Mahari sio lazima, ni mila potofu ya kupingwa

Kwa nini unaona mahari ni jambo la wanawake tu?
Wao ndio wanajua kama mahari ni wao wanauzwa au la kama wanaume humunwNa dai mahari ni kugeuza mwanamke bidhaa na slave trade

Let women speak their position jwa hii ya vidume koko maskini ambavyo havitaki kulipa mahari kwa visingizio kibao kuwa ohh maharizimepitwa na wakati ohh ni slave trade ohh ni kama mwanamke anageuzwa kuw bidhaa sokoni kwa bride price nk kumbe vidume vyenyewe vilofa hela havina they free drive

Kutaka free drive ndio vinakuja na concepts za ku justify ulofa wao kibao
 
Haya yote yanaletwa na hali ngumu ya maisha,huwezi ukawa na hela alafu ukaanza kulialia kutozwa 2M.
2M inasaidia kama sio yote inaishia kwenye shughuli za harusi
2M mbona ni shopping ya weekend tu?

A couple of Tom Fords, a couple of dinners, some food shopping, something for the grill to BBQ, some drinks, a new tablet here, full tank of gas (petrol) for the SUV there, 2M inamalizika within a weekend na shopping haijaisha!

2M is not even a thousand dollars. A thousand US dollars is more than 2M.

Sasa mbona wengine tunaishi maisha hayo na bado tunapinga mahari kifalsafa tu?

Kuna watu wanapinga mahari kwa sababu za kifalsafa.

Unaelewa hilo? Falsafa, usomi, usawa wa watu? Kukataa mtu kuuzwa kama kwenye biashara ya utumwa?

Unaelewa kwamba kuna watu wanapinga mahari halafu hiyo hela ya mahari inatumika weekend moja tu kwenye manunuzi, tena mengine ya anasa tu?

Kwa nini jamii masikini zinaona kila tatizo ni la kiuchumi? Hazielewi kabisa ukisema unapinga mahari kwa sababu za kifalsafa, si za kiuchumi kwamba huna pesa.

Ni umasikini wetu umetufanya tuangalie kila tatizo kama tatizo la pesa? Wakati mengine ni matatizo ya itikadi za kifalsafa?

Ni kwa sababu watu masikini hawasomi na wana anxiety kuhusu pesa, hivyo wanaangalia kila kitu kwa kutumia pesa, pesa, pesa tu?
 
Achana na hizo sababu,huwezi kuwa na hela alafu ukawa eti nimemnunua mwanamke kwa 2M shida ni hela
 
Umeiongelea mahari, sifahamu kwa imani, mila, desturi au utamaduni upi.

Nikaona tukupe darsa dogo la kuifahamu mahari Kiislaam:

Kwanza kabisa ningependa tufahamu kuwa tunaposikia neno "mahari" kwa mila, desturi au imani nyingine yoyote nje ya Uislam wanakuwa wameliazima neno hilo kutoka Kiarabu linalotokana na sharia ya ndoa ya Kiislaam.

Mkataba wa ndoa ya Kiislamu
-Maher (iliyotafsiriwa kama mahari) ni mkataba ambao Waislam huingia kabla ya kufunga ndoa. Hairejelei kwenye mkataba wa ndoa yenyewe, bali mahari ni mkataba ambao mume atalipa kwa mkewe katika tukio la talaka au kifo ikiwa haijatimizwa wakati wa mkataba wa ndoa.

Katika sharia za Kiislam, Mahari ni zawadi au mchango unaotolewa na mume mtarajiwa kwa mke wake mtarajiwa, kwa mali waliyokubaliana, kama ishara ya heshima kwa bi-harusi, na pia inakuwa ni utambuzi wa uhuru wake kutoka kwa wazazi au walezi wake.

Mahari si zawadi kwa njia ya kitamaduni, lakini kwa hakika ni lazima na mke mtarajiwa huipokea kama haki yake.

Mahari inaweza kuwa pesa taslim, au aina yoyote ya mali iliyotolewa kabla ya ndoa au kugawanywa katika malipo ya mapema na yaliyoahirishwa (kopwa). Kiasi na muda wa malipo utategemea mambo ya kimila (kumbuka, mila na desturi za Waislam ni zile zisizokiuka Uislam) chini ya sharia ya Kiislam.

Ikitokea malipo ya mahari yameahirishwa (cheleweshwa au kopwa), sehemu iliyoahirishwa ina athari ya kumtunza mke baada ya talaka au baada ya kifo cha mumewe. Ingawa mke anaweza kusamehe malipo ya Mahari, anastahiki hilo kama suala la kanuni za dini ya Kiislam.

Kila Mahari itafsiriwa kwa masharti yake na kwa kuzingatia nia ya wahusika wakati mkataba ulipofanywa.

Ingawa sharia sheria ya nchi ni lazima iwe kwa maandishi yaliyotiwa saini na pande zote mbili na kushuhudiwa.

Makubaliano ya Mahari Kiislaam yanatambuliwa kuwa ni halali kisheria nchini Tanzania na nchi nyingi Ulimwenguni.

Ndoa ya Kiislam haitimii bila makubaliano ya mahari kwa pande mbili.

Nimejitahidi kuielezea Mahari Kiislaam kwa uchache wake, kama kuna makosa yoyote katika hayo basi ni yangu binafsi. Allah ndiye mjuzi zaidi.
 
Sumu zako dhidi ya Watanzania zishamaliza watu wako.

Nishasema na nitaendelea kusema kuwa wewe ni Mkimbari. Kuwa,wewe ni mkereketwa wa mfumo dume, mfumo wa kibeberu na wa kikaburu.

