Mbona u.ekuwa mwendawazimu hivyo!! Mleta mada amesema watende haki. Tunafahamu kila taasisi kwa sasa zimetekwa na genge la wauaji. Iwe ni mahakama, bunge, polisi na hata baadhi ya taasisi za dini, zimetekwa na wauaji, na zote zinamtumikia ibilisi shetani.
Ndiyo maana mleta mada anewakumbusha majaji kama watu binafsi, kuwa pamoha na taasisi zao kutekwa na genge la wauaji, watambue kuwa wao ni binadamu, siku zao zikifika, hakuna kujitetea kuwa nilielekezwa, watahukumiwa wao kama wanadamu binafsi.
Kwa kweli nawaonea huruma sana waliopo kwenye taasisi kama za polisi, Tiss, Mahakama, Bunge, maDC, maRC, na viongozi wote wa chama kile cha mauaji, maana kwa kweli kuwa watu wa haki, kuwa watu wema, inahitaji jitihada binafsi za pekee, kwa sababu juu yao yupo shetani anayewateka wamtumikie shetani kwa kutenda uovu!! Yaani upo kwenye nyumba ya mwovu, unaelekezwa utende uovu, wewe uende ukatende wewe, ni kazi ngumu sana.
Hongera sana mleta mada, umetimiza wajibu wako kama kiumbe wa Mungu, wajibu wa kushauri na kuwakumbusha majaji, wakienda jehanamu kwa sababu ya kutenda uovu, hawatamlaumu yeyote, maana uliwakumbusha. Na huo ni wajibu wa kila mcha Mungu anapoona kuna mwanadamu anapotea na kujitenga na upendo wa Mungu.