Unaogopa kung'olewa kucha, meno na jicho bila ganzi? Na kama wewe ni akina kajamba nani lazima ufe kwani kwenda kutibiwa sauzi yahitaji kunako vijisent
mimi nafikiri suala kubwa hapa ni kupingana kwa hoja,ripoti zimeandikwa hivyo na wengi tumeamini hivyo,sasa kama unaona hizo zote ni falacies then bring here your arguments ili tupime na tuone uhalisia wa mambo.Kukashifu tu hakuwezi kuwa suluhisho kwasisi tulioamini kuhusu hili jambo.
mimi nafikiri suala kubwa hapa ni kupingana kwa hoja,ripoti zimeandikwa hivyo na wengi tumeamini hivyo,sasa kama unaona hizo zote ni falacies then bring here your arguments ili tupime na tuone uhalisia wa mambo.Kukashifu tu hakuwezi kuwa suluhisho kwasisi tulioamini kuhusu hili jambo.
kama walio muua wametuonyesha hiyo... we uliye hapo Kariakoo unabisha je unao uthibitisho upi? kwamba sio yenyewe kama uthibitisho unao basi uweeke tuuone...
Hiyo nyumba ipo Abbottabad Pakistan nadhani hadi serikali ya Pakistan ilithibitisha kwa sababu operation ilipigwa hapo na baada ya operation nyumba hiyo ilibomolewa baada ya kufa Osama na mwili wake kuchukuliwa...
Unajua bwana Ritz usibishe vinginevyo njoo na ushahidi mwingine utuambie washikaji walitupiga changa la macho usitake kufananisha Intelligence za wenzetu wa dunia ya kwanza na hii yetu ya kina Rama...
Ebwana jamaa wako njema sana...
Acha uwongo, mbona report ya mission yake ilishawekwa wazi tokea alipouwawa kaisome acha stori za vijiweni. Taarifa za Osama zilitolewa na detainee watatu wa alqueda waliopo Guantanamo. wa kwanza ni Mastermind wa 9/11 Khaleed Sheikh Mohamed (KSM), huyu ndie alimtaja Courier wa Osama ajulikanaye kwa jina la Al Kuwait ambaye ndiye anaebeba maelekezo na mawasiliano yote kutoka kwa osama na kupeleka kwa foot soldiers, Wa pili kumtaja Al Kuwait ni Abu Zubeida, Huyu Abu zubeida pamoja na Ramzi Yousef ndio waliolipua WTC kabla ya 9/11. Abu zubeida kwanza aliteswa na CIA kwa kutumia Enhanced Interogation techniques kama water borne akagoma kutoa information yoyote, mpaka CIA wakamtishia kumkabidhi kwa intelligence ya Saudi Arabia wakiamini ataogopa maana Saudi Arabia wanajulikana kwa kutesa, wakashangaa anawaambia wampeleke Saudi. Hapo ndio CIA wakacheza trick wakampakiza kwenye ndege na kuzunguka naye muda mrefu angani wakijifanya wanampeleka Saudi Arabia mwisho wakatua naye sehemu hukohuko marekani wakawachukua maofisa wa CIA waarabu wakiwa na nguo za jeshi la Saudi Arabia wakaanza kumuuliza maswali hapo ndio akamtaja Al Kuwait, halafu akawataja wafadhili wa Osama akiwepo Mtoto wa mfalme wa Saudi, Generali wa Jeshi la Saudi na maofisa wengine wawili wa serikali ya Saudi na akawapa namba ya motto wa mfalme wampigie ili awaamrishe wamwachie. watu wote waliotajwa na Abu zubeida CIA waliwaua kuanzia mtoto wa mfalme alikutwa amekufa akiwa vacation, yule General wa jeshi alikutwa amekufa jangwani kwa kiu na kukosa maji na wale maofisa wote. Huo ndio ukawa mwanzo wa Osama kukosa hela (financial suffocation). wakaanza kumfuatilia Al Kuwait Pakistani wakamtrace akitokea sokoni hadi nyumba aliyokuwa akienda Abbottabad. Osama aliishiwa hela mpaka wake zake walikuwa wanaenda kwa sonara wanauza mikufu na herein zao ili wapate hela ya kula. Ndio CIA wakamkodia nyumba karibu na nyumba ya Osama Afisa wake aliyekuwa anafanya kazi katika Shirika la Save the Children ambalo lilikuwa linafanya kampeni ya kinga ya magonjwa ya watoto. Na sio kwamba eti marekani walikuwa wanachukua DNA za watoto na ku-match na za Osama huo ni uwongo kwa sababu kinga iliyokuwa inaratibiwa na Save the Children ilikuwa ni ya Matone sasa kuwapa watoto matone uta-extract vipi DNA. Aliyebaki sasa ni second in command wa alqaeda daktari wa Misri Ayman Al Zawahil ambaye naye inaaminika amejificha kwenye mpaka wa Afg na Pak.
Osama alizikwa wapi?
mkuu kama haya unayoyasema umesoma kwenye report mimi naiomba hiyo report au source ya haya maneno yako!! ni maneno mazuri kuyasoma kutoka kwenye chanzo halisi sio kuyasikia!! ntafurahi kama nikipewa hiyo nakala
kama walio muua wametuonyesha hiyo... we uliye hapo Kariakoo unabisha je unao uthibitisho upi? kwamba sio yenyewe kama uthibitisho unao basi uweeke tuuone...
