Maisha yamejaa huzuni kuu, nini kinaleta furaha maishani?

Furaha ni kuridhika, accomplishment of what you have set out to do..., Hivyo mtu asiye na kitu huenda akawa na furaha kuliko wewe mwenye all material things (tofauti ni yeye anachotaka amekipata na wewe huenda una chase an illusion)

Kumbe nimechekesha😀
Imenibidi nicheke maana sioni kama nasumbuliwa na upweke wa kukosa mwanamke. Zamani sana nilikuwa na nawaza kwamba furaha inaweza pia kuletwa na ndoa au mahusiano mazuri. Si hivyo kwa aslimia Mia moja. Nimekuwa na nimeona watu wengi walivyoteswa na mahusiano. Wengine watu wa kariba kabisa wakiwa na maisha mazuri ila kwa sasa ni kama hawakuwahi kabisa kufanikiwa. Wana maisha magumu kabisa na wenza wao wakawaacha. Sina hilo wazo kwa sasa na halinipi shida. Nashukuru.
 
Life is purposeless which makes it even much boring.

Pesa itakupa furaha ya muda mfupi tu kwa sababu utaweza kukidhi mahitaji ya hapa na pale, lakini hiyo sio furaha ya kweli.

Hata uwe na magari na majumba huwezi kupata furaha ya kweli, utakuwa unajifariji tu huku ukiyaangalia matofali na kuta za nyumba na kujipiga kifua kuwa wewe ni mwamba lakini hakuna lolote.

Ukipata pesa hakikisha unakula kuku, kitimoto za kutosha kisha gida bia mbili za nguvu.

Maisha bila BIA yana faida gani?

Kula BIA.

Cc: mshamba_mwingine Poor Brain
You kill everything kinachoweza kupumua
 
Jichanganye km sio mtu wa kuwa peke yako.
Mimi furaha yangu kukaa peke yangu kuna vimichezo nachezaga nikiwa peke yangu vinanipa furaha sana.!!!
Marafiki zangu siku hizi wananishangaa siwapi muda wangu kabisa.!! Hata outings nimepunguza weekend.
 
Habari za wikiendi familia? Ni kitu gani huweza kuleta furaha katika Maisha? Mali? Mke? Watoto? Marafiki? Ibada? Au ajira?

Mwenzenu siku za karibuni nakuwa mwenye huzuni sana. Sijioni kuwa mwenye furaha japo mambo mengi niliyoyatamani kuyafikia angalau kwa kiasi namshukuru Mungu.

Wakati mwingine nafikiria pengine nioe lakini akili inagombana na moyo. Ni nini hasa huleta furaha katika Maisha?

Kwanza unatakiwa ujue ya kuwa huwezi ukawa na furaha siku zote wala huwezi kuwa na huzuni siku zote.

Furaha ya moyo ipo katika uchache wa madhambi. Hapa ndipo furaha ilipo.
 
Hakunaga kitu kinachoujaza moyo amani ya milele.
Ukipata hiki utataka kile! Maisha yametengenezwa kimchakamchaka unatakiwa uwe busy sana ili usipate muda wa kufikiria. Ila ukipata muda tu wakufikiria unajikuta mpweke sana! Upweke ni mbaya ndo mana Mungu aliumba mtu mke na mtu mume ili kusaidia kupunguza upweke na namna ambayo pengine SIo direct, ukiwa na familia utajikuta uko busy kuipambania kwahiyo akili itahama...
Usiombe uwe huna hela/huna mpenzi /huna mchongo unaweza hata ukaambiwa jitoe mhanga ukajitoa maana kuna upweke mkuu unakukuta.

Japo binafsi naamini nikiwa na uwezo wa kusafiri safiri zitokua mpweke
 
Purposeful life naona wengi mmeoongelea lakini purpose hutengeneza expectations na struggles zisizokwisha.

Kwa upande wangu naona watu ambao hawana purpose wala expectations kubwa katika maisha huku wakiwa hawa_fake maisha ili kulinda hadhi fulani. Watu kama hawa wakipata chakula, nyumba na watoto kwenda shule. Wanaridhika na kufurahia maisha

Sisi tunaotaka MORE kwenye maisha ndio huwa wapweke kwa kuendeshwa na kupata na kukosa
 
Imenibidi nicheke maana sioni kama nasumbuliwa na upweke wa kukosa mwanamke. Zamani sana nilikuwa na nawaza kwamba furaha inaweza pia kuletwa na ndoa au mahusiano mazuri. Si hivyo kwa aslimia Mia moja. Nimekuwa na nimeona watu wengi walivyoteswa na mahusiano. Wengine watu wa kariba kabisa wakiwa na maisha mazuri ila kwa sasa ni kama hawakuwahi kabisa kufanikiwa. Wana maisha magumu kabisa na wenza wao wakawaacha. Sina hilo wazo kwa sasa na halinipi shida. Nashukuru.
Basi tuambie shida nini😀
 
Purposeful life naona wengi mmeoongelea lakini purpose hutengeneza expectations na struggles zisizokwisha.

