Maisha ya Mtumishi wa Serikali ni Magumu mno. Mungu aingilie kati

Kwahiyo mnahitaji huruma??????

Sasa nini faida ya kusotea elimu isiyo na faida huku mkingoja huruma za wanasiasa?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfumo wa watumishi wa serikali ni mgumu mno yaani unasomeshwa Kwa mkopo wa serikali Kwa million kumi na nne14,000,000 halafu unakuja kulipwa mshahara wa laki tano na elfu sitini na Tisa wa TGSD shilling 569,000/= . Changamoto ni kubwa kuliko ilivyo kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikufuru mkuu, kuna watumishi tuna familia kubwa lkn mishahara yao ata bila ya mikopo haifikii iyo laki 4 uichukuayo ww kwa xx

Tunaiishi hivi,
1. Tunatumia sehem ya mshahara kulima chakula cha ambacho kitaliwa mwaka mzima..so kwenye mavuno unakuwa na mahindi, maharage, viaz, alizeti kwa ajili ya mafuta ya kupikia na karanga

2. Baadhi ya mazao yasiyo yalima hununua msimu wa mavuno bei ikiwa ndogo mfano. Mpunga kpnd cha mavuno gunia huwa na tshs 42000/= so unajibana unanunua magunia km 10 yatayotumika hadi msimu wa mavuno tena

3. Uku vijijini hatunaga gharama za umeme coz huo umeme haupo tunauonaga tukija mjini tu so tumejiongeza kwa kununua solar panel

4. Tunafuga mifugo km bata na kuku km kitoweo lkn pia hii inasaidia kupunguza ugumu wa maisha upatapo dharura ndogo ndogo ili tusiende kwa mangi kukopa

Kwa mgawanyo huu mshahara wa tshs 360,000/= hufikia baadhi ya miezi hatuhangaiki nayo so tunaacha akiba kwa ajili ya hatua zingine za kimaendeleo zaidi

Karibuni vijijini mle maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha sio magumu ukiishi maisha yako uache kufake mi mbona nakula Bata tu nachokipata naridhika nacho na hakuna wa kunipangia niishi vipi
 
Mkuu umeongea mengi mazuri lakini hapa umekosea sana.
Kuna mengi sana yanachangia watu wawe ktk hali kama ile, wewe ukifanikiwa unashukuru kwa kupata elimu na ajira au mtaji wa biashara inayo eleweka.
Nimekuelewa mkuu, I will try harder next time.

Thanks mkuu!
 
Ndiyo maana nakukubali, huwa nashangaa sana unapoelezea matatizo yako then mtu anakuja anakulinganishia matatizo yako na ya mtu mwingine wakati tunatofautiana.
Ndio binaadamu walivyo ndugu yangu.

Ila kwa vile hapa tunasomeshana tu, kila mmoja muache aandike atakalo, tutasoma, yatakayofaa tutayachukua na ambayo hayatofaa tutamuachia mwenyewe.
 
Yeah sure, twatakiwa kuyachukua yale yatufaayo kwa kweli.
Ndio binaadamu walivyo ndugu yangu.

Ila kwa vile hapa tunasomeshana tu, kila mmoja muache aandike atakalo, tutasoma, yatakayofaa tutayachukua na ambayo hayatofaa tutamuachia mwenyewe.
 
Kwa nini sasa usiende(asiende) huko??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na bado watampigia kura ********....miaka mingine mitano ya kilio na kusaga meno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…