Maisha ya Hussein Jumbe ni ushuhuda tosha kwamba jamii zetu zina wachawi, watu wenye roho mbaya sana na makatili. Tuwe na Imani kwa Mungu

Maisha ya Hussein Jumbe ni ushuhuda tosha kwamba jamii zetu zina wachawi, watu wenye roho mbaya sana na makatili. Tuwe na Imani kwa Mungu

Hakuna kitu kibaya duniani kama ugomvi wa kifamilia ama kati ya ndugu.. Lakini sometimes kinga za kiroho zinapokuwa chini bila hata ushirikina hakuna rangi utaacha kuona
Jumbe kwa sehemu kubwa kauliwa na hofu, hofu ya kurogwa na ndugu, hofu ya kurogwa na wasiompenda nknk.. Hiyo dhana ikishakuingia hata ukipaliwa utadhani umerogwa
Mzee wa kilingeni akisema jambo kwenye sector yake, Uzi unatakiwa kufungwa
 
Nachechemeaaaaa
IMG-20230403-WA0003.jpg
 
Thibitisha.
Ukitaka uthibitisho kwa hii Sayansi iliyofungwa, haitowezekana. Ni mpaka utakaporuhusu Fikra za uwezekano wa uwepo wa Sayansi beyond the bookish science.

Na ukipata ushahidi wa uwepo wake basi tambua kuwa hicho ndicho tunacholazimishwa kukiita Uchawi na kwamba ni kiovu.
 
Biology ya wapi hio umefundishwa kwamba mtoto anaishi kwa Kula Damu?
Biology ? Nimesema wewe tumboni mwa mama yako chakula chako cha pekee kilikua ni damu ya mama yako, ulikua unakula damu unashiba damu via placenta,
Screenshot_20230413-192321.png
unahitaji kutulia kidogo ili uelewe hili, naona kuna sehemu walikuacha patupu hukuambiwa
 
Hakuna kitu kibaya duniani kama ugomvi wa kifamilia ama kati ya ndugu.. Lakini sometimes kinga za kiroho zinapokuwa chini bila hata ushirikina hakuna rangi utaacha kuona
Jumbe kwa sehemu kubwa kauliwa na hofu, hofu ya kurogwa na ndugu, hofu ya kurogwa na wasiompenda nknk.. Hiyo dhana ikishakuingia hata ukipaliwa utadhani umerogwa
Chanzo ilikua ni mgogoro na wenzake wa band aliokua anafanya nao kazi kabla ya kuanzishwa kwa band yake ya Talent Band anaturudisha nyuma tangu enzi za uhai wa Mzee Komba na TX Moshi akieleza Visa tofauti tofauti alivyovipitia kwenye masuala ya band, kwa Imani yake aliamini wale waliomzunguka ukiondoa mke na watoto wake walikua hawataki yeye apate mafanikio pamoja na kwamba alikua na kipaji Cha sauti, na alikua akisema pamoja na kwamba ana kipaji kikubwa Cha sauti, utunzi na uimbaji Ila hana mafanikio kiivyo ukilinganisha na wasanii wa sasa hawa wa kizazi kipya maana siku anahojiwa redioni aliulizwa maswali mengi na wachangiaji walikua wengi na alijibu maswali mengi pia, Ila hicho ndio alichokiamini marehemu Hussein Jumbe

Apumzike pahala pema peponi
 
Kwani wewe unajua uchawi ni nini? Maana yaweza ikawa kuna mbishano mwingi humu Ila kumbe kila mmoja ana maana yake ya neno uchawi, mfano kuna maneno ya mtaani (rahaja na misimu) utasikia anasema 'mchawi Pesa' au mwingine anasema 'mchawi Ndugu', Sasa wewe km wewe unajua nini maana ya uchawi ?

Ushirikina - Imani, mazoea, au ibada isiyo na mantiki inayodumishwa na ujinga wa sheria za asili au kwa imani katika uchawi.

Uchawi - Uchawi kwa kawaida humaanisha matumizi ya nguvu za uchawi au zisizo za kawaida kuwadhuru wengine.

Uchawi - Kijadi, zoezi au wito wa madai ya nguvu zisizo za kawaida kudhibiti watu au matukio.

Uchawi - Sanaa au mazoea ya kutumia hirizi, maneno/matamshi, au matambiko ili kujaribu kuzalisha athari zisizo za kawaida au kudhibiti matukio katika asili.

Uchawi - Kugawanywa kwa msaada, au msaada unaodhaniwa, wa pepo wabaya, au nguvu ya kuamrisha pepo wabaya.
Unapo define neno uchawi, usitumie neno uchawi, kwa sababu neno uchawi ndilo linakuwa defined, ukilirudia neno uchawi katika definition ya uchawi una short circuit definition yako.

