Mahojiano ya Rostam na Tido Mhando ni maigizo kwa 100% (staged interview)

Mahojiano ya Rostam na Tido Mhando ni maigizo kwa 100% (staged interview)

Bwahahahahahaaaaa!
Si ajabu amemeza tu kama lilivyokuja.
Most likely ulikuwa kindergarten na hujui kitu gani kilikuwa kinatendeka. Nimetoa hizo links pitia kwanza usome ujielimishe. Watu tulikuwa na copies za hiyo mikataba feki ya Rostam kulipwa fedha na BOT!!!
 
Rostam aziz Yuko smart Sana,
Ile interview kiukweli imenimotivate Sana,
Inabidi watz tuache roho za Kwanini,
Ifike hatua tufurahie mafanikio ta mtanzania mwenzetu, na sio kujenga chuki.
Ni kosa kwa jamii kuelekeza chuki kwa Rostam, badala yake chuki ielekezwe kwa viongozi wenye kumpa access na "mali za umma" utaratibu usio sahihi. Kiuhalisia, kukinzana na Rostam ni kukinzana na serikali inayo mu entertain.
 
Rostam aziz Yuko smart Sana,
Ile interview kiukweli imenimotivate Sana,
Inabidi watz tuache roho za Kwanini,
Ifike hatua tufurahie mafanikio ta mtanzania mwenzetu, na sio kujenga chuki.
Tufurahie mafanikio hata kama mafanikio hayo yanapatikana Kwa kuteka watu kuwaua na kuingia mikataba isiyo natija Kwa Taifa ili watu wachache waliopo ktika cycle Yao wapate kunufaika !??

Mkuu you're better than this kinacho fanywa na hao Jamaa ni ujambazi ni sawa na useme kwamba Majambazi yanapaswa kujivunia Kwa kile wanacho kifanya maana kina wapa mafanikio licha ya kwamba kazi Yao inaumiza watu wengine na kudhulumu haki ya uhai wa wengine
 
Kwamba unauliza, ina maana wewe ndio hujui hata EPA ni kitu gani. Sina muda wa kukueleza labda nikupe links hizi zingine fanya research mwenyewe.



Nakuongezea na hii link


Kwamba unauliza, ina maana wewe ndio hujui hata EPA ni kitu gani. Sina muda wa kukueleza labda nikupe links hizi zingine fanya research mwenyewe.



Nakuongezea na hii link

Na hii tena
 
Nimesikiliza na kutazama kwa makini mahojiano kamili kati ta Rostam Aziz na Tido Mhando ambayo yamerushwa hewani kupitia Azam Tv (UTV) kuanzia mida ya saa tatu usiku mpaka mida ya saa nne na dakika kadhaa usiku huu (tarehe 5/9/2025). Na bila kumumunya maneno, mahojiano yale yalikuwa ni maigizo ya kisanii (full staged), yaani Tido Mhando 'ametumika' kufanya coverage, maswali yaliandaliwa na majibu yakaandaliwa na wahusika walifanya mazoezi ya pamoja ya mahojiano, ushahidi ni huu hapa.

1. Mahojiano hayakuwa live na yalikuwa na vipande vingi vilivyokatwa katwa na kuungwa ungwa kiufundi baada ya kuhaririwa kabla ya kurushwa hewani.

2. Maswali yote Tido alikuwa akiyasoma kwa mtitiriko kutoka kwenye notebook yake na Rostam alikuwa akiyajibu kwa mtiririko huku akionyesha kama anayajua maswali yote na mtiririko wake.

3. Kuna maswali kadhaa hayakuwa relevant kabisa na lengo la mahojiano yale lakini yaliulizwa kimakusudi ili kumpa Rostam public sympathy and positive attention (kwa mfano suala la bima ya Afya, utoaji misaada kwa jamii nk).

4. Katika maswali yote ya msingi ambayo Tido aliuliza hakuna hata swali moja Tido aliamua kumbananisha Rostam katika kona ya kumchimba. Yaani jibu la msingi la Rostam lilishindwa kuzaa swali la kukera kutoka kwa Tido Mhando. Kwa kifupi kabisa, Tido Mhando alilidhishwa na kila jibu la Rostam katika swali la msingi.

5. Kuna maswali mengi sana ya kimsingi ambayo Tido alikwepa kabisa kumuuliza Rostam Aziz. Ni kama vile Rostam alitaka kuulizwa yale maswali ambayo angependa tu kuulizwa na sio vinginevyo. Kwa mfano, utata wa kifo cha Magu nk.


NOTE:
Kwa wataalamu wa tasnia ya uandishi wa habari wakichunguza haya mahojiano wanaweza kumtazama Tido kama mwandishi asiyekuwa na chembe ya sifa za uandishi wowote wa habari ukiwa utamlinganisha na mwanafunzi yoyote wa ngazi ya cheti aliyejiunga na chuo cha uandishi wa habari na kukaa darasani nusu mwezi kujifunza uandishi wa habari. It was a poor interview!
Rostam alitakiwa kuhojiwa na Dada yangu Mange Kimambi, Maria Sarungi au Polepole wengine hao ni maigizo mxiuuu
 
Kwa mananchi yenyewe hamnazo. Iba tu..yaani mwizi anaambia yupo humble
Kwakuwa hata usipoiba hakuna faida utapata mkuu .

Mimi mwaka 2022 niliiba vishikwambi 100 nikauza 50-80K so ukiwa mzembe ur going to die poor.

Kwakuwa Tanzania huwa hatulipwi mshahara Ila tunalipwa posho.

MTU unalipwa 1M na Una miaka karibia 40 Una watoto wanasoma , n.k usipoiba utawezaje kumudu gharama za maisha
 
Nilichogundua,
Rostam aziz ni mtu humble na Yuko poa Sana tofauti na wengi wanavomzungumzia,

Nilitarajia atakua na kebehi na maneno ya shombo Kama wanasiasa wetu wanavokurupuka.

Jamaa Ana vision kubwa sana ya kimaendeleo, sio TU Kwa nchi, Bali Hata Kwa uchumi WA mmoja mmoja.

Kwa wafanyabiashara WA ndani na wawekezaji WA kitanzania.

Kama kweli mlipata kumsikiliza kipind Cha uzinduzi WA dira ya taifa, pia Leo kwenye mahojiano na Tido.

Mtangundua kua,
Sekta binafsi imepata mtu poa Sana WA kutuzungumzia na kutupigania tusonge mbele.

Binafsi,
FROM THE BOTTOM OF MY HEART,
NMEMWELEWA SANA ROSTAM AZIZ🙏
Kwako wewe maybe ni boss wako
 
Kwa majibu ya wengi kuhusiana na mahojiano ya RA na TM inaonyesha kuwa Tanzania bado tunasafari ndefu ya kuzuia ufisadi na wizi wa mali za umma. RA hata angekuwa tajiri vipi lakini kama ananufaika kupitia kuiba na kufisadi rasilimali zetu akishirikiana na uongozi wa nchi ulioko madarakani kwakweli hastahili kutetewa kusifiwa.
 
Tido muhando salimu kikeke kitenge zuhura yunus wapo kwwnye payroll za wanamtandao
 
Rostam aziz Yuko smart Sana,
Ile interview kiukweli imenimotivate Sana,
Inabidi watz tuache roho za Kwanini,
Ifike hatua tufurahie mafanikio ta mtanzania mwenzetu, na sio kujenga chuki.
Ww unajulikana ni ...
 
Back
Top Bottom