Malaika wa Misukosuko
JF-Expert Member
- Jul 16, 2021
- 2,470
- 7,376
Labda umeme wa Kinyesi Pumbavu kabsa
Hivi watu wamekatazwa kuwekeza kwenye Solar n.k., Wale Dowans na Symbion walikuwa sio wawekezaji ? Au unataka wafanye transmission ? Na wakifanya transmission unadhani watakwenda kule ambapo ni pagumu na hakuna faida ?
Issue kubwa sio Competition; Competition kwenye kitu kama umeme ni ngumu kutokea matokeo yake ukifanya hivyo watu wata-create opportunities za kupiga na kupanga bei (hili linaendelea huko Europe)
Kwa wingi wa vyanzo hakuna sababu ya Tanesco ku-fail; Iendelee kuwa state owned na watu kupewa targets wakishindwa mbona sheria zipo na wengine wa kujaliza nafasi wapo ?
Jinsi ya kuifanya Kampuni ya Tanesco kuwa Kampuni Bora na ya Kujivunia Tanzania na Afrika kwa Ujumla
Tanzania tumebarikiwa vyanzo vingi vya nishati, Na Tanesco ni kati ya Makampuni mama ya Tanzania ambayo yanaweza yakaitangaza nchi yetu Africa na Pote Duniani (Yaani mfano wa kuigwa) Sio tu kutupatia nishati hapa bali tuweze kuwapa hata majirani zetu na kutuingizia fedha badala ya sasa kutumia...www.jamiiforums.com
Naangalia waliojaribu kufanya na kilichotokea ni Desi ngoja nikupe mfano wa reli tuseme ubinafsishe reli sio zile trains bali na njia za train kupita; sababu tayari njia zipo huwezi kusema ujenge mpya kwahio kitakachotokea ni watu kushindanishwa tender anayeshinda kwa wakati miaka kadhaa anapewa targets asipofikisha anapigwa chini anachukuliwa mwingine na mwingine and the cycle continues sababu hio sekta sio rahisi kama vile ilivyo simu ambapo kila mtu anaweza akawa na vyanzo vyake minara yake n.k. (hata simu unaweza ukakuta wanakuwa forced kulipia miundombinu ya state na wenyewe kutoa huduma; Yaani Tier ISPs wanaununua jumla na kuuza na kuuzia wengine na wengine)Naheshimu mawazo yako japo sikubaliani nayo.
Unaposema "TANESCO iendelee kuwa state owned" unakuwa una hofu gani?
Unajua kilichotokea USA kipindi cha Direct Current na kila mtu kuwa na misitimu yake na nyanya zake ?;Ndio nazungumzia "Transmission" yaani waruhusu pia firms zizalishe na zifanye ugavi kuwepo na "Soko huria" kwenye umeme. Umeme ni bidhaa mzee na hakuna bidhaa itakosa mwekezaji kama inatoka.
Nishakujibu hapo juu..... kitakachotea ambacho ni feasible na realistic ni private firms kuwa madalali yaani zitachukua umeme katika wazalishaji walewale na transmission zilezile kitakachofanyika ni wewe Bill yako itasoma amekupa nani Huduma ingawa huduma inatoka kule kule kwa wao kununua kwa jumla na kuuza kwa rejareja; na kila wakikaa na Waangalizi na kulalamika kwamba gharama ya uendeshaji imezidi bei itaongezwa kuwafidia ili wapate profit (Hio sio kwamba ninaitoa kwenye theory bali ndicho kinachotokea katika Prices za Gas kwa Watumiaji wa Europe (Bei zinakuwa inflated ili watu wapate their foreseeable profit)Wabadiri sera ya nishati ya 2003 kuruhusu Private sector participation in electricity business na wasiingie katika ununuzi bali waruhusu firms zisambaze (Ugavi) wa umeme.
Hivi ushaona cable tu za TV zinavyozagaa kama utitiri na watu kutokuzihudumia; just imagine umewekeza wire zako kupeleka nyumba kumi za mtaa wa nane alafu kesho wanahama kwa provider B au wanashindwa kuhama sababu provider B hafiki kwao ?Ninachokiona kwako ni hufo tuu, watu wa telecoms wanatandika "Deploy" Optic fibre broadband 4000Km kupeleka huduma itakuwa nguzo na transformers!!
