jingoloji
JF-Expert Member
- Nov 6, 2017
- 449
- 544
Mparee2 Umenena vyema
Mimi siwezi kumuongelea Muheshimiwa Maharage kwa kuwa nipo huku Nje hivyo sijui yaliyokuwa yanaendelea huko ndani ILA nina ushauri
Ukiwa kiongozi unatakiwa ujue kipimo wanachokupima nacho wale unaowafanyia kazi ili ukijumlishe kwenye kipimo (goals) zako; kwa upande wa Muheshimiwa hapa namaanisha ajue kipimo wanachompima nacho wananchi...
Mfano:
1. Wananchi wanataka umeme wa uhakika
2. Bei rafiki ya huduma zinazo ambatana na umeme (kufungiwa, gharama kwa unit nk)
3. Kupata majibu/Msaada kwa haraka mara wanapopata changamoto
4. Hivi kuna haja gani ya mwananchi masikini kusafiri hadi wilayani kuomba zero tarifu wakati TANESCO wanaweza kuona mita ina pengine mwaka mzima haijazidisha matumizi ya unit 40 kwa mwezi? najiuliza tu
5. Hadi leo karne 21 bado hatuna technologia ya kuweka umeme kwenye Mita (token iende moja kwa moja kwenye mita mtu akinunua?)
Sasa hata akilala ofisini akifanya kazi kama wananchi hawataona matokeo ya hayo niliyotaja (kwa uchache) wanaweza kufikiri ni Business as usual...Kumbe alikuwa anafanya kazi nzuri ila kwa kipimo tofauti na cha wananchi