Maharage ana uwezo kweli kuendesha shirika la kitaalam kama TANESCO?

Bwana Maharage Ally Chande, rasmi sasa AMEONDOLEWA TANESC0 na Rais Samia Suluhu na kupelekwa TTCL, mahali pa mawasiliano(ina shabibiana na DSTV).
Asante mama, unapitia maoni mitandaoni(hasa JF) ingawaje watu kama Nape wanaidharau.
Kweli mama na watu wake wanapitia hii mitandao na kuchukua hatua kwa constructive ideas.
 
Simjui Mr Maharage ila kiukweli TANESCO ni shirika gumu sana kuongoza. Linahiitaji Bodi na Menejiment makini ngazi zote na uadilifu mkubwa kupita kiasi. Tumwombee huko aliko na huyu ajaye; they are doing their best.
 
WATANZANIA walipiga kelele nyingi sana baada ya januari na maharage na bodi mpya kuteuliwa wakapuuzwa sasa matokeo yameprove wamefeli vibaya nchi iko gizani

Aibu kwa samia na mamlaka yake ya uteuzi waliteuwa kimihemko badala ya kuangalia weledi ona sasa kamrudisha Mhandisi kuwa Mkurugenzi

Na bodi kaiweka Mwenyekiti mpya

Rais apunguze kuziba masikio 😕
 
Mama kafanya kweli!.
 
Siwatetei hao wahuni najua ni watu wa hovyo tuu , ukiangalia vizuri tatizo la umeme Tanzania ni kwa sababu ya sheria na sera zetu wenyewe tulizojiwekea katika sekta ya umeme, kwanini shirika moja tuu ndio lipewe monopoly kwenye nchi ya watu zaidi ya milioni 70? huoni kama hilo ni tatizo? shirika linakusanya trillions lakini bila ruzuku ya serikali umeme unazima nchi nzima, CEO wa TANESCO anachaguliwa kisiasa sio kiutaalam kwa hiyo akiwa rafiki au akimfurahisha aliyemteua atakuwa safe, tuwe serious tuje na sheria mpya zitakazo tupatia strong regulatory body ya kulinda wadau wote wa umeme, capital, technology na utaalam sio tatizo, viko pembeni tuu vinasubiri, siamini na gas yote tuliyonayo bado tuna shida ya umeme, tatizo ni sisi wenyewe
 
January Makamba kajiwekea historia mbaya sana katika uongozi wa wizara ya Nishati. Kaingia yeye, muda mfupi ti mafuta hamna na umeme hmna.
Mbaya zaidi hakuwa na hata aidea atafanya nini kuondoa Taifa kwenye taabu aliloliingizia Taifa.
Kule China watu kama hawa ni rsasi inawahusu.
 
Hakika rekodi ya kuliacha Taifa gizani na petrol juu haitamuacha salama huko aliko ajitafakari japo Nina uhakika anajiona kakwepa kihunzi kwenda kufichwa mambo ya nje ambako hata akiunderpeform vipi haina direct impact kwa jamii

Ila tunashukuru ujinga wake na kubebwa kwake kumedhihirika wazi wizara ya nishati
 
Naafiki, inakuwaje tena aliyeharibu huko Nishati akapelekwa kwingine alimradi ni failure ktik uongozi.
 
TTCL Napo ametolewa ni posta masta mkuu
 
Makamba maekuja kulinajsi tenesco halafu akasepa sojui saa100 huwa anatuonaje kwa kweli
 
Mkuu si kweli, Tanesco ni ng'ombe wa maziwa wa wakubwa, Tanzania tuna kila kitu ambacho ni chanzo cha nishati, tuna maporomoko na mito,tuna gesi, tuna jua ,tuna upepo, nenda hapo Kenya uone shirika lao la stima linavyofanya kazi na kutafuta vyanzo vya nishati, sisi tukiamua tunaweza kufanya tatizo la mgao wa umeme liwe la historia, naamini kabisa angekuwepo Magufuri uhuni huu wa akina Kipara na Mabeans usingekuwepo na umeme usingekuwa mgao, hili taizo la umeme ni la kutengenezwa na baadhi ya genge la wahuni wachache, baada ya kuuona uhuni huo Magufuri akaamua kulivalia njuga suala la bwawa la Nyerere, kwani gesi ya Mtwara ambayo watu waliifanyia maandamano na kutaka eti wajitenge yote imechukuliwa na wajanja ambao wanaiuzia Tanesco hiyo gesi badala ya Tanesco wenyewe kuwa ndio wenye gesi, najua utasema Tanesco hawana uwezo wa kuchimba gesi na nitakujibu wana uwezo mbona wamechimba mabwawa ya maji kwa kushirikiana na serikali, na hata gesi si ndio hao hao wa remote ndio walikuwa na mamlaka ya juu ya gesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…