Maisha ya Hussein Jumbe ni ushuhuda tosha kwamba jamii zetu zina wachawi, watu wenye roho mbaya sana na makatili. Tuwe na Imani kwa Mungu

Maisha ya Hussein Jumbe ni ushuhuda tosha kwamba jamii zetu zina wachawi, watu wenye roho mbaya sana na makatili. Tuwe na Imani kwa Mungu

Nikipitia maisha ya Hussein Jumbe, naona kama hakuwa na furaha, japo alikuwa anatumia muda mwingi katika kumbi za burudani zilizotarajiwa au zinazosemwa ni sehemu za furaha.

Moyo wake ulijaa mambo mazito, mzigo mzito, malalamiko, na kilio kwa Mungu. Alikuwa akionewa bila hatia. Hata uso wake haukuwa na Nuru ya furaha.

Mara kadhaa alilalamika kwamba Kuna vitendo vya kishirikina vilikuwa vinafanywa kwake. Aliugua sana, kipindi kile mpaka akatunga wimbo "nachechemea". Chanzo Cha kuugua, aliota nyoka anataka kumdhuru au amemdhuru, baada ya siku kadhaa, yule nyoka akaonekana chumbani kwake katika suruali, nyoka akauliwa na wanamtaa, hapo ndipo aliugua karibu kifo.

Baadae akajikuta tu anavunjika mfupa wa mguu, bila kujikwaa chochote. Hapo napo aliota ndoto ya ajabu, mara hiki na kile, anaamka asubuhi anaenda kusali, anarudi, mguu ukapata shida.

Stori ya huyu ndugu inanifanya niendelee kuiogopa Tanga. Na pia inanifanya nione jamii ya kiafrika Ina ushenzi fulani, kwa baadhi yetu.

Pumzika kwa amani Hussein Jumbe.

N.B: katika mahojiano fulani anaonekana kumsema kaka yake kwamba alikuwa anamzushia kuugua ngoma, kama kuzuia watu wasimsaidie, akapima akawa safi. Lakini bado anaumwa!!!!!

Medi Mpakanjia akampeleka Mombasa, akakutana na fundi, ndio akaponea huko, ila mchawi wake hakuchoka, aliendelea kumpa vitimbi. Bila shaka Sasa roho ya huyo mwanga itakuwa imetulia na atachinja kuku baada ya kusikia habari za kifo.

Sasa jamani mziki wa bendi posho kiduchu, ndio kumpiga mtu misumari hivyo?
Kafa kaacha bendi yake ya talent band
 
Anayeamini uchawi unaweza kuendelea kuamini. Mwanzo sikuwa najua hata mambo ya uchawi, tukaja kupata dada msaidizi wa ndani toka Singida Mwenyezi Mungu ampumzishe mahala pema. Alishatangulia mbele za haki.

Huyu dada ndiyo alianza kunifundisha, kuna uchawi duniani nami nikaamini.
Nashukuru Mungu ni majuzi nimekutana na watu sahihi, uchawi uko kwenye mind tu. Ukiamini na itakuwa hivyo.

Usipoamini hakuna kitu kitakudhuru, nami nimeamini, kabla sikuwa nimesikia na niliishi kwa amani bila uoga. Nilipotajiwa nikawa muoga. Ila sasa imesha hiyooo, hakuna uchawi na sitodhurika.
Madam Bantu Lady acha nikae kimya, ila witchcraft is there na nime experience Sparks zake. Damn it
 
Nitakuuliza swali dogo sana najua unaamini tumeumbiwa vitu vitatu mwili, nafsi na roho je! umewahi kuigusa Nafsi au Roho yako hata siku moja ukaona inagusika vipi ? (Swali fikirishi sana)
1. Siamini katika "kuumbiwa".
2. Siamini katika "roho".
3. Siamini katika umuhimu wa kuona. Nikikwambia thibitisha maana yake si kwamba nataka unioneshe kwa macho.
4. Siamini katika kuamini.

Kwa hivyo ume assume naamini vitu fulani wakati mimi siamini hata katika kuamini.

Thibitisha uchawi upo.
 
TASLIMA

Dr. Joe Dispenza is an international speaker, researcher, author, and educator who is passionate about the findings from the fields of neuroscience, epigenetics, and quantum physics to explore the science behind spontaneous remissions.

Huyu anatumia saysansi, si uchawi.
 
Maisha bila kumjua Kiongozi wetu Yesu Kristo ni hasara tupu.

Mwanafalsafa Mwisraeli Yesu Kristo alifundisha kanuni bora kabisa za maisha.

