PreGE2025 Majaliwa: Zawadi pekee ya kuwalipa Rais Samia na Rais Mwinyi kwa maendeleo waliyoyaleta kwenye michezo ni "mitano tena"

PreGE2025 Majaliwa: Zawadi pekee ya kuwalipa Rais Samia na Rais Mwinyi kwa maendeleo waliyoyaleta kwenye michezo ni "mitano tena"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

View: https://www.youtube.com/live/2AL9sZGpSbA
WhatsApp Image 2025-04-22 at 11.08.07_26a166d5.jpg

WhatsApp Image 2025-04-22 at 12.59.34_e1090789.jpg

​

Ufunguzi wa kikao kazi cha Mafunzo na Mazingativu cha Maafisa Utamaduni na Maafisa Maendeleo ya Michezo Tanzania Bara, mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).

Ufunguzi huo unafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre -JNICC, ambapo mijadala mbalimbali inafanyika.
WhatsApp Image 2025-04-22 at 11.21.11_1bb2a5f9.jpg

WhatsApp Image 2025-04-22 at 11.21.25_db7189f7.jpg

WhatsApp Image 2025-04-22 at 11.21.24_66f41f55.jpg

WhatsApp Image 2025-04-22 at 11.21.14_c6cdbaf6.jpg

WhatsApp Image 2025-04-22 at 11.21.06_545c02a2.jpg

Majaliwa: Zawadi pekee ya kuwalipa Rais Samia na Rais Mwinyi kwa maendeleo waliyoyaleta kwenye michezo ni "mitano tena"
WhatsApp Image 2025-04-22 at 12.54.38_3baf1698.jpg

WhatsApp Image 2025-04-22 at 12.54.40_e8345548.jpg

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye ni mgeni rasmi kwenye Kikao Kazi cha 15 cha Maafisa Utamaduni na Maafisa Maendeleo ya Michezo, akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Aprili 22, 2025.​

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi Maafisa Utamaduni na Maafisa Maendeleo ya Michezo Tanzania Bara, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kutokana na mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta ya utamaduni Sanaa na michezo katika kipindi cha hivi karibuni zawadi pekee ambayo wanaweza kuzawadiwa viongozi (Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hussein Mwinyi) ni kuwachagua kuendelea na nafasi zao kwa miaka mitano mingine.

Amesema kuwa mafanikio katika sekta ya Michezo katika kipindi cha viongozi hao ni makubwa, ametolea mfano Timu za Taifa ikiwemo Taifa Stars, Serengeti Boys na Timu ya Wanawake kufuzu kushiriki mashindano ya Africon.

Aidha amesema akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Africon, anaridhishwa na jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kuwezesha uwepo wa miundombinu rafiki ambayo itatumika kwenye 'Africon' 2027 ambayo itafanyika kwenye Nchi za Afrika Mashariki Tanzania ikiwa miongoni.

Amesema viwanja mbalimbali vinajengwa pamoja na vingine kufanyiwa maboresho makubwa ili kuviweka tayari kwa ajili ya kutumika kwenye mashindano hayo.
WhatsApp Image 2025-04-22 at 13.27.56_c4abc6e5.jpg

WhatsApp Image 2025-04-22 at 13.28.00_c9e8cad2.jpg
 
Back
Top Bottom