mudy92
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 671
- 531
Si umesema Muhammad ni mfano wa Musa, ndio ueleze kivipi!? ndio useme Muhammad na Musa tabia zao zinafanana kivipi!?
Nani alimpa utume Muhammad!? hivi Musa na yeye alikuwa ni ummy!?
Muhammad alitumwa kwa jamaa zake
Quran 26:214 Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.
Quran 41:44 Na lau tungeli ifanya Qur'ani kwa lugha ya kigeni wangeli sema: Kwanini Aya zake haziku pambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwaarabu? Sema: Hii Qur'ani ni uwongofu na poza kwa wenye kuamini. Na wasio amini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali.
Quran 34:44 Wala hatukuwapa Vitabu wavisome, wala hatukuwatumia Mwonyaji kabla yako wewe.
Quran 12:2 Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani kwa Kiarabu ili mpate kuzingatia.
Quran 46:12 Na kabla yake kilikuwapo Kitabu cha Musa, kuwa chenye uwongozi na rehema. Na hichi ni Kitabu cha kusadikisha na kilicho kuja kwa lugha ya Kiarabu, ili kiwaonye walio dhulumu, na kiwe ni bishara kwa watendao mema.
Quran 43:3 Hakika Sisi tumeifanya Qur'ani kwa Kiarabu ili mfahamu.
Quran 26:195 Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi.
Wewe ndio haujui kabisa hebu kula hii kwanza
Yohana 4:42 Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu.
Halafu uniambie hapa chini, je kwenye hii aya Musa alitumwa kwa ulimwengu wote!?
Quran 7:144 (Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Musa! Mimi nimekuteuwa wende kwa watu na Ujumbe wangu na maneno yangu. Basi chukua niliyo kupa na uwe katika wanao shukuru.
Kwenye huo mstari ni kitu gani hujaelewa hapo!?
Karibu kwa Yesu, kijana maana habari za Roho hauna ujuzi nazo na Quran imekiri, upo sawa kabisa, Mungu ni Roho, nao wamwubudio imewapasa kumwabudu katika roho na kweli, kwa hiyo ile kuvua viatu kuwaza Mahurulaini unaweza ukawa unasubiri meli airport
Quran 17:85 Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu.
wapi nyie Mmepewa Elimu ya roho?? Huyo mnaemwita Mungu?