Kwani serikali hiyo unayo itetea ilichukua hatua gani baada ya ule mlipuko wa bomu kule Soweto, Mbona sikuelewi kwa maana nyingine unasema ya kwamba video haipo na lile tukio ni la uongo au!?
Unaposema Uzushi, unamaana ya kwamba wala hata ule mlipuko haukutokea ama!? je hao CCM wenyewe wanafanya siasa ambazo si za uzushi ama!?
Kwanza nataka kujua unapotaka kuthibitisha ni kwa namna ipi!? Halafu tukirudi kwa Zitto unataka kusema kipindi kile Saed Kubenea kwenye lile gazeti lake lililofungiwa alipoweka mawasiliano ya Zitto na Jack Zoka pamoja na maeneo na zile namba za simu, unataka kusema ni uongo!? mpaka Zitto Kabwe akayamind makampuni ya simu...
Vipi mbona huongelei ushahidi wa Mwigulu, vipi ile sio conspiracy!? hauoni ya kwamba hiyo ni double standard!?
Lakini pia nashangaa inakuwa vipi haujiulizi ya kwanini mahakama imemkuta hana hatia licha ya huo unaouita ushahidi... Halafu na lengo la Ludovick kurekodi ilikuwa ni nini!?
1. sijasema tukio ni uzushi nimeraise doubt juu ya uwapo wa video ambayo haitolewi mpaka kwa masharti maalum. Masharti ambayo ni sawa na kuiamrisha serikali nini cha kufanya bila kuwa na reasonable doubt ya kufanya hivyo. Hivi kweli hata serikali iwe ya haki kiasi gani, unategemea iunde "tume ya kimahakama" just because kiongozi wa upinzani kasema hivyo?
2. Uthibitisho uko wa aina nyingi: unapodai zitto kapokea bilioni 3 toka kwa dr kimei na usalama wa taifa tunahitaji kujua WEWE UMEJUAJE! Una mkanda wa video, una transcript za mazungumzo yao, unaweza kutuonyesha bank statement ya zitto inayoonyesha miamala hiyo to that effect au?
3. Zitto kuwasiliana na jack zoka tatizo liko wapi? zitto ana uhuru wa kuzungumza na yoyote yule. kwani chadema wana uadui na vyombo vya serikali? jack zoka ni usalama wa taifa kwa raia wote including wanachama wa vyama vya upinzani, polisi, jeshi, wizara n.k vyote hivyo ni vya raia wote. Chadema inafanya kana kwamba ukiwa chadema then wewe automatically ni adui wa serikali! Je Chadema kwenye katiba yake inatii sheria za nchi gani? au kuna kipengele kinasema "chadema member shall not talk to usalama wa taifa" humo ndani ambacho ndio zitto kavunja?
vile vile, kama nakumbuka vizuri (nisahihishe kama nakosea), gazeti halikutoa mazungumzo (transcript), bali lilitoa namba za simu na call duration, je unaweza kutuambia walikuwa wanazungumzia nini? au kwa sababu zitto ni "adui wa mbowe" basi "lazima awe anapanga mipango dhidi ya chadema". Bila kujua kilizungumziwa nini the rest is mere speculation. Hivi gazeti likichapisha simply namba za simu na call duration kati ya Mbowe na Kikwete utaconclude hivyo hivyo kuwa Mbowe anauza chama kama ilivyo kwa zitto au?
4. Ushahidi wa mwigulu ambao siuongelei ni upi huo? sijaona video ya mwigulu popote pale, naomba link tafadhali niione kisha ndio nijadili.
5. Mahakama haijadili video kama video inajadili mashataka ambayo video ni ushahidi. Nilichotaka mimi ni maelezo kwa mtu kama wewe kuwa pale lwakatare kwa nini alikuwa anaongea yale? hivi wewe hujiulizi hili swali? Mipango ile haikupi maswali? Mpaka sasa hakuna alternative story ya video ile, kinachoonekana ni lwakatare kupanga mipango miovu baas! Chadema walitakiwa kusema kuwa the real story ni hii: "lwakatare alikuwa anaanda mswada wa bongomuvi", kitu kama hicho! sio kushabikia ushindi wa technicalities za kisheria mahakamani. Mwisho wa siku video iko pale pale bila maelezo.
Pili, Ludovick pia ni mwanachama wa chadema, sababu za yeye kurekodi mimi nisiye chadema siwezi kujua. Lakini je, kama mwananchama wa chadema anapanga mipango ya kuvunja sheria kama ile, si wajibu wa mwanachama wa chadema kuifichua? au mwananchama wa chadema anatakiwa kulinda mipango miovu ya chadema wenzie? Kwangu mimi yoyote aliyefichua video ile ni mwananchi mwema anayetakia mema nchi yetu. Unless of course chadema/lwakatare waseme kuwa lwakatare alikuwa ana-act or something, then aliyefichua ndio tutamuita mchochezi. Lakini kama tunavyojua Chadema hawajawahi kutueleza lwakatare alikuwa anapanga mipango hiyo kwa sababu gani....perhaps ni mipango ya kichama?