Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Kazi nzuri,lakini hakuna njia rahisi ya kupata angalau mmoja akiwa hai ili aweze kurahisha kazi ya kuwakamata au kujua the motive behind these killings?
 
Hahahah...nimecheka sana! hiyo staili aliitumia sana kamanda Kova! alikuwa anaita press conference na kuchimba mkwara kuwa wamekamata majambazi yenye siraha na kuonyesha siraha hizo kwa waandishi wa habari. sasa watu wanajiuliza kwa nini hatusikii majambazi yakipandishwa mahakamani or hata kuonyeshwa sura zao. jamaa alifanikiwa sana kwa staili hiyo though mwishoni watu walimshitukia kuwa ni msanii...
 
Eti wenyewe nikuuwa tu! Hahaahaa! Ataenda the uolanzi huyu! Siasa nyingi sana kwa sito!
Kazi nzuri,lakini hakuna njia rahisi ya kupata angalau mmoja akiwa hai ili aweze kurahisha kazi ya kuwakamata au kujua the motive behind these killings?
 
naona sirro anatoa maelezo ina maana wakati wa ambush na yeye alikuwepo?
 
Chama cha kutetea majambazi watakuja kusema wameonewa.......
Hao majambazi wako wapi , uraia wao ni wa wapi, hawana id zozote mifukoni ? Jee kuna popote penye msiba maeneo hayo? Au sio watu wa kibiti wamekuja tuu.
Na jee kuna askari yoyote walau kapitiwa na risasi karibu ?
 
Hakuna majeruhi/survivor hata mmoja tu asaidie kueleza kwa nini walikuwa (allegedly) wanavamia na kuua viongozi wa CCM tu? Kwanini tumewaua wote? Kwanini hata mmoja tu hakupigwa shaba ya mguuni badala ya kifuani au kichwani?
Kwenye majibizano ya risasi huchagui pa kipiga
 
Wewe mtu, majambazi wana bunduki nane kumbukuka vinginevyo askari wetu ndio wangeuwawa, waache polisi wafanye kazi yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa wanaobeza hii wanalao jambo, kama ni utawala wa sheria hao wanaoua viongozi wapeleke shauri lao mahakamani tujue
 
Sasa wasipo tangaza Magufuli na watanzania watajuaje kwamba Siro na vijana wake wanafanya kazi
mkuu... kumbe hilo ndilo lengo lenyewe?
kweli kufa kufaana....
dokta anataka watu waugue!
mchonga jeneza anataka watu wafe!
hakimu anataka watu washitakiwe!
mwenye chuo cha QT anatamani failure wengi std 7!
masikini anapata faraja (siyo ahueni ya maisha) akiona tajiri anafilisika - kama ilivyo Tz sasa hivi!
mengine ongezeeni.......
 
Unawezaje Ku enforce law katikati ya majibizano ya risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi ama magaidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…