Maharage wa TANESCO atimuliwa kwenye kikao cha Waziri Mkuu Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Biteko. Apewa siku tatu

Boss wa TANESCO atimuliwa kikaoni. Sioni nyota njema kwake. Siku tatu zinamtosha kweli au ndo wanamkomoa baba wa watu?

Na Biteko akija kujua dili za Luku atamla kichwa mazima.

Kaambiwa nenda kashughulikie Umeme. Alikuwa high Table ametabasamu na furaha zote amekaa kwenye Maonesho yanayoendelea ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam

Tarehe 25 Septemba 2021, Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO akichukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka

Kutokana na Mgao Mkubwa wa Umeme unaoendelea Nchini, Maharage anadai hakuna Mgao bali ni Upungufu wa umeme.

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Maharage Chande aliwaomba Wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho kuna Upungufu wa Umeme unaosababisha baadhi ya Maeneo kuwa na Umeme na mengine kukosa Huduma hiyo

Maharage alisema "Katika Mtandao wa Umeme hitilafu huwa zinatokea mara kwa mara na pale zinapotokea Wateja wetu huwa tunawataarifu. Tunapopata upungufu sio Nchi nzima inakuwa haina Umeme ila ni kwa baadhi ya maeneo na huwa tunatoa taarifa"

Sasa baada ya kwambiwa aende kushughulikia umeme, nilijua ataenda site. Cha ajabu yupo Ofisini kwake Ubungo kakaa huku tai ameilegeza, inaonekana ana mawazo sana.

Tumuombee presha yake isipande.

Baadhi ya Watanzania wamesema mgao wa umeme umekuwa ukisababisha hasara katika biashara zao mara kwa mara. Na wamelitaka shirika la umeme (TANESCO), kutoa taarifa rasmi ya jinsi mgao huo unavyoendeshwa. Je, kwa sasa Tanesco inazalisha kiwango gani cha umeme? Ni upungufu wa aslimia ngapi?
Mtoto pendwa haaa anazunguka kwenye mambo ya nje tu.
 
Nimeishia kucheka

Alienda kufanya nn na waziri yupo ,katibu mkuu pengine yupo

Yeye mkurugenzi !! Halali afukuzwe
 
Watu wengi wanafikiri umeme unatosha nchi hii...
Umeme hautoshi na kwa kipindi kirefu hakukuwa na chanzo kipya cha umeme..

Tunasubiri Julius Nyerere Dam ikamilike..
Naona ile connection ya line kutoka Arusha kwenda Namanga inakaribia kuisha... Wanunue hata megawatts 400 kutoka Ethiopia unaopitia Kenya pengine unafuu utapatikana
Kama umeme hautoshi, iweje Mtoto wa mama Abdul aende UG kuwauzia umeme wetu?
 
Mkuu unatakiwa uwe na taarifa sahihi...
Hatuna uwezo wa kuuza Uganda kwa sasa bali tunanunua kwao kupitia Masaka Mtukula na sehemu nyingine ni Mulongo..
Huyo sijui Abdul amekwenda mwenyewe kama mwekezaji wa kutaka kuanzisha kampuni ya umeme huko Ug.. Terms na makubaliano sijayajua bado
 
Alaa!!
 
Ndiyo maana leo umeme unaenda "masaa" 13 sasa bila kukatwa leo hapa mtaani.

Mara ya mwisho ilikuwa 15th August 2023 ndiyo tulipata umeme 24hrs hapa mtaani.

Alaaniwe yule jamaa.
 
Boss wa TANESCO atimuliwa kikaoni. Sioni nyota njema kwake. Siku tatu zinamtosha kweli au ndo wanamkomoa baba wa watu?
View attachment 2756107
Na Biteko akija kujua dili za Luku atamla kichwa mazima.