Mtu anakwambia anataka umwambie uchawi ni nini, halafu unamwambia uchawi ni uchawi, mpaka hapo ushafeli.

Umeshindwa ku define uchawi, unarudia neno uchawi katika definition ya uchawi!

Hao pepo wabaya unaowasema ukiambiw authibitishe huwezi.

Umeambiwa uthibitishe uchawi ni nini, unaongeza habari z apepo mbaya ambazo nazo huwezi kuthibitisha.
 
Ukitaka uthibitisho kwa hii Sayansi iliyofungwa, haitowezekana. Ni mpaka utakaporuhusu Fikra za uwezekano wa uwepo wa Sayansi beyond the bookish science.

Na ukipata ushahidi wa uwepo wake basi tambua kuwa hicho ndicho tunacholazimishwa kukiita Uchawi na kwamba ni kiovu.
Tutajua vipi haya maneno yako ni ukweli na si hadithi za kujidanganya tu?
 
Haya mambo ya shirki ni ya kawaida sana uswahilini na yanatokea mnapochanganyika au kukutana mara kwa mara wanandugu na jamaa. Hapo ndo mnajuana nani anapiga hatua kwenda mbele nani anaenda nyuma na ndo chanzo cha roho za chuki na husuda huanza hapo.

Anaeona hakumudu mchana atakufata usiku yeye mwenyewe au la akutumie watu wake.

Wewe ukiweza ishi maisha yako mwenyewe kuwa na umbali kiasi na ndugu/washkaji jitahidi wasijue saana mambo yako kiundani na hata kama umetoboa kimaisha acha mawoye fanya mambo kimya kimya.

rip mwamba Jumbe.

Nimeskiza kibao chake kimoja matata sana kinaitwa 'pombe'. Sijui alishakirekodi kile wakulungwa?
 
Tutajua vipi haya maneno yako ni ukweli na si hadithi za kujidanganya tu?
Nimesema uzipe Fikra zako kwanza kuwa hujui kuhusu hili, ili kutoa uwezekano wa kuwa kweli ama laa. Ukishajifungia mahali kuwa hili ni uongo na haliwezekani, linageuka kuwa Imani kwako na kimsingi hatuwezi kuhangaika nayo imani yako, maana haina ukomo.
 
Hakuna kitu kibaya duniani kama ugomvi wa kifamilia ama kati ya ndugu.. Lakini sometimes kinga za kiroho zinapokuwa chini bila hata ushirikina hakuna rangi utaacha kuona
Jumbe kwa sehemu kubwa kauliwa na hofu, hofu ya kurogwa na ndugu, hofu ya kurogwa na wasiompenda nknk.. Hiyo dhana ikishakuingia hata ukipaliwa utadhani umerogwa
Na nyimbo zake 95% zilikuwa za kulalamika kuonewa...
 
Jamii za Kitanzania nyingi kama sio zote zinafanya uchawi ila tunapenda sana kujibaraguza kujifanya hatuamini uchawi!
Siyo nyingi ni jamii zote, ukisoma history kabla ya kuletewa dini na waarabu na wamisionari wazee wetu mpaka machifu waliheshimika na kuogopeka kwa mambo ya kishirikina...
 
Nimesema uzipe Fikra zako kwanza kuwa hujui kuhusu hili, ili kutoa uwezekano wa kuwa kweli ama laa. Ukishajifungia mahali kuwa hili ni uongo na haliwezekani, linageuka kuwa Imani kwako na kimsingi hatuwezi kuhangaika nayo imani yako, maana haina ukomo.
Bado hujajibu swali langu, maana na wewe pia unatakiwa uishi kwa kanuni yako uliyonipa.

Kanuni ya kujiwekea kwamba inawezekana ukawa hujui ni nzuri, na mimi ndiyo maana sikukuambia wewe hujui, mimi najua.

Nimekuuliza tu. Tutajuaje (wote) kwamba maneno yako ni ukweli na si hadithi za kujidanganya tu?

Tuweke njia ya uhakiki vizuri ili tusiende kwa mihemko ya kutaka upande fulani ushinde ligi.

Tutajua vipi haya maneno yako ni ukweli na si hadithi za kujidanganya tu?

Hujajibu swali hili.
 
Mtu wa pwani yoyote haingii kazini bila kujipaka sijui madude gani, ukikaa naye karibu harufu inakera lakini kwao bila hayo haingii kazini. Awe amesoma hata P.H.D awe anasali masaa yote lakini manukato hayo yapatikanayo kwa ma sangoma lazima ajipake
Pemba pia
 
Nikipitia maisha ya Hussein Jumbe, naona kama hakuwa na furaha, japo alikuwa anatumia muda mwingi katika kumbi za burudani zilizotarajiwa au zinazosemwa ni sehemu za furaha.