Kanuni zinazomstawisha binadamu na kumlinda dhidi ya adui wa kimwili na Kiroho.

Bado hujachelewa soma kitabu c
Chake cha Habari Njema kwa jina lingine Injiri, kitakusaidia sana.
 
Nikipitia maisha ya Hussein Jumbe, naona kama hakuwa na furaha, japo alikuwa anatumia muda mwingi katika kumbi za burudani zilizotarajiwa au zinazosemwa ni sehemu za furaha.

Moyo wake ulijaa mambo mazito, mzigo mzito, malalamiko, na kilio kwa Mungu. Alikuwa akionewa bila hatia. Hata uso wake haukuwa na Nuru ya furaha.

Mara kadhaa alilalamika kwamba Kuna vitendo vya kishirikina vilikuwa vinafanywa kwake. Aliugua sana, kipindi kile mpaka akatunga wimbo "nachechemea". Chanzo Cha kuugua, aliota nyoka anataka kumdhuru au amemdhuru, baada ya siku kadhaa, yule nyoka akaonekana chumbani kwake katika suruali, nyoka akauliwa na wanamtaa, hapo ndipo aliugua karibu kifo.

Baadae akajikuta tu anavunjika mfupa wa mguu, bila kujikwaa chochote. Hapo napo aliota ndoto ya ajabu, mara hiki na kile, anaamka asubuhi anaenda kusali, anarudi, mguu ukapata shida.

Stori ya huyu ndugu inanifanya niendelee kuiogopa Tanga. Na pia inanifanya nione jamii ya kiafrika Ina ushenzi fulani, kwa baadhi yetu.

Pumzika kwa amani Hussein Jumbe.

N.B: katika mahojiano fulani anaonekana kumsema kaka yake kwamba alikuwa anamzushia kuugua ngoma, kama kuzuia watu wasimsaidie, akapima akawa safi. Lakini bado anaumwa!!!!!

Medi Mpakanjia akampeleka Mombasa, akakutana na fundi, ndio akaponea huko, ila mchawi wake hakuchoka, aliendelea kumpa vitimbi. Bila shaka Sasa roho ya huyo mwanga itakuwa imetulia na atachinja kuku baada ya kusikia habari za kifo.

Sasa jamani mziki wa bendi posho kiduchu, ndio kumpiga mtu misumari hivyo?
Ukiona mtu anapiga kelele za wachawi ujue yeye ni muumini
 
usiku wa kuamkia jana nimeona kaja mgeni hapa kwangu anapiga hodi, nilipofungua door ni rafiki yangu wa enzi za shule ila ghafla alitoa mkuki na kunichoma tumboni

pia kuna hii ndoto naiota toka mwaka jana kati kati, kwamba nipo kitandani natoa uzi mrefu mdomoni usiokuwa na mwisho
Huo uzi mdomoni ulikua ni udenda tu

Funga mdomo ukilala
 
Hiyo ni baiolojia, baiolojia si uchawi.
Uelewa wako ni mdogo sana, hio sio biology hio ni moja ya uthibitisho kua uchawi upo hutaki kuamini macho unayo huoni unatumia macho gan kutazama ? Hujawahi kumtia mwanamke mimba ? Hujawahi kuelewa kua mnachokifanya pale kitandani mkiwa wawili ni uchawi ? Au km wewe ni mwanamke hujawahi kutiwa mimba ? Haujawahi kushuhudia mwanamke akajifungua mtoto ? Unahisi watoto wanaozaliwa hua wanatoka wapi ? Yaan mpaka hapo hujui km kweli uchawi upo ? Bado hauamini kwamba uchawi upo ikiwa wewe pia umeishi tumboni ? Na pia utasema hakuna MUNGU Ila biology tu ndio ipo ?

Kweli Kiranga KOMO hio KOMO ungeongeza kwenye jina lako iwe ubini maana linakufaa

Katika hili umeniangusha Kiranga nilijua una akili kubwa kumbe akili zako hazitofautiani na za mtoto ambae hajakatwa kitovu bado upo tumboni unanyonya damu,
 
Ukiona mtu anapiga kelele za wachawi ujue yeye ni muumini
Mwamposa namba 1 daily topic yake kuu ni wachawi, Kuhani Musa Richard Mwacha main topic yake ni wachawi wachawi wachawi, je yeye pia ni muumini wa wachawi ? Una akili sawa sawa wewe kweli? Au fuse zimeungua ? Mwamposa km unakatiza cordon hapo pardon my French
 
1. Siamini katika "kuumbiwa".
2. Siamini katika "roho".
3. Siamini katika umuhimu wa kuona. Nikikwambia thibitisha maana yake si kwamba nataka unioneshe kwa macho.
4. Siamini katika kuamini.

