Mahojiano yangu na washirika wa FDLR kuhusu uhasama wao na RPF- Inkotanyi

Mahojiano yangu na washirika wa FDLR kuhusu uhasama wao na RPF- Inkotanyi

INAENDELEA.............!!!
KITABI NEAR NYUNGWE NATIONAL PARK 1993.
Afande""F"" anasema baada ya kuweza kuwashawishi wakuu wake wa kijeshi wakubali kurudi nyuma mpaka mjini Bugarama na wapafanye pale kama makao yao makuu ya kijeshi kwa mda.
Anasema alifika katika mji mdogo wa Kitabi ambao bado ulikua chini ya majeshi ya serikali na alijisikia vibaya sana kushuudia maiti za watu zikiwa zimelala hovyo barabarani.
""""""""""""Namnukuu"""""""""""""
Mimi ni mwanajeshi ila kuua raia wasio na hatia ilikua inanikwaza sana.
Raia hawa walikuawanakimbia mapigano na walijikuta ama katikati ya vikosi vya serikali na waasi au ama wanajeshi wa vikosi vya serikali na intarehamwe waliokua wanaua watu kimakusudi kwa sababu za ukabila na chuki binafsi na ushawishi wa wanasiasa na iliumiza sana.
Hivyo hivyo upande wa RPF nao walikua wanaua raia kwa kuwasingizia kua ni washirika wa intarehamwe na vikosi vya Serikali ya Juvenail.
"""""""Mwisho wa kunukuuu""""""""""""
Anasema wakati huo huo vikosi vya RPF navyo vilikua mjini humo na kulikua na mapigano ya ana kwa ana kwa zaidi ya masaa tisa.Yalikua mapigano ya nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa na yalikua mapambano makali kweli kweli sababu vikosi vya RPF vilikua vinashirikiana na vikosi vya Uganda waziwazi na hata afande""F""alithibitisha hilo kwa kukagua na kuona maiti kadhaa za wanajeshi wa Uganda ndani ya vikosi vya RPF.
Anasema wanajeshi wa RPF walikua na silaha nyingi mpya ambazo zimetokea urusi.Na hata rafiki yake wa zamani bwana PAULO alimwambia kua namnukuu hapa.
PAULO: Kama nyinyi mnavyofadhiliwa na wafaransa na hata sisi tunadhaminiwa UPDF.
PAULO: Wafaransa wametusaliti na sisi hatuwategemei tena kwa sababu wanaupendelea upande wenu na kushindwa kuzuia mauaji ya watu wetu kwenye makambi ya wakimbizi.
Mwisho wa kumnukuu.
Anasema afande"f" kilichokua kinawagharimu wanajeshi wake ni ule morali wa kupigana ulikua chini sababu walikua wakijua wazi kua karibia asilimia 75% ya nchi nzima imeshachukuliwa na RPF.Na ilikua haina maana kupigana na wanyarwanda wenzake na waganda wakati wakuu wake kijeshi wameshakimbilia mjini Bugarama,na ilikua sio ajabu kusikia kua tayari wameshavuka mpaka na kukimbilia nchini Zaire
Ilibidi aje na mbinu mpya kama kamanda wa kikosi chake chenye wanajeshi 4800 ukijumlisha na majeruhi na wale waliofia pale mjini Kitabi toka mapambano ya asubuhi mpaka saa kumi kasoro jioni siku hiyo.
Aliamua kuwaambia wanajeshi walio chini yake wajigawe katika SEHEMU KUU NNE
SEHEMU YA KWANZA: Wabebe majeruhi na kuelekea mjini Bugarama na sehemu hiyo hiyo ya kwanza wafukie maiti za wanajeshi wote watakaoweza kupatikana haraka iwezekanavyo kwa kuzifukia kwenye mashimo mafupi fupi ili kutowapa faida adui na kuheshimu wanajeshi waliofia vitani.
SEHEMU YA PILI: Wahakikishe wanarudi nyuma huku wakiwa na logstic zote muhimu ambazo wamezitoa kwenye mstari wa mapambano ili zisiharibiwe na adui.Maana haina maana kuharibu logistic muhimu wakati vita venyewe hali halisi inaonyesha kabisa wameshashindwa kimkakati.
SEHEMU YA TATU: Ni kikosi cha makomandoo waliokua chini yake wakati anamlinda raisi,, kikae tayari kumsubiri kwa amri yake yoyote ile.Walikua askari wa kikomando wa kikosi cha kumlinda raisi akiwa aridhini ambao idadi yao kamili ilikua 1800 na logistic zao walizotoka nazo mjini Kigali mpaka mjini Gitarama.Na hiki ndicho kikosi ambacho afande ""F""alivuka nacho mpaka Bukavu na ni batalion za mwanzo kabisa za wanajeshi wa FDLR PHASE ONE.
