Mahusiano ya kimapenzi kati ya kaka na dada wa tumbo moja

Mahusiano ya kimapenzi kati ya kaka na dada wa tumbo moja

Inategemea ukaribu wao dada na kaka, na pia inategemea mazungumzo yao kaka na dada ni aina gani, hivi viwili huleta mahusiano ya karibu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtu mwenye akili sawa, hata ukiwa unaimbisha kabinti dada yako wa damu akapita, stimu zinakata sasa sijui unaanzaje kushika hata chupi ya dada ako
 
Mabinti siku hizi wanamavazi ya ajabu sana.
Niliwahi kuongea na ndugu mmoja,
Alinambia x anavaa vibaya sana.kwa mwanaume rijali yoyote hawezi kuvumilia uvaaji ule akamwacha apite salama.
Alinambia hajawahi fanya naye chochote,
Ila aliwahi mtamani kwa sababu ya mavazi yake anayovaaa

My take....wazazi wawe waangalizi na mavazi wanayovaa watoto mbele ya ndugu zao.kaka mmoja...
Acheni uzungu...
 
Haya mambo yanawatokea tu wale wanaoyaanza wakiwa wadogo hata wasijue kuwa sio sahihi..wakija kujua its wrong wamenogewa,wanateseka kuacha,kama ushoga vile


There's no way una mahusiano na watu nje ya familia afu uweze kuwa na mahusiano na ndugu zako pia..haipo
 
Mabinti siku hizi wanamavazi ya ajabu sana.
Niliwahi kuongea na ndugu mmoja,
Alinambia x anavaa vibaya sana.kwa mwanaume rijali yoyote hawezi kuvumilia uvaaji ule akamwacha apite salama.
Alinambia hajawahi fanya naye chochote,
Ila aliwahi mtamani kwa sababu ya mavazi yake anayovaaa

My take....wazazi wawe waangalizi na mavazi wanayovaa watoto mbele ya ndugu zao.kaka mmoja...
Acheni uzungu...
Kuna ukweli hapa
 
1. Usiruhusu Watoto wako wa kike na wakiume kulala chumba kimoja au kitanda kimoja hata kama ni wadogo kamwe usiwazoeshe kulala kitanda kimoja, weka mpaka kati ya wakike Na wakiume.

2. Zungumza Na wanao mara Kwa mara, wafumdishe maadili mema haswa ya kuheshimiana Na pia kujitambua , dada ni nani Na kaka ni nani.

3. Hakikisha wanao wanapata mafundisho ya kidi, nyumbani au kanisani au madrasa au msikitini bila kukosa.

4.
 
mara nyingi hii inatokana na too much uzungu na jufungia watoto ndani..ni bora kumfungia kijana wa kiume na beki 3 ndani kuliko yeye na dada yake hususani kwa vijana waliopo kwenye kipindi cha balehe.......mwisho wa siku huwa wanakulana wenyewe kwa wenyewe...

jamani jambo la msingi ni kuwapa elimu ya afya ya uzazi na kuwapa freedom huku ukimonitor mwenendo wao..lasivyo utavuna viumbe visivyokuwa na majina....
 
Hilo la kufuatilia ukoo nakubal asee..niliishi sehemu moja..
Kaka na Dada walikuwa wanakulana ikaleta shida.. Uncle yao mmoja akawa anwapa hela ya guest wasiwe wanafanyia nyumbani..
Kuja kuskia..karbia robo ya ukoo wanakulana..ko ishakuwa kama laana wao wanaona kawaida tu
 
Hiyo ni kutokana hasa familia za geti kali. Watoto unawazoesha kuwa pamoja wa kike na wa kiume muda mwingi. Watoto hawaoni mambo mengine huko nje. Na mbaya sana kama mkubwa ni wa kiume. Watoto wa kiume anachelewa zaidi kukua kiakili kuliko wa kike. Kama hicho kisa cha kwanza huyo wa miaka 17 angekuwa wa kike then huyo wa 15 awe wa kiume isingetokea hivyo,sabubu ni moja huyo wa miaka 17 angekuwa wa kike angejielewa mapema yeye ndio wa kuulizwa hivyo angejielewa mapema hata kama wangefanya wasingepata mimba. Tatizo la kike kuwa na umri mdogo kuliko wa kiume ni kwamba sasa hao wa kike wakawekeza akili yao yote kwa kakaako,kwamba ndio kiongozi wao,chochote atakachofanya kwao ni sawa,ksbb ndio kiongozi wao. Kisa cha pili ni bora tu ujitenge na ukoo muoe tu dadaako endelea maisha mapya kivyako. Watakuelewa mbele baada ya kuendeleza kizazi,piga sana watoto. Uwe nao hata 8.

