Nimekuja kujifunza kitu muhimu sana. CCM na ule mkutano mkuu wao wa kuchagua wagombea wa nafasi ya Urais huwa ndio wenye maamuzi ya mwisho.
Yeyote atakayepitishwa pale, watanzania tupende tusipende ndie atakae kuja kuwa Rais, sasa tatizo linakuja huyo wanaempitisha wamewahi kumfanyia vetting ya kutosha kujiridhisha kama ana weledi na hekima ya kutosha kuliongoza taifa letu.
Inavyoonekana na 2015 in particular, JK alikurupuka kumpitisha huyu mtu, hasa baada ya ushindani uliokuwepo baina ya Membe na Lowassa, akaona bora awatose wote ampitishe jiwe, mazingira ya wakati ule yalimlazimisha kufanya vile, matokeo yake akampa madaraka mtu aliejua vizuri hana tofauti na kichaa, mwenyewe akamuita "bulldozer", matokeo yake sasa kila mtu anajutia matendo ya huyo "bulldozer"
CCM kwa sababu wanalindwa na TISS na vyombo vingine vya usalama, ni wajibu wao kumfanyia uchunguzi wa kutosha mtu wanaetarajia kumpa nafasi ya urais, ili wakati ukifika wasije kuwa na wasiwasi na tabia au matendo ya huyo mgombea wao.
Kinyume na hapo watanzania tutaendelea kuumizwa kwasababu ya ulinzi wanaopewa CCM na TISS, lakini pia; maamuzi ya hovyo yanayofanywa na mwenyekiti wa CCM kwenye kumchagua mgombea wao wa urais.
Uchaguzi wa mwaka huu nadiriki kusema bila shaka; TISS ndio wamehusika kuwapa ubunge Tulia - Mbeya Mjini, Gambo- Arusha Mjini, yule mgombea wao wa Hai, na yule wa Moshi Mjini, na pengine pote ambapo upinzani ulikuwa mkubwa. Wananchi hawakuwa na maamuzi yoyote kwenye kuwachagua hao wagombea wa CCM.