Umeme Nishati ni Nguzo muhimu katika taifa lolote, bila Nishati bora kila kitu kinasimama, hivyo basi Umeme haipaswi iwe chanzo cha mapato ya nchi (unless tunauza nje) umeme inabidi uwe kichocheo cha mapato ya nchi kwa kuhakikisha umeme ni wa uhakika na affordable ili viwanda na uzalishaji uwe wa gharama nafuu; Kuchaji watu pesa nyingi kwenye umeme ili upate mapato makubwa ni kama kujiibia kwenye mfuko wa suruali na kuweka mfuko wa shatiUsizunguke Umeme ni chanzo "kikubwa" cha mapato kwa nchi hii kwa hiyo wanaona ni bora tuteseke ila wapate mapato hayo ndio maana wamehodhi sekta hiyo. Hawajaipa kipaumbele huduma bali mapato.
Kwa sasa hata ukiwa na solar panels unazalisha umeme wa ziada ambao unataka kuuza kwenye grid ya taifa huwezi.Nakubaliana na wewe, ingeruhusiwa hata watu kuwekeza kwenye min grids kwa level hata ya mkoa au wilaya.
Umeme ni bidhaa waruhusu soko huria kama telecoms industry maana washashindwa kuleta umeme wa uhakika miaka 60 toka uhuru
Sidhani kama private companies hazipo zimekuwepo na kuna fursa kwa wanaotaka kuzalisha umeme na kuuzia kwenye sehemu ambazo umeme haujafika (kama alivyofanya mobisol) ingawa realistically bila economy of scale hailipi ndio maana mobisol alifeli na kuuza kampuni...., as wawekezaji kuwauzia Tanesco soma hapo chini:-Kwa sasa hata ukiwa na solar panels unazalisha umeme wa ziada ambao unataka kuuza kwenye grid ya taifa huwezi.
Kwa sababu TANESCO ina monopoly kwenye kuzalisha umeme.
Halafu ukimueleza mtu kwamba monopoly hii ni mbaya haelewi.
Ndiyo maana nchi ina matatizo.
Wananchi wengi hata hawayaoni matatizo kama matatizo.
Wanatafuta mchawi tu, kufukuzana kazi na kukaripiana bila mkakati.
Tunaenda kujenga bwawa kubwa la umeme, la kutegemea mvua, wakati tuna tatizo la mvua na mabadiliko ya tabianchi.
Hii nacheka sana aisee...
Hiyo mikataba ilikuwa mikataba ya kazi au MoUs? Waliishia wapi? Sikuijua hiyo.Sidhani kama private companies hazipo zimekuwepo na kuna fursa kwa wanaotaka kuzalisha umeme na kuuzia kwenye sehemu ambazo umeme haujafika (kama alivyofanya mobisol) ingawa realistically bila economy of scale hailipi ndio maana mobisol alifeli na kuuza kampuni...., as wawekezaji kuwauzia Tanesco soma hapo chini:-
KAMPUNI 6 ZASAINI MKATABA NA TANESCO KUZALISHA UMEME WA MAJI NA JUA
Meneja Mwandamizi wa Mipango Mikakati wa Tanesco, Eng. Costa Rubagumya akitiliana saini mkataba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kampuni ya Lung...issamichuzi.blogspot.com
Kuhusu suala la kila mtu kuweza kuuzia Tanesco nimeliongelea kwenye huu uzi
Jinsi ya kuifanya Kampuni ya Tanesco kuwa Kampuni Bora na ya Kujivunia Tanzania na Afrika kwa Ujumla
Tanzania tumebarikiwa vyanzo vingi vya nishati, Na Tanesco ni kati ya Makampuni mama ya Tanzania ambayo yanaweza yakaitangaza nchi yetu Africa na Pote Duniani (Yaani mfano wa kuigwa) Sio tu kutupatia nishati hapa bali tuweze kuwapa hata majirani zetu na kutuingizia fedha badala ya sasa kutumia...www.jamiiforums.com
Ila kuweza kufanikisha hilo itabidi Tanesco ku-invest in smart meters ambazo zinaweza kumpa mtu credit akizalisha zaidi....
In short this is a goldmine kutokana na vyanzo vyetu vingi Tanzania tukiitumia vizuri Tanesco itatutoa kimasomaso ila kikachotokea ni kuendelea kuipa Tanesco a Bad name waiuze alafu kwa mlango wa nyuma wainunue waendelee kulamba asali.... (with no change in efficiency)
Ofcourse muundo / management inabidi ubadilike sasa hivi tatizo kubwa Tanesco ni Kibubu cha Serikali, wanachota pesa wanavyotaka hawalipi bili na kuanzisha miradi isiyo na tija na kupeana tender ili watu wapige pesa.... (am sure hata hizo Kampuni huenda wana share au 10%, thus selling the power (au kuuza hewa) at inflated prices.....Hiyo mikataba ilikuwa mikataba ya kazi au MoUs? Waliishia wapi? Sikuijua hiyo.
