Mtemi mpambalioto
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 3,436
- 7,955
kutoka katika gazeti la mwananchi:
Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande amesema hadhani kama ni busara kushusha bei ya umeme baada ya mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) kuanza uzalishaji.
Chande amebainisha hayo leo Mei 26, 2023 wakati akijibu swali na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Beatrice Bandawe aliyetaka kujua kama bei ya umeme itashuka baada ya mradi huo kuanza uzalishaji.
Amesema huwezi kushusha bei ya umeme baada ya kuanza kuzalisha JNHPP wakati hata miundombinu inayojengwa kwa kutumia mapato yanayotokana na uuzwaji wa umeme haijakamilika.
"Mimi sidhani kama ni busara kushusha bei ya umeme ili fedha tutakayobaki nayo ibaki kuhudumia umeme. Hapa ni vizuri kutofautisha bei na gharama, ni vitu viwili tofauti," amesema Chande.
Mkurugenzi huyo ameongeza kwamba ukitaka kukua, usishushe bei ya umeme, bali ubaki vile vile ili yale mapato yatumike kujenga miundombinu na kuendelea kuzalisha umeme
NIONAVYO MIMI:
maharage ametuchukulia sisi watanzania watu wa kupandishiwa tu bei! ni mtu asiyejali hali ya wananchi! hajui kama hilo Bwawa litashusha gharama za uendeshaji kwenye mafuta huko na SONGAS then ndio itumike kufanya mambo mengine:
Watanzania wanataka unafuu wa maisha halafu huyu mpuuzi aliyenogewa hela za walala hoi anakula na kuvimbiwa maharage yake analeta ujinga huu! Sijui ndio akili ya makamba?
No wonder wanatamani kupunguza wafanyakaz wakati Tanesco yenyewe haina watu wa kutosha