LuisMkinga
JF-Expert Member
- Jan 10, 2012
- 3,394
- 6,550
Mkopo wa Bodi umechukua umekula wewe. Mkopo wa NMB umechukua wewe, unajua ulichofanyia lakini hela umechukua. Unalia nini na makato? Mimi naita hii ni dhihaka. Basic salary yako ipo vizuri kuliko watumishi wengi sana wa serikali. Wapo ambao hiyo take home yako ndio basic salary Yao na wapo ambao hiyo take home yako, nikubwa kuliko basic salary zao.
Tatizo watumishi wengi wa umma wanakopa pesa kufuata mkumbo. Hela ya mkopo anatumia ndani ya wiki au mwezi lakini makato anasota nayo miaka 4 mpaka 7. Hii ni hatari wakati mkopo haumuingizii hata shilingi tano.
Pia watumishi wa umma wengi hawana utaratibu wa kujiwekea akiba ili hata siku akipata shida ya ghafla badala ya kukopa anachukua akiba yake.
Watumishi wengi wanatakiwa wajiongezee kwa kuweka vyanzo vingine vya mapato.
Mkifanya mchezo mukistaafu au kufukuzwa kazi, huku mtaani mutateseka sana.
ExactlyUsikufuru mkuu, kuna watumishi tuna familia kubwa lkn mishahara yao ata bila ya mikopo haifikii iyo laki 4 uichukuayo ww kwa xx
Tunaiishi hivi,
1. Tunatumia sehem ya mshahara kulima chakula cha ambacho kitaliwa mwaka mzima..so kwenye mavuno unakuwa na mahindi, maharage, viaz, alizeti kwa ajili ya mafuta ya kupikia na karanga
2. Baadhi ya mazao yasiyo yalima hununua msimu wa mavuno bei ikiwa ndogo mfano. Mpunga kpnd cha mavuno gunia huwa na tshs 42000/= so unajibana unanunua magunia km 10 yatayotumika hadi msimu wa mavuno tena
3. Uku vijijini hatunaga gharama za umeme coz huo umeme haupo tunauonaga tukija mjini tu so tumejiongeza kwa kununua solar panel
4. Tunafuga mifugo km bata na kuku km kitoweo lkn pia hii inasaidia kupunguza ugumu wa maisha upatapo dharura ndogo ndogo ili tusiende kwa mangi kukopa
Kwa mgawanyo huu mshahara wa tshs 360,000/= hufikia baadhi ya miezi hatuhangaiki nayo so tunaacha akiba kwa ajili ya hatua zingine za kimaendeleo zaidi
Karibuni vijijini mle maisha
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi wewe unaishi Tanzania ipi?Maisha ya wafanyakazi sio magumu Kama unavyojaribu kuelezea. Wanauhakika wa chakula Lakini Hawana Uhakika wa anasa.
Mtazame mama mwenye watoto wanne Anaelea watoto wake peke yake kwa kutembeza machungwa, akikusikia ataona unamdhihaki Mungu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Rudisha na pesa ya bodi piaNikisomeshwa kwa HESLB nikapata kazi , baada ya ongezeko la makato ya Bodi ya mkopo niliacha kazi ..Bora nipambane kimpango wangu kuliko kunyonywa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Apewe japo mmoja anachoitaji, hakuna salary increment wala employment opportunity za waitimu wa fani mbalimbali. Nchi imesimamaWasio na ajira nao wanataka ajira wenye ajira nao wanataka mshahara uongezwe
Hapo kipi kifanyike?
Mimi naona JK arudi madarakani
Subiri namna mkopo unapokua mchungu, kuna rafiki yangu anakatwa 300k per month, mfano mimi wanakata 100k per month , makato ni mengi mnoMkuu Mimi Ni mwanafuzi mnufaika wa HESLB, kumbe wanakata bila huruma?!
Sent from my Infinix X650B using Tapatalk
Na bado mtaisoma nambaApewe japo mmoja anachoitaji, hakuna salary increment wala employment opportunity za waitimu wa fani mbalimbali. Nchi imesimama
Huko alichukua ili kuweka mambo ya kitaa sawa!Sasa mkuu ulikopa NMB unategemea mshara ubaki ule ule... Hapo ungeacha hilo lomkopo unalokatwa 128k ungekuwa na pesa ya kueleweka ..[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16
Sent using Jamii Forums mobile app
Bora mjomba arudi teh tehWasio na ajira nao wanataka ajira wenye ajira nao wanataka mshahara uongezwe
Hapo kipi kifanyike?
Mimi naona JK arudi madarakani
Ukiona hivyo ndo anasa yake jamaa anadhani wote wanawaza hivyo!Umejaribu kujiuliza sababu za maana zinazoweza kuwa zimepelekea yeye kukopa au umewazia ununuzi wa Noah tu?
Tutajenga vipi kula kwenyewe kwa filimbi!Huku kwenye kujiajiri na biashara ndio usiseme, kwa siku unaweza unauza cement mifuko 3. Halafu faida ya mfuko mmoja ni 500, mabati hayatoki nondo hazitoki yaani watu hawajengi sijui wenzangu wa hardware biashara mnaionaje.[emoji16][emoji16][emoji16].
Sent using Jamii Forums mobile app
Well said la kuongezea ni kuwa pengine Huyo mama wa nyumbani alikimbia umande kwa kupenda msitake tufanane!Unachosahau ni kwamba huyu dada amesota miaka na miaka akilala njaa kule chuoni, akitembea umbali mrefu kwa miguu kuelekea kipindini, sometimes akiftari darasani mwezi wa ramadhani ili asikose kipindi darasani, sometimes wengine wakiuza utu wao ili wale, ili tu siku moja awe na ajira.
Mnakera sana mnaomlaumu eti alipochukua pesa ya heslb alifikiria nini. Hao waokota chupa za maji wengi wao (sio wote) walijitakia.
Kuna mtu eti anasema amuangalie mama mwenye watoto wanne, tunajuaje huyu dada hana hao watoto wanne wanaomtegemea?
All in all pole sana dada yangu na wadau wote mnaopitia magumu. Mungu yu pamoja nanyi
Kweli kabisa watumishe wanasema hali ni mbaya
Umeongea kwa uchungu sana! Pole sana rafikiNi heri yenu nyie wafanyakazi angalau mnapata kitu pamoja na makato yote hayo.
Lakini wengine biashara zetu zimekufa , na ajira ni ngumu sana na zinakuja kwa oda ya ujamaa na undugu. ?
Hata ela ukipata inaishia kwenye kula tu hata suruali kununua shida.
Zidumu fikra za awamu ya tano . Tuendelee kuungamkono Juhudi
Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo wasimamizi teh tehTatizo la wafanyakazi wengi sio risk takers, 90% hawaamini kufanikiwa nje ya mshahara na hawataki kupata ushauri nje na watu wa kazi.
Kama kuna kundi ambalo lilipaswa kufanikiwa sana ktk ujasiriamali basi ni wafanyakazi wa serikali, mna dhamana ya kukopa bila kuweka nyumba, hivyo biashara yako haina stress kulinganisha na hawa wa kuweka nyumba rejesho kuzalishwa na biashara.
Kulingana na hiyo slip mtumishi huyo anaweza kopa mpaka 15m, hizi ukimpa mjasiriamali mzoefu zinazalisha kwa uchache 2m profit monthly. Tatizo hawafahamu haya.
Sent using Jamii Forums mobile app