Majaji wa Kesi ya uhaini inayomkabili Lissu, wanatosha? Wanatenda haki?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Kwa kusiliiza hoja za mawakili wa serikali na hoja za Lissu, majaji wa hii kesi kweli wanatenda haki kwa hii kesi kuendelea kuwepo mpaka muda huu?

Kwa maneno mengine, majaji hawa wanatosha,?

Labda niulize: Je, maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kwa kesi za aina hii zilizotangulia, hayatoshi kufuta hii kesi?

Na je, kutoa uamuzi kuwa kesi iwe live, nalo ni jambo la kusubiri siku zote hizi?
 
Mtume ﷺ amesema:

"Majaji ni wa aina tatu: mmoja ataingia Peponi na wawili wataingia Motoni. Yule ambaye ataijua haki na akahukumu kwa haki – huyo yuko Peponi. Lakini yule ambaye ataijua haki na akahukumu kinyume nayo – huyo yuko Motoni. Na yule ambaye akahukumu kwa ujinga, bila elimu – huyo pia yuko Motoni."
(Sunan Abu Dawud, Tirmidhi, Ibn Majah)

👉 Hii inatufundisha kwamba:

Hakimu au kiongozi anapotoa hukumu kwa haki, kwa uadilifu, na kwa ujuzi sahihi – anapata thawabu kubwa na nafasi ya Pepo.

Lakini hakimu anayejua ukweli halafu akapindisha hukumu kwa upendeleo, rushwa au chuki – anakuwa miongoni mwa watu wa Moto.

Pia, hakimu asiye na elimu na akatoa hukumu bila ujuzi – naye anahesabiwa miongoni mwa waliokosea vibaya.
 
Nitawaelewa iwapo lengo la kuahirisha hii kesi mpaka Jumatatu ni ili wapate muda wa kutosha kuandika hukumu lakini sio kuendelea na hii kesi kabisa.
 
Ndiyo wanatosha Lissu apunguze kupanic katoa hoja za ajabu sama leo huko mahakamani
 
Tanganyika wamesema ataendelea kukaa rumande hadi kizimkazi aapishwe kuwa Raisi.......mahakama ya rufaa ndio watautupa upuuzi huu......
 
Jumatatu ndiyo itakuwa siku ya hukumu kwa Majaji wote wanaofanya kazi zao kwa kufuata maelekezo ya wanasiasa, badala ya kusimamia haki kwa mujibu wa viapo vyao.
 
Niliwaza ilikuwaje mkoloni mmoja anawatesa waafrika wengi kiasi hicho.

Leo mwanamke mmoja tena mbibi hivi anatuamulia tuiishije? Anateka ana ua anafunga. Aiseee
 
Back
Top Bottom