kinja kinja
Member
- Jan 28, 2026
- 7
- 6
Pole sana k a k pamoja na familia
Huwa nawashangaa sana vijana, sijui huwa wanataka ku-prove nini!!!!pole sana mkuu
Japo wanasema ajali hubeba hadi mwenye tahadhari lakini Dar hadi rombo kwa bike ni hatari. Tukiwa vijiweni tukumbushane kuchukua tahadhari
Hakika.Mental health is real
Vijana wa Moshi na Arusha wanabidi wajifunze kuwa afya ni mtaji na Haina mbadala,pole sana mkuu
Japo wanasema ajali hubeba hadi mwenye tahadhari lakini Dar hadi rombo kwa bike ni hatari. Tukiwa vijiweni tukumbushane kuchukua tahadhari
Oh maskini hasara,hao majambazi Mungu atawaalani.Kama hujaoa nakushauri muoe huyo mke wa rafiki yako umstiri pamoja na huyo mtotoHabari za usiku wakuu bila shaka, mupo salama.
Leo imekuwa siku mbaya sana kwangu baada ya kupokea taarifa za kifo cha rafiki yangu, gERVASS maarufu kama Baraka. Alikuwa anaishi maeneo ya Malamba Mawili, sehemu inaitwa Bwawani. Ni mitaa ambayo niliwahi kuishi pia. Baraka alihamia huko tangu mwaka 2022 na akaanza biashara yake ya duka la mangi. Biashara ilimwendea vizuri sana hadi akanunua pikipiki yake mpya mwezi mmoja uliopita.
Hivi majuzi alisafiri na pikipiki yake pamoja na rafiki yake anayeitwa Macho. Walianza safari kutoka Dar kwenda Rombo. Safari ilikuwa inaendelea vizuri hadi walipoingia Mkoa wa Kilimanjaro usiku wa manane. Kumbe njiani kulikuwa na sehemu majambazi waliweka waya barabarani. Inasemekana walikuwa kwenye mwendo wa kasi, wakakunasa kwenye huo waya na kuanguka vibaya sana. Helmet yake ilipasuka na kichwa kikapata majeraha makubwa pamoja na sehemu nyingine za mwili.
Bila huruma, majambazi wakamshambulia kwa mapanga kisha wakachukua pikipiki yake na begi lake ambalo lilikuwa na kadi ya pikipiki, fedha na vitu vingine kadhaa.
Aliwahishwa katika Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC). Madaktari walijitahidi kupambana kuokoa maisha yake, lakini usiku wa kuamkia leo alifariki dunia.
Taarifa hii imeniumiza sana, hasa ukizingatia kuwa mwaka juzi alioa na tayari ana mtoto mdogo wa takriban miaka miwili. Leo nilipopita kumuona mke wake, nimejikuta nikiishiwa nguvu. Ni binti mdogo sana, hata miaka 25 hajafikisha, sasa anaenda kubeba jukumu la kulea familia peke yake akiwa mjane.
Baraka alikuwa na ndoto kubwa sana maishani. Ndoto zake zimekatishwa kikatili na watu wenye tamaa ya mali ambayo hawakuitafuta kwa jasho lao.
Nitaenda Rombo kumzika rafiki yangu Baraka. Nitaenda hadi Useri kuomboleza pamoja na familia yake. Nimeambiwa Macho hakupata majeraha makubwa, aliumia kidogo tu na tayari ameruhusiwa kutoka hospitalini.
Majambazi nawachukia sana. Mmeua kijana mdogo mwenye ndoto zake. Bora hata mngemchukulia pikipiki, lakini uhai wake mkamuachia.
Kifo kiko busy hakisubili TUMALIZE MISHE MISHE...Habari za usiku wakuu bila shaka, mupo salama.

Kusafiri ni pikipiki inawezekana ila sio hizi bodaboda.Duh Nchi hii unasafiri usiku na pikipiki
poleni sana kwa yote Mungu awe mfariji wenu poleni sanaHabari za usiku wakuu bila shaka, mupo salama.
