Mahari sio lazima, ni mila potofu ya kupingwa

Mahari sio lazima, ni mila potofu ya kupingwa

MAHARI SIO LAZIMA, NI MILA POTOFU YA KUPIGWA VITA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Moja ya Mila potofu isiyo na maana ni suala la Mahari. Hakuna sababu hata Moja yenye Maana ya MTU kutoa Mahari ndipo akabidhiwe MKE au Mume. Ni ujinga tuu! Na jamii ambayo sio za kiungwana ndio hufanya desturi hizo.

Uliwahi kujiuliza Kwa nini unatoa/unatolewa Mahari?
Mahari inamaanisha nini kwenye mahusiano ya ndoa?
Mahari inaongeza au kupunguza nini kwenye mahusiano ya ndoa Mpya?

Utoaji wa Mahari ni Mila na desturi za kizamani zilizopitwa na Wakati. Zimepitwa na Wakati Kwa sababu hazina uhalisia wowote. Na zimelenga kufanya biashara ya kumuuza MTU(Mwanamke) kama Bidhaa Fulani hivi.

Ni marufuku mabinti wa Tibeli kutolewa Mahari. Marufuku! Mimi kama Baba Yao, nimetamka kuwa Binti zangu hawatatolewa Mahari Kamwe. Kwa sababu Watibeli hawatolewi Mahari wala hawatoi Mahari.

Mfumo dume wa kununua Wanawake Kwa kile kiitwacho Mahari umelenga kuwageuza Wanawake kama Bidhaa fulani, kwamba Mahari ya Binti huyu ni milioni 2 au tatu au Ng'ombe nne. Ndio nini sasa, upumbavu tuu!
Unajua haya mambo wamefanya Wazee wetu(tunawaheshimu) lakini lazima tukubali kuwa kuna mambo hayakuwa na maana yoyote Ile.

Matokeo yake wazazi walafi na wenye uroho WA fedha waliwauza mabinti zao Kwa wanaume wenye vipato bila kujali hisia za mabinti zao kama wanawapenda hao wanaume au Laah!

Watumwa ndio wanauzwa, Watu huru hawauzwi. Binti za Tibeli ni Watu Huru. Hawauzwi wala kujiuza. Binti aliyehuru au wazazi wenye Hekima kamwe hawawezi mgeuza Binti Yao mtumwa na kumuuza Kwa mwanaume mwingine Kwa Ile biashara yenye jina la Mahari. Hilo halitotokea.
Binti huru anahaki zote za kuchagua Mume ampendaye, akaolewa na kuanzisha mji wake Kwa Moyo WA mapenzi. Na sio Aolewe Kwa Pesa ili baadaye Huko ndoani kitu kidogo tuu nilikutolea Mahari. Kitu kidogo tuu haukunitolea Mahari. Come on!

Ni jamii ya Watu wajinga wenye Akili za gizani wanaolipishana Mahari. Ujingaujinga tuu!
Yaani wazee wazima mnakaa mnajadili na ku-bargain kiasi cha Pesa za Binti yenu. Huo ni ujinga wa kiwango cha juu Kabisa. Alafu mwishowe ati mmoja anakuwa na deni kisa ameshindwa kumaliza.


Sijui mwingine anatolewa Mahari ya laki mbili, mwingine elfu 80, mwingine milioni tano mwingine milioni kumi. Yaani kama Watu waliochanganyikiwa. Hivi kweli Baba mwenye Akili kabisa unayempenda Binti yako unakubali kabisa kujadili thamani ya Binti yako na Pesa. Wanaume tuweni serious kidogo. Tuache mambo ya kijingajinga.

Binti amepata Mchumba, anayoruhusa ya kuja nyumbani kumtambulisha, kisha taratibu za sherehe za kumuaga Binti zianze huku upande wa pili wa Bwana harusi wakiandaa sherehe ya kumpokea Bibi Harusi. Sio lazima iwe sherehe kubwa Ila ni muhimu kufanyika kulingana na kipato chenu.

Kwa Vijana WA Zama hizi mambo yasiyo na maana yoyote yatazidisha mitafaruku isiyo na maana. Ndio maana Wazungu wao walishaachanaga na mambo ya Mahari miaka mingi iliyopita.

Mwanaume unapoenda kuoa sehemu au kwenda ukweni ni lazima uwe na Zawadi kadiri ya uwezo wako. Sio unaenda mikono mitupu kama mjinga. Halikadhalika na Mwanamke uendapo ukweni lazima uende na Zawadi. Hiyo Zawadi haitahesabika kama Mahari. Kumaanisha Hautapangiwa na yeyote Ila utaifanya Kwa mapenzi na uwezo wako WA Wakati huo.
Hivyo ndivyo Watibeli tunavyoendesha mambo yetu.

Nimemaliza! Mwenye swali aweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mtibeli nakuunga mkono asilimia zoooteeeee!
 