Sent using Jamii Forums mobile app
umechambua kwa usahihi kabisa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEX TALK!
Niliandika kuhusu mahusiano ya kingono miongoni mwa wanafamilia. Halafu Jana nikakutana na kisa cha mjane ambaye watoto wake wawili wamepewa mimba na kaka yao.

Wengi hawaamini wanadhani ni hadithi za kufikirika. Ukweli ni kwamba haya mambo yapo ndani ya jamii ila Mara nyingi hufanywa siri sana. Ukiacha huyu ambaye wamepata mimba kuna ambao hawapati mimba na huendelea na hiyo michezo.
Niliwahi ongea na binti ambaye hataki kuolewa sababu ana mahusiano ya kingono na kaka yake. Na alikua akibeba mimba anatoa, kaka MTU alipooa ikawa vita na WiFi mpaka ndoa ikavunjika, kaka akachukua mdogo wake kuishi naye. Wazazi hawajui kinachoendelea wanajua ni upendo wa kindugu tuu.

Nyakati hizi zimebadirika sana, unapoongea na watoto wengi wanakwambia wamefundishwa ngono na ndugu zao wa karibu.

Hata wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (usagaji na ushoga) wengi wao huanzia nyumbani. Akitoka hapo ndiyo ataenda kwa watu wengine.

Nyakati hizi kuna matumizi ya simu na kompyuta, watoto wanaangalia picha za ngono. Hawa ambao wapo kwenye umri wa balehe ni hatari zaidi, wakishaona hizi picha wanatamani kujaribu walichokiona, sasa wahanga wa karibu ni wale walio karibu naye..

Mambo yamebadirika sana, usiogope kuongea na watoto wako. Ongea nao kwa uwazi kulingana na umri wao.

Pia tupunguze uzungu, mambo ya kupakatana na kukumbatiana Dada na kaka ni hatari. Unakuta binti amevaa kikaptura, tumbo wazi, vichuchu vimechomoka anazunguka humo ndani na kuna kaka zake.. Huyu kaka ambaye anakula na kushiba, anashinda nyumbani anamtizama Dada anazunguka tuu ndani, mbaya zaidi awe ametizama hizi video za ngono unatarajia nini?

Tuwafundishe watoto wetu kuwa na adabu. Wajiheshimu na kujitunza miili yao wao wenyewe. Waambie madhara ya ngono kati ya ndugu. Wajifunze kuheshimiana waoa kwa wao .

Wakati huu wapo nyumbani wasikae tuu, watafutie shughuli za kufanya katika mazingira waliyopo. Walime bustani, Michezo mbali mbali, inayoweza kuwafanya wachoke, wapangie shughuli mbalimbali za mikono, zitakazowatoa jasho. Kuna msemo usemao "an idle mind is the workshop of the devil" . Hawa vijana waliobalehe miili yao INA nguvu na wana mihemko, ndiyo maana hata shuleni huwa wana ratiba za kufanya mambo mbalimbali nje ya masomo ili wasikae bure.

Kuna ambao wanapewa masomo kwa njia ya mtandao, ni bora ukawatolea kwenye karatasi(download) kuliko ukawapa simu maana ni wadadisi, hawataishia kusoma masomo yao tuu, watatafuta zaidi.

Watoto wa kizazi hiki wanajua mengi kuliko unavyojua we we . Unaweza fikiri hajui kutumia simu, kumbe anaijua kuliko wewe unayeimiliki.

Tenga muda wa kuongea na watoto wako, watafutie filamu,vitabu na majarida yanayofundisha kuhusu vijana na ujana,mahusiano na ngono.

Zaidi ya yote WAOMBEE SANA, shetani yupo kazini,anaandaa jeshi lake na hawa watoto ndiyo wanatakiwa sana. Kwasabau wao ni rahisi kuamini na kusambaza mambo haya. Hivyo pamoja na kuongea nao wakabidhi kwa Mungu, maana kuna mambo ambayo kwa uwezo wetu ni magumu na hatuyawezi. Kuna mambo watoto wanafanya ukisikia masikio yanawasha.

#MZAZI ONGEA NA MWANAO

Mwl. Doris Mboma
umetoa somo la kutosha hongera na asante kwa ushauri mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom