Maisha ya uswahili kama hujayazoea unaweza pata shida

Maisha ya uswahili kama hujayazoea unaweza pata shida

Uswazi kwetu!
Supu za mimba za ng'ombe!
Sembe la hamira mboga pandu na nyanya masalo, ukichoma ngulu unalaaniwa mtaa!
mzima
mlango wa chooni pazia la kipande cha junia au kiroba! Kona ya mti nyeusi kwa kukokona! Ukiingia utakutana na makimba mengine kama koni, makimba mengine gololi zilizo changanyika na damu na makamasi.....
Ukisha yaruka makimba ili unye salama urojo wa mavi usikurukie unafunika na gazeti....
Uswazi kwetu....!
Wewe hauongelei uswazi unaongelea kijiji kwenu huko au uswazi ya vijijini sio dasalam .
 
Habari za mchana,

Maisha ya uswahili sio poa poa kama hujayazoea unaweza pata shida sana kuna.

Kuna kipindi nilienda kwa Azizi Ally kumsalimia mtu huko sasa kufika pale tunapiga story gafla kaingia mtu hila hodi anatoa taarifa nachukua mboga kule nini ugali kidogo nilishangaa ase akaona pembeni kuna matunda akabeba.

Ikabidi nimuulize mwenyeji wangu hivi huku ndio maisha gani haya mnaishi mtu anaingia kama kwake anachukua vitu kiholela holela why akawa anacheka.

Siulizi kwa ubaya hila nataka kujua hizo tabia za kienyeji zinatokaga wapi?
Gafla[emoji117]ghafla
Hila[emoji117]ila
 
Badala ya kufurahi upige mtoto wa mtu utahama kijiji bila kupenda!
Sasa wale wanao wahi asubuhi nyumbani kwako kudai chai na andazi kama ww umewazaa!
Heri uwasongee sembe la hamira mboga chumvi+ndimu+plpl...kuepusha soo...

[emoji847][emoji23][emoji23] kwamba watanipga
 
Habari za mchana,

Maisha ya uswahili sio poa poa kama hujayazoea unaweza pata shida sana kuna.

Kuna kipindi nilienda kwa Azizi Ally kumsalimia mtu huko sasa kufika pale tunapiga story gafla kaingia mtu hila hodi anatoa taarifa nachukua mboga kule nini ugali kidogo nilishangaa ase akaona pembeni kuna matunda akabeba.

Ikabidi nimuulize mwenyeji wangu hivi huku ndio maisha gani haya mnaishi mtu anaingia kama kwake anachukua vitu kiholela holela why akawa anacheka.

Siulizi kwa ubaya hila nataka kujua hizo tabia za kienyeji zinatokaga wapi?
Kaka mwachi karibu mbagala🤣🤣🤣🤣🤣😋Maji matitu
 
Wengi mmeongopa sana kuhusu uswazi au neno uswazi halijaeleweka kwenu .

Eti uswazi ukute kimba chooni ? Nop wadanganye wa kwenu .

Eti uswazi wana style zao za kunyoa hasa vijana ? Acha uongo uswazi unyoaji wengi uwafuatisha wasanii

Eti uswazi sijui bla bla gani , punguzeni kukariri maisha wakati wengine mmetoka huko vijijini mnakunya kwenye misitu leo mnajifanya kuyashangaa maisha ya uswazi .

Sifa za uswazi ni hizi .

Mazoea yaliyopita mipaka kwa watu wake .

Matusi kwa rika zote si babu wala bibi .

Maisha ya bei za chini sana mfano kupata sukari ya mia .

Watu kuishi chini ya dollar ila maisha yanaenda .

Uchawi hasa kwenye viduka vyao yaani tunaita chuma ulete.

Watu wa huko kupenda masherehe yasiyokwisha tunaita shughuli .

Elimu kwa watoto wa kule sio kipaumbele kwa wazazi .

Ukabaji na wizi uliokithiri .

Kujiita majina ya wasanii wa mbele mara Fatuma kuitwa Fetty Rish .

Kupata vitu vya ndani kwa bei za chini kupita kawaida .

Uwepo wa watu ambao ni wababe wa mtaa yaani unaweza ibiwa usiku asubuhi ukaripoti kwa hawa wababe na ukapata mali yako safi .

Uswazi hakuna mtu atakuuliza unafanya kazi gani ? Zaidi usiwe mtu official sana kimavazi sababu watakuita wa kishua na pia watakuhisi ni usalama sababu hiyo kazi sio mtoto wala mkubwa wote wanaijua .

Uswazi kila ukipiga story na watu wa huko si ajabu kila mtu kukuambia ana nduguye ni afisa usalama

Uswazi sio polisi wala baka baka yaani wajeda hawaogopwi na pia wanakaa vijiweni kula story na wana mtaa ikabidi hata ganja wanavuta wote
Cc .keko magereza na askari wake hasa vijana .

Uswazi hawaogopi cheo chako ila wanaogopa hela yako kwa msemo wa dolari zako tu .

Uswazi kila familia ina ndugu alizamia nje hajarudi mpaka leo .

Uswazi kwa dar wengi ni waislamu isipokuwa wachache sana hasa watu kuja waliowahi mjini zama zile

Uswazi ishi na rika zote vizuri hutajutia ila ukijitia huna muda na wana mtaa huwezi kuendelea utaibiwa mpaka ukome

Uswazi si ajabu choo kimoja kutumika na nyumba tatu kwa mpigo na ratiba ya usafi inazihusu nyumba zote .

Ukifika uswazi usikubali kusema unatoka mkoa gani sema ni wa dar utaheshimika kiasi chake ila kujitabanaisha mkoa utokao wao uanza kukuhisi wewe ni mshamba .

Oya jamani dar asilimia 80% ni uswazi japo kila sehemu inatofautiana uswahili wake hivyo msijipe presha wengi wenu mnaishi uswahilini tu ila hamjajua tu.

Haya nayaeleza kupitia exprience yangu huko KEKO, TANDIKA , TEMEKE na kwingineko katika viunga vya jiji la dasalam

Wale wa Masaki tukutane hapa tukumbushane enzi.
 
Back
Top Bottom