Kaambiwa nenda kashughulikie Umeme. Alikuwa high Table ametabasamu na furaha zote amekaa kwenye Maonesho yanayoendelea ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam

Tarehe 25 Septemba 2021, Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO akichukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka

Kutokana na Mgao Mkubwa wa Umeme unaoendelea Nchini, Maharage anadai hakuna Mgao bali ni Upungufu wa umeme.

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Maharage Chande aliwaomba Wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho kuna Upungufu wa Umeme unaosababisha baadhi ya Maeneo kuwa na Umeme na mengine kukosa Huduma hiyo

Maharage alisema "Katika Mtandao wa Umeme hitilafu huwa zinatokea mara kwa mara na pale zinapotokea Wateja wetu huwa tunawataarifu. Tunapopata upungufu sio Nchi nzima inakuwa haina Umeme ila ni kwa baadhi ya maeneo na huwa tunatoa taarifa"

Sasa baada ya kwambiwa aende kushughulikia umeme, nilijua ataenda site. Cha ajabu yupo Ofisini kwake Ubungo kakaa huku tai ameilegeza, inaonekana ana mawazo sana.

Tumuombee presha yake isipande.

Baadhi ya Watanzania wamesema mgao wa umeme umekuwa ukisababisha hasara katika biashara zao mara kwa mara. Na wamelitaka shirika la umeme (TANESCO), kutoa taarifa rasmi ya jinsi mgao huo unavyoendeshwa. Je, kwa sasa Tanesco inazalisha kiwango gani cha umeme? Ni upungufu wa aslimia ngapi?
Rais Dkt Samia tulimuonya sana tena sana hakutusikia. Yaani huwezi fanikiwa kiuongozi kwa kukomoa uliowakuta. Maharage na Jan ndicho walikifanya. Kibaya kabisa Maharage kavuruga maslahi ya watumishi TANESCO, yaani ananikumbusha sawa na HR mmoja aliingia na kuharibu maslahi ya CRDB kilichotokea CRDB ingekufa maana watu hawakuwa na moyo wa kazi. Mh. Biteko akitaka kufanikiwa amfukuze saa saba mchana Maharage na arejeshe uongozi ulioondolewa na ateue bodi mpya kwa sababu iliyopo sasa ni ya kundi la watu wanaofaidika na mgao wa umeme. Maharage afungwe mpiga dili
 
Labda alikuwa na bifu nae si unajua wabongo kwa kulipiza
Ujinga Mtupu February ameondoka amemfundisha Propaganda za kishamba eti hakuna mgao ispokuwa ni upungufu wa Umeme, ameshusha welevu wake wa Technolojia akajitwika Ujinga wa aliyekuwa waziri wake February Marope!!.
 
Maharage ni Pro makamba ameletwa pale na Makamba, Biteko achague Watu wake aanze Fresh start, MD na Board haviwezi kumpa matokeo hata kidogo
 
Nani anaemteua? Halafu kwani Maharage Chande ndio kaleta ukame? Maharage ndio mtoa pesa za kuanzisha vyanzo vipya? Upuuzi.

Ila Sasa Kwa Afrika Jamaa wanaodhalilisha hivi na kuongea ndio huonekana Viongozi Sasa 😁😁
Wewe acha upumbavu kukosa uwajibikaji na mipango mikakati kwa mkurugenzi mkuu TANESCO ndio chanzo cha tatizo la umeme msisingizie maji , kwanza wana deal lao la mita za LUKU na mwenzie makamba.
 
Maharage ni Pro makamba ameletwa pale na Makamba, Biteko achague Watu wake aanze Fresh start, MD na Board haviwezi kumpa matokeo hata kidogo
Sana, kibaya kabisa kabisa Maharage kaharibu mno kama jinsi yalivyo maharage. Na Mh. Biteko asipojua pakubonyeza he will never get better results. Kalemani alikuwa siyo kiongozi mzuri ila kwenye motisha ya kazi aliwaacha ila sasa huyu kaja na theory zake za eti kutoa gawio serikalini wakati watumishi wako hawana hata morali ya kazi
 
Back
Top Bottom