Mahusiano ya kimapenzi kati ya kaka na dada wa tumbo moja

Mahusiano ya kimapenzi kati ya kaka na dada wa tumbo moja

Hii sio jambo jema kabisa, ila tatizo ni pale mkuyenge unapo soma 4G hapo hua ni vigumu kuangalia sura.
 
Mi nadhani chanzo kinaanzia kwenye malezi na lifestyle ya familia, hii dhana ya kujenga majumba yenye fence na kuwazuia watoto wasiende kuchanganyika, ina athari nyingi sana kwa socialization ya mtoto.

Kuna umri mtoto anahitaji kujua na kufaham yale yaliyo nje ya uzio wa home kwa ku practise, sio kwa socio media wala kwa TV.

Mbali ya shule, inabidi mtoto kujua kama mtaani kuna watu wanaitwa "Wajuba" , "Mabaharia" n.k.

Wazazi kuweni makini kweny ulezi, yaani hapo mawili kama sio hili mnalosema linakuja kwa kasi basi linatokea lile la ushoga na usagaji, inategemea na structure ya familia.


Alexander
 
Haya mambo yalikuwepo ila ilikuwa ni siri kubwa sana na wazee walijua sana kutunza siri na waliweka mazingira ya kuweka vijana wao mbali na Dada zao hivyo walilijua hili.

Mimi babu Yangu alikuwa hapendi kabisa nikae jikoni au nyumbani na wanawake alipenda nifanye Kazi au nitembee ntarudi wakati Wa kula.

Lakini siku hizi watoto wakiume na Wa kike wamewekewa ukaribu mkubwa sana hasa familia zenye kauwezo hivyo hii huwa inachagiza kuwaona Dada zao kama wanawake wengine na wanaona ni jambo la kawaida.



Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi mara wakumbatiane mara kiss za undungu mara aitwe dada kipenzi ndiyo mwisho wa siku inakuwa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nadhani chanzo kinaanzia kwenye malezi na lifestyle ya familia, hii dhana ya kujenga majumba yenye fence na kuwazuia watoto wasiende kuchanganyika, ina athari nyingi sana kwa socialization ya mtoto.

Kuna umri mtoto anahitaji kujua na kufaham yale yaliyo nje ya uzio wa home kwa ku practise, sio kwa socio media wala kwa TV.

Mbali ya shule, inabidi mtoto kujua kama mtaani kuna watu wanaitwa "Wajuba" , "Mabaharia" n.k.

Wazazi kuweni makini kweny ulezi, yaani hapo mawili kama sio hili mnalosema linakuja kwa kasi basi linatokea lile la ushoga na usagaji, inategemea na structure ya familia.


Alexander
Uko sahihi maana mtu akikosa msaada kwa jilani anaanza kufanya kutafuta solution hapo hapo kwa ndugu zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku niliko kunakaka amezaa na mkewe

Na mdogowake huyo kaka pia anatoka na mdogo wa mke wake ,

(ingawa hawa wakike baba mmja mama tofauti inakaaje, hii)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jibu ni kwamba huo ni ushetani! Watoto wa familia moja hamuwezi kufanya hayo! Huwezi kukaa karibu na Dada zako nyumbani kama wewe ni mtoto wa kiume utaenda kucheza na rafiki zako! Dada zako wako home! Mawazk hayo yanakuwaje!
Huu ni ushetani kweli

121.
 
Hiyo ni kutokana hasa familia za geti kali. Watoto unawazoesha kuwa pamoja wa kike na wa kiume muda mwingi. Watoto hawaoni mambo mengine huko nje. Na mbaya sana kama mkubwa ni wa kiume. Watoto wa kiume anachelewa zaidi kukua kiakili kuliko wa kike. Kama hicho kisa cha kwanza huyo wa miaka 17 angekuwa wa kike then huyo wa 15 awe wa kiume isingetokea hivyo,sabubu ni moja huyo wa miaka 17 angekuwa wa kike angejielewa mapema yeye ndio wa kuulizwa hivyo angejielewa mapema hata kama wangefanya wasingepata mimba. Tatizo la kike kuwa na umri mdogo kuliko wa kiume ni kwamba sasa hao wa kike wakawekeza akili yao yote kwa kakaako,kwamba ndio kiongozi wao,chochote atakachofanya kwao ni sawa,ksbb ndio kiongozi wao. Kisa cha pili ni bora tu ujitenge na ukoo muoe tu dadaako endelea maisha mapya kivyako. Watakuelewa mbele baada ya kuendeleza kizazi,piga sana watoto. Uwe nao hata 8.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEX TALK!
Niliandika kuhusu mahusiano ya kingono miongoni mwa wanafamilia. Halafu Jana nikakutana na kisa cha mjane ambaye watoto wake wawili wamepewa mimba na kaka yao.