Moyo wake ulijaa mambo mazito, mzigo mzito, malalamiko, na kilio kwa Mungu. Alikuwa akionewa bila hatia. Hata uso wake haukuwa na Nuru ya furaha.

Mara kadhaa alilalamika kwamba Kuna vitendo vya kishirikina vilikuwa vinafanywa kwake. Aliugua sana, kipindi kile mpaka akatunga wimbo "nachechemea". Chanzo Cha kuugua, aliota nyoka anataka kumdhuru au amemdhuru, baada ya siku kadhaa, yule nyoka akaonekana chumbani kwake katika suruali, nyoka akauliwa na wanamtaa, hapo ndipo aliugua karibu kifo.

Baadae akajikuta tu anavunjika mfupa wa mguu, bila kujikwaa chochote. Hapo napo aliota ndoto ya ajabu, mara hiki na kile, anaamka asubuhi anaenda kusali, anarudi, mguu ukapata shida.

Stori ya huyu ndugu inanifanya niendelee kuiogopa Tanga. Na pia inanifanya nione jamii ya kiafrika Ina ushenzi fulani, kwa baadhi yetu.

Pumzika kwa amani Hussein Jumbe.

N.B: katika mahojiano fulani anaonekana kumsema kaka yake kwamba alikuwa anamzushia kuugua ngoma, kama kuzuia watu wasimsaidie, akapima akawa safi. Lakini bado anaumwa!!!!!

Medi Mpakanjia akampeleka Mombasa, akakutana na fundi, ndio akaponea huko, ila mchawi wake hakuchoka, aliendelea kumpa vitimbi. Bila shaka Sasa roho ya huyo mwanga itakuwa imetulia na atachinja kuku baada ya kusikia habari za kifo.

Sasa jamani mziki wa bendi posho kiduchu, ndio kumpiga mtu misumari hivyo?
Tanga inahusikaje
 
Mkuu ushawahi kukutana nae mkaongea??
Umeongea kwa hisia na kueleza like ulikuwa nae kabisa...ila inasisimua haijalishi ni kweli au umetunga
 
Nikipitia maisha ya Hussein Jumbe, naona kama hakuwa na furaha, japo alikuwa anatumia muda mwingi katika kumbi za burudani zilizotarajiwa au zinazosemwa ni sehemu za furaha.

Moyo wake ulijaa mambo mazito, mzigo mzito, malalamiko, na kilio kwa Mungu. Alikuwa akionewa bila hatia. Hata uso wake haukuwa na Nuru ya furaha.

Mara kadhaa alilalamika kwamba Kuna vitendo vya kishirikina vilikuwa vinafanywa kwake. Aliugua sana, kipindi kile mpaka akatunga wimbo "nachechemea". Chanzo Cha kuugua, aliota nyoka anataka kumdhuru au amemdhuru, baada ya siku kadhaa, yule nyoka akaonekana chumbani kwake katika suruali, nyoka akauliwa na wanamtaa, hapo ndipo aliugua karibu kifo.

Baadae akajikuta tu anavunjika mfupa wa mguu, bila kujikwaa chochote. Hapo napo aliota ndoto ya ajabu, mara hiki na kile, anaamka asubuhi anaenda kusali, anarudi, mguu ukapata shida.

Stori ya huyu ndugu inanifanya niendelee kuiogopa Tanga. Na pia inanifanya nione jamii ya kiafrika Ina ushenzi fulani, kwa baadhi yetu.

Pumzika kwa amani Hussein Jumbe.

N.B: katika mahojiano fulani anaonekana kumsema kaka yake kwamba alikuwa anamzushia kuugua ngoma, kama kuzuia watu wasimsaidie, akapima akawa safi. Lakini bado anaumwa!!!!!

Medi Mpakanjia akampeleka Mombasa, akakutana na fundi, ndio akaponea huko, ila mchawi wake hakuchoka, aliendelea kumpa vitimbi. Bila shaka Sasa roho ya huyo mwanga itakuwa imetulia na atachinja kuku baada ya kusikia habari za kifo.

Sasa jamani mziki wa bendi posho kiduchu, ndio kumpiga mtu misumari hivyo?
Tatizo letu baadhi yetu hasa waisilamu mtu afanya mziki uchawi ulevi jamari anakula na kutoa riba uzinzi ushoga ubasha akiambiwa haya matendo mabaya ya ibirisi hayafai anachukia kibaya zaidi baadhi yao kutwa wako misikitini kwani mtu usichague 1 tu kuyahepuka kisha akaenda msikitini au kuyaendeleza ukahachana na habari za msikitini?hili tatizo
 
Back
Top Bottom