Kwa upande wangu naona watu ambao hawana purpose wala expectations kubwa katika maisha huku wakiwa hawa_fake maisha ili kulinda hadhi fulani. Watu kama hawa wakipata chakula, nyumba na watoto kwenda shule. Wanaridhika na kufurahia maisha

Sisi tunaotaka MORE kwenye maisha ndio huwa wapweke kwa kuendeshwa na kupata na kukosa
Nakubaliana na wewe mkuu , Watu wanashindwa kujua Mafanikio ya kimahusiano pamoja na kuridhika ndio chanzo kikuu cha furaha.
 
Purposeful life naona wengi mmeoongelea lakini purpose hutengeneza expectations na struggles zisizokwisha.

Kwa upande wangu naona watu ambao hawana purpose wala expectations kubwa katika maisha huku wakiwa hawa_fake maisha ili kulinda hadhi fulani. Watu kama hawa wakipata chakula, nyumba na watoto kwenda shule. Wanaridhika na kufurahia maisha

Sisi tunaotaka MORE kwenye maisha ndio huwa wapweke kwa kuendeshwa na kupata na kukosa
Nakubali kwa kiasi.
Ukienda kijijini, mtu analima chakula ana watoto, nyumba, Azam tv ana furaha na amani kushinda sisi. Watoto wanamzunguka, mkewe yupo home muda wote wanaongea kilugha na kuangalia sinema zetu. Mara kaenda ktk kikundi, kanisani, shamba wiki imeisha. Hata JF au twita haijui. Ana furaha na amani. Sasa tazama sisi wenye dreams kila siku unaona ulichelewa kusoma. Elimu haijakulipa. Ccm mizinguo. Mbowe dikteta. Mshahara mdogo, mke anakiburi, mume anazingua, marafiki wanafiki, ndugu wanafiki yaani kila kitu ni stress. Hauwezi kuwa na furaha.
 
Habari za wikiendi familia? Ni kitu gani huweza kuleta furaha katika Maisha? Mali? Mke? Watoto? Marafiki? Ibada? Au ajira?

Mwenzenu siku za karibuni nakuwa mwenye huzuni sana. Sijioni kuwa mwenye furaha japo mambo mengi niliyoyatamani kuyafikia angalau kwa kiasi namshukuru Mungu.

Wakati mwingine nafikiria pengine nioe lakini akili inagombana na moyo. Ni nini hasa huleta furaha katika Maisha?
Furaha yangu naipata kwa watoto wangu. Muda wangu wote wa ziada natumia na watoto wangu for real wanqnipq pumziko bahati nzuri age na watoto wangu ni wadogo.
 
Furaha ni wewe mwenyewe, furaha unaitengeneza mwenyewe, hailetwi na mke wala mme wala rafiki.

Jitengenezee furaha yako, furaha yako unaitengenezaje?? Kuwa na pesa? Basi zitafute sana....furaha yako ni kuzagamua?? Nenda kafanye. Furaha yako ni nini??

Uzi ufungwe hapa...

Akiifungamanisha furaha yake na vitu au kitu bhas ajue hiyo sio furaha... Maana bila vitu hivyo pia furaha yake inakuwa haipo...

Ajipende... Ajikubali... Afurahie na kushukuru kuwa hai kwa wakati huu. Ndio jambo la msingi hilo... Mengine ni ziada tuu
 
Furaha yako ni wewe mwenyewe.

Huna furaha wakati uko single, je ukioa itakuwaje? Labda upate mke mwema.
 
Nakubali kwa kiasi.
Ukienda kijijini, mtu analima chakula ana watoto, nyumba, Azam tv ana furaha na amani kushinda sisi. Watoto wanamzunguka, mkewe yupo home muda wote wanaongea kilugha na kuangalia sinema zetu. Mara kaenda ktk kikundi, kanisani, shamba wiki imeisha. Hata JF au twita haijui. Ana furaha na amani. Sasa tazama sisi wenye dreams kila siku unaona ulichelewa kusoma. Elimu haijakulipa. Ccm mizinguo. Mbowe dikteta. Mshahara mdogo, mke anakiburi, mume anazingua, marafiki wanafiki, ndugu wanafiki yaani kila kitu ni stress. Hauwezi kuwa na furaha.
Kabisa na hapo bado hujaangalia classmate wana ndinga kali, flights za kugusa na majumba. Unaanza kuchanganyikiwa kwa kujiona failure

Hapo furaha itatoka wapi
 
Back
Top Bottom