Uchaguzi 2020 Maisha Baada ya Uchaguzi: CCM won the Battle and lost the War

Uchaguzi 2020 Maisha Baada ya Uchaguzi: CCM won the Battle and lost the War

Nimekuja kujifunza kitu muhimu sana. CCM na ule mkutano mkuu wao wa kuchagua wagombea wa nafasi ya Urais huwa ndio wenye maamuzi ya mwisho...
Kuanzia mwanzo mpaka mwisho sugu alikuepo kituoni akahojiwa akasema uchaguzi unaenda vizuri,

Upinzani wa Tanzania tulishawazoea
 
Kuna tofauti ya Barabara ya Ubungo na Mega Projects.

Mega Projects kama ujenzi wa SGR unaohitaji consortium banks ku-finance. Sidhani kama unajua gharama ya huu mradi.

Au Nyerere Hydropower inayochukua karibu 30% ya bajeti yetu ya mwaka.
Kwahio SGR watapanda wabeligiji?
 
Kwani Ukihamia na wewe CCM Kama Mtanzania wa kawaida utapata Hasara gani Mkuu. Hujistukii tu hata hapo ulipo watu hawawazi Kama unavyowaza wewe watu wetulia kabisa maanake we ndo unaakili kuwazidi wao ama?

Upinzani kuongoza Hii Nchi bado Sana. Kama majimboni tu wameshindwa nchi wataiweza kweli Mkuu, Watanzania tumebarikiwa na Mungu, uwe na Imani na uongozi wa Magufuli Ila hao wabunge wenu huko majimboni ruksa kuwa doubt!

Ungeelewa yaliotokea majimboni ungekaa kimyaa.

Nikulipe mshahara gari nikupe nyumba nikupe alafu utangaze mpinzani KASHINDA.

Hayaa maneno yamechangia Sana wateule kuharibu huu uchaguzi.
 
Wacha wote tulimie meno. Mungu anipe uhai mrefu wa kushuhudia nchi yangu inapoelekea
 
Yaani Pimbi wa kutupa mhutu amepanga awape upinzani viti vitano vya ubunge wasivikubali , tiss mnasaidia mgonjwa wa bipolar disorder kuongoza ? Kabisa?
 
Hakuna aliyetegemea uchaguzi uwe wa huru na haki. Lakini hakuna aliyetegemea wizi uwe wa wazi na wa kijinga hivi.

Chama Cha Mapinduzi, kama chama kikongwe barani Afrika, kimethihirisha hakipo tayari kuachia madaraka kwa njia ya sanduku la kura. Si Bara wala si Visiwani.

CCM si chama cha siasa tena, CCM ni mfumo uliyoishikilia nchi hii mateka. Hamna tofauti na CCP China, Putin’s Russia, Kim’s Korea, Castro’s Cuba, Lukashenko’s Belarus, n.k. Mifumo ya kisoshalisti na kikomunisti iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere.

CCM kwanza, Tanzania baadae. Wakuu wa vyombo vya dola pamoja na wakuu wa majeshi wapo kulinda kwanza maslahi ya Mwenyekiti wa CCM kisha CCM na mwisho Tanzania.

Kwao adui wa Mwenyekiti wa CCM ni adui wa Tanzania. Adui wa Chama ni adui wa Tanzania.

Huu uchaguzi ni kichekesho kingine kama ilivyokuwa 1995, 2000, 2005, 2010 na 2015. Mawakala wa vyama vya upinzani wanakamatwa na kutolewa kwenye vituo. Kura feki kwenye mabegi na maboksi zinaingizwa kujumuishwa kwenye mahesabu.

Haya yanasimamiwa na wakurugenzi, wakuu wa wilaya, wakuu wa Usalama wa Taifa na wakuu wa mikoa. Nani mnamdanganya?

Majeraha ya Uchaguzi huu, tofauti na miaka mingine, ni mpasuko mkubwa na kuhatarisha umoja wa nchi.

Watu wameenda kupiga kura ili roho zao ziwe na amani tu, haijalishi mtaiba kura zao au la! Hii ni chuki kubwa imepandwa.

