Maisha ya Hussein Jumbe ni ushuhuda tosha kwamba jamii zetu zina wachawi, watu wenye roho mbaya sana na makatili. Tuwe na Imani kwa Mungu

Maisha ya Hussein Jumbe ni ushuhuda tosha kwamba jamii zetu zina wachawi, watu wenye roho mbaya sana na makatili. Tuwe na Imani kwa Mungu

Kwa taratibu za kichawi ni rahisi kulogeka endapo mchawi ataweza kukufikia kwenye mwili wako, nguo au msosi. Inawezekana kuna watu wengi nje nao wanakuloga ila wanafeli kwasababu uchawi wireless ni ngumu sana ku-connect
Hapana unaweza kurogwa wewe ukiwa Uingereza na Mrogaji akiwa Kigoma.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Huamini katika kuzaliwa ? Haujatoka kwenye tupu ya mwanamke wewe ? Hujawahi kuishi gizani peke yako miezi 9 tumboni mwa mama yako ukila damu tu, hufanyi kazi, huogi, hutembei, wewe kazi yako kula damu tu, hujawahi ? Huo pia ni moja ya uchawi (inafikirisha sana), au ulikua haujui ?

Utasema biology, nimekwambia kithibitisho Cha kwanza ni wewe kuachishwa kutoka kua mla damu (mtoto tumboni) kwenda kua mnyonya maziwa ambayo pia ni damu, usichokijua wewe ulikua unaishi gizani peke yako chakula chako kikuu kilikua ni damu ya binadamu (mama yako), ukaja kuzaliwa kutoka pangoni (tumboni) mwenye Giza mpaka unaletwa duniani kwenye Nuru kisha unatenganishwa na msosi wako pendwa wa damu kwa kukatwa kitovu (wewe ulikua mla damu ya binadamu) umekua ukila damu ya mama yako miezi 9 ukiwa tumboni damu ndio kilikua chakula chako cha pekee, huo ni uchawi (inafikirisha sana) that's Magic acha kua mbishi,
Kwa tafsiri yako hii, inamaana Binaadamu wote ni wachawi!!?
 
asubuhi sihisi chochote Mkuu, sure inabidi nianze maombi maana huwa nalala tu bila kuomba

Inabidi uombe. Kama alikuchoma ina maana alifanikiwa, hata kama sio rafiki yako ila kuna mtu anakushambulia. Ungeona umekwepa ina maana hatafanikiwa katika mashambulizi yake. Omba sana mkuu, mpaka uote umeshinda hilo shambulizi.
 
Tuache dhambi na tushike imani kikamilifu uchawi hautatupata, ila ukiwa michanganganyo basi utapata shida sana.
 
Watz wengi wanachanganya magonjwa hasa UKIMWI na uchawi au ulozi. Mathalani hapo kwa Jumbe atakuwa alipata hallucinations ( kuona maluweluwe) aidha kutokana na dawa ( Efavirenz-waliowahi kutumia PEP ni mashahidi) au ugonjwa wenyewe km ulimletea HIV encephalitis ( infection ya bacteria au fangasi kwenye ubongo wa mbele).

Tatizo ninaloliona ni Watz wengi wakipata UKIMWI kusingizia kulogwa na majini, vitu ambavyo havipo. Kuhusu kuvunjika bila kupigwa ni kweli mtu anaweza kuvunjika bila kupata ajali( kitaalam inaitwa pathological fracture) na kuna sababu zake chungu nzima na wala sio ulozi. Watu wengi walioathirika na UKIMWI pia hupata magonjwa mbalimbali ya mifumo na mishipa ya fahamu hivyo sio ajabu kuhisi anaguswa, moto unawaka n.k ilhali sio kweli ( kitaalam inaitwa HIV polyneuropathy)

Tatizo letu kubwa ni kupenda majibu mepesi kwenye maswali magumu. Mtu akienda dispensary anapima Typhoid, mkojo na Malaria anakwambia kapima kila kitu hana shida hivyo basi amelogwa. Madaktari wetu na wao akishindwa kutambua tatizo la mgonjwa ( kakosa diagnosis ama kwa kutojua au incomptence yake) basi anamwambia mgonjwa ajaribu upande wa pili atakuwa kalogwa. Hapo aliyelogwa ni mgonjwa au Daktari?
 
Mkuu unayoongea ni sahihi ila dont underestimate hoja za mleta mada, Uchawi upooo na mambo yA halucination yapo
 
Tuache dhambi na tushike imani kikamilifu uchawi hautatupata, ila ukiwa michanganganyo basi utapata shida sana.
Ni Kweli mkuu ila kwa uzoefu wako ushakutana na watu wangapi ambao wameshika dini kikamilifu??? Hapo ndo shida inapoanza.
 
Hakuna uchawi. Ni watu tu wanaendekeza imani za uchawi.
Aisee. Wachawi wapo, walikuwepo na watakuwapo. Hawa watu wanaumiza watu sana mtu asikuambie. Uamini usiamini hiyo haibadilishi kitu wao wapo tu. Jinsi ya kuwashinda ni kumwabudu Mungu wa kweli.
 
Inabidi uombe. Kama alikuchoma ina maana alifanikiwa, hata kama sio rafiki yako ila kuna mtu anakushambulia. Ungeona umekwepa ina maana hatafanikiwa katika mashambulizi yake. Omba sana mkuu, mpaka uote umeshinda hilo shambulizi.
asante sana kwa ushauri Mkuu, ninaufanyia kazi
 
Mkuu umesahau kuweka no ya kupokelea sadaka baada ya maombezi yako!!
Hahahaha. Najua Mungu amemtetea. Juu ya sadaka, anaweza kutoa kwenye madhabahu yoyote iliyo sahihi au hata kuwapa maskini mkuu. Maana amhurumiaye maskini humkopesha BWANA. Mithali 19:17.
 