SEHEMU YA NNE: Ni makuruta wa jeshi ambao hawana tofauti na intarehamwe ila wao wanavaa sare za kijeshi na aliwakuta tayari mjini Kitabi wakitokea mjini Munini na Ruramba walikokimbia baada ya kushindwa na vikosi vya serikali ambao aliwaweka wawasumbue waasi ili wasijue kama vikosi vyote vya serikali vinarudi nyuma.
Afande""F"" anasema yeye plan yake ilikua ni kwenda mpaka mjini Kamembe na akiona vikosi vya RPF vinamkaribia basi atavuka ziwa Kivu na kuelekea mjini Bukavu.
Afande anasema kua aliachana na maagizo ya wakuu wake wa kijeshi na kuamua yeye na ataingoza vikosi vyake kwa njia sahii anayoiona inafaa ili waweze kurudi nyuma wakiwa salama na jukumu lake la kuwazuia RPF aliachana nalo kwa sababu moja kuu.Anasema ukiwa na akili timamu hata kama una kikosi cha askari makomando 1800 waliojizaziti,huwezi kuzuia kombania zaidi ya kumi za wanajeshi 6000 wa waasi kukushambulia.Chaguo sahii ni kurudi nyuma na kujipanga upya either kwa mapambano au kukimbia au kusalimu amri.
Hivyo kanali f au afande"f" aliamua kuangalia mustakhabali wa yeye na askari wake.Hadi kufikia mda huo hakua na mawasiliano na wakuu wake wa kijeshi mjini Bugarama na alikua hataki kabisa kuwasiliana nao.
NB: KUMBUKA HAPA NAWAVUTA TARATIBU ILI TUJUE MWANZO WA KUUNDWA KUNDI LA FDLR CHINI YA AFANDE""F"" NA UHASAMA WAKE NA RPF - INKHOTANYI
ITAENDELEA...........!!!!!!!
 
SASA TUENDELEEE...................!!!
SAFARI YA KANALI""F"" KURUDI NYUMA MPAKA MJI WA KAMEMBE NEAR ZIWA KIVU.
Haikua kitu rahisi kwa kanali f kurudi nyuma mpaka mji wa Kamembe.
Kwanza alikua na uchungu mkubwa moyoni katika vitu vikuu vitatu.
MOSI: Yeye aliamini kua rwanda imetumbikizwa kwenye vita na mauaji na wanasiasa wenye uchu wa madaraka.Na aliamini kabisa wakuu wake wa kijeshi walimgeuka hasa katika yale makubaliano ya Arusha Tanzania ya kusitisha vita.
PILI: Kanali au afande"f"aliamini kua waasi wa RPF wamemsaliti kwa yale yote waliyokubaliana mwaka 1987 na 1992 na nia yao ilikua ni kuchukua nchi na kumfukuza yeye na wahutu wwngine nao wakaonje adha ya kua wakimbizi ughaibuni.
TATU: Aliamini wafaransa walihusika na kupanga mauaji ya kimbari kwa kuwashawishi wakuu wake wa kijeshi kutekekeza mauaji hayo na vivile walihusika na kumuua raisi Juvenal ambae alikua bosi wake na alikua anamlinda mpaka siku ile aliyosafiri kwenda nchini Tanzania.
NB: KUMBUKA YEYE KANALI ALIKUA ANAMLINDA RAISI AKIWA ARDHINI NA SIO ANGANI...JUKUMU LA KUMLINDA RAISI AKIWA ANGANI HALIKUA LAKE YEYE.
Anasema raisi Juvenal alimwambia maneno haya kabla hajapanda ndege kwenda mjini Dar es salaam nchini Tanzania.
""""""""NAMNUKUUU""""""""""""""
JUVENAL : Kanali kama unavyoona hii hali ya kivita sio nzuri upande wetu na hata hawa wanajeshi 600 wa RPF waliopo hapa Kigali mimi siwaamini kabisa katika lolote,,,,maana wapo karibu na uwanja wa ndege,hivyo wanaweza kuniua wakati wowote.
AFANDE""F"": Mkuu najua na ningekushauri ukirudi kutoka Tanzania basi makao yako makuu yahamishie mjini Gitarama.
JUVENAL: Sawa Kanali nimekuelewa na nikirudi tutajadili hili suala kwa kina.
AFANDE""F"": Nikutakie safari njema mkuu
JUVENAL: Ilinde familia yangu kwa gharama yoyote ile Kanali sawa.
JUVENAL: Ni aibu sisi kushindwa na RPF na sura yangu nitaiweka wapi.
JUVENAL: Tafadhali Kanali ilinde familia yangu kwa gharama yoyote ile.
JUVENAL: Najua wewe na Aghata mna tofauti zenu,,lakini usisahau yule ni mke wangu na usisahau pia wewe ni mdogo wangu Kanali.