Kibaya zaidi tofauti na watangulizi wa nyuma, Rais Magufuli hajui na hawezi kuunganisha Taifa kwa kauli na matendo yake na amezungukwa na wabinafsi wa hali ya juu.

Ni rahisi kushangilia na kusema wameshinda na kuwagaragaza wapinzani.

Ni rahisi kwa wachambuzi wa mambo ya siasa kusema "Upinzani bado sana" au "Upinzani haukujipanga". Unabaki kujiuliza, kwa mazingira haya unategemea upinzani ujipange vipi ili kuwe na haki.

Media zote zimefungwa mdomo. Hakuna uchambuzi, sharia ni kusoma kile watawala wanataka basi.

Mediocrity (Sabaya, Makonda, Mambosasa, Polepole, Kabudi et al) is the order of the day. Short-termism is the norm.

Ipi gharama ya ushindi huu kwa CCM? Kupasua umoja wa nchi? Kutumia silaha na nguvu kuhalalisha ushindi hakukupi ushindi bali kunakuongezea maadui.

Mfano leo hii Kusini kuna tishio la Ugaidi bado tena unawaibia hao watu haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka. Wakuu wa Usalama na Ulinzi wanategemea nini?

Inasikitisha haya yanafanywa na tume iliyoundwa na Majaji na Wasomi. Haya yanasimamiwa na Majenerali wa vyombo vya Ulinzi na Usalama. Hii yote ni kumfurahisha Mwenyekiti.

Imemchukua Baba wa Taifa zaidi ya miaka 20 na Watanzania wamepitia sacrifices nyingi kujenga Umoja katika nchi hii.

CCM Mpya chini ya miaka 5, inafanikiwa kuvunja hii legacy na kujisifu wao ni wazalendo.

Nchi inaingia kwenye giza kubwa na kuishi mawazo ya mtu mmoja tu ambaye si mwerevu.

Taifa linaelekea kwenye mpasuko mkubwa tokea tupate Uhuru.
Noted
 
Kuanzia mwanzo mpaka mwisho sugu alikuepo kituoni akahojiwa akasema uchaguzi unaenda vizuri,

Upinzani wa Tanzania tulishawazoea
Kura hazikupigwa kituo alichokuwepo sugu tu, hilo jibu alilitoa kwa muktadha wa eneo ambalo yeye alipigia kura
 
Tanzania haitakua the same baada ya huu uchaguzi.

Nchi itaendeshwa kwa mawazo ya mtu mmoja tu. Hakuna opposition nje ya chama wala loyal opposition ndani ya chama.

Itafuatia purge kubwa ndani ya chama na vyombo muhimu vya dola.

Udikteta hauji kwa sababu ya mapenzi juu ya nchi bali hofu baada ya maisha nje ya madaraka kwa maovu waliyotenda.

Uchaguzi huu umetuzogeza kwenye giza nene.
 
Kuna giza nene kwa Tanzania.

Mtu mmoja anaweza kuliangamiza Taifa, na mtu mmoja anaweza kuliokoa Taifa.

Mtu mwerevu, hata akifanya uovu, huwa kuna kiwango fulani cha ustaarabu. Lakini kichaa akiamua kufanya uovu huwa hana haja hata ya kujificha kwa namna yoyote. Anaweza kukuua hata ukiwa umezungukwa na kundi la watu.

Kosa walilofanya CCM mwaka 2015, litaandikwa kwenye historia ya Tanzania na kukumbukwa na vizazi vingi vijavyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jiwe hanatofauti na PAPA DOC Aliekuwa Rais wa Haiti
 
Sikuwahi kuota kama kuna siku Tanzania itakuwa kwenye kiwango hiki cha uharamia.
 
This was expected. Aliyeamini kitu tofauti alikuwa akiota mchana au alikuwa akijifariji moyoni tu ili kujipunguzia stress

Huwezi kushinda uchaguzi kwa TUME hii. Lissu, Zitto, Mbowe etc wote wanajua hili.
Yes, expected but NOT to this level.
 
Huyu bwana aelewe kuwa Nkurunziza hakuuwawa na mtu bali Mungu. sisi tuamini Mungu huyu huyu aliyetulinda kwa corona atashughulika na viongozi wadhalimu
 
Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.
watanzania bado wanaimani na CCM.
 
Back
Top Bottom