Kwa hivyo ume assume naamini vitu fulani wakati mimi siamini hata katika kuamini.

Thibitisha uchawi upo.
Huamini katika kuzaliwa ? Haujatoka kwenye tupu ya mwanamke wewe ? Hujawahi kuishi gizani peke yako miezi 9 tumboni mwa mama yako ukila damu tu, hufanyi kazi, huogi, hutembei, wewe kazi yako kula damu tu, hujawahi ? Huo pia ni moja ya uchawi (inafikirisha sana), au ulikua haujui ?

Utasema biology, nimekwambia kithibitisho Cha kwanza ni wewe kuachishwa kutoka kua mla damu (mtoto tumboni) kwenda kua mnyonya maziwa ambayo pia ni damu, usichokijua wewe ulikua unaishi gizani peke yako chakula chako kikuu kilikua ni damu ya binadamu (mama yako), ukaja kuzaliwa kutoka pangoni (tumboni) mwenye Giza mpaka unaletwa duniani kwenye Nuru kisha unatenganishwa na msosi wako pendwa wa damu kwa kukatwa kitovu (wewe ulikua mla damu ya binadamu) umekua ukila damu ya mama yako miezi 9 ukiwa tumboni damu ndio kilikua chakula chako cha pekee, huo ni uchawi (inafikirisha sana) that's Magic acha kua mbishi,
 
Mwamposa namba 1 daily topic yake kuu ni wachawi, Kuhani Musa Richard Mwacha main topic yake ni wachawi wachawi wachawi, je yeye pia ni muumini wa wachawi ? Una akili sawa sawa wewe kweli? Au fuse zimeungua ? Mwamposa km unakatiza cordon hapo pardon my French
Wote ni hao hao tu

Maandiko hataabudu wachawi kama wewe na hao uliowataja
 
Sio Tanga tu Wachawi na Wanga wapo kila sehemu, usichokijua leo nikufumbue macho km unavyoona huku nje kuna dini na madhehebu na huko kwenye ulimwengu wa wachawi na wanga Wana dini na madhebu (inafikirisha sana) hujawahi kujua, ipo hivi kuna wachawi wanajiunga na dini ya kichawi na kuna wachawi wanaingia kwenye uchawi na wengine ni wachawi wanaowanga bila kujua kua wanachokifanya wanaroga wengine

Uchawi upo kila sehemu, usibishe Tena Sasa hivi uchawi umerudi kwa kasi watu wanarogana vibaya, maisha magumu hali ngumu na wachawi wanaroga

R.i.p H Jumbe
Dah! Wachawi wametamalaki, halafu dini nyingi zimejaa matapeli, au zinaendeshwa na wachawi haohao, wanakuroga ili waje wakuombee, wanaita waumini kishirikina.

Kuna kanisa ambalo, baada ya Misa/ibada, wanafagia mchanga ulioletwa na watu walioingia kanisani, wanaupeleka kwa fundi, lazima urudi tena jumapili ijayo.

Kwa waganga wa kutibu, nao matapeli wamejaa, waganga wa ukweli nao, hawarithishi taaluma, wako radhi wafe naye, sijui ndio uchoyo, roho mbaya, au miiko
 
Mtu wa pwani yoyote haingii kazini bila kujipaka sijui madude gani, ukikaa naye karibu harufu inakera lakini kwao bila hayo haingii kazini. Awe amesoma hata P.H.D awe anasali masaa yote lakini manukato hayo yapatikanayo kwa ma sangoma lazima ajipake
Wanauza misikitini yale madude yao yenye harufu kali
 
Kosa kubwa sana. Ila kwa kuwa tumepewa neema ya kuombeana, kwa jina la Yesu nakufungua na vifungo vya mauti kuanzia sasa kwa jina la Yesu. Bwana Mungu akutetee mbele ya watesi wako. Walilolikusudia lisifanikiwe kwa jina la Yesu.
Mkuu umesahau kuweka no ya kupokelea sadaka baada ya maombezi yako!!
 
Sasa tuamini nini ushirikina una nguvu au dini ina nguvu,mana umeandika Jumbe alitoka kuswali na Bado mchawi akawa na nguvu dhidi ya dini na akavunjika mguu....???
Ume reason kitaalam sana!!
 
Back
Top Bottom