JUVENAL: Na tumetoka mbali sana mdogo wangu toka nilipokutoa jeshini miaka ile
AFANDE""F"": Sawa Mkuu (copied) huku akipiga saluti na hiyo ndio ilikua saluti yake ya mwisho na mazungumzo yake ya mwisho na raisi Habyarimana akiwa hai ikulu.
Afande anasema na hili lilikua linamuuma sana sababu alijua mkuu wa vikosi vya kulinda wanadplomasia wa RPF waliokua Kigali kwa mujibu wa makubaliano ya amani ya Arusha.
Brigedia Rwegema alihusika na mauaji ya Rais Juvenal.
NB: Brigedia Rwegema na yeye aliuawa katika mazingira ya kutatanisha wakati waasi wa RPF wanaichukua na kuidhibiti Kigali.
Basi afande""f""aliendelea na utaratibu wa kujihami huku akirudi nyuma mpaka mji wa Kamembe akiwa na askari makomandoo 1800 na malori ya kijeshi 116 na magari ya deraya 66 na maroli ya kawaida 75 na vifaru 14 na askari wa miguu wasiokua makomandoo zaidi ya 3000,hapa ukijumuisha na vikosi vya wanamgambo wa kiraia ambao ni tofauti na intarehamwe militias.
Hakutaka kupigana au kuzuia waasi wa RPF kuchukua miji ya Rulamba na Kitabi sababu aliona hakuna sababu ya kupoteza nguvu kazi kwa jambo lisilowezekana kwa namna yoyote ile iwe kiualisia au kidhaaniana maana tayari kimahesabu walikua wameshashindwa vita na RPF.
Mnamo tarehe 26 january 1994 ilimkuta afande ""f"" akiwa mjini Kamembe akiwa amechoka na amepoteza mawasiliano kati yake na wakuu wake wa kijeshi.
NA WAZO KUU LILIKUA NI KUVUKA ZIWA KIVU NA KUINGIA ZAIRE NA KUJIPANGA UPYA KIJESHI NA KUANZISHA UPYA MAPIGANO ILI KURUDISHA NYUMA VIKOSI VYA RPF VILIVYOKUA VIMETAMALAKI NCHI NZIMA YA RWANDA MPAKA WAKATI HUO JANUARY 26 1994
Na alichukua simu ya upepo na kumpigia rafiki yake wa zamanj na adui yake kwa sasa PAULO mjini Kigali na kusema maneno haya.
AFANDE: PAULO UMENISALITI
PAULO: KANALI WALIOKUSALITI NI RDF WOTE KWA KUSHINDWA KUPIGANA KWENYE UWANJA WA MAPAMBANO NA KUISHIA KUUA RAIA WA KITUSI
AFANDE: HUKUTIMIZA WAJIBU WAKO
PAULO: NI KWELI ILA NDIO SIASA HIZO
AFANDE: NA ULIBUNI MAUAJI YA HALAIKI
PAULO: UNA USHAHIDI KANALI??
AFANDE NDIO PAULO NINAO
PAULO:UR DEAD KABLA HAUJAONEKANA
AFANDE: NIFE MARA NGAPI PAULO?
PAULO: UNANIJIBU KWA UJEURI SABABU YA HUYO MZEE MOBUTU?
NINA VIKOSI HUKO KIVU NA VINASUBIRI TU AMRI YANGU KUMSHAMBULIA HUYO MZEE MLA RUSHWA
AFANDE: WE ARE ENEMIES NAKUJIBU HOW I FEEL TOWARDS YOU
AFANDE: KWA SABABU ULINISALITI BASI HAUTOKAA KWA AMANI TAKE THAT CARD YOU PLAYED ONCE.
PAULO: HABARI ZA RWEGEMA UNAZO?
PAULO: BAS NA WEWE UTAISHIA HIVYO
AFANDE: NIMEKUPIGIA SIMU KUKUAMBIA BADO SIJAFA NIPO NA NINAONDOKA NDANI YA RWANDA KWA SASA ILA NITARUDI MDA SI MREFU NA WEWE UNAJUA HILO.
NA KAMA ULIMUUA REGWEMA,HUO NI UOGA WAKO NA TAMAA ZAKO ZA MADARAKA PAULO NA MIMI HILO HALINIHUSU.
BAS AFANDE"F""AKAKATA SIMU YAKE YA UPEPO NA IKUMBUKWE HAPO ALIKUA MJINI KAMEMBE NJE KIDOGO YA ZIWA KIVU NA HIYO ILIKUA JANUARY 26 1994.
NA HII SIKU NDIO WAZO LA FDLR LILIPOZALIWA KICHWANI MWA KANALI AU AFANDE""F"""
ITAENDELEA...............!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom