Vile vile katika ripoti hiyo ya commission inamtaja afisa mmoja wa shirika la kijasusi la Pakistani (ISI) kuwa kuna uwezekano alihusika katika njama za marekani kumkamata Osama kwa kuwa wiki moja kabla ya tukio la kumkamata Osama, aliwatuma watu kukata miti mikubwa iliyokuwa inazunguka ile nyumba Abbottabad ikiwa ni maandalizi ya helicopter kutua. Vile vile baada ya tukio la kukamatwa Osama aliuza vitu vyake na kuondoka Pakistani. Tofauti kati ya mashirika ya intelligence ya huku kwetu na nchi zilizoendelea ni kuwa wenzetu mashirika yao yanafanya mission zenye maslahi kwa taifa siyo kwa chama tawala. Ndio maana mission ikishakamilika wanatoa taarifa yote in detail kasoro baadhi tu ya tactics ambazo wanaona wataendelea kuzitumia kwenye mission nyingine. Huku kwetu mission zilizojaa TISS ni zile za kukandamiza Upinzani kama kumuua Kombe, kuua viongozi wa upinzani, kuwarushia mabomu Chadema n.k hizi mission hauwezi kuja kujua ukweli mpaka mmoja wao awageuke aropoke. Wenzetu mission zao zinakuwa high classified, lakini ikishakamilika tu wana-disclose kila kitu. Kwa mfano mission ya kumkamata Khaleed Sheikh Mohamed (KSM) the ring leader and mastermind wa 9/11 na akina Ramzi Yousef inajulikana ilifanywaje. Walifuatilia trail ya hela zote zilizokuwa wired kwenye account ya Mohamed Attar (kiongozi wa magaidi waliobamiza ndege WTC) Walianzia Dortimund Ujerumani ambakao Mohammed Attar alikuwa anasoma master of Science in Urban Planning katika chuo kikuu cha Dortimund. Walifuatilia trail ya ufadhili wa hela, msikiti aliokuwa anaswali hadi wakajua cell yao ilikuwa na kina nani, safari zake Pakistani na watu aliokuwa anakutana nao. Mohamed Attar ndio alikuwa ana-distribute hela kwa wale wengine za kusomea u-pilot wa ndege marekani. lakini hadi wanasomea upilot walikuwa hawajui mission yao itakuwaje. aliekuwa anajua mission ni KSM na Mohamed Attar. Kuna gaidi mmoja ambaye alikuwa yupo kwenye kikosi cha kwanza lakini alinyimwa viza ya kuingia marekani ndio alimtaja KSM kuwa ndie aliekuwa anawafadhili. Tofauti na kina Osama, KSM alikuwa anaishi maisha ya kifahari, anaingia kwenye club za usiku, anatumia vileo, anatumia simu, anachukua machangu, hakuwa anaishai maisha ya kiislamu. Kosa la kwanza na kubwa ambalo KSM na Ramzi walilifanya ni kumualika mwandishi wa habari wa Al-jazeera kwenda kuwahoji Pakistani. Ikieleweka kuwa kabla ya 9/11, Osama alikuwa anajulikana lakini hakuwa maarufu sana, hivyo kulikuwa na struggle kati ya magaidi kila mtu akitaka kupata umaarufu kuwa yeye ndio gaidi zaidi. Hiki ndicho kiliwasukuma KSM na Ramzi kumualika yule mtangazaji wa Al-jazeera kwenda kuwahoji. Yule mtangazaji alienda Islamabad akafungwa kitambaa usoni akazungushwa kwenye gari kuanzia asubuhi hadi jioni ili asijue muelekeo, mwishowe akashushwa kwenye gari wakamuingiza kwenye nyumba ambayo ina bunker alipofunguliwa kitambaa akakutana uso kwa uso na KSM akiwa na Ramzi Yousef. Pale KSM aka-declare jihad against American na ku-confess yeye ndiye aliyepanga na ku-finance mission nzima ya kubamiza ndege WTC. Yule mtangazaji wa Al-jazeera alipomaliza kuwahoji akaomba aondoke na Video footage wakamkatalia ila wakamruhusu achukue Audio record, hilo ndilo lilikuwa kosa kubwa sana maana ile audio iliporushwa tu Al-Jazeera, CIA wakaenda kuichukua Al-Jazeera wakatenganisha voice print za kila mtu alieongea kwenye ule mkutano wakaingiza kwenye mashine yao inayo-identify voice print ya kila mtu kama finger print. Hapo ndio ukawa mwanzo wa Drone attack Pakistani. Mtu akiongea kwenye simu kabla hajakata simu anashangaa bomu limeshatua. Kuna tukio moja walikuwa wamewasiliana wahudhurie harusi na Ayman Al Zawahil atakuwepo, machale yakawacheza Zawahili hakwenda, ile harusi ilibutuliwa na drone walikufa watu ukoo mzima. Baada ya kukamatwa Ramzi, KSM alistuka kuwa anafuatiliwa kwenye simu hivyo alikuwa hatumii simu yake, anaomba watu atumie simu zao ndio maana zoezi la kumkamata KSM lilishindikana zaidi ya mara 20, wakimtrace sehemu wakienda hawamkuti, alikuwa halali sehemu moja mara mbili mfululizo, Mpaka walipoamua kumtengenezea ramani kwa kutumia simu anazotumia, waka-identify sehemu 14 ambazo kuna uwezekano mkubwa wa kumkuta. Hizo sehemu zote zikafanyiwa kitu kinaitwa "synchronized ambush", yaani vikatengenezwa vikosi 14 vya askari wa Pakistani vikishirikisha maafisa wa CIA katika kila kikosi ambavyo vita-ambush sehemu zote 14 kwa muda mmoja, hapo ndipo walipomkamata KSM lakini walichoshangaa ni kuwa kwenye location moja katika zile 14 walikuta kiwanja hakina nyumba. walipofuatilia waya wa simu unaotumika kwa ID ya kiwanja hicho uko kwenye nyumba ipi ndipo ofisa wa ISI mtaalamu wa IT akai-trace nyumba inayotumia ID ya kile kiwanja humo ndipo walipomfurumusha na kumpiga risasi Abu Zubeida ambaye alipelekwa kutibiwa ujerumani akapona na kutoa siri kibao.