Leo imekuwa siku mbaya sana kwangu baada ya kupokea taarifa za kifo cha rafiki yangu, gERVASS maarufu kama Baraka. Alikuwa anaishi maeneo ya Malamba Mawili, sehemu inaitwa Bwawani. Ni mitaa ambayo niliwahi kuishi pia. Baraka alihamia huko tangu mwaka 2022 na akaanza biashara yake ya duka la mangi. Biashara ilimwendea vizuri sana hadi akanunua pikipiki yake mpya mwezi mmoja uliopita.
Hivi majuzi alisafiri na pikipiki yake pamoja na rafiki yake anayeitwa Macho. Walianza safari kutoka Dar kwenda Rombo. Safari ilikuwa inaendelea vizuri hadi walipoingia Mkoa wa Kilimanjaro usiku wa manane. Kumbe njiani kulikuwa na sehemu majambazi waliweka waya barabarani. Inasemekana walikuwa kwenye mwendo wa kasi, wakakunasa kwenye huo waya na kuanguka vibaya sana. Helmet yake ilipasuka na kichwa kikapata majeraha makubwa pamoja na sehemu nyingine za mwili.
Bila huruma, majambazi wakamshambulia kwa mapanga kisha wakachukua pikipiki yake na begi lake ambalo lilikuwa na kadi ya pikipiki, fedha na vitu vingine kadhaa.
Aliwahishwa katika Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC). Madaktari walijitahidi kupambana kuokoa maisha yake, lakini usiku wa kuamkia leo alifariki dunia.
Taarifa hii imeniumiza sana, hasa ukizingatia kuwa mwaka juzi alioa na tayari ana mtoto mdogo wa takriban miaka miwili. Leo nilipopita kumuona mke wake, nimejikuta nikiishiwa nguvu. Ni binti mdogo sana, hata miaka 25 hajafikisha, sasa anaenda kubeba jukumu la kulea familia peke yake akiwa mjane.
Baraka alikuwa na ndoto kubwa sana maishani. Ndoto zake zimekatishwa kikatili na watu wenye tamaa ya mali ambayo hawakuitafuta kwa jasho lao.
Nitaenda Rombo kumzika rafiki yangu Baraka. Nitaenda hadi Useri kuomboleza pamoja na familia yake. Nimeambiwa Macho hakupata majeraha makubwa, aliumia kidogo tu na tayari ameruhusiwa kutoka hospitalini.
Majambazi nawachukia sana. Mmeua kijana mdogo mwenye ndoto zake. Bora hata mngemchukulia pikipiki, lakini uhai wake mkamuachia.
umewaza mbali sana Macho anaonekana hahusiki kwa scenario nzima hawezi safiri umbali wote huo marehemu inaonekana alijaribu kupambana naoHapana, hawa wanafunga wire unalala barabani pande zote mbili, mmoja anakuwa mbali kidogo. Sasa yule ndio anatoa taarifa kwa wenzie nyanyua wire wanakuja wanafunga juu upande wa pili. Wakimaliza wanashusha tena.
Huu uwizi wa namna hii wakati pikipiki za kichina zinashamiri waliwahi kutumia hata jangwani dar es salaam usiku wa manane.
Pole kwa wafiwa, lkn wanaohusisha hili jambo na huyo aliyepakiwa kwangu mimi siafikiani nao labda kama tukio hilo lingetokea dar.
Yani mtu awe na risk ya kupanda pikipiki kutoka dar avuke mikoa miwili kwenda kupora pikipiki kilimanjaro ambayo wakigawana hela haizidi laki tano.
afu ni hapo hapo HimoKm alipita njia ya himo mwika kutega waya ni mazoea ya hawa vibaka...hasa hasa kutoka himo km unapanda marangu
hahaha MkuuOh maskini hasara,hao majambazi Mungu atawaalani.Kama hujaoa nakushauri muoe huyo mke wa rafiki yako umstiri pamoja na huyo mtoto