Wengi hawaamini wanadhani ni hadithi za kufikirika. Ukweli ni kwamba haya mambo yapo ndani ya jamii ila Mara nyingi hufanywa siri sana. Ukiacha huyu ambaye wamepata mimba kuna ambao hawapati mimba na huendelea na hiyo michezo.
Niliwahi ongea na binti ambaye hataki kuolewa sababu ana mahusiano ya kingono na kaka yake. Na alikua akibeba mimba anatoa, kaka MTU alipooa ikawa vita na WiFi mpaka ndoa ikavunjika, kaka akachukua mdogo wake kuishi naye. Wazazi hawajui kinachoendelea wanajua ni upendo wa kindugu tuu.

Nyakati hizi zimebadirika sana, unapoongea na watoto wengi wanakwambia wamefundishwa ngono na ndugu zao wa karibu.

Hata wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (usagaji na ushoga) wengi wao huanzia nyumbani. Akitoka hapo ndiyo ataenda kwa watu wengine.

Nyakati hizi kuna matumizi ya simu na kompyuta, watoto wanaangalia picha za ngono. Hawa ambao wapo kwenye umri wa balehe ni hatari zaidi, wakishaona hizi picha wanatamani kujaribu walichokiona, sasa wahanga wa karibu ni wale walio karibu naye..

Mambo yamebadirika sana, usiogope kuongea na watoto wako. Ongea nao kwa uwazi kulingana na umri wao.

Pia tupunguze uzungu, mambo ya kupakatana na kukumbatiana Dada na kaka ni hatari. Unakuta binti amevaa kikaptura, tumbo wazi, vichuchu vimechomoka anazunguka humo ndani na kuna kaka zake.. Huyu kaka ambaye anakula na kushiba, anashinda nyumbani anamtizama Dada anazunguka tuu ndani, mbaya zaidi awe ametizama hizi video za ngono unatarajia nini?

Tuwafundishe watoto wetu kuwa na adabu. Wajiheshimu na kujitunza miili yao wao wenyewe. Waambie madhara ya ngono kati ya ndugu. Wajifunze kuheshimiana waoa kwa wao .

Wakati huu wapo nyumbani wasikae tuu, watafutie shughuli za kufanya katika mazingira waliyopo. Walime bustani, Michezo mbali mbali, inayoweza kuwafanya wachoke, wapangie shughuli mbalimbali za mikono, zitakazowatoa jasho. Kuna msemo usemao "an idle mind is the workshop of the devil" . Hawa vijana waliobalehe miili yao INA nguvu na wana mihemko, ndiyo maana hata shuleni huwa wana ratiba za kufanya mambo mbalimbali nje ya masomo ili wasikae bure.

Kuna ambao wanapewa masomo kwa njia ya mtandao, ni bora ukawatolea kwenye karatasi(download) kuliko ukawapa simu maana ni wadadisi, hawataishia kusoma masomo yao tuu, watatafuta zaidi.

Watoto wa kizazi hiki wanajua mengi kuliko unavyojua we we . Unaweza fikiri hajui kutumia simu, kumbe anaijua kuliko wewe unayeimiliki.

Tenga muda wa kuongea na watoto wako, watafutie filamu,vitabu na majarida yanayofundisha kuhusu vijana na ujana,mahusiano na ngono.

Zaidi ya yote WAOMBEE SANA, shetani yupo kazini,anaandaa jeshi lake na hawa watoto ndiyo wanatakiwa sana. Kwasabau wao ni rahisi kuamini na kusambaza mambo haya. Hivyo pamoja na kuongea nao wakabidhi kwa Mungu, maana kuna mambo ambayo kwa uwezo wetu ni magumu na hatuyawezi. Kuna mambo watoto wanafanya ukisikia masikio yanawasha.

#MZAZI ONGEA NA MWANAO

Mwl. Doris Mboma
 
Back
Top Bottom