TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI
SEHEMU YA 12.
1. Ni kumuua au kujaribu kumuua Rais — 39(1)(a).
2. Kuendesha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano — 39(1)(b).
Waheshimiwa Majaji, tunaingia 39(2). Kuna matendo manne ambayo ukitenda unakuwa umetenda uhaini.
3. Kutengeneza nia ya kuwezesha au kusababisha mtu au kikundi kumjeruhi Rais. Kumpiga Rais, kumjeruhi Rais, huo ni uhaini.
4. Kutengeneza nia ya kuwezesha au nia ya wengine kuwezesha au kusababisha Rais apinduliwe kwa njia zisizo halali kutoka katika nafasi yake ya Urais, au kumtoa katika nafasi yake ya Amiri Jeshi Mkuu — 39(2)(a).
5. Ukitengeneza nia ya kuwezesha mtu au kikundi kusababisha au kuwezesha kulimdukiwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano — 39(2)(c).
6. Ukitengeneza nia ya kuwezesha au kutengeneza nia ya mtu kuwezesha au kikundi cha watu kutishia Bunge au Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kosa mengine yapo kwenye 39(3).
7. Ukijiunga au kujishirikisha na maadui wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, au ukawapa kinywaji au chakula maadui wa Jamhuri — 39(3)(a).
8. Kuchochea mtu yeyote kuivamia nchi ya Jamhuri ya Muungano kwa silaha. Mfano, ukileta M23 Tanzania, ni uhaini — 39(3)(b).
9. Mtu yeyote atakayechukua silaha ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kulazimisha mambo dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania — 39(3)(c).
10. Mtu yeyote aliye na utii kwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania akisaidia maadui wa Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kuzuia shughuli za kijeshi au kuhatarisha maisha katika operesheni za kijeshi — 39(3)(d).
Sasa, Waheshimiwa Majaji, kama hayo ndiyo uhaini kama ilivyotafsiriwa na sheria.
Tuanze na “tutavuruga uchaguzi.”
Ipo wapi katika hayo yaliyofafanuliwa na Kifungu cha 39 cha Kanuni ya Adhabu?
Twende kwenye “tutazuia uchaguzi.” Haipo, siyo constructively.
Twende kwenye “tuhamasisha uasi.” Ipo wapi?
Kwa Kiingereza ni “rebellion”, ama kama ambavyo tulisomewa katika kamusi: “Kupinga jambo kwa nguvu.”
Twende kwenye “kukinikisha.” Ipo wapi?
Ili walau leo wanangu, wherever they are, wajue baba yao yupo gerezani kwa mwaka mmoja na nusu. Baba yao kuna kosa kafanya. Haipo.
Waheshimiwa Majaji, kwenye haya ya sheria yapo wapi? Hayapo.
Nimefungwa mwaka mmoja na nusu kwa uonevu.
Nimeonewa.
Nina ndugu hapa, wanakuja kila siku hapa nimefungwa.
Nina wanachama hapa, wanakuja kutoka kila mahali. Mwenyekiti wao nimefungwa, nipo gerezani.
(Watu wanalia.)
Nalindwa na askari kama vile ni muuaji. Kwa kosa gani?
Waheshimiwa Majaji, kama haya hapo, ugomvi hapa ni uchaguzi.
Tulitaka kuzuia uchaguzi, tulitaka kuvuruga uchaguzi.
Twende break.
Lissu: Sawa, Mheshimiwa.
Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka?
Job Mrema: Hatuna pingamizi, Mheshimiwa.
Jaji Ndunguru: Bado sana kuwasilisha.
Lissu: Siwezi kusema nikajifunga.
Nisije nikafanya mambo kwa hisia.
Jaji Ndunguru: Basi tutabreak kwa saa moja na nusu. Tutarudi hapa saa 8:30.
Majaji wanatoka.