Nikipitia maisha ya Hussein Jumbe, naona kama hakuwa na furaha, japo alikuwa anatumia muda mwingi katika kumbi za burudani zilizotarajiwa au zinazosemwa ni sehemu za furaha.

Moyo wake ulijaa mambo mazito, mzigo mzito, malalamiko, na kilio kwa Mungu. Alikuwa akionewa bila hatia. Hata uso wake haukuwa na Nuru ya furaha.

Mara kadhaa alilalamika kwamba Kuna vitendo vya kishirikina vilikuwa vinafanywa kwake. Aliugua sana, kipindi kile mpaka akatunga wimbo "nachechemea". Chanzo Cha kuugua, aliota nyoka anataka kumdhuru au amemdhuru, baada ya siku kadhaa, yule nyoka akaonekana chumbani kwake katika suruali, nyoka akauliwa na wanamtaa, hapo ndipo aliugua karibu kifo.

Baadae akajikuta tu anavunjika mfupa wa mguu, bila kujikwaa chochote. Hapo napo aliota ndoto ya ajabu, mara hiki na kile, anaamka asubuhi anaenda kusali, anarudi, mguu ukapata shida.

Stori ya huyu ndugu inanifanya niendelee kuiogopa Tanga. Na pia inanifanya nione jamii ya kiafrika Ina ushenzi fulani, kwa baadhi yetu.

Pumzika kwa amani Hussein Jumbe.

N.B: katika mahojiano fulani anaonekana kumsema kaka yake kwamba alikuwa anamzushia kuugua ngoma, kama kuzuia watu wasimsaidie, akapima akawa safi. Lakini bado anaumwa!!!!!

Medi Mpakanjia akampeleka Mombasa, akakutana na fundi, ndio akaponea huko, ila mchawi wake hakuchoka, aliendelea kumpa vitimbi. Bila shaka Sasa roho ya huyo mwanga itakuwa imetulia na atachinja kuku baada ya kusikia habari za kifo.

Sasa jamani mziki wa bendi posho kiduchu, ndio kumpiga mtu misumari hivyo?
Hapo hakuna uchawi,ni umaskini tu,kwenye umaskini na ufukara kila kitu ni uchawi,na mambo ya kiswahili tu,kama alikuwa hali vzr,Hana kipato Cha kutosha kuweza kupata huduma Bora za matibabu sio za muhimbili,huduma za kibingwa,angeweza kupona,
Linganisha ugonjwa wake na ugonjwa wa kuoza Koo uliompata Ommy dimpoz,Ommy angekuwa Hana pesa,angekufa na watu wsngesema karogwa,alikuwa na pesa akaenda Bondeni,akapata tiba,akapona na sasa hv yupo poa,
Mchawi wa matatizo ni pesa tu.
 
Mtu ni ROHO anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.

Mtu huyo ambaye ni Roho yupo katika ndoto unazoota.

Usipuuze ndoto, mtu yeyote akikupangia baya sirini mahala popote, lazima utaota ndoto.

Ukipigwa na kuuwawa ktk ndoto na ukaamka mzima, usijifariji,

Baada ya muda Fulani, ulichokiota ndotoni kitatukia vile vile.

Usipuuze NDOTO, chukua hatua haraka,

Makinika na ndoto uotazo.

Amen
 
Cha msingi kwanza elewa uchawi upo, ila achana nao Fanya yako.

Kuna stage ukiona mambo huyaelewi jiongeze.

Ukijifanya wewe ni mtu wa dini nakuhakikishia wapo wachungaji wanakwenda kwa waganga wa kienyeji, na upande wa masheikh ndio sina hata la kusema wao ndio mafundi wenyewe.
Urogwe na agent wa shetani, halafu uende Kwa agent mwingine wa shetani Ili akupe ulinzi?

Watapigiana simu na hutopata msaada wowote.

Ili upone ktk kujiongeza kwako ni uchague kuwa MCHAWI uchukue mikoba, au Uokoke na kumtegemea Mungu.

Wachungaji wanaoenda Kwa Waganga au mashehe wanaopractice uchawi ni Agents wa SHETANI.

Ukimwomba Mungu wako na asikusikie au achelewe kukujibu ktk changamoto unayopitia, ni kheri kufa kuliko kwenda Kwa mganga kuuliza majibu huko.

Amen
 
Maisha bila kumjua Kiongozi wetu Yesu Kristo ni hasara tupu.

Mwanafalsafa Mwisraeli Yesu Kristo alifundisha kanuni bora kabisa za maisha.

Kanuni zinazomstawisha binadamu na kumlinda dhidi ya adui wa kimwili na Kiroho.

Bado hujachelewa soma kitabu c
Chake cha Habari Njema kwa jina lingine Injiri, kitakusaidia sana.
Yesu Si mwanafalsafa,

Yesu ni Mungu aliyekuja katika Mwili Ili kuukomboa Ulimwengu na mateso ya dhambi.

Yesu ndiye dalili ya kiama sawasawa na Islam,

Kama yupo mtu hamwamini Yesu, na haendi Kwa mganga au Si mchawi, mtu huyo atakuwa sawa na Kondoo anayezurura porini bila MCHUNGAJI, ataliwa tu.
 
Back
Top Bottom