.Twende break kwanza tutarudi baada ya lisaa limoja.
Tukirudi, uwaelezee waheshimiwa majaji kama nna uwezo wa kuuvunja moyo wako, na namna nilivyo uvunja na kuuacha vipande.
Hata mimi nauona mfanano 😅 Ila kuna utofauti, wakati unatandikwa na baridi JJ angekuwa kijana wa hovyo angekushauri uhovyo, fortunately JJ ni kijana wa Mungu, umebaki mwenyewe siku hizi hata hatuimbi nyimbo za kanisani. 😏Unajua kabisa sio ndugu moya mimi na JJ. Ila tulikutana nae Arusha kwenye jambo flani wakati ule nakwambia baridi inaniadhibu, yulielewana sana, kuna tu vitu tuchache tunamfanano.
Aiseeeee!Lissu Swala hilo hilo la Mwenyekiti Mbowe uliulizwa kama alishitakiwa na Watu wengine.
Ulisema ni Makomandoo na walikuwa walinzi wakena Wanahabari
Hebufafanua hapo
Mnyika walikuwa ni Makomandoo na walishatoka Jeshini na wakawa walinzi wake
Nassoro Katuga Wakileta hii ya mambo ya Makomandoo sioni haja ya kufafanua
Wale Makomandoo hawakustaafu.
Lissu Waheshimiwa Majaji with all due respect hili Pingamizi halina maana yeyote
Swala la hawa Makomandoo wamelileta wao kama wasingetaka tuukize wasingelileta
Kama Wamelileta wao ni lazima lifafanuliwe hapa, tusitishane.
Kwamba eti Makomandoo Wanasheria za jeshi tusizungumze ni perfect none sense am fearing to day that but its perfect none sense
Nassoro Katuga naomba kufanya rejoinder kuhusu hii area hii, tufuate sheria sasa.
Nitaomba kufanya Cross eneo hili la makomandoo
Lissu Huwezi kufanya Crosss examination hapa
Nassoro Katuga Unajua Mahakama siyo Mama yako.
Lissu its not your mother either
Jaji Ndunguru Subirini kidogo.
😀😀😀
Mimi ndiye shahidi waniamini niko chini ya kiapo.
Hata mimi nauona mfanano 😅 Ila kuna utofauti, wakati unatandikwa na baridi JJ angekuwa kijana wa hovyo angekushauri uhovyo, fortunately JJ ni kijana wa Mungu, umebaki mwenyewe siku hizi hata hatuimbi nyimbo za kanisani. 😏
Mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi ili washiriki uchaguzi.Tathmini yangu baada ya Mnyika kumaliza ushahidi
🔴 Conviction: 54%
🟢 Acquittal: 46%
CHADEMA ilikuwa na msimamo wa “No Reform, No Election”
↓
Mkakati wa kuzuia uchaguzi ulianza 3 Desemba 2024
↓
Mkakati wa kuhamasisha wananchi “kuasi” dhidi ya mifumo kandamizi ulianza Desemba 2024
↓
Lissu akiwa Mwenyekiti wa Taifa akatoa hotuba 3 Aprili 2025
↓
Katika hotuba hiyo kukawa na maneno ya “tutazuia uchaguzi” / “tutahamasisha uasi” / “tutakinukisha”
↓
Mnyika akathibitisha baadhi ya maneno hayo
↓
CHADEMA ilikuwa imeazimia kutumia mobilisation ya umma kutekeleza “No Reform, No Election”
↓
Katiba ya CHADEMA iliruhusu TEHAMA kutumika kuhamasisha umma
↓
Waandishi wa habari walikuwepo kwenye mkutano na ujumbe ukaweza kufikishwa kwa umma
↓
Mpango + uongozi + kauli + mobilisation + public dissemination
↓
Lengo lilikuwa kushinikiza Serikali ikubali mabadiliko; isipopokea, uchaguzi uzuiwe/usiendelee
Haya ni wewe unayasema hajayasema MnyikaMabadiliko ya mfumo wa uchaguzi ili washiriki uchaguzi.
Kama ni nje napokea simu.Maneno yako sio msahafu, maneno yasilete hitilafuuu...sitaki chupa ya soda nayaka energy
Nnae safari ingine inanukia, ila kwa vile umenitenga, acha tuendelee kufuatilia mwenendo wa kesi.
Hahaha haha, 😆 Katuga bhana.Mhe. Lissu: Wamesema kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba haukuwa huru na haki?
Mnyika: Kuna ripoti mbalimbali zimesema ikiwemo Common wealth Anasimama
Katuga: Hizo ripoti naziogopa asiende huko hakuzitaja kabisa
Mhe. Lissu: Sasa ripoti zinawapa presha usiende huko.
Katuga: Sio Presha tu zinanipa hadi Kisukari.
Mkuu, unaelewa uhaini? Huo mtiririko ulioweka, ni wa Katuga au Ndunguru?Haya ni wewe unayasema hajayasema Mnyika
Kama ni nje napokea simu.
Kama ni ndani pambana na hali yako mwenyewe nimechoka nimetoka mikoa mi4 mwezi wa 7-8.
Tuendelee kufuatilia kesi.
Gereji yako iko wapi?Sasa ingekua ndani ningesema ni safari?
I repair broken hearts 💕
Anza kwenye Maoni yaliyotolewa katika Kamati ya kudumu ya bunge "Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria ", kisha kesi iliyofunguliwa kupinga Uchaguzi usiwepo bila mabadiliko lakini Mahakama ikasema "Mambo ya kisiasa yawe solved by siasa ways" (Naomba niweke ufafaunuzi hapa kwamba Demokrasia ya kisiasa ndio sehemu ya mwanzo ya tafsiri ya neno Demokrasia, so kama mahakama ilishatoa hukumu ya kutumika kwa njia za kidemokrasia za kisiasa means No Reforms No Election ni sehemu ya njia za kidemokrasia za kisiasa).Tathmini yangu baada ya Mnyika kumaliza ushahidi
🔴 Conviction: 54%
🟢 Acquittal: 46%
CHADEMA ilikuwa na msimamo wa “No Reform, No Election”
↓
Mkakati wa kuzuia uchaguzi ulianza 3 Desemba 2024
↓
Mkakati wa kuhamasisha wananchi “kuasi” dhidi ya mifumo kandamizi ulianza Desemba 2024
↓
Lissu akiwa Mwenyekiti wa Taifa akatoa hotuba 3 Aprili 2025
↓
Katika hotuba hiyo kukawa na maneno ya “tutazuia uchaguzi” / “tutahamasisha uasi” / “tutakinukisha”
↓
Mnyika akathibitisha baadhi ya maneno hayo
↓
CHADEMA ilikuwa imeazimia kutumia mobilisation ya umma kutekeleza “No Reform, No Election”
↓
Katiba ya CHADEMA iliruhusu TEHAMA kutumika kuhamasisha umma
↓
Waandishi wa habari walikuwepo kwenye mkutano na ujumbe ukaweza kufikishwa kwa umma
↓
Mpango + uongozi + kauli + mobilisation + public dissemination
↓
Lengo lilikuwa kushinikiza Serikali ikubali mabadiliko; isipopokea, uchaguzi uzuiwe/usiendelee