Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 8,508
- 15,276
Katika maisha, tujifunze kuishi kwa maadili, heshima na adabu. Hata maisha yawe magumu kiasi gani, ukipata nafasi ya kupumua na kuona hatua moja mbele, usisahau kumshukuru Mungu.
Kila mtu ana muda wake wa kufanikiwa. Wapo wanaowahi kufika kwenye mafanikio, na wapo ambao safari yao huchukua muda mrefu zaidi. Hilo lisikufanye ujione umechelewa maishani.
Changamoto inaanza pale unapokuwa kwenye kundi la marafiki ambao wao wamefanikiwa mapema, halafu wewe bado unapambana. Mara nyingi utagundua umeanza kutengwa, kupuuzwa, simu zako hazipokelewi na hata uwepo wako haupewi tena thamani kama zamani.
Lakini maisha yana tabia ya kubadilika.
Wapo wengi waliowahi kukataliwa, kubezwa na hata kuonekana hawana mwelekeo. Baadaye Mungu alipowafungulia milango ya neema, wale wale waliowapuuza wakaanza kuwatafuta, kuwapigia simu na kutaka kurudisha ukaribu kana kwamba hakuna kilichowahi kutokea.
Ndipo unapotambua kuwa si kila anayekuita rafiki ataendelea kuwa rafiki katika kila msimu wa maisha yako. Wengine wanakupenda ukiwa juu, lakini hawana muda na wewe ukiwa chini.
Ndiyo maana usijenge maisha yako juu ya matarajio ya watu. Watu hubadilika kulingana na mazingira, lakini Mungu habadiliki.
Jifunze kuweka balance katika mahusiano. Waheshimu watu wote, lakini usiweke furaha yako mikononi mwao. Kuna ambao wakati ulikuwa na shida hawakutaka hata kupokea simu yako, lakini Mungu alipokufungulia milango ya neema, hao hao wakaanza kukutafuta kwa bidii.
Usiwe na kinyongo. Usilipize kisasi. Endelea kuwa na moyo mwema, lakini pia usisahau waliokuwa pembeni yako wakati kila kitu kilipoonekana hakina matumaini.
Kumbuka, maisha yanaweza kubadilika kwa muda mfupi sana. Leo unaweza kupuuzwa, kesho ukawa unatafutwa.
Usikate tamaa kwa sababu ya namna watu wanavyokuchukulia leo. Endelea kufanya kazi kwa bidii, kuwa na subira, na mtangulize Mungu katika kila hatua. Wakati wako ukifika, hutahitaji kujitangaza-matokeo yako ndiyo yatakayoongea.
Na wewe je, umewahi kupitia kipindi ambacho watu walikupuuza, halafu baada ya maisha yako kubadilika wakaanza kukutafuta tena?
Note: Nlichoandika hapa ni theory tuu practically hakihusiani na maisha yangu binafsi