Muache na kuwahonga basi kama hamtaki kutoa mahari. Kutoa mahari hamtaki lakini kila s iku mpo bize kuwhonga pesa ili mkalale nao.. Hii mada naitafsiri kama shambulio jingine dhidi ya jinsia ya kiume..

Mahari ina maama kubwa sana katika maisha ya wanandoa zaidi ya unavyofikiria..
 
Muache na kuwahonga basi kama hamtaki kutoa mahari. Kutoa mahari hamtaki lakini kila s iku mpo bize kuwhonga pesa ili mkalale nao.. Hii mada naitafsiri kama shambulio jingine dhidi ya jinsia ya kiume..

Mahari ina maama kubwa sana katika maisha ya wanandoa zaidi ya unavyofikiria..

Embu tupo mantiki ya mahari kwèñye Ndoa ili tuone hoja yako inanguvu kiasi gani
 
Nashukuru.
Uje úkiwa na hoja kuntu na ZENYE mashiko. Kizazi Hiki kinahitaji hoja zaidi kuliko zile hadithi zetu za Zamani za sungura na Fisi
Zamani mahari ilikuwa ni shukrani kwa mzazi wa mtoto wa kike.. Mahari ilikuwa ni kuunganisha koo mbili tofauti.. Ilikuwa heshima kwa mzazi wa mtoto kike..

Leo hii mahari haijabadilika maana yake katika jadi zetu bali imeongezeka.. Mahari ni ishara ya utayari wa mtoto wa kiume kuingia katika ndoa.. Mahari kwa asilimia kubwa ni usalama wa mtofo wa kike katika mahusiano.. Mahari ni kutimiza mapenzi ya Mungu.. Kumbuka Yakobo alifanya kazi miaka 14 kama mahari ya wake zake wawili..

Mahari kwa kiasi kikubwa inamfanya mtoto wa kike awe na amani na utulivu katika mahusiano akitambua fika kuwa mtu aliyenaye ni wa uhakika.. Mahari inaonyesha umakini wa kijana wa kiume katika ndoa..
Naomba niishie hapo.. I stand to be corrected..
 
Kitu kikiwa kwenye Biblia au Quran au kitabu chochote hakimaanishi kitu hicho ni lazima au ni Sahihi.
Labda kitu hicho kiwe ni neno la Muumba mwenyewe, amri na sheria yake.
Na sio Mapokeo ya Watu.
Hata kwenye Biblia na Quran kuna Mapokeo ya wanadamu hicho ndicho nikisemacho.

Kula chuma hiyo;
Marko 7
7 Kuniabudu kwao ni bure. Wanafundisha watu amri zao badala ya sheria yangu.’ 8 Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushikilia desturi za watu.”9 Akawaambia, “Mnaepuka kwa ujanja amri za Mungu ili mpate kutimiza desturi zenu!

Mathayo 15:
7Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu:
8‘Mungu asema: Watu hawa huniheshimu kwa maneno tu,
lakini mioyoni mwao wako mbali nami.
9Kuniabudu kwao hakufai,
maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.’”

Sasa unaweza ukatupa sheria au amri ya Mungu inayotaka Watu walipe Mahari.
Nafikiri unajua Sifa za amri na sheria za Mungu.
Karibu kwenye reference,
Katika Qur'an haina mapokeo ya watu usizue! Lete ushahidi.

Qur'an ni true revelation from Almighty Allah.

Biblia ndio kuna maneno mengi ya watu yenyewe inajitambulisha hivyo.

Wakorintho wa vitabu vinginevyo.
 
Mahari ni swala lililoegemea katika misingi ya Kidini/imani na tamaduni za kimakabila/mila.

Ndoa nyingi zimefungwa katika misingi ya aina hiyo (kidini/kimila) misingi ambayo mahari ni sehem ya jambo la wajibu katika kukamilika kwa tukio lenyewe (ndoa)

Tunaweza kutoa maoni juu ya kinacho tolewa as mahari ikiwa itatumika kama fursa ya mtu/watu kumkomoa mtu au kuona hiyo ndio njia ya kutoka kimaisha... na maoni yetu yakapokelewa.

Ila maoni juu ya kutokuwepo kwa mahari katika ndoa hayana nafasi katika misingi ya ndoa kidini hasa uislam.
Kwa sababu mahari ktk uislma ni jambo la wajibu, japo sheria haikuweka bayana juu ya nini kitolewe na kwakiwango gani. Ila makusudio ni kuwepo kwake...


Nje na misingi ya Kidini au kimila mahari si jambo lililotiliwa mkazo, linaweza kuwepo na hata lisipo kuwepo haliathiri wala kuzuia ndoa isifungwe, muhimu ni makubaliano ya wanao oana, uwepo wa mashahidi na mfungisha ndoa.
 
Back
Top Bottom