Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Wanapeleka watu kule na kuwapiga risasi na kuwawekea bunduki na silaha halafu wanajitekenya kuwa tumeua majambazi kibiti. Ndio tatizo la afrima uongo mwingi kwa kuogopa kufukuzwa kazi. Kwani unafukuzwa kazi pasipo hata kuchunguza kosa. Hakuna majambazi ambao tunaambiwa ni waliobobea na wamepata mafunzo nje leo hii wakae pmj. Watu wanapelekwa kibiti wanauwawa then polisi wanasingizia majambazi wa kibiti. Tusubiri muda utasema ndio polisi tanzania
Sisemi napingana na wewe, lakini natamani kujua, je unauhakika na haya uliyo yaandika...[emoji45] [emoji45]
 
IGP wetu sisi Watanzania tuna imani na wewe!! Mzee wa Field safi sana mambo ya kuletewa taarifa ofisini kwako hayana nafasi wanaweza kuleta taarifa hewa ila wewe unaingia mwenyewe front line kuwapa support vijana hiyo inaongeza morali sana na inapobidi unaingia kazini mwenyewe safi sana!! UONGOZI NI VITENDO!!!
 
Ni kweli waliouawa walikuwa majambazi!!?
 
Kurzwell
Media za TZ inaonesha Katika picha kuna silaha mbili siyo SMG bali ni maalum za kurushia mabomu ya machozi / mortar yaani "bunduki" zenye mitutu mipana.

Je hizo silaha za kurushia mabomu ya machozi / kujaza moshi ktk eneo dogo kama chumba / pango kumfanya adui kukosa hewa / kutoka machozi ni mojawapo ya silaha zilizoibwa toka vituo vya PolisI ?
 
Hakuna kitu hapo! Hivyo vitu wamekusanya kwa muda ndo wanakuja kutuaminisha! Hahahaaaa kazi kwelikweliii!
 
Ni kweli waliouawa walikuwa majambazi!!?

Wewe ukutwe porini na mzigo huo wote wa Bunduki usio na maelezo wala nini tunakuitaje? Ni jambazi tu na dawa ya jambazi ni moto, hicho kizazi kiteketezwe kabisa naona Polisi hawataki usumbufu wa kuyapeleka hata Mahakamani yakaenda kula sembe ya bure bora wayafyeke tu maana kaka, mama, baba , dada na askari wetu wamepoteza maisha kwa ajili ya hiyo mishwaini.
 
Huo mzigo ni wakuigiza wewe!

NDO HATA NA MIMI NASHANGAA,AU HUENDA HAWAITAJI KUSAIDIWA UPELELEZI.

Upelelezi wa nini sasa hivi ni kazi tu, ni utekelezaji na matokeo kuonekana upelelezi ulishafanyika sasa hivi ni kazi tu kumaliza hicho kizazi cha nyoka
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Embu tupe mbinu za kumkamata mhalifu mwenye silaha za moto kabla hajakudhuru wewe!
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Walikuwa wanajibizana.
 
Back
Top Bottom