Hiyo nyumba ipo Abbottabad Pakistan nadhani hadi serikali ya Pakistan ilithibitisha kwa sababu operation ilipigwa hapo na baada ya operation nyumba hiyo ilibomolewa baada ya kufa Osama na mwili wake kuchukuliwa...
Unajua bwana Ritz usibishe vinginevyo njoo na ushahidi mwingine utuambie washikaji walitupiga changa la macho usitake kufananisha Intelligence za wenzetu wa dunia ya kwanza na hii yetu ya kina Rama...
Ebwana jamaa wako njema sana...
Osama alizikwa baharini...
Jamaa atakuwa amesikia habari zile za vijiweni ndio anabisha sasa watu wanaleta na proof yeye bado kama haamini halafu anataka kutuambia sio kweli bila kutuletea mbadala wake tujue ukweli ni upi na tuweze kuuchambua...Hapa huyu ritz atakuwa kapotoka labda hajui source of knowlegde???
Hapa kuna habr ambyo imetoka kwenye authority amboyo osama amekuwa akiish,we utasema n uongo kwa mantiki ipi labda?
Souc nyingne n mtu kusma kama wewe ulivyfanya, napia umetazama kwenye vyomb vya habr ambvyo vina mamlaka ya kuhabarisha watu,yeye anachobshia n chanza habri au mleta habri?
Ritz
hata nikikuambia hautonisadiki...Baharini wapi? Bahari kubwa.
Wakuu nitaendelea kuwapa
simulizi hizi za mission za CIA, MOSSAD na KGB maana wenzetu wanaziweka
wazi hawana cha kuficha kama bongo. Ile mission ya kumkamata Osama ni
kali lakini kwa watu wanaojua mission zilizofanyika hapa duniani, hakuna
mission kali kuizidi ile ya Entebbe iliyofanywa na MOSSAD, hata hii ya
Osama ilichukua items nyingi kwenye mission ya Entebbe. Ukitaka kujua
ile ya Entebbe ni kali kuliko ya Osama linganisha technologia
zilizotumika, hii ya Osama walitumia chopa za shinoku zenye technology
ya stealth inayoweza kukwepa rada wakati ya Entebbe hakukuwa na
technology hiyo. Ndege zilizohusika kwenye mission ya Osama ziliruka
kutoka kwenye military base ya marekani iliyopo Jalalabad Afg ambayo ipo
ka 20 km kutoka kwenye mpaka na Pak wakati Ndege zilizohusika kwenye
mission ya Entebbe ziliruka kutoka Tel Aviv kupita nchi mbili ambazo ni
hostile Egypt na Sudan 5,000km kuja Entebbe. Operation ya Osama
kulikuwepo na maofisa wa CIA waliokuwa kwenye ofisi ya ubalozi ambao
walielekea Abbottabad mapema kwaajili ya ku-monitor situation na kuna
maofisa wa ISI ambao walikuwa kwenye jeshi la Pakistani ambao walikuwa
wanatoa taarifa kwa maofisa wa CIA kila kinachoendelea kuhusiana na
response ya jeshi la Pakistani. Siku nikipata nafasi nitawasimulia ile
operation ya Entebbe ilivyopangwa na failures na success zake. kama
ilivyokuwa ya Osama zilipangwa plana 4 za kuifanya ile mission ya Osama
na zote zilifanyiwa mazoezi ndio maana ile helicopter ilivyokosa thrust
na kudondoka walibadili plan kutoka Plan A kwenda plan C, sasa siku
nikipata nafasi nitawaeleza Plani A ilikuwa ikoje, plan b,c na d. Na kwa
nini ile helicopter ilivyodondoka walibadili plan kutoa A kwenda C, kwa
nini hawakuenda plan B.
hata nikikuambia hautonisadiki...
utakuja na swali jingine unaweza kuniuliza nitajie majina ya walio kuwa kwenye msiba wake au utaniuliza alizikwa saa ngapi? au unaweza ukaniuliza hitma yake ilikuwa ni lini?
bwana Ritz unachekesha sana...
Leta basi we ukweli...
ambaye umeshikiwa akili na story za vijiwe vya kahawa...
Osama alizikwa baharini...
Teh teh teh teh teh!
Hapo mkuu haki ya nani nimecheka mno!
Unanikumbusha mwalimu wangu wa nursery,
Anaitwa magdalena!
Akisema "a" na mimi nasema "a" akisema " be" na mimi "be". Hata siku moja sijawahi kuuliza kwa nini ni "a" na wala sio "k"?
Yaani wao kusema alizikwa baharini baasi! Wewe umeridhika kabisa! ili siku nyingine usije jiingiza kwenye ushahidi na ukapata matatizo ya kuulizwa ni bora useme"nimeskia wanasema kwenye radio au nimeona kwenye runinga kuwa kazikwa baharini!.
Halafu baharini hawaziki! Wanatupa tu!
Kwa hiyo usimlaumu mkuu Ritz kukukatalia na kukuuliza maswali hayo. Hii inatokana na kauli yako uliyotoa!
Yaani kwa majibu yako ni kama mtu alikuwa kwenye tukio.
We mpira ukipigiwa mpasie huyohuyo aliye kupigia hakuna mtu atakulaumu.
inasemekana Osama alizikwa baharini na hata wavuvi hakuna aliyeona hilo tukio...Jibu swali ndiyo maana ya mijadala kisha na mimi takuja na mashiko yangu.
Osama alizikwa bahari ipi na sehemu gani hayo yote uliyoyasema hayana uhusiano na ninachouliza.
Nipe jibu kisha tupanue mjadala.