Ila nafikiri bado kuna ukiritimba kwenye hayo makampuni kuweza kuuza umeme.
Suluhisho lilikuwa hiyo habari ya wananchi kuuza umeme moja kwa moja kwenye grid, kuna siku Maharage Chande alihojiwa hili, inaonekana kuna technical issues kama ulivyosema.
Lakini pia, kimsingi TANESCO wanapata conflict of interest hapo wao wenyewe kusimamia ugavi wa umeme halafu wakawa wanashindana kwenye biashara.Yani ikitokea kitu kinaweza kuja kuchukua market share yao, unafikiri watakiruhusu? Halafu wao wapate wapi biashara?
Hapo inawezekana tukatakiwa kutenganisha anayesimamia ugavi wa umeme na wanaofanya biashara ya umeme ili kuondoa conflict of interest.
TANESCO imeondolewa majukumu ya kusimamia ugavi wa umeme? Hayo yangeachwa EWURA halafu TANESCO ifanye biashara tu.
Sikumbuki vizuri majukumu ya TANESCO kwa sasa yakoje, miaka ya kati hapa muundo umebadilishwa sana.
Hili jambo ulilolisema kama nimekuelewa vizuri- nalielewa na nishawahi kuliongelea.Ofcourse muundo / management inabidi ubadilike sasa hivi tatizo kubwa Tanesco ni Kibubu cha Serikali, wanachota pesa wanavyotaka hawalipi bili na kuanzisha miradi isiyo na tija na kupeana tender ili watu wapige pesa.... (am sure hata hizo Kampuni huenda wana share au 10%, thus selling the power (au kuuza hewa) at inflated prices.....
Ila nadhani perception yangu ambayo ni tofauti na wengi Nishati ambayo ni nguzo ya productivity Kampuni kama Tanesco inabidi ipimwe (at-least ndani ya nchi) kwa kiasi gani watu wanapata nishati ya uhakika kwa affordable prices na sio kiasi gani cha fedha inakusanyia nchi (kuna domino effect inayogusa nyanja zote kama hakuna umeme wa uhakika na wa gharama rafiki); hii ni kama binadamu kujipiga ganji kwenye balanced diet ambayo mwisho wa siku unalipia kwa gharama ya matibabu
Kwahio kwa muktadha huo ningekuwa mimi Tanesco nisingeiangalia kama mshindani wa wadau wengine bali facilitator na mshirika ambaye anafanya nao kazi; Kwahio yoyote anayeweza ku-generate umeme cheaply kuliko vyanzo vyake Tanesco wachukue;(hapa washindani ni individuals whom can generate to supply to the GRID - bei yao lazima iwe cheaper or atleast the same as what Tanesco can generate) Biashara ifanyike kwa kuuza surplus nje ya nchi ili kujipatia pesa ya kusaidia kampuni na nchi na kuwahudumia watu wa ndani; from that perception utaona kwamba kutakuwa hakuna conflict of interest na wadau wazalishaji (ambao kila mtu mwenye paa la nyumba na yeye atakuwa mzalishaji) bali itakuwa ni symbiotic relationship..., kila mtu ananufaika kwa productivity ya mwingine na sio competing....
Lakini realistically that is a Pipe Dream, Tanesco ni Kibubu cha Serikali na wanufaika wachache wanaotumia technicalities kuwahadaa watu; and now they are giving the Dog a bad name, and soon they will hang it......
Hao wamefungulia maji kule mtera makusudi, hakuna ukame bwana wewe, huu ni mwendelezo wa mambo ya kishenzi ya serikali hii iliyojaa weziNani anaemteua? Halafu kwani Maharage Chande ndio kaleta ukame? Maharage ndio mtoa pesa za kuanzisha vyanzo vipya? Upuuzi.
Ila Sasa Kwa Afrika Jamaa wanaodhalilisha hivi na kuongea ndio huonekana Viongozi Sasa [emoji16][emoji16]
Ila ni kitu gani?Maharage sio mboga
Hivi kumbe Kuna watu mna akili za kipumbavu hivi? Wanaojiita baba Wana hasara ikiwa mwanaume unaweza amini Kila unachoambiwa kama mwanamke.PoleHao wamefungulia maji kule mtera makusudi, hakuna ukame bwana wewe, huu ni mwendelezo wa mambo ya kishenzi ya serikali hii iliyojaa wezi