Robert Heriel embraces a Mysoginist, Racist and bigoted Ideas.


Naona genge lenu limeamka tena kumwaga sumu zenu tena Tanzania. Mlaaniwe
 
Achana na hizo sababu,huwezi kuwa na hela alafu ukawa eti nimemnunua mwanamke kwa 2M shida ni hela
Katika dunia yako.

Katika dunia yangu, naenda dinner moja weekend ya watu wawili ya 500,000.

Kabla sijafanya shopping 2M nishamaliza robo.

Najua unaona hatari kwa sababu unaendekeza umasikini.

Mimi na Nyerere tumepinga mahari kwa falsafa kubwa. Nyerere hakuwa masik8ni, lak8ni alipinga mahari.

Wewe huwezi kuona zaidi ya 2M katika hili.

Kwa sababu ndiyo mwisho wa uwezo wako.
 
Haya yote yanaletwa na hali ngumu ya maisha,huwezi ukawa na hela alafu ukaanza kulialia kutozwa 2M.
2M inasaidia kama sio yote inaishia kwenye shughuli za harusi
Harusi kwa Waafrika huwa ni mzigo wa mwanaume.
 

Ninyi mnaoona binti zenu ni Watumwa endeleeni kuwauza kama Ng'ombe.
Narudia hakuna Baba mwenye Akili timamu ambaye amepata Nuru na kuutambua ukweli atakayethubutu kukubali Mahari(kumuuza Binti yake).

Kweli unaweza kuishi miaka mingi na bado ukawa kama Umezaliwa Jana. Na unaweza kusoma Sana lakini ukawa mjinga
 
Achana na hizo sababu,huwezi kuwa na hela alafu ukawa eti nimemnunua mwanamke kwa 2M shida ni hela

Haujamuelewa Kiranga Mkuu.

Anachojaribu kukueleza ni kuwa Pesa sio tatizo, Ila lengo la hiyo Pesa ndio utata ulipo.
Kwa nini ukienda kuoa utoe Mahari, na usipotoa Mahari unaonekana hujaoa? Hiyo ndio Hoja. Je Mahari ndio bei ya kumpata Mwanamke ili awe Mkeo(logically Ipo hivyo).

Zingati Mahari pia hata wanaume wanatolewa baadhi ya jamii. Lakini haina maana yoyote Ile.
 

Ni Kweli Kabisa. Nilichoandika ni maoni na mtazamo wangu wa kifalsafa ambao Watu wa Aina yangu na wanaopenda Kutumia Logic wataungana na Mimi.
Na wale conservative watapingana na Mimi. Huu NI mjadala.
Watu wajadili Kwa Hoja.

Mahari haitakuwepo Karne chache zijazo na hii ni Kutokana na kuwa kundi la Watu wenye fikra za Giza linazidi kutoweka.
 
Mahara yana wenyewe wewe nenda uwanja wa fisi kajitwalie mke wa bule

Biashara ni biashara.
Mmoja ananunuliwa uwanja wa fisi Kwa kujiuza mwenyewe rejareja. Mwingine anauzwa na Wazazi na ukoo wake Kwa bei ya jumla. Tofauti iko wapi?
 
Usiache mbachao ......
Hata baba ako alitoa , toa tu

Sio kila alichofanya Baba yako kilikuwa sahihi. Na sio kila utakachofanya wewe ni Sahihi hivyo Watoto wako wafanye.
Vingine ni Kutokana na Akili za Wakati huo zilikuwa za kitumwa.

MTU Huru hanunuliwi. MTU Huru hatolewi MAHARI.

Siku ukiujua ukweli utakuwa Huru kwelikweli.
 
Mkuu kule India wanaume ndio wanalipiwa mahari vip hapo wanaume pia tunafanywa bidhaa?

Ndio maana nikamuambia mpuuzi mmoja hapo mwenye athari Mbaya za ushoga wa kiasili kuwa Mahari haimhusu Mwanamke pekee Bali inahusu mnunuaji na muuzaji. Mwanamke na Mwanaume. Ni biashara.

Lakini Akili zake za kishoga akabaki kuleta upumbavu wake aliofundishwa Huko kwao
 
Acha makasiriko lipa mahari mkuu
 

Yes Umeeleza vizuri Kwa Hoja za kiimani, hasa dini ya uislam. Hata Biblia inaeleza kuhusu Mahari lakini haielezi kama Sheria au amri ya Mungu Bali inaeleza kama Mapokeo (Mila na desturi za mababu) ambazo hazipo kwenye amri na sheria za Mungu, Torati ya Musa.

Kwenye misahafu iwe ni Biblia au Quran zipo sheria za Mungu ambazo Mungu mwenyewe amezitanabaisha na nyingi zilishushwa kwenye Torati ya Musa. Na yapo Mapokeo ambayo ni maelekezo ya mitume, manabii na Wazee waliotangulia. Hayo Mapokeo sio lazima kuyafuata ni Mtazamo na Maoni Yao kulingana na nyakati zile jinsi Maisha Yao yalivyokuwa.

Sheria za Mungu hazibadiliki Kwa sababu zimefungamanishwa na Nature. Lakini Mapokeo ya wanadamu yanabadilka.

Marko 7
7 Kuniabudu kwao ni bure. Wanafundisha watu amri zao badala ya sheria yangu.’ 8 Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushikilia desturi za watu.”9 Akawaambia, “Mnaepuka kwa ujanja amri za Mungu ili mpate kutimiza desturi zenu!

Mathayo 15:
7Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu:
8‘Mungu asema: Watu hawa huniheshimu kwa maneno tu,
lakini mioyoni mwao wako mbali nami.
9Kuniabudu kwao hakufai,
maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.’”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…