Maisha ni kuchagua: Ili kuagiza BMW 3 series cheap kabisa kutoka JP unatakiwa uwe na Mil 14, ila IST lazima uwe na angalau Mil 17!

Maisha ni kuchagua: Ili kuagiza BMW 3 series cheap kabisa kutoka JP unatakiwa uwe na Mil 14, ila IST lazima uwe na angalau Mil 17!

Hiyo BMW, Kwa barabara zetu zinazotengezwa na Wabongo wenye roho za husda, kula ukipita tuta lazima unique TAKO,. Unashangaa gari uko Kwao imebonda km 100,000 lakini Hata kuchunika Bampa hakuna, bongo endesha wiki tu tena umeweka spacer kuifanya gari isiwe stable (Kwa sababu design specs hatikuweka issue ya spacer) lakini bado inakwaruka tu. Huwa inaniuma sana nabaki kuwatukana Hawa mamlaka kututia umaskini.
 
Niliona juzi kati kunaa mdau anaulizia gari ambalo akiendesha watu wajue amejipata.

Sasa leo nikawa nafanya comparison ya kutaka kuagiza magari mawili, yote ya mwaka mmoja 2006.

BMW 3 series, 2006 generation ya E90, model 320i, ikiwa mpya 2006 iliuzwa $40,000 na leo naweza ipata kwa $930 bila usafiri na $2,800 hadi inafika Dar.
View attachment 3185154
Ukiileta ukakutana na TRA wao watakuomba kama Mil 6.5 tu.
View attachment 3185155
Kwahiyo roughly jumla Mil 14 top top umemiliki Germany machine.

View attachment 3185156
Toyota IST, 2006 ya engine ya 1.5L ilivyokua mpya huo mwaka 2006 iliuzwa kwa $16,000 ila leo used naipata kwa $1,600 bila usafiri na $3,200 hadi inafika Dar.
View attachment 3185157
TRA wao watataka Mil 8 kwahiyo ukijumlisha na Mil 8 ya kununua na malipo mengine top top ni Mil 17.

Hii mifano tu, ila inatufundisha nini?Mi naona Luxury cars zina depreciate kwa kasi ya ajabu sana. Umeona BMW imetoka $40,000 hadi $900 wakati IST imetoka $20,000 hadi $1,600!

KWa wanaonunua gari uku wakiwaza kuna kuliuza mbeleni, ili nalo la kulitazama.
Aisee IST imekomaa kwenye game kwa muda mrefu. Juzi baada ya kipindi kirefu nikapanda na kuendesha IST nilihisi nimekalia kigoda na ile gear lever yake ndefu kama rungu la kipepe.
 
Tuseme kweli, ukiachana na kukimbizana na status ambayo kihalisia haipo na mambo mengine yoote ambayo unayafanya kwa ajili ya watu wengine na si wewe, kuagiza bmw ya zamani hivyo ni hasara kuliko faida.
 
Mi hata nikipata ka zamani haina shida
Hakuna mpya. Zote za zamani. Carina zilianza kutengenezwa 1970 hadi 2001 zilipokuwa succeeded na Allion (Japan) na Avensis (Europe). Kwa Beforward leo, Carina T.I My Road ya 99 ni $4000 (roughly 10mil) na ya bei nafuu ni ya 94 ($3500). TRA kwa hiyo ya 99 wanataka 7.2mil. Andaa 18mil hapo zikiwemo charges za bandarini.
 
Back
Top Bottom