Maisha ya machimbo ya dhahabu ni zaidi ya jeshi, nilikimbia

hongera mkuu mdingi wako nampa pongezi kubwa sana,kwani alikupeleka kwenye chuo cha maisha ujue pesa inatafutwaje,mpaka kufikia hapo sizani kama utakuwa na matumizi mabaya yapesa au kuwadharau wengine hawajui kutafuta.mi baada ya kumaliza form six nilitimuliwa hom .maisha yangu ya kawa ya kimtaa kwetu wakishua lakini ilifikia hatua nikajiunga na wachonga kalai nashindia maji na chikichi nikaugua madonda ya tumbo lakini nika kaza.kwa siku nilikuwa napata 1000,nikadunduliza ikafika 30000 nika acha kazi hiyo.nikahamia kuchinga vyombo nanunua besen 30 napata faida 3000, nashukuru mungu nilipanda mpaka mtaji ukafika milion,..baba akawa anaulizia tu niko wapi ila taimu namimi hana.sasaiv na maisha yangu biashara kubwa,na baba anajivunia mimi, aliniita akasema sio kwamba sikupendi,niliambiwa na mchaga ili mtoto awe na akili mtimue ujifanye humpendi..baadae akaita ndugu akasema naona mwanangu shule ime mkaa sasa.namuongezea mil 2.je asingenitimua nika sota mtaani ninge kuwa na nidhamu yapesa? maisha ni chuo ndugu.
 
Ni sahihi. Ni Kweli kazi ngumu.
Mazingira ya uchimbaji wa madini (uchimbaji mdogo) Kwa nchi za kiafrika ni magumu sana. Angalia DR Congo watu wengi wameangamia Kwa sababu ya kufukiwa na vifusi Vya udongo.
Nakumbuka machimbo ya dhahabu ya kitunda-Sikonge Tabora Kuna watu wengi walifunikwa na gema kisa wanagombania mchirizi wa dhahabu.
 
Nmecheka sana et nilivoona mwaktolyo ni mwaka Gani? Ilikuwa
 
Ulidhani kupasua kimaisha ni rahisi tu ? Pole sana. Lazima uteseke kwanza kabla ya kutusua
 
Huko ndio anapotea mazima mwisho wa siku apate msongo wa mawazo kisha ajimalize kabisa
 
Machimboni sio kabisa aisee bora ukae town uwe dalali.

Imagine sehemu ya kutafutia riziki ambayo 80% ya wajuba wanaamini ramani za waganga, 80% ya raia hawana connection na dunia civilized maana yake hamna mwenye address wala ID yoyote, 80% wanajisaidia porini na ni hadi ale ugolo vinginevyo ngoma haitoki na hii husababishwa na kuishi kwa mandazi ya azam na energy drink za mo.

Watu hawaendi kwao hata miaka 10 ni mwendo wa kuhama mgodi hadi mgodi. Unaenda na mamilioni ya hela kwa namna biashara isivoeleweka unarudi na begi chakavu lenye nguo chakavu.

Kuna dingi aliingizwa king na madalali akaingia mgodini mazima bila kushirikisha kichwa katika tani 540 ya material aliondoka na gram 49, aisee almanusura ampige nyundo meneja wa Elution plant.

Hii biashara tuwaachie wazungu kiukweli haieleweki kwa asilimia 90.
 
Daa hii stori imenikumbusha tulivomaliza skuli ile praimari bado tukiwa wadogo kuna wenzetu walienda uko machimboni kutafuta maisha. Walivorudi tulikuwa tunawaskia wanalalamikia mazingira ya uko. badae wakazoea mazingira wakawa wanaenda na kurudi. badae wengine waliumwa matumbo walisema maji ya yalikuwa machafu sana. Mmoja hakurudi alifia ukouko.
 
Dahhh maisha haya.Ila umenikumbusha kisa fulan hivi.Jamaa alienda kuchimba na yeye alitokea town alikuja vizuri yaan kifedha.alichimba kama wiki mbili hivi bila kupata akijitahid anapata 8000 ahhh akaamua kuacha.Na kutangazia umma kuwa ile kazi haifai.jamaa mmoja akamwomba lile shimo aendelee kuchimba mwenye shimo kakubali,ehhh bwana haikupita siku jamaa kangusha mzigo milion mia mbili.sasa ule ugomvi uliwa sio wa inchi hii. na yule jamaa aliye achia shimo.Maisha kaka ni kujifunza si mpaka upate
 
Mkuu niazime I'd yako
 
Kimsingi huo wako haukua uchimbaji hata level ya mchimbaji mdogo ulikua hujafika bali ulikua mbangaizaji tu. Watu mnachafua sana sifa za uchimbaji wakati mnaofanya sio uchimbaji.

Ni sawa na mtu awe anauza pair moja ya kiatu Kariakoo akose mteja aseme kkoo pagumu. Huyu hana duka, hata level ya umachinga hajafikia, hajui anything kuhusu ins and outs za Kkoo afu aseme kkoo pagumu, utamchukulia seriously kweli?

Chunya inatoa 300-400Kg of gold yani over 35 Billion TSH monthly. Mnadhani hizi dhahabu zinatoka mbinguni?

Uchimbaji kama biashara zingine unahitaji uwekezaji tena uwekezaji wa maana na maarifa na uchimbaji sio a get rich quick scheme kama wengi mnavyojazana. Wengine tukitoa story zetu hapa mtashangaa. Hizo kona zote nazifahamu na nitakua huko soon.
 

Kwa 25M alidhani atapata nini? 25M kwenye madini is nothing Bora angefuga kuku tu. Tatizo wengi wanadhani uchimbaji is a get rich quick scheme it's absolutely not.
 

Apex the biggest tax payer wilaya ya Chunya wanachimba Itumbi. Achimwene wenye Mabasi ya achimwene wanachimba Itumbi. Mdimi ana shafts Itumbi. Hawa wamefanya uwekezaji wa nguvu.

Watu wengi including mleta Uzi hawajafanya uchimbaji bali ubangaizaji tu kama machinga hawapo hata level ya mchimbaji mdogo. Tatizo watu wanajazana ujinga kwamba wataenda migodini na sululu na jembe watoboe, that will never happen. Watarudi kwao wamechakaa ndugu zao wawasahau.
 

Word. Nawaambia waende pale pale Chunya Itumbi kwa Achimwene mwenye mabasi ya Achimwene, Apex, Kyando, Mdimi na Sauli mwenye Mabasi ya Sauli waulize wanavuna kiasi gani kwa mwezi na uwekezaji wao wajionee tofauti.

Uchimbaji kama biashara zingine zote inahitaji uwekezaji wa nguvu, maarifa na utaalam sio kubahatisha kienyeji enyeji tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…